Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Monday, December 6, 2010

Aisifuye mvua imemnyea-6


Nilimpa hela na kumwambia nashukuru kwa kumjua na ningefurahi nipate muda niongee nay eye zaidi, akasema yupo muda wowote, akaipokea na kushukuru halafu akaondoka. Kichwani nikawa najiuliza hayo maneno ya huyu mzee yana maana gani kwangu, na usemi wake wa `sasa wew sijui utakaa siku ngapi…’ mimi nina mpango wa kuishi hapo kama nyumba yangu, halafu naambiwa nitakaa siku ngapi…nikaguna.

              ******Endelea na kisa cha docta, ilikuwaje baadaye*******

Wakati mikakati ya nyumba ikiendelea mipango ya kumpata mchumba nayo ilikuwa ikifanyika , na niligundua kuwa wazazi wangu walikuwa wakiwaalika wasichana ambao walion wananifaa mara kwa mara kuja nyumbani ili kunifanya nishawishike na mmojawapo, lakini kila aliyekuja hakuwa mwenye sifa ninazozitaka. Na wao hawakutaka kunilazimisha au kuniuliza zaidi kuwa nina mpango gani, lakini kwa ujumla wasichana wote hawo sikuwahi kupata hata mmoja anayenifaa.

Siku moja siku ya kumapili, nikiwa nimeamua kupumzika nyumbani na wazazi walitoka kwenda kuwaona jamaa, nikawa sina la kufanya, nikaona nijipumzishe chumbani kwangu, wakati nikiwa nimejipumzisha kitandani, mara nikasikia mtu anagonga mlangoni mwa chumba changu. Nikijua kuwa ni wadogo zangu nageukia ukutani, na kujifanya nina usingizi, halafu kwa sauti ya usingizi nikasema.

‘Karibu ingia, mlango upo wazi,,,’

Dakika ikapita na sikusikia mlango ukifunguliwa, nikageuza kichwa kuangalia mlangoni, nikaona mlango umefunguliwa kidogo kidogo na mara macho yangu yakakutana na macho ya binti mmoja mrembo, alikuwa kaonyesha kichwa tu huku kiwiliwili kingine kikiwa nje. Moyo ukanilipuka na kuingiwa na muwashawasha wa kutaka kumjua huyu binti vyema. Nikajiinua kitandani na kumkaribisha, lakini hakuingia, akawa kaganda pale mlangoni.

‘Mbona huingii, karibu ndani…’ nikainuka kitandani na kuelekea pale mlango,

‘Samahani, nilikuja…kuku, samahani nina haraka nilikuja mara moja, baba na mama mwenye nyumba hii wako wapi, walisema wanahitaji mfanyakazi wa nyumbani, sasa nimekuja sikuwakuta, …’ nikaguna kidogo, kwani moja ya sifa ya mke nimtakaye, ni awe kidogo kasoma, sasa huyu anaonekana kaishia darasa la saba, hanifai… Lakini yale macho yake, mmmh, na sura yake mmmh…


Nikatoka nje ili kumwangalia vizuri, na hapo nikakiri kuwa Yule msichana kajaliwa na umbo zuri na sura pia, na nilishangaa kwanini hajaolewa mpaka anahangaika kutafuta kazi za ndani. Kwani kwa uzoefu wangu, mabinti wazuri kama huyu huwa wameshaolewa, labda wawe na tatizo fulani, nikamchunguza kwa makini huku akiwa kaangalia chini, akichezea vidole vyake! Nikaona nimdadisi kidogo kujua historia yake. Alikuwa anasita kuniambia lolote kuhusu ukweli wa maisha yake, lakini baadaye akanifunulia kisa cha maisha yake ambacho kilinifanya nimuonee Huruma sana.

'Kaka mimi simjui baba wala mama yangu,..’ akaonyesha uso wa huzuni alipotamka maneno haya, nikaingiwa na simanzi na kujuta kwanini nimemuuliza swali hilo, kichwani niliwaza mbali nikadhani ni miongoni mwa wahanga wa hili gonjwa la ukimwi, labda wazazi wake walifariki akiwa mchanga. Nikajipa moyo nimdadisi zaidi..

‘Huwajui kwa vipi huwezi kuzaliwa kutoka mbinguni, lazima ulizaliwa na baba na mama, au nimekosea,..’

‘Akajitahidi kutabasamu na kuinua uso kuniangalia, na pale nikaona mchirizi wa machozi mawili yakimtoka. Nikatoa leso yangu na kumfuata pale aliposimama, nikamfuta taratibu, akatabasamu wakti nafanya tendo lile, na pale uzuri wake ukaongezeka zaidi.

‘Kaka yangu, mimi sipendi kuwasimuliwa watumaisha yangu haya, kwani wengine walidiriki kuniona muwongo, na ninaelezea haya ili nipate wasmaria wema wa kunisaidia…’ akaangalia chini tena.

‘Usitie shaka, mimi nimeshakuamini, na utakachoongea, ujua kitabia humu humu..siunajua kuwa mimi ni dakitari, huwa naficha siri za watu wengi, usijali ongea tu…’ nimapma moyo

nililelewa na msamaria mwema aliyeniokoja nikiwa nimetupwa jalalani nikiwa kichanga. Msamaria huyu ndiye ninayemtambua kama mzazi wangu, ingawaje naye maisha yalimshinda akanikabidhi ustawi wa jamii. Na huko ustawi wa jamii wakanikabidhi kwa kituo cha kulelea watoto wasio na wazazi.

‘Kwahiyo kaka ukitaka kujua maisha yangu, ni hivyo tu, mengine ni yale ya kuteseka vituoni kama unavyojua, kule kuna watoto wa kila namna, wengine watukutu, wengine walikuwa wakivuta bangi, kunywa madawa ya kulevya, sasa mnakuta mumechanganywa pamoja. Inabidi uwe na kichwa kigumu kuvumilia. Mimi nilikuwa napenda sana kumcha mungu, kwahiyo walimu na walezi wangu walinipenda sana, na wakwa na hamu ya kunisomesha zaidi.

Baadaye kile kituo wafadahili wakaondoka kwenda kwao wakakikabidhi kwa wazawa, na kwa vile kulikuwa hakuna fungu maalumu la kutulea, sanasana tulikuwa tukitegemea misaada ya watu mbalimbali, na hili likakifanya kituo hicho kiyumbe. Walezi waliokabidhiwa wakawa wanatushauri wale ambao ni wakubwa, tutafute kazi za ndani, nami nikafanya hivyo. Nilibahatika kupata kazi ya ndani kwa Mhindi mmoja, lakini pale palinishinda, kwasababu kazi nyingi, na wanakufanya kama mtumwa, na haya Yule baba akawa na tabia mbaya, mimi nikaona niache nirudi kwenye kituo changu kwani ndiye baba , ndiye mama.

Jana ndio nikasikia wazazi wako walikuja pale wakaniona wakaniuliza nina kazi gani, mimi nikawaambia maisha yangu , na wakanionea Huruma, wakaniambia hata wao walikuwa wakihitaji mfanyakazi wa ndani lakini hawatanilipa mshahara mkubwa. Mimi nikawaambia hamna taabu ilimrdi nipate sehemu ya kujishikiza, kama nitapata sehemu nyingine yenye maslahi zaidi nitashukuru…’ akasema huku anatka kuondoka.

Nilimuomba awasubiri wazazi wangu, kwani hata mimi nitamsadia apate kazi hapo, na nitamlipa mshahara mzuri asiwe na wasiwasi. Alipopata uhakika ule akakaa kwenye kiti, nami nikaendelea kumdadidi kuhusiana na maisha yake, hadi wazazi wangu walipofika na kuwaachia wanendelee kuongea naye. Nilikuwa nimevutika sana na huyu binti, lakini nilijua kuwa tofauti ya elimu inaweza ikawa kikwazi kikubwa kwangu, hasa katika mipangilio ya kazi zangu, pili nikiondoka kwenda ulaya, inabidi niondoke naye, je huko mawasiliano yatakuwaje!

Ikapita siku kadhaa, wakati naongea na wazazi wangu, tukawa katika utani wa hapa na pale, nikataka kuwachokoza wazazi wangu, nikawauliza kuhusu huyu binti, wanamuonaje akiwa mchumba wangu, wazazi wangu walicheka sana, na hawakutaka hata kunisikiliza maelezo yangu niliyotaka kuwapa, ….

‘Hivi wewe wasichana wote warembo, wenye sifa nzuri, elimu, tumekuletea, unamtaka huyu mfanyakzi wa ndani, ambaye historia yake ni mtoto wa vituo vya mayatima…hilo hatukuungi mkono, lakini ni uamuzi wako..’ akasema baba.

Nikawaambi nilikuwa nawatania tu, ila ni vyema tukamjali kama sehemu ya familia, nikawaambia hatua ya kwanza tumsomesha, ili baadaye aweze hata kujiajiri mwenyewe, atakuwa anafanya kazi za nyumbani ikifika saa sita, atakuwa anakwenda shule kusoma hasa lugha na hesabu na baadaye tutampeleka kusomea unesi. Kama atafanya vizuri, mimi nina mpango wa kuanzisha hospitali yangu, atakuwa akinisaidia kama nesi. Na kwasababu hilo ni la mipango ya mbeleni, itawezekana tu. Wao wakawa hawana kipingamizi kwa vile gharama zote nilikuwa natoa mimi.Na ikawa hivyo, anafanya kazi za nyumbani ikifika saa sita anakwenda shule.

Hutaamini watu kama hawa waliokulia katika mazingira magumu, wanajaliwa kuwa na akili za ajabu, ni kwa vile tu hawakupta watu wakuwasimamia, kwani msichana yule alikuwa na uwezo mkubwa wa kielimu, kwenye masomo yake alikuwa kifanya vizuri, nami kila akirudi nikawa namfundisha na kuongea naye kumpima, alikuwa ni kipaji cha lugha, na hata yale machache niliyomfundisha kuhusiana na madawa, huduma kwa wagonjwa, binadamu alivyo, aliyashika kwa muda mfupi sana. Nikamnunulia vitabu vya awali vya unesi, nikiwa na imani kuwa atakuja kuwa nesi mzuri.

Kwa ile hali ya kuongea naye mara kwa mara tukawa tumejenga mahusiano ya kuwa naye karibu. Siku zilivyozidi kwenda, nikawa navutika sana nay eye, lakini sikuweza lolote la mapenzi, nilimuona kama mtoto wa nyumbani. Lakini wazazi wangu wakanihisi kuwa huenda nimeshampenda huyu binti na kwahiyo wakaingiwa na wasiwasi… hadi siku moja baba akaniuliza nina uamuzi gani wa kutafuta mchumba!

Nikawadanganya kuwa nina msichana ambaye nimeanza kuzoeana naye na huenda akaweza kuwa mchumba wangu, wao wakafurahi sana wakaomba kama ikiwezekana nimlete hapo nyumbani wamuone, na wazo la kuwa kweli sina nia ya kumchukua huyo mfanyakzi wa ndani kama mchumba wangu likawaondoka kichwani mwao.. Hata mimi kwa muda ule, zaidi ya kuvutiwa naye kwa sura, maumbile na tabia, na uhudi zake katika masomo sikuwa nimefikiwa uamuzi wa moja kwa moja wa kuwa yeye anaweza kuwa mchumba wangu.

Siku moja nilimchukua kwenda katika nyumba yangu, ili akanisaidie kufanya usafi. Nilikuwa sijahamia rasmi, kwani kulikuwa na matengenezo madogo madogo ya hapa na pale, na nilipanga ikikamilika vizuri, nihamie na mke nitakayemuoa. Nilipofika niliwakuta mafundi wapo nje, nikawauliza vipi maendeleo, wakawa na wasiwasi kuniambia chochote, baadaye mmoja akasema kuwa fundi wao mmojawapo kakimbia, kasema hawezi kuendelea kujenga eti kuna mambo yamemtisha akiwa ndani , kwani yeye alikuwa akilala humo kulinda nyumba pamoja na vifaa vyao vya ufundi.

‘Mambo gani na nyie, mafundi wazima mnatishwa na kitu gani..’ nikawauliza kwa mshangao

‘Aaah, huyo na mambo yake siunamjua anatokea huko Bagamoyo, basi ana yale mambo ya kikwao,..lakini bisi, usiwe na wasiwasi sisi tutapiga mzigo, tumetoka bara, kuja kufanya kazi, hayo mambo mengine hayatutishi, ila mzee nakushauri kabla ya kuhamia hapa, soma kisomo cha nguvu, nyumba nzuri kama hii inahitaji ulinzi, huko bara tunaita zindiko, waite watu wa dini, waisomee nyumba hii, ili kuwe na amani, kwani huwezi jua aliyeondoka mwanzoni alipaachaje…’ akasema Yule fundi.

‘Sawa kabisa mimi nitafuata ushauri wako, nyie malizieani sehemu iliyobakia ili nianze maadalizi mengine..’ nikasema huku nakagua huku na kule.

Baadaye nilimuita Yule binti ambaye kwa muda huo alikuwa bado ndani ya gari, akaja na kuingia ndani, nikamwambia aangalie utaratibu uliopo mle ndani kama anaweza kupamba, au kubuni uwekaji wa vitu , kwa vile nilimuona ni mjuzi sana wa kupamba nyumba na usafi, nikaona anweza kusaidia kwa muda.

Akawa anazunguka kukagua huku na kule mara, akasimama ghafla, na akaanza kutetemeaka kwa nguvu sana, na macho yakamtoka pima. Akaanza kuweweseka na kupiga kelele. Mimi nikashikwa ma mshangao, na hata kabla sijachukua uamuzi, akakurupuka mbio kunifuata pale niliposimama, akanishika mkono, na kunizungusha kama kitoto kidogo, na kunitupia mbali, nikagonga ukutani .

‘Wewe ndio unataka kumchukua kiti wangu, leo nitakuonyesha kuwa mimi ni nani…akawa anazungumza maneno yasiyofahamika huku ananifuta pale niliposilala, nikiwa na maumivu ya kugonga ukutani. Nikaona hapa hakuna jinsi, ngoja nimkwepe na kukimbilia kwenye kibegi change ambacho huwa natembea na vifaa vya kihospitali. Kama kuna sindani ya usingizi nimdunge…

Wale wafanyakazi walisikia vurugu hizo wakaa mbio kuangalia nini kimetokea, walinikuta napekua mkoba, huku Yule binti akinijia akiwa ananguruma kama samba dume, wote wakaduwaa wakiwa hawajui wafanyeje, na yule mkuu wa ujenzi niliyeongea naye mwanzoni alionekana kuyajua hayo majambo, akawa anamsogelea Yule binti huku anasoma maneno mbalimbali mdomoni, akiwa kama anamuomba huyo sijui shetani amsamehe huyo binti… na ghafla Yule binti akasimama, na taratibu akawa anageuka, kwa yule fundi mkuu, akawa kasimama naye sambamba.

Ghafla, yule fundi mkuu akashikwa shingo kwa mikono miwili, akainuliwa juu miguu ikawa inachezacheza chini. Nilishangaa, nguvu gani yule binti alizo nazo kuweza kunirusha mimi kama katoto, na sasa kamuinua huyu fundi ambaye ni pande la jitu! Nikawaangalia wale mafundi wengine, kama watakuja kumsaidia mwenzao, lakini wote walikuwa wamekodoa macho ya uwoga.

Yule fundi mkuu alikuwa akijaribu kujiiokoa mikononi mwa yule binti bila mafanikio, na kifo kilikuwa kikimkodolea macho, nikaona lazima nifanye jambo la haraka, nikaweka dawa ile kwenye sindani nikawa namfuatilia yule binti kwa nyuma.

‘Ukimpiga sindano utamuua…’ nikasikia mmoja akisema miongoni mwa wale mafundi, na yule binti akamrushia mbali yule fundi mkuu akawageukia wale mafundi wengine, wao kuona vile wakatimua mbio….

Ni mimi: emu-three

6 comments :

Jane said...

Jamani nini tena hicho kilichomkamata huyo dada???????????? Mmmmh! ngoja tuone maana inaanza kunitisha. kazi nzuri Mzee.

elisa said...

jamani mbona mambo ..mmh sina la zaidi

Faith S Hilary said...

Mmmh! Kimempata nini bidada

Jane said...

Mmmmmh! jamani kwema huko?????????? Mbona leo kukavu??? Boss kabana nini??? Tunakumiss jamani wana jamvini.

Jane said...

Mwe mwe mwe, jamani M3 leo mpaka computer yangu imenikoma maana kila wakati nachungulia hakuna kitu. Hope kesho utatupia kitu kidogo. Jioni jema na kazi njema pia.

emuthree said...

Samahanini sana nilikuwa nimetingwa, boai alinikalia begani, sikuweza kufanya lolote, lakini leo hiyo nimeshaiweka, karibuni sana