Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Thursday, November 25, 2010

Utangulizi wa kisa kipya-aisifuye mvua imemnyeshea


  
  Jamaa yangu dakitari kanitembelea leo nyumbani kwangu, unapapata watu kama hawa unakuwa makini sana, hasa katika mongezi yako, aidha unapata faraja kubwa kuwa, huenda katatizo kako ka siku nyingi katapata ufumbuzi, ki- hali au na-mali, lakini bora zaidi ni msaada wa mawazo. Kwahiyo katika akili yako utakuwa umejenga hisia ya kupokea, hisia ya kupata sio kutoa.


‘Rafiki yangu, nimekutembelea leo, unajua nyie watu mnaoishi huku ndani ndani wengine hupaita `uswazi’ na wale watumwa wa akili wanapaita `uswahilini’ mimi sipendi jina hilo, kwani lina dhana potofu. Najua mnaoishi maeneo haya mnajua mambo mengi, kwani mpo karibu na watu, sio sisi muda wote upo ndanii ya geti la nyumba yako.

‘Rafiki yangu hili lililonipata linahitaji uzoefu na fikira pana. Nimefika mahala nimekwazika, na hata sijui nifanye nini. Lakini mimi ni mtaalamu, na utaalamu wangu ni wa kisayansi, sio wa imani , hasa imani za kufikirika. Siunajua tena sisi madakitari, tunahitaji uthibiti wa kitaalamu, vipimo na maelezo yakinifu…’ akatoa kumputa yake ndogo na kuifungua.

‘Unajua maisha haya, unaweza ukakata tamaa kwa siku moja tu, na mara mtu ukajitundika, watu wakasema aaah, aah, lakini wasijue kuwa kuna sehemu umefika ukasema , maisha basi…lakini huo ni udhaifu wa akili. Mtu kama mimi siwezi kufikia hatua hiyo. Lakini kuna mazingira yanaweza yakakulazimisha, ukajiona mwenyewe bila utashi wako unachukua kamba unajitundika, huyo unachukua suma unakunywa, hujijui kabisa! Unatanabi, na kujijua wakati mambo yameshaharibika, sijui ukiokoka utawaambiaje walimwengu!!?’ Akaniangalia, usoni, sikujua kuwa ananiuliza swali au ni sehemu tu ya maelezo yake!

`Kuna kisa kimenikuta, na kisa hiki nimeamua kukivalia njuga, nafikiri nikifika mwisho wa uchunguzi wangu nitakuwa katika sehemu nzuri ya uamuzi,na huenda nikagundu kitu Fulani, na hapo nitakuwa na uhakika na dhana yangu, dhana za watu. Dhana….’ Akatizama komputa yake halafu akaifunga.

‘ Unajua rafiki yangu, sisi wanadamu tumetawaliwa na `imani’ lakini imani yetu ni ya `dhana’ na haipo thabiti,mara nyingi imani zetu zinategemea sana ujaji wa tukio. Wengi wetu tunadai kuwa tunamcha mungu, kweli si kweli?’ akauliza, na kabla sijasema kitu akainuka. Akasimama na kuonyesha mfano wa jinsi watu wanavyofanya ibada, kwa jinsi anavyojua yeye, halafu akarudi kukaa.

‘Hivyo basi, hiyo ndiyo imani yetu..’ akaonyesha mkono wafanyavyo Wakristo, na halafuu akainua mikono juu kama Waislamu wanavyoomba dua, halafu akainama chini kama anatafakari kitu.

‘Imani hiyo ni ya kujionyesha kuwa mimi ni dini gani, mimi ni mcha mungu wa namna gani , mimi najua kuabudu…lakini kweli watu hawa wanamuabudu mungu, kweli wanaimani thabiti ya kumcha Mungu, sidhani…sidhani. Nasema hivi kwasababu kama kweli wewe unamuogopa mungu, kwanini unafanya matendo mengine ya dhambi kisirisiri, huku unaangalia pembeni kuhakikisha kuwa hakuna mtu anayekuona. Kwanini ofisini unakwiba kwa kutumia karatasi, kwanini hospitalini una….’ Akatikisha kichwa kwa kusikitika.

‘Ina maana hapo umesahau kuwa Mungu yupo nawe wakatii wote, kama kweli ungemwamini mungu ungeogopa zaidi ya kumuogopa binadamu mwenzako kwani yeye muda, mahala popote, na vyovyote iwavyo anakuona, au atajua madhambi yako, au… kwasababu yeye anakujua zaidi ya hawo unaowaogopa, anakuona wakati wote na akitaka jambo lake liwe yeye ``husema tu, kuwa na linakuwa’’.Huyu ndiye wa kuogopwa ukweli wa kuogopwa, na kama tungekuwa tunamuogopa huyu, kiukweli kama tunavyodai kuwa tunamcha yeye, haki, usalama, amani na upendo vingejaa dunia hii…lakini wapiiiiiiiii’ akainuka kama anataka kuondoka, halafuu akakaa.

‘Kisa ninachotaka kukuhadithia, kimenikuta mimi mwenyewe, na mateso niliyopata, makashikashi, yamenifikisha mahala ambapo natakiwa kuamua mara moja, vinginevyo, nitaumiza familia yangu. Isingekuwa familia yangu, aah, ningekaza buti nipambane kiume, lakini mmmmh, hapa nataka subira na uamuzii wa hali ya juu.

Kwani ndugu yangu, hizi sasa ni imani za kishirikina, lakini huwezii kusema jambo mpaka likukute. Wahenga wanasema `aisifuye mvua imemnyeshea..’ mimi kama dakitari mvua imeninyeshea na kisa hiki sio nahadithiwa na mtu, kimenikuta na …na…sidhani kama utafiti wangu utakamilika mapema kabla ya uamuzi nitakaochukua. Lakini dhamira yangu ni kuwa , ambayo imenivuta sasa nikusoma mambo haya kiundani, kwenye vitabu na kupitia watu waliokumbwa na majanga haya ili baadaye niweze kuwasaidia watu wnaoteseka na mambo kama haya. Yamenikuta, na nisingependa wengine wayakute na yaendelee kuachwa hivihivi…hapana, lazima mtu afanye kitu…’ akakuna kichwa akiwaza saana.

‘Wapo binadamu wengine hapa duniani wanajifanya wao ni miungu watu. Wanatesa wenzao, hawataki maendeleo ya wenzao, sijui kwasababu ya ujinga, sijiu kwasababu ya umasikini, sijui…kabisa, lakini dhana hii ya ushirikina, imenigusa mimi, na nina elimu yangu nzuri, sio mjinga, nina pesa za kunitosha mimi na familia yangu, sio masikini, na nina akilii yangu timamu sio mgonjwa. Na imani yangu ya dini sio haba, Sasa je tuya-amini haya…’ akafungua lap top yake, nafikiri kutaka kuanza kunihadithia kisa hiki kinachokuja ambacho tutakiita `AISIFUYE MVUA IMEMNYEA..’

Ndugu wapendwa, nimekuwa nikikutana na visa vingii vyenye dhana ya imani ya `uchawi’ na ajenda ya ushirikina. Na wengi wakikuhadithia unaweza ukasema, `hivi kweli mambo haya yapo, na mwisho wa siku ukasema, `mimi siamini’ mimi namwogopa mungu, mimi nina imani yangu, siwezi kuamini hayo na hayawezi kunidhuru. Sasa leo nimekutana na dakitari, bingwa, ana pesa zake hana shida ya kusema labda akili imetatika. Ametoka kwenye imani iliyojengeka kidini, na bahati nzurii kazisoma, sio kwa mapokeo ya kuhubiriwa tu, bali kaingia ndani ya vitabu, na mkibishana naye kuhusu imani za dini anakutolea maandik0 na tafsiri inayoheshimika.

Leo dakitari huyu ananipa kisa kilichompata na hatima yake anataka kuchukua uamuzi ambao sikuamini kuwa mtu kama yeye angefikia kudhamiria kuchukua uamuzi huo. Naomba tusicheze mbali, wakati tunamalizia kisa chetu cha `asiye na bahati habahatishi’ tujiweke tayari kusikia kisa hiki, na ningekuomba usikisome usiku peke yako…

Lakinii usiogope…!

karibu sana!

Ni mimi: emu-three

6 comments :

Jane said...

Mmmmh! Bora yangu sina access nyumbani kwangu so kusoma nasoma mchana tu. Itakuwa babu kubwa kweli hadi pale Doctor anapowaza kujitoa uhai kwa mambo ya kishirikina kweli balaa. Tunasubiri kisa chenye, japo ningependa kujua mwisho wa yule dada msahaurifu itakuwaje??. Kazi njema M3 tuko pamoja daima.

elisa said...

mmh siwezi kusubiri hiyo inayofuatia..mambo ya kichawi/kishirikina nayaogopa sana, hata kuyakusoma tu...japo najua yapo.
haya sisi tupo tayari.

emu-three said...

Mhhh, naona wengine mshaanza kuogopa! Sasa wewe unaogopa kwa kusimuliwa, je yule yaliyomkuta? Hebu fikiria unaambiwa kuna mchawi kageuka paka, na umelala kitandani, ghafla unshitukia paka yupo ndanii ya shuka ulilolalia utafanyaje?
Oh, usiogope, wewe shikamana na ibada kama kweli unamwamini mungu, kama kweli...tatizo hapo ni `imani haba' kama kweli una imani, na imani haidanganyi, utatudanganya sisi tunaokuona, lakini Je huyo siyedanganyika utamdanganya!
Tusuvute subira kidgo tuweke mambo sawa!
Mkao wa kula jamani!

Joe said...

Mdada uko juu sana, jipange utengeneze kitabu cha visa/mikasa/matukio kama bado haujatengeneza. Nlikuwa nakusomaga kwa Dinahicious nikaja kuibamba na hii bog yako, makala ndeeeeeeeefu lakini bado nakodolea tuu macho mpaka namaliza. Ur writing skill is excellent, big-up urself!

sami said...

mimi siogopi kwani yashanikuta mengi nimeteseka miaka na naendelea kuteseka nasubiri niyamalize nikutafute usimulie watu
yaani acha tu

emuthree said...

Joe naona tumetoka mbali pamoja, kweli kule ndipo nilipoingiwa na hamasa ya kuanzisha hii blog, na nimefurahi kuwa ulikuwa ukisoma yale ninayoandika. Ahsante sana na nitafuta ushauri wako.
Tuwepo pamoja hapa pia.
Sami, ningefurahi sana kusikia kisa chako, we kiandike kwa kutumia e-mail ya hii blog; miram3.com@gmail.com. Hata kama ni kwa kifupi, kazi nyingine niachie mimi. Mara nyingi watu hunipa visa vyao kwa kufupi sana, mimi ninachofanya ni-kudadavua kwa undani zaidi, kama ingelikuwa hivi, ingekuwaje, na ili uweze hilo, unatakiwa ujiweke kama ndio wewe ....hiyo nii moja ya siri ya kutunga kisa/hadithi/tamithilia!