Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Friday, November 26, 2010

mvumilivu hula mbivu


Nillitwa ofisi ya masijala na kwa mshangao nikakutana na bosi wa idara ndani ya ofisi hiyo, nikashangaa, kwanini hajaniita ofisini kwake, kama ni maswala ya kikazi. Labda kuna jambo jingine, sio la kikazi nikjipa matumaini.

‘Sikia ndugu, kazi ni muhimu sana, wote tumekuja hapa kutafauta riziki zetu, na riziki hii haiji hivihivi, unatakiwa uchape kazi iliuweze kupata haki yako. Nimeshangaa sana, kila nikiulizia kazi zako naambiwa hujafanya, nikiulizia utendaji wako naambiwa haurizishi, sasa jamani mnataka nini…kunilaumu nikitimiza wajibu wangu?’ akaniangalia kwa jicho la Huruma

Nilibaki nimeduwaa, kwani ilikuwa kama mtu aliyekutana na baba mkwe, baada ya salamu tu, anakuchapa kibao cha usoni! Utabakia umeduwaa, ushindwe kujitetea…na ndivyo ilivyotokea kwangu, kwani maneno yale yalikuwa kama kuzwaba kibao na baba mkwe, bila kujua kosa lako.

‘Sikiliza bwana mdogo, umebakia mwezi mmoja tu, kipindi cha majaribio kuisha, jitahidi sana uweze kunishawishi kuwa kweli unaweza kazi, vinginevyo, mimi sitaweza kuharibu kitumbua changu, kwa kukubeba wewe. Hapa sote ni waajiriwa na utendaji wangu wa kazi utaonekana vyema kama nyie mliopo chini yangu mtafanya kazi yenu vizuri, na mkivurunda, mimi nawajibishwa, na hilo sitakubaliana nalo kabisa, ni bora lawama, kuliko fedhaha…’ akainuka kwenye kiti na kuondoka.

Niligeuka kumwangalia katibu muhtasi wa meneja utawala, ambaye naye alishikwa na butwaa, kwani ananijua vyema, anaujua utendaji wangu wa kazi ulivyo, na alishawahi kunisifia kuwa katika kundi letu tulioajiriwa pamoja, mimi naonekana kuchapakazi zaidi ya wenzangu! Leo hii anasikia tofauti, ilibidi hata yeye agune, na baadaye akasema

‘Usijali, huenda anazungumza kinyume chake, wewe chapakazi tu, …’ maneno yake yalikuwa kama wimbo ndani ya gari lenye mngurumo mkubwa, huwezi kujua nini kinachoongelewa zaidi ya kujua kuwa nii wimbo unaoimbwa!

Nilitoka mle masijala hadi ofisinii kwangu, na kuwakuta wenzangu wamekaa kwenye kikundi, na nilipoingia wakatawanyika na kila mara nilipowaangalia niliwakuta wakinitupia jicho la `kinafiki’. Nikajua kuna jambo linaloondelea mle ofisini ambalo mimi silijui. Mimi kawaida yangu sihangaiki na maneno maneno, huwa nikifika ofisini nachangamkia kazi yangu, na nahakikisha majukumu yote nayamaliza kwanza, na kuwakilisha kwa bosi ambaye yupo juu yangu, huyo bosi naye hupeleka kwa bosii mkuu wa idara ambaye ndiye aliyeniita leo na kunipa maneno ya kunivunja nguvu. Sikujali nikasema , hivyo ndivyo vikwazo katika mbio za nyika.

Mwezi ukapita, mwezi wa hukumu, na kabla haujaishia wenzangu watatu tulioajiriwa nao wakapata barua zao za uthibitisho, kuwa sasa  wao ni wafanyakazi halali na wanahaki kama wafanyakazi wengine! Wakapongezana, na kujisifia kuwa wao nii wachapakazi wa kweli, huku wakiniangalia kwa jicho la kunidharau, nafikiri walikuwa wakisema kimoyomoyo, `ipo wapi sasa',  wewe wajifanya kujituma, unajipendekeza, kama walivyozoea kusema, kuwa nahangaika kuchapa kazii ili nijipendeekeze kwa wakubwa!
Nilifikiria sana, nimekosea wapi, kwani sio siri, kila kitu nilikuwa nikifanya kama kinavyotakiwa, kazi naimaliza bila matatizo, na nawakilisha kwa huyo bosi aliyejuu yangu, na ninapompa haniambii kuwa ina matatizo, anaichukua pamoja na za wenzangu anaipeleka mbele, kwa ajili ya taarifa za kimahesabu, sasa kuna nini , kuna kosa gani…nikasema ngoja nikamuulize bosi wangu wa karibu.

‘Mimi siju, wewe ndiye nikuulize una matatizo gani, manake hueleweki, kazi huwezi kwa ujumla, ni bora uka…ukauze karanga mitaani…’ akasema maneno ambayo yaliniuma kupita kiasi, nikasikia wenzangu wakicheka kwa kauli ile.

Niliinama kwenye kiti changu nakumalizia kazi yangu halafu nikampelekea jamaa yetu huyu, akaniangalia kwa dharau halafu akaifutika ndani ya droo zake. Nikashangaa, mbona za wenzangu kaziweka kwenye faili lake, lakini yangu kaifutika kwenye droo zake, mwanzoni nilijua ndio mpangilio wake wa kwazi, labda baadaye anakuja kuzihakiki ndipo azipeleke. Nikasubiri, alipoondoka nikafungua droo yake na kuzikuta kazi zangu zote zimo mle, nikazichukua na kuelekea kwa meneja, bosii wa idara, nikajaribu kumwelezea na kumuonyesha zile kazi zangu, lakini nilimuona hana bashasha na mimi kama ilivyokuwa awali, nafikiri bosi wangu wa chini alishanisemea mengi ambayo hakuyapenda.

‘Bwana mdogo, nilikuwambia mwezi huu uliokuwa umebakia ni sehemu ya kujirekebisha, lakini sikuona matokea mazuri. Huyu bosi wenu nimekaa naye miaka mingi,anaijua kazi yake vyema,hawezi akakuchongea uwongo, ili iweje…namheshimu sana Yule jamaa, yeye ndiye hii kampuni, katokea nayo mbali, mimi mwenyewe ndiye aliyenifundisha kazi nilipofika hapa mara ya kwanza, sasa iweje abadilike na kukuona wewe peke yako mbaya, mimi nahisi una kasoro…jichunguze mwenyewe…Lakini sawa, siwezi jua, labda mwenzetu una mipangilio yako mingine, jitahidi sana kweny mipango yako hiyo, kwani sijui nitakusaidiaje. ..’ akasema na kukatisha maneno wakati bosi wangu wa `section’ alipoingia na kuleta mafaili yaliyojaa kazi za wenzangu, alipoliweka pale chini, nikaichomoa kazi yangu na kuiweka juu ya lile faili halafu nikatoka!

‘Niliona wanazozana kwa muda huku bosi wa idara akimuonyeshea kazi zangu, lakini Yule jamaa alikuwa kifoka, kulalamika kitu fulani, baadaye akatoka mle ofisini akiwa amekasirika. Alifika mbele ya meza yanguu akaniangalia kwa jicho baya, halafu akachukua fungua ya gari lake na kuondoka!

Baadaye mchana tuliporudi kutoka kupata chochote nikakuta barua mezani kwangu, nilijua nini kimeandikwa, na kweli maneno haya yalianzia kuwa `samani, kutokana na utendaji wako usiorizisha, tumeona kuwa tukusimamishe na kwa mujibu wa mkataba wa majaribio, unatakiwa….’ Nikaifunga na kuchukua kile kicho changu , nakuishia nje.

Nilipofika nje nikakaa kwenye `benchi' lililopo hapo nje, na kulikuwa na kimeza cha wageni, mara nyingi hatukai hapo kama wafanyakazi wa humo, ni maalumu kwa wateja. Na nikiwa nimezingwa na mawazo, akaja dada mmoja, yeye namfahamu ni mhasibu toka kampuni moja kubwa ambayo ni mteja mkubwa wa kampuni yetu. Alinisalimia na kwa vile ananijua akaniomba nimsaidia kufuatilia malipo yake.

‘Oh, samhani mimi sitaweza kufanya hivyo, unajua tena utaratibu wa kampuni, mkataba ukiisha huwezi tena kufanya kazi kama hiyo, mkataba wangu umeisha na …’ nikajikuta natoa machozi.

Yule binti akaniacha na kuingia ndani na baadaye akatoka haraka na kuniwahi kabla sijakatisha barabara kuelekea kituoni.

‘Kaka samahani, nimesikia taarifa zako, nimesikitika sana, kwani wewe ndiye mchapakazi mzuri, kuliko hawo wote walioachwa humo ofisini, lakini najua hali halisi za makampuni yetu, Na bahati nzuri, kampuni yetu inahitaji mhasibu kama wewe, naomba twende sasa hivi ukaonanae na bosii wangu. Sikuamini, nilimwangalia Yule dada kama malaika aliyeteremshwa toka mbinguni kuniokoa, kwani dhamira yangu ilikuwa inanipeleka pabaya, nikikumbuka familia yangu ambayo inanitegemea, wazazi wangu ambao hawana mbele wala nyuma, ndugu …yaani nilijua sasa mimi sina changu katika dunia hii.

Nilimshukuru sana mungu, kwani sasa nipo kwenye kampuni nzuri, mshahara mzuri, na hapa nijiandaa kwenda nje kwa ajili ya kusoma zaidi…mungu anipe nini, namshukuru sana, kwani naukubali usemi usemao, `mvumilivuu hula mbivu…’ haya ni maneno yake nilipokutana naye kwa mara ya mwisho.

Huyu alikuwa rafiki yangu ambaye kwa hivii sasa yupo nje anapata `ya zaidi’ na nasikia `ni mtaalamu wa kubeba maboksi ile mbaya’ namtakia kila-laheri, kwani anawakilisha wale wote wanaodhulumiwa maofisni, sio kwasababu ya ubaya, bali sababu ya `wivu’ kuonenana donge, husuda ambayo hailipi, kwani alipoondoka kwenye ile kampuni, lilizuka balaa la wizi na idara nzima ikafukuzwa. Hutoamini bosi wake Yule wa karibu anapiga lapa huku na kule, na sasa anauza karanga mitaani…mungu ni wa jabu kabisa. Na usomi wake wote ule…alishindwa kutumia taaluma yake vyema, akajiingiza kwenye majungu!
 Mnapokutana na vikwazo kama hivi, msivunjike moyo, vumilieni kwani mlango mmoja wa riziki ukifungwa mwingine hufunguka, cha muhimu ni kutimiza wajibu wako, na ukifuata taaluma yako vyema!

Ni mimi: emu-three
Enhanced by Zemanta

9 comments :

Jane said...

M3 umegusa sehemu ya maisha yangu yaani ni kama uliyaona, Nimetoka machozi nilipokuwa nikisoma hiki kisa. Ukweli yaliwahi kunitokea hayo yote uliyoyasema hapa, yaani Admin wetu alikuwa akinichekea tukiongea vizuri nikadhani ni mfanyakazi mwenzangu ambae tunaelewana kumbe nikitoka nasemwa vibaya kweli mbele ya staff wenzangu hadi kwa Boss, Nilikuwa nafanya kazi hadi jumapili siku nyingine napigiwa cm hadi sikukuu na nilikuwa siulizi kwa nini naenda kwa moyo mweupe kwa sababu nilijua hiyo kazi ndo kila kitu kwangu na ndo inayonifanya nithaminiwe na kujikimu. Yaliponishinda nikaamua mwenyewe kubaga manyanga baada ya kupata kazi mkoani, cha ajabu sasa aliyekuwa akipika majua mpaka ninapoandika hivi hayupo tena kazini baada ya kupewa barua ya kusimamishwa kazi kutokana na utendaji wake wa kazi. Nashukru mungu kwa ninachokipata kwa sasa maana ni mara 3 ya nilichokuwa nikipata mwanzo, jamani tuache kuchongeana tuwapo kwenye sehem za kazi maana tupo pale kwa ajiri ya kutafuta riziki sasa ya nini kuingiliana???? sorry kwa kuleta story ndani ya story.

emuthree said...

Jane pole sana na nashukuru kuwa umethibitisha ukweli wa visa tunavyotoa, na hii ndiyo tunayotaka, kuwa kama imekugusa na kwa namna moja ulipata janga kama hilo, tuelezee ili kuongezea makusudio mema ya diary yenu.
Usiogope kabisa kuleta kisa ndaniya kisa, ndivyo `twataka'
karibuni sana!

elisa said...

mmh pole Jane kweli ,kweli nimesoma hii ..nimesikitika sana , japo mimi sijawahi kutokewa na kitu kama hicho .Ila sijui binadamu wengine huwa tunakuaje na kufanyiana mabaya sehemu ya kazi tunasahau kuwa dunia ni duara, pale unapoanzia , ndipo unapoishia .

Anonymous said...

Hayo ndio maisha ya watu kujiona wamesoma, kumbe hawajasoma. Unaweza ukawa na digrii au ukawa profesa, lakini ukawa huna lolote katika kutafakari, hasa katika nyanja ya hekima!
Popote unapokuwa, lolote unalofanya, jaribu sana kufikiri `kama ningefanyiwa mimi ' ningefurahi...je maumivu gani ningeyapata kama ningefanyiwa mimi...
Hapa ubinfsi unaingia, kujifikiria wenyewe.
Haya yana mwisho , kama ni ajira usitegemee kuwa wewe utaajiriwa milele, unapomfanyia mwenzako leo jua kesho na wewe utalipwa vivo, hivyo.
Kisa hiki ni kizuri, umelenga mahala pake M3.
M3, mimi nauliza swali binafsi, kuhusu wewe, ni mwanamke au ni mwanaume..samahani sana kwa swali hili, kwani sote twatumia nembo ya `anyn' lakini tukijua ni bora kwetu, kuliko kukisia na huenda mtu akakuita kaka au dada kumbe sivyo!
Ahsante sana kwa visa vyako, nami naungana na wengine kuwa ni bora utunge kitabu, au anzisha jarida
Ni hayo tu mpendwa wetu

Yasinta Ngonyani said...

nanukuu "Mnapokutana na vikwazo kama hivi, msivunjike moyo, vumilieni kwani mlango mmoja wa riziki ukifungwa mwingine hufunguka, cha muhimu ni kutimiza wajibu wako, na ukifuata taaluma yako vyema! nimeupenda msemo huu. Kwa kweli maisha ni maisha, ni kujifunza kweli.

Anonymous said...

Haya ya maswala ya imani ni mtu na mungu wake, kwasababu hata wakuu wa dini hawohawo wanatuhubiria, wana yao maovuu ya siri, ina maana wao hawajui kuwa mungu anawaona? Wakiwa mahubirinii wanajua, lakini wakiwa katika tendo la dhambi wameshahau...
Mungu ni mwema anatusamehe kwani , angekuwa mkali wa kuhukumu hapohapo, tungeumbuka!
Hebi fikiria madhambi mnagapi tunayafanya kificho. Unaangalia kushoto, kulia unahakikisha hakuna anayekuona, unakwiba, au unafanya la kufanya, umesahau kuwa mungu yupo nawe wakatii wote, mbona humuogopi?
Kweli M3, Unahekima sana na visa vyako, mungu akuzidishie hicho kipaji na ubarikiwe wewe na familia yako!

Anonymous said...

Hii story imeniumiza sana, nimeona kama unanisema mie moja kwa moja. Kisa kama hiki kiliwahi kunitokea kazini, nilikuwa mfanyakazi wa kusifiwa na kila mtu pale Hotel niliyofanyia kazi, nilifanya kazi pale miaka minne na mara nyingi hadi Mkurugenzi alikuwa ananitolea mfano wa kuigwa na wafanyakazi wengine.

Nikaweza kuoa nikiwa pale pale kikazi, mwaka 2005 mke wangu akajifungua kwa Operation, gharama nyingi sana zilinitoka lakini tulishukuru Mungu mtoto alitoka salama. Kesho yake naripoti kazini kama kawaida naambiwa nisifanye kazi nije tena kesho asubuhi!!! Nilijiuliza lakini nilikosa jibu, aliyenieleza ndio alikuwa Meneja Utawala wetu. Basi nikarudi home na sikuweza kumweleza chochote mke wangu maana niliogopa nisije kumshtua na ule mshono alionao.

Kesho yake nikaenda kazini, nikaonana na Meneja Utawala, akanieleza kuwa amepewa maagizo na Mkurugenzi kuwa nifukuzwe kazi, nilipouliza sababu? Akaniambia hajui chochote zaidi ya hayo maagizo aliyopewa! Jamani mbona nilichanganyikiwa. Akiba niliyokuwa nayo ilikuwa ni ndogo sana kutokana na kutumia pesa nyingi kwa wife kujifungua.

Basi nikarudi home na sikuthubutu kumweleza mke wangu yaliyojiri huko kazini.

Jioni nikapiga simu kwa baadhi ya wafanyakazi wenzangu niliokuwa nao pale kazini kuwauliza kama walisikia chochote, lakini nao walisema hawajui chochote na zaidi ya kunipa pole na kunitakia heri na maisha mapya.

Kesho yake asubuhi nikapigiwa simu na aliekuwa mmoja wa wateja wetu pale Hotelini, akaniambia jinsi alivyosikitika na habari za mie kufukuzwa kazi tena akaahidi kunisaidia kwa hali na mali.

Kweli katika kipindi kifupi tu nikapata kazi sehemu inayoeleweka na mshahara unaoeleweka plus matibabu na marupurupu kibao.

Nikaja kukutana na yule Mkurugenzi wetu wa zamani nikiwa ndani ya Kampuni hii mpya akaanza kuniambia kuwa nimtafute na tuyamalize, maana watu wengi sana walimlaumu kwa kunifukuza mie so akawa anataka anirudishe kazini!! Weeeh nilimpa za uso moja kwa moja kuwa sitaki tena mawasiliano naye ya namna yoyote ile.

Hivi ninavoongea ile hotel ni kama inakufa taratibu, kila kitu kinaenda kombo na wafanyakazi wengi tu wameamua kuacha kazi kutokana na mambo yaliyokuwa yanajitokea.

Any way ni story ndefu lakini naona hadi hapa nimeeleweka vyema

emuthree said...

`Anyn' WA tarehe 27, 2010, 6:48pm, nshukuru sana kwa kisa chako, nacho kinathibitisha ukweli wa haya mambo, kwani yapo, watu wanatendewa 'haya' sana, kwenye maofisi. Mtu akiwa nacho anasahau kabisa, kuwa `MPANDA NGAZI HUSHUKU' na RIDHIKI MAFUNGU SABA.
Sasa kisa chetu hiki tutakipa kibwagiza kimojawapo kati ya misemo hii..tukijaliwa, ngoja nikifanyie kazi!
Ahsante sana!

Unknown said...

Haswa stori imenibamba na kunipa motisha.nimeshukuru sana