Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Thursday, November 25, 2010

Asiye na bahati habahatishi-8

 Kwa kipindi hicho Yule mzee alishapata nafuu akainua kichwa kuangalia nini kinaendelea, kwani licha ya ushauri kuwa apelekwe mjini kwa matibabu na mapumziko yeye hakukubali. na mara akawaona hawa akina dada wakitaka kukaribiana na mapango mikononi, alimuona ni binti yake na msichana mwingine, kwasababu ya kizunguzungu alikuwa akiwaona kwa shida na bahati nzuri akaweza kuiona sura ya yue binti mwingine…Loooh, kila akijaribu kuinua mboni za macho zinakuwa nzito, mmmh, ina maana ndio nakufa nini akawaza, huku akijaribu kwa nguvu zote kujiinua, na giza likatanda usoni …!


                       ****************** Sasa endelea **************

Mkuu wa ukoo na kabila lile akawa kafanikiwa kuwatuliza vijana wake, akishirkiana na wazee wengine na wakakubali kusitisha mapigano, kwani hawakuwa na uwezo wa kupambana na dola, kwa masharti kuwa viongozi wa hao vijana hawatachukuliwa hatua yoyote kwani wao walikuwa wakilinda mila na desturi zao. Ombi hilo likakubaliwa kwa muda, kwa msharti kuwa uchunguzi huru uwepo ili kubaini kuwa kweli kuna utekaji na ubakaji unaofanywa na vijana hao ili kutokutokea madhara mengine baadaye, na wapo lazima sheria ichukue mkondo wake.

‘Katika taratibu na mila zetu hairuhusiwi kubaka, kama wapo wanafanya hivyo, ni vijana makaidi, na zipo taratibu za kuwafunza adabu, kwa kulipa faini na kumuoa binti aliyemfanyia kitendo hicho, na adhabu nyingine, lakini kama wamekubaliana sisi hatuna mamlaka ya kuwapinga na kuingilia upendo wao, na kawaida alzima wazee waitwe kuwafungisha ndoa…’ akawa mzee Yule akielezea mila na desturi zao, na alipinga kabisa maelezo mengi kama ya watu kula nyama za watu, akasema na wao wanasikia hizo hadithi kuwa walikuwepo, lakini ni zamani sana.

Askari wa serikali wakahakikisha kuwa hakuna madhara mengine na kuwakusanya vijana wote waliosadikiwa kuhusika na silaha mbali mbali za kiienyeji zilikusanywa na kuteketezwa licha ya wazee kudai kuwa ni silaha za kulindia usalama wao, na zinahitaika sana. Vijana wengi walikuwa majeruhi na walihitaji misaada ya kitibabu. Magari ya wagonjwa yakaletwa na majeruhi wote wakapelekwa hospitalini.

Yule Mzee mjomba wa Tausi alizindukana akiwa hospitalinii baada ya kuongezwa damu, na alipofumbua macho cha kwanza kuulizia ni binti yak yupo wapi. Binti yake muda ule alitoka kidogo, ikabidi aitwe na akaja kuongea na baba yake. Alifurahi sana kumuona baba yake anaendelea vyema.

‘Yule binti mliyekuwa mkigombana naye yupo wapi?’ akauliza baba yake.

‘Sijui , kwani walivyotuamulia tu, Yule dada akaondoak zake…sijui atakuwa wapi…aah, nasikia wengii wameshikiliwa na polisi mpaka maamuzi yafikiwe…’ akasema bintii yake.

Baba yake akaomba mkuu wa polisi aitwe na alipokuja akaongea naye kwa muda, halafu Yule mkuu wa polisi akaondoka na kuwaacha binti na baba yake. Baba mtu alikuwa ndani ya mawazo mazito, alikuwa akiwaza kitu Fulani kwa undani sana, lakini hakutaka mawazo yake yajulikane kwanza kwa binti yake. Alitaka ahakikishe kwanza kuwa anachokifikiria ni kweli au ni dhana tu.

‘Hebu nieleze binti yangu, unamipango gani baada ya tukio hili, maana mimi naona ukasome tu, kwani sidhani kama mchumba wako watakuwa badoo anakusubiri, labda atakuwa keshaoa mtu mungine, au unasemaje?’ akauliza baba mtu ili kupitisha muda

‘Sawa baab, mimi kwangu haina kikwazo, hata hivyo nimejifunza mengi, hasa kutokana na tukio hili, nahisi nilikimbilia kuolewa mapema sana, bado akili yangu haijajiweka sawa kuwa mke wa mtu. Nikipata nafasi hiyo ya kusoma nitashukuru sana…Akasema na kabla hajaendelea mlango ukagongwa na baadaye akaingia Yule mkuu wa polisi akiwa kaandamana na binti amabye bado alikuwa kavaa nguo za ngozi ya wanyama, na huko nje kila alipopita ilikuwa kivutio cha aina yake.

‘Mkuu huyu binti ndiye huyu hapa, anasema jina lake ni…’ akamgeukia Yule binti ili amalizie mwenyewe. Lakini Yule binti akawa anamwangalia Yule mzee kwa makini akiwa kama anajaribu kukumbuka kitu, huku machozi yakimlengalenga! Na Yule binti mwingine, Maua akawa naye anamtizama mwenzake kwa macho ya udadisi sana, alivutiwa sana na yale mavazi na kichwani mwake akawa anafikiria kuwa mbunifu wa mavazi na vazi mojawapo litakuwa la namna hiyo. Hakuwa akijali mengine, hakuwa akiwaza kwanini Yule binti alikuwa akimwangalia baba yake kiasi hicho!

‘Tausi ndio wewe, umebadilika sana, oooh, au sababuu ya hayo mavazi …’ akasema Mjomba mtu.

‘Mhh, nime…oh, unajua kichwa change sijui kina nini, ninakuwa sikumbuki sana, lakini wewe ni mjomba wangu…’akasema na kumsogelea pale kitaandani. Ile hali ya kusogea pale kitandani ulimfanya Maua ainuke na kutaka kumzua, akidhaniia kuwa Yule dada analengo baya, lakinii alishangaa kuwaona polisi wakiwa hawafanyi lolote!

`Maua mwanangu huyu ni binamu yako, umemsahau kwasababu ya hayo mavazi mwangalie vizuri, umemsahau Tausi…’ akasema baba mtu

‘Tausi…oh, kweli baba, ndiyo yeye, yaani wewe ni Tausi , mmmh, hizo nguo zimekubadili kweli, na hizo nywele kakusuka nani kama mmasai,…mungu wangu … wasingetuwahi wale askari,itungeuana siku ile, kwasaababu ya hawa wajinga…’ akasema kwa hasira na kumwendea mwenzake akiwa na nia ya kumkumbatia, lakinii alipomsogelea akasita, kwani mwenzake alikuwa akionekana ana mawazo mengi sana, na hakuonyesha dalili ya furaha.

Kipindi cha vita, uhasama kikaisha, Tausi na Maua wakachukuliwa kwenda kuishi mjini na nia ya mjomba wa Tausi ni kuwasomesha wale mabinti na hata kuwaendeleza, lakini taarifa aliyoipata kuwa Tausi ni mja mzito ikamshitua kidogo.

‘Tausi una mimba, ni ujauzito wa nani?’ akauliza mjomba mtu kwa huzuni kidogo!

Tausi alikaa kimya akiwaza mengi kichwani mwake na hata huo wasiwasi wa mimba hakuwa nao tena, alikuwa keshejua kuwa anayo hiyo mimba na kwa uhakika alipewa na mume wa msituni, na kapewa kwa kubakwa, licha ya kuwa wao walisema wamemuozesha. Akawaza mengi, kwanza matukio yaliyompata yalikuwa yakimwandama kichwani, kiasi kwamba alikuwa akihangaika sana hasa usiku kwenye njozi. Baadaye alipelekwa hospitali akaonekana pamoja na mimba ana malaria mengi sana.

Tausi akajiinamia na kujikuta machozi yakimiminika, alijiona mtu asiye na bahati katika maisha yake, akalalamika kimoyomoyo, kuwa kwanini yeye aandamwe na matatizo hayo, amekosa nini… akalia kwa kwikwi …

‘Ukilia itasaidia nini Tausi cha muhimu ni kwetu sisi ni kujua mwenye mimba ili tuweze kujua hatua gani tuchukue, ukilia ndio tuseme tunakuonea au …’ akasema shangazi yake huku kamkazia macho.

‘Mimi …aliyenipa najua ni Yule mume wa porini, kama nilivyowaambia kuwa ali..ali…’ akawa hamalizii kwani ile taswira ya kule msituni ilikuwa ikimkera, ingawaje mwishoni alimsamahe na akazoeana naye kutokana na Huruma zake, lakini kile kitendo cha mwanzoni kilimuumiza sana, na hakupenda kimjie akilini mwake,lakini cha ajabu kila mara kinamkera na wakati mwingine anaota yale maumivu yanavyounguza ….

‘Mume wa porini, na unadiriki kumuita mume wa porini, ina maana akiletwa hapa upo tayari kumuiita mume wangu, au una maana gani kusema mume wa porini...’ akafoka shangazi yake.

‘Hebu usimsakame sana kwa hilo, kwani mazingira yenyewe yalivyokuwa huwezi kumlaumu, kwani huko alitekwa, huko wanabaka, huko tunasikia ni wauaji, kwahiyo hilo limeshatokea labda tujue nini cha kufanya baada ya hili..’ akasema mjomba mtu.

‘Tatizo lako unapenda sana kuwadekeza mabinti, mimi hiyo kwangu haipo, kwani kama ni aibu, mimi ndiye ninayeingia aibu. Wakimuona watamnyoshea kidole kuwa ni Malaya, na lawama nitatupiwa mimi kuwa sikuweza kuwalea vyema…hapana, lazima kwanza aletwe huyo jamaa hapa akiri na awajibike..’ akasema shangazi akiwa katoa macho ya hasira.

‘Wewe wasema tu kwasababu hujui nini kilichokuwa kikiendelea huko, sina uhakikika kama jamaa huyo yupo hai, kwani alipoteza damu nyingi sana, na utashangaa wakiwa hospitali kwenye matibabu akatoroshwa na watu wake, na kwa vile mambo hayo yalishapangwa yamalizwe kienyeji, hakuna aliyejali kufuatilia. Lamuhimu kwanza aanze dozi ya malaria, kwani malaria aliyo nayo ni nyingi sana, na sijui dawa alizoandikiwa…mmmh, chloraquin, mmmh dawa hizo mimi sizipendi zinawasha sana, lakini kwa vile kasema hazimsumbui akaanze dozi. Hakikisha unameza na panadol, sawa Tausi, mengine tuta’ akasema mjombe huku akitoke kwenda kwenye shughuli zake.zungumza baadaye, usiwe na wasiwasi…’

Tausi akabakia na shangazi yake ambaye aliendelea kumsakama kuwa kafanya makosa kujirahisisha sana,

‘Mimi katika ujana wangu nilipambana na midume mitano iliyotaka kunibaka, nilihakikisha kuwa hawafanikiwi, kila aliyejaribu kunisogelea nilimpiga teke sehemu zake za siri, na ukimpatia teke zuri mwanaume sehemu hizo lazima atainama kwa maumivu, nawe unapata nafasi ya kukimbia. Sawa, labda hiyo mijamaa ilikuwa na nguvu sana, lakini ulitakiwa kuwaarifu polisi mapema, ili Yule mhusika awekwe kwenye orodha ya wakosaji, kwanini hukutoa taarifa mapema, sheria ikachukua mkondo wake, ina maana uliridhika na hicho kitendo ulichotendewa, sasa unaona matunda yake, mwenzako yupo wapi, kakuachia mzigo, mwisho wa siku anakuja kudai mtoto wake……’ akakatishwa na mlio wa simu.

Aliipokea ile simu huku akitababsamu kwani aliyepiga alionekana mtu muhimu sana kwake.

‘Ndio tupo na mdogo wako hapa, aah hajambo, lakini ndio katutia aibu kweli kwenye familia yetu, yaani yeye , mara akatae ndoa, mara sasa kapachikwa mimba…simjui bwana mwenyewe, anasema eti ni hawo watu wa msituni. Hata kama angekuja kudai kumuoa nani angekubali, lakini angewajibika gharama. Mnasema mpo …oooh, karibuni sana, tutakuja uwanja wa ndege kuwapokea..’ akampa Tausi simu kuwa dada yake anataka kuongea na yeye.

Tausi alisita kidogo kuipokea,akikumbuka kuwa huyo ndiye aliyemchukua aliyetakiwa kuwa mume wake na alivyosikia ni kuwa wanarudi karibuni, na wakija anajua ni kusakamwa kuwa yeye aligoma ndoa, na sasa kapachikwa mimba, eti hajui kujilinda…akaichukua ile simu kwa shingo upande na kumsikiliza dada yake.

‘Pole sana mdogo wangu, usijali nikija tutafanya mpango uje tukaishi wote huku, na….shemeji yako anakusalimia sana…’ maneno aliyokuwa akiambiwa hayakuwa yakimwingia akilini, kwani alikuwa mbali sana, akijaribu kumkumbuka huyo shemeji yake kuwa alikuwa na sura gani. Huyo ndiye alitakiwa kuwa mume wake matarajiwa, sasa bahati yake imechukuliwa na mtu mwingine tena dada yake, halafu… akazima ile simu na kuingia chumbani kwake.

‘Tausi anza kunywa dawa zako za malaria, najua ni chungu unaweza usizinywe ulivyo na kichwa kibovu, halafu udai umesahau..’ akasema shangazi yake.

Tausi alipofika chumbani kwake akachukua vidonge vine alivyoambiwa akavimeza kwa hasira, huku akisema `vichungu, nina machungu zaidi ya haya’ akatulia kimya akiwa kakunja uso kwa uchungu wa ile dawa. Ikapita nusu saa, akashikwa na usingizi, na mara akisikia sauti ya shangazi yake akiita, kuulizia kuwa keshameza hizo dawa, akazindukana toka kwenye usingizi akionyesha kushituka sana kutokana na ndoto mbaya, akafikiria, na kujiuliza hivi nimeshameza hizo dawa, akasema bado ngoja nimeze manake nitaishia kubarazwa, akachukua dawa vidonge vine, akaviweka mkononi, akasema, `vidonge vine…’ akameza na kujisikilizia.

‘Tausi umeze dawa na ukumbuke kumeza na panadol’ akasikia shangazi yake akisisitizia.

‘Panadol…nimeze na panadol ehe, haya, ‘ akanyosha mkono kwenye meza na kuchukua ile pakti iliyowekwa dawa, bila kuangalia zile dawa akameza vidonge vingine viine, hakukumbuka kuwa alitakiwa ameze vidonge viwili yeye akajua zote ni nne- nne, na kwenye karatsi vilibakia vidonge vichache akavimeza vinne…uchungu ukazidi kiasi! Mbona panadol inawasha kama chloraquin..akajiuliza, na huku anajisikia vibaya.

‘Tausi umeshameza na panadol…’ akasikia shangazi yake akiulizia

‘Ndio lakini…mmh, sijisikii vizuri’ akasema kwa shida.

‘Meza panadol, utajisikia vizuri.’ Akasema shangazi mtu.

Tausi akasikia tumbo linacheza cheza, kichefuchefu si kichefuchefu…, huku kichwani anasikia vitu vikisema `meza panadol, hujameza panadol…’ akachukua karatasi na kumeza vidonge vingine viwili. Akasema mbona panadol inawasha kama…’ akasoma nyuma ya ile karatasi…Mungu wangu, ina maana, oh, mungu wangu…macho yakawa mazito, hali ikawa sio hali akajaribu kutembea kuelekea mlangoni, akakumbuka kuwa alijifungia kwa ndani, ufunguo upo, hauonekani, hakumbuki aliuweka wapi…alijaribu kuita, sauti haitoki…akainuka pale alipokaa, akadondoka, akainuka , akadondoka…!

Mwisho

Ni mimi: emu-three

9 comments :

Jane said...

Jamani mbona kama haijaisha vizuri??? nahisi kama nimebaki pending??? Pole sana Tausi, Shangazi nae nahisi kachangia Tausi kujiover dose. Msisitizo aliyokuwa anautoa mara kwa mara na ukawa unajirudia kichwani mwake ndo uliyomfanya aongeze kumeza dawa. Ok ngoja tujiandae kusoma hiki kisa kipya.

Koero Mkundi said...

NI kariwaya katamu jamani.....

chib said...

Hii blogu naona sio diary ya emuthree peke yake....

emuthree said...

``Hii blogu naona sio diary ya emuthree peke yake....'' yah, ni kweli ni yanguu mimi na wewe na wengineo, tuwepo pamoja, lete kumbukumbu zako ulizokutana nazo, visa, mikasa tuzisome pamoja!
Hii ni diary ya wote, kusema `kusema diary ya emu-three peke yake ni makosa!
Ahsante sana na karibuni tuwe pamoja!

Pamela said...

nini kilitokea jamani ni kama umeniacha njia panda! vp alipata msaada wa ugonjwa wa kusahau je alienda ulaya kwa 'mume'?? mimba ilipona kweli na miklorokwini yote aliyokunywa?
Kwa Tausi pole sana mamii ila shangazi ni wakilisho la cc wanajamii kwani hupenda kuhukumu bila kujua chanzo au sababu ya mtu kutenda atendayo.

emuthree said...

Pamela, hujaachwa njia panda. ili ukielewe vyeme hiki kisa, ukifika mwisho, anza tena mwanzo. ni kama duara vile.

Anonymous said...

Mmmm!! M3 hongera sana mzee.
SALUTI.
Sina zaidi.

Ni kweli huyu shangazi amechangia sana Tausi kujiova dozi.

Masikin Tausi pole sana. Mungu yupo nawe. Usikate tamaa, utafika tu.

BN

Faith S Hilary said...

ahaaa!!! kwahiyo ile mimba iliharibika kutokana na hivyo vidonge...anzeni mwanzo wapendwa, mtaielewa vizuri tu...ila M3 hii inaweza kuwa part 2 maana kama maisha ya Tausi yangeendelea basi labda kuwe na kisa kingine labda akienda huko alipo shemeji yake ambaye alitakiwa kuwa mumewe...just an idea!...But I loved this!!!

emuthree said...

Hilo ni wazo zuri sana mpndwa Candy, mmmh, labda tukitunga kitabu tutaweza kuweka pati nyingine na zaidi ya hiyo, kweli hata mimi najiuliza maswali mengi zaidi ya hayo, lakini wakati mwingine unaogopa kuweka chumvi zaidi ya kisa kilivyokuja. Ila tukitunga kitabu, mmmh,...tuombe mungu, na naomba mawazo yenu, na najua wewe uko kwenye media, unaweza ukawa masaada mkubwa kwa haya!
Nashukuruu sana mpendwa, tuwa pamoa daima!