Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Friday, December 24, 2010

Aisifuye mvua imemnyea-17

‘Kwani chakula hicho nichakawaida tu, au kuna sherehe au mualiko, maana kama ni mualiko na kadi zimetolewa tunaweza kusema vinginevyo, lakini kama ni chakula cha kawaida kama ufanyavyo kila siku , basi siku nyingine sio mbaya. Lakini ngoja tumuite Maua ataamua mwenyewe..’ akasema mama mwenye nyumba.


  **Je ni nini maamuzi ya Maua, na kilindeleaje, karibuni tena, kwenye mfululizo wa kisa hiki***
 Na kwasababu ya mapumziko ya sikukuu, huenda mundelezo utakuwepo mwakani ,labda kama nitapata nafasi kwenye internet cafe.    Kwahiyo  Blog inawatakia sikuku njema.
Tuendelee na kisa chetu sehemu inayofuatia tukumbuke Maua kasimama mbele ya Wazazi na madakitari wawili, kama picha inavyoonyesha juu. Ikawaje, soma mwenyewe.....

            *************                                                                       ***************
‘Maua unaitwa barazani kuna wageni..’ kijana wa bustani aliitwa kuja kumita Maua, wazee wale hawakutaka kwenda kumita wao isije ikaonekana wamemshawishi aamue wapendavyo. Maua akagutuka toka kwenye lindi la mawazo ikabidi amuite yule kijana karibu na mlango akamuuliza kuna wageni gani, yule kijana akasema yeye anahisi wote waliofika hapo ni madakitari na mmojawapo ni yule dakitari wa hapo jirani. Akataka kumuuliza kuna nini kinaendelea lakini akasita na kurudi ndani.

Maua akajiweka vizuri huku anajiuliza ataenda kusema nini, na kwanini wamemuita, huenda kuna kutokuelewana kati ya hawo madakitari na yeye anaweza akawa chanzo. Akasimama,halafu akakaa tena, akatembea huku na kule akarudi kukaa, hakujua afanye nini, na atasemaje akifika mbele ya hawa madakitari, tena mbele ya wazazi wake. Mwishowe akaamua kwenda akijipa moyo kuwa uamuzi ni mmoja wa kuolewa, mengine yatafuata baadaye.

Alitoka mle chumbani na kuelekea chumba cha maongezi na alipofika hapo aliwakuta wote wanamkodolea macho yeye. Ilibidi atizame chini wakati anatembea, akakumbuka alivaa gauni la Rozi ambalo ni zuri sana na mapambo yake, kwa vile alijua anakwenda kupata chakula mara moja nakurudi, na hata hivyo alitaka aonekane mrembo kwa anayetaka kumuoa.

Madakitari walishusha pumzi na kupandisha walipokiona hiki kiumbe kilichojitokeza mbele yao kilikuwa mvuto na kila mmoja aliomba moyoni ajaliwe kiumbe hicho kiwe mkewe. Lakini ilikuwa kazi kubwa kujua ni nani atakaypata bahati hiyo. Na Maua mwenyewe alikuwa akitembea huku anamuomba Mungu wake amsaidie aweze kutoa maamuzi ya msingi, kwani hapo yupo kwenye mtihani wa kuamua kuolewa au kusoma. Alishahisi huo ndio mgongano uliopo…

‘Karibu Maua usiwe na wasiwasi natumai wote hawa unawajua vyema, na huenda unawajua zidi yetu, yule ni dakitari wetu jirani’ Mzee mwenye nyumba akaanza utambulisho licha ya kusema awali kuwa Maua anawajua, lakini kiheshima akafanya hivyo. Alipomtaja huyo dakitari wa Sinza, Maua akainua uso kumwangalia na kumsalimia kwa heshima. Na dakitari akaitikia huku uso umejaa tabasamu.

‘Na yule ni dakitari ambaye najua ndiye mliyekuwa mkiishi naye kabla ya kurudi tena hapa..’ Maua akamwangalia Dakitari wake na akatabasamu, na kumsalimia. Alitabasamu kwasababu anakumbuka dakitari huyu alikuwa hapendi kusalimiwa kwa kupewa shikamoo, na mara nyingi walikuwa wakisalimiana kama kijana mwenzake. Lakini kwa hapo ilibidi aonyeshe kuwa anaheshimu kwahiyo shikamoo ikatoka kama kawaida.

Dakitari wangu aliitikia na kutababasamu, alimtizama Maua kwa makini, na alihisi moyoni kuwa kuna mabadiliko makubwa kwa msichana huyu, alionekana kuwa na mtizamo fulani moyoni ambao hakuwa nao kabla, inaonekana kawa mjanja, au kujiamini kidogo. Akasema moyoni kwa shaka, kuna kitu kinaendelea hapa ambacho yeye hakijui , lakini cha muhimu ni kumuelimisha na huenda kama ana fikira nyingine awahaiwe kabla hajapotea.

‘Sasa Maua tumekuita hapa kwasababu tumekwama kuamua jambo, kwani asubuhi ulikuwa umejiandaa kwenda kwa Dakitari mliyekuwa mkiishi naye, na bahati mbaya hakutokea kwasababu ilitokea dharura hospitalini kwao akaitwa alifajiri na unawajua madakitari hiyo ikitokea hawana jinsi ni wajibu wao kufanya hivyo, na alikurupuka nyumbani akasahau na simu yenye namaba zetu kwahiyo ikawa shida kuwasiliana nasi, sisi tumeliona hilo na hatutakiwi kumlaumu na badala yake tumpe pongezikwa kuokoa maisha ya mtu aliyehehitaji huduma yake…’ mzee akaongea na kumtizama yula dakitari halafu Maua.

‘Sasa tatizo likajitokeza kuwa rafiki yake huyu dakitari wetu jirani alikua kakualika chakula cha mchana kwasababu hatukujua tena kuwa dakitari huyu atakuja, na tukakubali, kumbe ikawa tumezua mgongano. Na tumeshindwa tufanyeje, kwani kama alivyoelezea jirani yetu hicho chakula kimetolewa taarifa na kimeshatayarishwa kwa ajili ya watu wawili. Na ameomba kuwa ni muhimu muende wote wawili. Lakini dakitari mliyekuwa mkiishi naye anasema kama inawezekana muende wote watatu mkimaliza kula basi wewe usirudi huku uondoke na yeye…’ akasimama hapo nakuwaangalia wale madakitari.

‘Tatizo ni kuwa dakitari jirani anasema chakula hicho ni kwa ajili yenu wawili na anaona hakuna umuhimu wa wewe kuondoka leo kwani hata ukikosa shuke yeye anamipango ya kukutafutia shule nyingine, kwahiyo haina haja ya kuondoka…’ akatabasamu alipofika hapo.

‘Mimi najua vijana mna mambo yenu, na huenda mlishaongea na hicho chakula labda ni sehemu ya maongezi yenu, tukaona tukuite wewe uwe muamuzi kwasababu dakitari mliyekuwa mkishi naye anasema kesho ndio mwisho wa kujiandikisha na ameshalipia kila kitu ni wewe kwenda kujiandikisha na mambo mengine naaa…n i vyema mkaondoka wote leo hii, ili kesho uamukie kwake kwa ajili ya maandalizi zaidi. Sasa unaona jinsi tulivyowekwa njia panda, kwani wote wanaazima ya kufuata mtakwa yao. Na kama nilivyosema nyie vijana mna mambo yenu, tusije tukaamua jambo ukaja kutulaumu baadaye, sasa wewe ni uamizi wako kwenda kwa dakitari aliyekutafutia shule au kwend kwa chakula cha mchana na yeye mta…’ akakatisha kumalizia na kunywa maji kwenye gilasi.

Maua alimwangalia dakitari wa sinza na kumuona akitabasamu kuonyesha kuwa ana uhakika na maamuzi yake na hili lilimpa Maua wakati mgumu, kwani hakutaka kabisa kumvunja nguvu yoyote na hapo hakujua aamue vipi. Lakini akaona ni vyema aende kupata chakula hicho cha mchana na akitoka hapo ndio aende kwa dakitari wake. Lakini je ataeleweka hivyo na je huko kwenye chakula cha mchana atamuelezaje huy mwenzake kuhusiana na uamuzi huo. Na kama kweli ana nia ya kumoa, na kumsomesha kwanini akimbilie shule ya dakitari wake na huku hajui nini itakuwa baadaye. Akilini aliona ndoa ina umuhimu sana…lakini …lakini

‘Wazee wangu naona munanipa wakati mgumu, kwasababu nia yangu haikuwa hivi,..najua hali iliyopo naweza kuamua jambo likamuuzi huyu au yule,na huenda likaleta kutokuelewana, mimi nafikiri ni vyema kwa vile chakula kipo tayari niende huko na kama …’ akamuangalia dakitari wake ambaye alikuwa kaanza kusimama. Aligundua kuwa maneno yake hayakumfurahisha, na hakupenda itokee hivyo.

‘Hapana dakitari usiondoke tuanataka kuyaweka sawa, huyu ni rafiki yako, na mnajuana vyema lakini kitu kidogo kama hiki kinaweza kuwafanya mkafarakana, mimi naomba uondoke hapa mkiwa mumekubaliana, sisi kama wazazi tunataka kuwe na amani …’ akasema baba mwenye nyumba huku akionyesha mkono wa kumkalisha dakitari asiondoke. Na mama mwenye nyumba akaona na yeye aingilie kati na kusema haya;

‘Jamani Maua ni mtoto wetu, nia ya kuwa naye ni kumsaidia, hatujui mna malengo gani na yeye zaidi ya hilo la kumsomesha, hatungependa kuwe na ajenda ya siri ya kumharibia maisha yake, tunaomba tuwe na busara na hili, na tujue huyu ni mtoto. Na kumuweka katika mazingira kama haya mnampa wakati mgumu sana. Nyie wawili ni wasomi na ni wakubwa kwake ni vyema mlitatue hili kwa busara. Kama nilivyosema awali kama ni chakula cha mchana cha kawaida tu, kila siku kipo, basi leo kisameheni jirani yangu, sizani kama kitakuwa kimepakuliwa kinasubiri kuwa kitapoa, labda kama una mengine…. Mimi ningepedna sana huyu binti asome kwanza, mpeni muda huo wa kusoma kwanza’ akasema mama yule na kumtizama yule dakitari jirani yao.

‘Mama kama kuna mengine yatajileta baadaye, mimi hicho chakula ni muhimu ili kama kuna mengine tuje kuwaambia, naomba tena Maua atuelewe, nia yangu sio mbaya, na haina haja ya kusema kuwa ukimaliza chakula uondoke, mimi nina mipango ya kukusomesha shule bora zaidi ya hiyo, wewe twende na …’ akamgeukia rafiki yake kumwangalia. ‘Naomba rafiki yangu unielewe hili sina nia mbaya ya kukuharibia mipangilio yako, ila naomba uniachie huyu binti kwani nina malengo naye muhimu…na chakula hicho kimeandaliwa kwa watu wawili itakuwa ajabu narudi pale peke yangu, au tunaenda watatu…nitaelewekaje kwenye hoteli kama ile..’ akasema na kumwangalia Maua Docta mwenzake halafu akamgeukia Maua.

‘Malengo hayo umeyaanza sasa hivi, mimi yalikuwepo kabla yako rafiki yangu, na unakumbuka niliwahi kukuhadithia kwa juu-juu mipangalio yangu na insi ya kumsaidia Maua na ukaniunga mkono. Leo imekuwa kinyume, vipi rafiki yangu, naona labda una mengine zaidi ya hayo…’ akasema Docta wangu , `Lakini uamuzi mkubwa upo kwa Maua, kama anaona niliyotaka kukufanyia hayana maana basi, lakini inabidi pia tuwaarifu wale wazazi wangu waliokuchukua kule ulipokuwa mwanzoni, sio kwa nia mbaya na siongei hili kukulaumu…sijui Maua unasemaje, kwani naona upo njia panda, na nakuonea sana Huruma kwa hili kwaani hata mimi haikuwa lengo langu kukuweka katika hali hii, na sikujua itakuwa hivi ila haina jinsi na ujue kuwa hili ni kwa ajili ya manufaa yako, nani vyema ukafikiri vyema uamuzi wako…’ akamwangalia Maua kwa makini.

‘Uamuzi mkubwa ni nyie mkubaliane, mimi ..’ Maua akanyamaza, kwani mlango ulifunguliwa ghafla, na wote wakageuka kutizama nani kaufungua mlangoni bila hata hodi na sauti nyororo ikasema kwa madaha. …

‘Mimi nitawasiadia kutatua tatizo hili msiwe na shaka…’

Ni nani huyu mtatuzi na atalitatuaje hili tatizo na kweli litatatulika..naomba tundelee kuwepo

Ni mimi: emu-three

12 comments :

EDNA said...

X-Mas njema Emu.....Swali la kizushi, Umeshanunua viungo vya Pilau? heheheeee.

emuthree said...

Na wewe pia Edna, sio vya pilau tu , kila kitu wewe njoo na ndizi tu...lol
Karibu sana na Xmas njema wewe na familia yako!

Albert Kissima said...

X'mass njema na mwaka mpya mwema.

..huyu alikuwa ni Rose, ambaye naye kwa mbali alikuwa akifuatilia kila kilichokuwa kinaendelea. Alishapanga ataongea nini na kwa namna gani atamnyang'anya Maua tonge aliloanza kulipeleka mdomoni, kwani tayari na yeye alishakuwa na wivu wa kimapenzi. Ukaribu na madakitari wale ni jambo ambalo lilimfanya naye asikae kimya, yani utata uliokuwepo usipite bila yeye kusema lolote. Naye alitaka kujaribu bahati yake. Alitaka kupima upepo kwa upande wake unaelekea wap.... Teh! teh! teh! Em-3, niachie mimi niendelezeeeeeeeee!

nyahbingi worrior. said...

nIMEPITA KUKUSALIMU NA KUKUJULIA HALI.MZIMA?

Faith S Hilary said...

Muendelezo utakuwepo mpaka mwakani?????? Mama yangu weeee M3 unanipandisha blood pressure lol! Ukipata nafasi usitusahau maana kiporo hiki kitakaa kutoka 2010 mpaka 2011 nafwa mie! Happy Holidays dear! xx

Anonymous said...

emu unaleta uhondo lakini unazungusha sana usiwe unazungusha sana maneno ili utamu ukolee.

Anonymous said...

Kimya jamani mbona dia? Wapi muendelezo wa ulipoishia?

Rachel Siwa said...

hahahha dada Edna maana sisi bila pilau sikuu haijafanyika!@emu miminilichelewa kuja xmas je mwaka mpya pilau ipo?

EDNA said...

HERI YA MWAKA MPYA 2011

Masangu Matondo Nzuzullima (MMN) said...

Emu-three: Kila la heri kwako wewe pamoja na familia yako. Hebu mwaka huu mpya na ukawe na mafanikio yasiyopimika. Mbarikiwe hadi utimilifu wa dahari!!!

Tunatumaini kwamba diary itakuwa kali zaidi...

emuthree said...

Nashukuruni sana wapendwa diary imejiandaa vyema, na mwaka mpya tutawaletea mambo kemkem. msikonde washikaji, tupo pamoja.

Anonymous said...

Vipi Tena Miriam, mbona hadithi mpya na hii haijesha? wapenda kutuweka tumbo juu nawe....akhaaaa