Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Friday, November 5, 2010

Kikulacho ki nguoni mwako(Somnambulism story) 8

 Alipokuja inspekta, mimi na mdogo wangu tulimkaribisha chumba cha maktaba ya kujisomea. Kitari mwalimu wake kapatwa na dharura kwahiyo hatakuwepo kwenye kikao chetu, lakini tunaweza kuendelea na kama tukimuhitaji tutakuwa naye baadaye au kesho.


Wakaanza kunionyesha ule ushahidi waliotaka kunionyesha kuhusian na mwanamke wanayesema anafanya vitu huku akiwa usingizini. Nilikuwa na hamu sana ya kumgundua kuwa ni nani, ni shemeji yangu au kuna mwanamke mwingine humu ndani.

Ule mkanda ukaanza kuonyesha mazingira yam le ndani, na baadaye ukavutwa hadi kama sikosei na mlangoni mwa chumba change, baadaye ilimuonyesha mwanamke, na kwa jinsi ilivyokuwa ikionekana, mwanzoni sikujua kabisa kuwa ni nani.

Kuna muda waliiukuza lakini mwanzoni mwa hiyo picha haikumtambulisha vizuri huyo ni mwanamke gani. Na kabla hatujaendelea mbele wakaja askari wawili wakitaka kuongea na inspekta. Inspekta alituomba samahani akainuka na kutoka nje na wale askari na baadaye wakarudi wote.

‘Jamani hawa ni askari ambao niliwaweka kwenye lindo la kumfuatilia huyo mwanamke kwenye hiyo picha tuliyoionyesha, na wana ushahidi wakutosha kuwa mwanamke huyo kaelekea Kibaha. Hebu tupate maelezo kabla hatujaendelea kuiangalia hiyo video kwa undani. Hebu constebo Juma elezea ilikuwaje.

Yule askari mlinzi akaanza kuelezea mbele ya inspekta, alisema aligutuka toka usingizini, na kumuona mwanamama akitembea kuelekea vichakani, na walipomfuatilia nyuma walimuona akiingia kwenye gareji iliyopo karibu, na humo akawa anazungukazunguka hadi kwenye eneo la jengo la zamani kidogo. Mwanamama huyo alipanda kwenye ukuta ambao kwa kawaida sio rahisi mtu kupdna, na kuweka kitu kwenye boksi ambalo alilifungua kwa fungua aliyokuwa ameishika.

‘ Halafu akateremka chini, na kuna muda alitaka kudondoka, lakini ki ajabu alijiokoa kwa namana yake. Alitoka mle na mara kukawa na lori la mizigo linatoka, malori haya nafikiri yanakwenda masafwa , cha aabu Yule mama alidandia kwa nyuma na kujificha kwenye mizigo. Hapo ilibidi nimwambie mwenzangu alifuate hilo lori la mizigo kwa pikipiki. Na mimi nakarudi huku aili nikupe taarifa, na kama nilivyouelezea usiku, nadhani ndiye huyo mama uliyesema tumtizame akitoka tujue anaelekea wapi.

Inspekta akakubali kwa kichwa halafu akamuuliza askari mwingine ambaye alifuatana na lile lori. Huyu allisema yeye alilifuatilia nyuma hadi liliposimama maeneo ya Kibaha, na Yule mwanamama akashuka, na kuanza kutembea kuingia katika mashamba ya watu hadi alipofika kweny kampuni ya Mzee mmoja aitwaye Mzee Tajiri, na humu akagonga mlango, na alipofunguliwa hakuonekana kutoak tena.

‘Mimi kwa vile mlitoa amri kuwa tusimsemeshe au kumgusa, tulipohakikisha kuwa kaingia humo, ndio nikatoa taarifa kwako mkuu!

Niliwaza kutokana na meelezo ya inspekta na askari wake, ina maana mtu wanayemuongela kwa taarifa zilizopatikana kwa simu toka Kibaha ni mke wangu, na ndiye wanayesma ana matatizo ya kutembea usiku wakiwa ndani ya usingizi na sasa yupo mikononi mwa wazazai wake. Nikataka kujua ukweli wa hisi hisa zangu kwa kuwauliza Inspekta na mdogo wangu.

‘Ina maana mnayemuongelea ni mke wangu?’ nikauliza kwa mshangao.

‘Ni mke wako ndio, ndio maana kaondoka usiku akiwa usingizini, huelewi bwana’ akasema inspekta.

‘Haiwezekani, mke wangu hana matatizo hayo,toka lini akaumwa huo ugonjwa nisimgundue siku zote nilizoishi naye, na sijawahi kumsikia akisema ana tatizo hilo au kusikia toka kwa wazazi wake. Mimi ninachojua ni kuwa mke wangu alitaka kunimaliza jana, alichukua kisu jikoni kwa nia ya kuniua, kwani jana nilimuona kwa macho yangu. Haiwezekani, mtu aamuke toka usingizini, ajue kisu kipo wapi akichukua, avae `gloves’ mikononi, ili sijulikane kwa alama za vidole, haiingii akilini mwangu…’ nikashituka kuwa nimeongea kile nilichokuwa sitakikukiongea, na hapa ina maana nimetia mke wangu hatiani.

‘Kaka, yote hayo aliyafanya shemeji bila kujijua, shemeji ana tatizo la kufanya kazi akiwa usingizini, na hilo uliloliona jana ni moja kati ya matendo ambayo kayafanya akiwa hajui ni nini anachokifanya. Inavyoonekna yeye ndiye aliyenichoma kisu siku ile, kama nilivyokuambia mtu aliyeingia chumbani mwangu ana tabia ya kupaka manukato ya harufu hiyo niliyoisikia chumbani.

‘Kwanini asiwe mdogo wake kwani naye anapaka mafuta ya namna hiyo…’ nikasema kwa jaziba.

‘Kaka ipo siku moja nikiwa najisomea nilimuona shemeji akitoka usiku, nikashangaa nikaamua kumfuatilia kwa nyuma, alikwenda hadi kwenye hilo jingo la gereji na kuingia humo kama walivyomuana hawo askari, na akaingia mle ndani. Nilimfuatilia na kumuona akipanda sehemu ambayo ukimbiwa upande leo huwezi, N akule alilichukua hilo kabati na kuweka vitu, na baadaye akalifunga . Kwaweli mimi mchana wake nilikwenda kuangalia kuwa aliweka nini, lakIni sikuweza kuipanda ile sehemu. Hebu tuone sehemu ya pili yah ii video tuliyoinasa jana ili umuone kwa uhakika.

Ile video ikaonyesha mwanamke Yule akichukua kisu kabatini halafu akavaa gloves mikononi, halafu akageuka, na hapo sura kamili ikaonekana, lakini cha ajabu kabisa ni machoni. Na hapo mdogo wangu akaikuza ile sehemu na kuyaona yale macho yalivyo. Kinachoonekana zaidi ni weupe, Na inatisha kidogo, kwani ni kama mfu…’ hapo nivuta pumzi.

‘Kaka sisi ndio tuliokuja chumbani kwako na kutengeneza ile mito kama mtu aliyelala, tulitaka kukuarifu, lakini kila mara tulipojaribu kukufikia tukawa tunapata kipingamizi. Tunashukuru kuwa na wewe hukahangaika kubomoa mitego yetu… Sas hebu angalia sehemu hii.

Kwenye sehemu ile inaonyesha sura kamili ya mke wangu kasoro macho hayakuonekana kama mke ninaye mjua, hapo ilikuwa kipindi anatoka chumbani kuelekea jikoni. Nikahakikisha kuwa ndiye mwenyewe. Kumbe hayo yote alikuwa akiyafanya akiwa usingizini, na kumbe…’ Tugasikia sauti ya kilio nje, kumbe ni mdogo mtu alikuwa pembeni ya mlango akiangalia tunachokiangalia. Na mdogo wangu akamfuata kumtuliza.

Baadaye mdogo wangu alikuja na mdogo wa mke wangu kwasababu alitaka na yeye ashuhudie hayo yanayoelezwa, kwani alishaona sehemu kubwa na alishajua nini kinaongelewa, na alimchukua ili kama kuna anachojua akieleze.

‘Mimi kwa uchunguzi wangu nafikiri huko ndipo alipokuwa akificha vile vitu vyako ulivyokuwa ukivitafuta. Naomba inspecta baadaye twende na ngazi ya Tanesco, ili tupande na kuangalia kuwa kweli kuna hivyo vitu….’ Akasema mdogo wangu.

Wakati wanajadili hili maara simu ikapigwa tena.

‘Halloh, nyumbani kwa mzee Tajiri. Nilikuwa naulizia kuwa mtafika saa ngapi, kwani kuna dakitari tumemualika kuja, yeye ni mtaalamu wa matatizo ambayo tunahisi yamemkumba mke wako..’ akaongea mzee tajiri.

                                                       *******
Je nini kitaendela baaada ya hapo. Tuwepo karibuni, kwani sasa kiini cha tatizo kimefika kwa wenyewe, je kuna matibabu, je polisi watachukua hatua gani?

Ni mimi: emu-three

6 comments :

Jane said...

Du!!!!!!!!!! Jamani M3 Mbona umeishia karibu????? ungeendelea kidogo. Du! story inasikitisha hiyo!!! Hope family haitafarakana, na mme atakuwa mstari wa mbele kumsaidia mkewe ili aweze kupata matibabu.

Simon Kitururu said...

Matatizo ya Sleep Walking yapo.Kwetu Shangazi yangu alikuwa anawekewa mpaka mabeseni ya maji pembeni ya kitanda kwa kuwa alikuwa anaweza usiku wa manane kuondoka kwenda shule. Uzuri wake alikuwa ana kelele wakati anajiandaa kuondoka akiwa kashavaa uniform kitu kilichokuwa kinasaidia ndugu kumdhibiti.

Mimi mwenyewe mpaka umri wa miaka kama kumi hivi ilikuwa kama nimelala na naota ukaniamsha kwa kurupushani nilikuwa siamki ila naanza kufanya yale nayoota kama vile niko macho kitu ambacho kilifanya nyumbani watu wafundishwe jinsi ya kuniamsha . Lakini kwa jinsi nilivyoendelea kukua tatizo hili likaisha bila tibabu.


Tukiachana na hilo;
M3 bonge la stori hili MTU wangu!

Faith S Hilary said...

sasa emu-three utanifanya niote maajabu maana nimesoma hii usiku tena niko peke yangu chumbani...hahahha! I love this, can't wait for the next one

Anonymous said...

M3, Jamani, umeipatia wapi hii stori, mbona inafanana na tatizo lililomkuta dada yangu!
Hongera sana

elisa said...

ungeimalizia leo jamani

Anonymous said...

Mmmh! Mimi sisemi hapo. Yaani ni kiboko. Na kila mtu akisoma anaikubali. Sio siri mdau mmoja hapo alipokwambia kuwa kuwa kuna jaama wana-copy na ku-paste na kuwatua watu. Nami ndio nikapata mwanga kuwa inawezekana kufanya hivyo ndio niliamua ku-copy na ku-paste ili niwapelekee ndugu zangu kijijini huko hili nao wajifunze, kuwa hili tatizo lipo na sio mtu najifanya au kudhani ni mapepo. Lakini huwa nawatambulisha kuwa ni story ya M3 na inapatikana kwenye blog. Na wengine nawaelekeza wafungue blog yako wasome.

Lakini kuwa makini asije mtu akajifanya kutunga wewe, kutunga kitabu akajifanya ni chake.

Kwakweli hii ni zinga la story na kila atakayesoma anakuliana nawe. "Take care"

"MI NILIKUOMBA KABLA SIJAFANYA HIVYO" THX. SINA TATIZO NAWE.

'SALUTI MKUU'

BN