Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Wednesday, November 10, 2010

Kikulacho ki nguoni mwako(Somnambulism story) 11


 Sasa leo hii Maua anataka kuniuliza swali kwa mtindo ule ule wa miaka miwili nyuma, je ni swali gani na lina maana gani kwake na kwangu.  Hebu tuendelee na kisa hiki, ambacho kitafichua swali hilo .....

                                              **************
 ‘Mume wangu je unanipenda ukweli wa kunipenda, na kwa upendo huo upo tayari kukubali chochote nitakachokuomba ilimradi kiwe kwa manufaa yetu , ilimradi kitanisaidia mimi kupona, ilimradi kitasaidia kuwaokoa wengine, ilimradi…ehe, je unanipenda kiasi hicho?’ Akaniangalia tena usoni na sasa alikuwa akiyazuia machozi yasitoke.

Unajua machozi huvuta hisia za mtu, ukimuona mtu analia inaweza ikakuvuta na wewe utamani kufanya hivyo hata kama hujui analia nini. Hata kucheka inakuwa hivyohivyo. Nilipomuona Maua machozi yanamlengalenga, Huruma ikanijia na kuhisi kuwa mke wangu ana nia ambayo inaweza ikaniumiza sana. Nikamvuta na kumshika begani huku nikimuomba mungu kuwa `anisaidie kulimaliza hili tatizo kwa amani’

‘Kwani toka lni nikawa sikupendi Maua, au kuna kitu nimekifanya ambacho kinaonyesha sina mapenzi ya kweli na wewe, je ungelitaka mapenzi gani ili nikuonyeshe kuwa na kupenda…’ nikamshika mikono yake na kuivutia kifuani kwangu.

Kwa maneno haya akaniachilia na kusogea nyuma kidogo, lakini mikono yetu ilikuwa bado imeshikana.

‘Mume wangu utajisikiaje kama ukipata watoto wenye matatizo kama mimi?’ akaniuliza na kunikazia macho.

‘Kwani nani kakuambia ukizaa watoto watapata matatizo kama hayo, hili ni sawa na matatizo mengine sio lazima yaaambukizwe kama malaria..’ nikamwambia, huku nikijua fika kuwa tatizo kama hilo linarithiwa, ingawaje sio lazima litokee.

‘Mume wangu usikwepe swali, hili ni swali la msingi, mimi kama mama nina Huruma sana na watoto, nah ii leo nimegundua kuwa nina tatizo ambalo huenda linaweza likampata mtoto wangu, na najua hilo, kwanini nisiwe na moyo wa Huruma. Mume wangu kama kweli tuna Huruma na watoto wetu wakati wa kuwahurumia ni sasa, utaonaje nikisema kuwa ndoa yetu iishie hapa ili tuwaokoe hawo Watoto wasijewakarithi tatizo hili..’ akatoa neno lilionivunja nguvu, ilikuwa kama mtu kapitisha kisu kwenye moyo wangu, nikamwachia mikono yake na kumwangalia kwa macho yaliyojaa uchungu

‘Unasema nini, mbona sikuelewi, mbona umekwenda mbali kiasi hicho, hilo halipo, na sitakubali kabisa..’ nikasem kwa msisitizo.

‘Kama ukiamua hivyo nitajua kuwa kweli hunipendi, na mapenzi yako kwangu sio ya kweli, kwani umesema kuwa upo tayari kunikubalia kwa lolote ambalo litanisaidia mimi kupona, na mojawapo ni hilo kuniachia mimi niwe huru na ‘Unajua mume wangu kuzaa Watoto wakapata maradhi ya kurithi kama hujui inakuwa haiumi, lakini najua kabisa uwezekano huo upo, najua kabisa kutokana na tatizo hili sitakuwa na amani katika maisha yangu, najua kabisa kutokana na tatizo hili jamii na familia nitakayoishi nayo itakuwa haina amani…jamani mimi nitakuwa na moyo gani, usiojali wenzangu. Hapana mume wangu, uamuzi wangu ni huo sina zaidi, ukubali usikubali, naona tuhitimishe ndoa yetu hapa, tubakie kama marafiki tu, kama kaka na dada, kama ndugu wema, ila….’

Kabla hajamaliza alichotaka kuongea mlango ukagongwa, akanitizama usoni halafu akasema `karibu, Tausi, mlango upo wazi’

Mara akaingia binti mmoja mzuri, nikahisi ni moja ya ndugu zake , mawazo yangu yalikuwa mbali kiasi kwamba hata kumsalimia huyo binti au kumuitikia salamu yake sikuweza. Nilitamani atoke haraka ili nipate njia ya kumshawishi mke wangu aachane na dhana hiyo, lakini Yule binti alikuja akakaa kwenye kitanda…

‘Mume wangu sitaki nikuache ukiwa mkiwa, sitaki nikuache ukihangaika kutafuta mke wa kuishi naye, hili nalijua kuwa utateseka sana, lakini nilifanya juhudi kubwa sana za kukutafutia mtu ambaye ataweza kuliziba pengo langu. Ninawependa sana watoto wetu, ninakupenda sana, na nainaipenda sana familia yangu, hili limeleta huzuni sana katika familia yangu, kwani tangu jana mama analia kwa uamuzii wangu, lakini nimemwambia na swala la muda, watasau na watafurahia uamuzi wangu huu..’ akasema na kumwendea Yule binti na kumshika mkono.

‘Huyu ndiye atakayekuwa mrithi wangu, huyu ana sifa zote ambazo mimi ninazo, na huenda zaidi yangu, nimjua na familia yao inajulikana. Kama kweli unanipenda basi muoe huyu binti awe mmke wako. Upendo sio lazima, na upendo ni makubaliano ya wawili wapendanao, hili halina shaka, lakini kwa mwanaume yoyote anayemjua huyu binti hatajuta akiwa mke wake. Yeye anakujua na nilipomshawishi alikiri kuwa `anakupenda pia’ tatizo ni wewe…’ akamtizama Yule binti kama anamkagaua halafu akanitizama na mimi.

Nilitabasamu kwa kebehi, nikitafakari pendekezo lake, nililiona kam mtu anayefanya mzaha, hivi wewe uachwe na mke wako, halafu aletwe ntu mwingine, eti ni badili ya mkeo, kweli kama mlipendana itakujia akilini, hapana naona Maua anafanya mzaha na akili za watu.

‘Nilibadilika na kujawa na hasira, nikamwangalia Maua na kutamani kutamka maneno makali lakini nikamuonea Huruma, kwani alichofanya ni kwasababu ya upendo, na sijui ana naia gani baadaye. Na kabla sijasema kitu mlango ukafunguliwa na walioingia ni mama mkwe na baba mkwe.

‘Wameshafika na una dakika tano za kujiandaa..’ akasema baba mkwe

‘Wamefika akina nani baba..?’ nikauliza kwa huzuni

‘Hajakuambia, kuwa yeye kajiunga na kundi la wasamaria wema, kundi hili limeundwa na akina mama ambao kwa nia yao safi wameamua kutoolewa na kazi yao kubwa ni kuwasaidia watoto na wajane. Wao watakuwa kambini kwamafunzo ya dini , na jinsi gani ya kuwalea watoto, kuwafundisha, na kadhalika, ni kama wanvyofanya watu wa dini, lakini hawa kila mmoja anakuwa katika dini yake, ila cha muhimu ni kujitolea wakati wote kuwahudumia wasiojiweza, watoto, wagonjwa wazee …’ akasema na malngo ukagongwa tena.

Niliona wanannichanganya, maana sipewi muda wa kujitetea, naona kila kitu walishaamua kama familia, na hili liliniumiza sana, kuwa mamlaka yangu kama mume yalipuuzwa, au kwasababu wao wanajiweza na hawataki kunithamini mimi…’ iliniuma sana, ilinifanya niwaone familia nzima hawana Huruma na mimi.

‘Aaah, kama mumeamua kiasi hicho, mimi nitafanya nini, lakini mjue kuwa mimi nitabakia na jeraha kubwa sana, inanifanya nijione sina thamani kwenu…maamuzi mumechukua na sikushirikishwa…’ nikasema huku machozi yananitoka, na mama mkwe kuona vile akanijia na kunishika bega. Mama mkwe wangu huyu tulizoeana kama mama mzazi, na wakati nahangaika kumpata binti yake ndiye aliyekuwa kufua mbele kunisaidia. Na hutaamini alikuja na kunikumbatia kama mwanae alieyemzaa. Na hapo pamoja na kudeka nikajikuta machozi yakitoka kama maji. Nilipoinua uso wangu nilimuona Maua keshabadili nguo, na anatabasamu.

‘Mume wangu ni swala la muda, mwisho wa siku utanisifia kwa uamuzi wangu huu, na kama nilivyokuambia, kama kweli unanipenda, basi binti huyo awe ndiye mke wako, na natumai baada ya mwaka ambao nitakuwa huko kwa mafunzo, nikija nitawakuta mna mtoto. Huko ninakokwenda haturuhusiwi kuonana na mtu mwingine yoyote, na hakuna mawasiliano na mtu yoyote, hadi mwaka uishe….samahani kwakuchukua uamuzi huu mimi na familia yangu, sio nia yetu, na hatukuwa na nia mbaya, ni kwa masilahi ya wote, mama alipinga sana, lakini nilishawaambia mwenye maamuzi ya mwishi ni mimi…’ akanishika mkono akachuku begi lake na kumkumbatia mama yake, halafu baba yake, akamkumbatia Yule binti, na mwisho akaja kwangu. Sikuweza kumkumbatia kama vile tufanyavyo, nilimwangalia kwa macho yasiyoamini kuwa kweli huyu mke wangu anaondoka, kweli ndio mwishoo wa ndoa yetu…hapana! Nikambusu kichwani nikiwa na hisia kuwa atarudi tu…

Ndugu wapendwa sasa imepita mwaka, sijaweza kumsahau mke wangu, siakata tama ya kumsubiri nikijua baada ya mwaka akirudi tutaendelea kama mke na mume. Yule bintiu aliyechaguliwa na mke wangu kuwa awe mke wangu mrithi, anaishi na mimi kama mtu wa kuisaidia familia yangu, na hatuna mahusiano yoyote, inagawaje anafanya kila liwezekanalo kunibadili mawazo lakini hajafanikiwa.

Lengo langu na nia yangu ni kuwa baada ya mwaka, Maua atarudi akiwa kapona kabisa, ana tutaishi naye kama ilivyokuwa , lakini hayo ni mawazo yangu, amabyo mama mkwe aliniambia niyaondoe kabisa akilini, kwani kwa ufahamu wake wale wote wanaopelekwa huko wakirudi sio wenzako tena, hawana tamaa na mambo ya kidunia, wao na ibada, wao na kusaidia watu…kwahiyo, nisipoteze muda, nimuoe Yule binti ,au kama simtaki nitafute mke mwingine…!

Hapa ndio mwisho wa kisa chetu, najua wengi wana maswali mengi ya kuuliza, sasa ilikuwaje, sasa mbona nimekatisha. Sijakatisha, kwani hapa ndipo mahala mhusika alipomalizia kuelezea kisa chake na mwaka umefika lakini Maua hakurejea kama ilivyokusudiwa, kwa taarifa ni kuwa yeye kateuliwa kuwa mwalimu wa taasisi hiyo na kurudi kwake labda baada ya miaka mitano.!

Ni mimi: emu-three

12 comments :

elisa said...

mmh yaani nimemaliza kusoma nikachoka kabisa..so sad ..ila ndio hivyo amuombe sana Mungu ampe nguvu na kumuwezesha kuyakabili yote yanayomzunguka .Mungu ni mwema naamini atamsadia tu.

Pamela said...

unajua uchungu ndio niliosikia na machozi kunitoka.. Pole sana kwa kaka aliekutwa na hili. Mimi nimeumia nashindwa kupata picha kwake ni Mungu amtie nguvu nae ajitahidi kujichanganya ktk maisha ya kawaida ingawa mwisho wa siku mwamuzi wa maisha yake ni yeye..

Jane said...

M3 Mbona inatia uchungu kiasi hiki??Imeniliza kweli but najiuliza huyo mhusika alikuwa katika hali gani??? Eeeeh mwenyezi mungu mpe ujasiri wa kuona kuwa kuna maisha baada ya hapo japo inauma but he has no choice.

emu-three said...

Ndugu wapendwa, tatizo likikupata ndipo unaweza kuelezea ule uchungu wa hilo tatizo, na hata usimulie vipi, uchungu hauelezeki.
Kisa kinasikitisha, lakini mazingatio ni kuwa unapopatwa na tatizo mkabidhi mungu wako.
Swali hapa ni wangapi wapo tayari kujitolea kama huyo mwanamama, kuamua kutozaa, ili asije akaendeleza huo ugonjwa. Wangapi wanaumwa na wanajue kuwa tatizo hilo linaweza likaambukiza, lakini hajali...huu ni ujumbe mmojawapo!

Anonymous said...

Yaani machozi yamenitoka, wakati nasoma hii stori, nimesikia uchungu sana. Sasa mimi ni msomaji tu je, huyo kaka ambae amepatwa na mkasa huu, alikuwa kwenye hali ya namna gani. Kwa kweli naungana pamoja na Pamela kwa jinsi alivyosema ni Mungu tu ambaye atakae muongoza. na Elisa, ni ya huzuni sana.

Kwa kweli hii stori imeleta changamoto sana ktk maisha yetu tunayoishi. Ni nzuri na Inamafunzo mno.

Jamani M3 tunga kitabu!!!!!!!!! Kitakuwa na soko zuri sana.

MUNGU ABARIKI KIPAJI CHAKO (KAZI YA MIKONO YAKO)

Kwakweli wewe ni mtunzi mzuri sana, hata kama mtu amekupa hii stori. Pia na wewe ni mjumbe mzuri kwetu na umewakilisha vizuri sana hii stori. Nilitamani iendelee jamani. Lakini ndio hivyo hakuna marefu yasiyo na mwisho.

AHSANTE SANA M3

Tunasubiri stori nyingine nzuri zaid ya hii.

UBARIKIWE

BN

Nasibu said...

Leo mimi sina la kusema kwasababu nimeumia saana,utadhani yalinitokea mimi.Pole sana ndugu yangu.

Anonymous said...

M3 NI KWELI, KABISA HUYO DADA ANASTAHILI PONGEZI KWA KUTAMBUA NA KULIKUBALI HILO TATIZO LAKE. KUAMUA KUTO ZAA ILI ASILITHISHE KIZAZI CHAKE. KWA KWELI MUNGU AMBARIKI SANA. NA AZIDI KUMUONGOZA.
KWASABABU WAPO WATU KATIKA HII JAMII YETU WANAJUA FIKA KUWA WAO NI WAATHILIKA WA VIRUSI VYA UKIMWI, LAKINI NDIO KWANZA WASEMA TUFE WENGI. WANAWAAMBUKIZA WENZIWAO KWA MAKUSUDI KABISA, PASIPO HAO WENZIWAO KUJUA. SASA JE, HUU SI UAJI KABISA.

JAMANI TUBADILIKE, TUKUBALI HALI NA TUSEME NA WENZIWETU KUWA MIMI NIKO HIVI NA WEWE JE, KULIKO KUFICHANA, TUTALIANGAMIZA HILI TAIFA LETU.

SAHANINI WADAU KUINGIZA MADA HII HAPA, INGAWA AIHUSIANI KABISA NA MADA YETU KWA SASA.

KWA JINSI YA HILO SWALI ALILOULIZA M3.

KAZI NJEMA.

BN

elisa said...

kweli BN ..Kazi ya Miram3 ibarikiwe ..inagusa sana maisha yetu tunayoishi na inafundisha..wewe ni mwandishi hodari..ila hujapenda kufahamika ungeuza sana vitabu na nakala zako

Simon Kitururu said...

Kisa kabambe hiki! Lakini ukiniuliza mimi bado nitadai Mume alitakiwa ashirikishwe kwenye maamuzi kama haya yamuhusuyo Mke wake.:-(

Faith S Hilary said...

kama walivyosema walionitangulia, kweli inahuzunisha yaani mmh, bora angejitahidi kumkubali huyo msichana, anyway I love the story yaani sana tu! Umesema kuna kisa kingine kinakuja, I can't wait!!! Ubarikiwi

KASHY said...

jamani M3,mimi sijawahi kuchangia lakini leo nimeguswa sana na hili.kwa nini huyu dada asingekaa na mumewe na kufunga uzazi ili akamlea mume wake na watoto wa mumewe?na pia kwa nini asingempa mumewe nafasi ya kumshauri lolote ktk maamuzi yake?mimi nipo upande wa mume kuwa hakutendewa haki .

emuthree said...

KASHY, karibu sana , naomba uwe unachangia, usiwe na wasiwasi hii ni blog yetu kwa wale wote wanaopenda visa kama hivi, maoni yako, ushauri, kukosoa, na hata kama una kisa chako andika, tu!
Ama kwa kwanini hikuwa hivyo au vile, mmmmh, siunajua tena visa vya ukweli inabidi ukubaliane na huo ukweli, na baadaye ushauri kama huo unafuatia!
Kweli hata mhusika mwenyewe amesononeka sana, kuwa `hakutendewa haki' hata ukimkuta leo analalamika, lakini natumai mwisho wa siku `atakubali yaishe' na atajua kuwa `yote ni maisha'