Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Friday, November 5, 2010

Ahadi ni deni

 Tulitembelewa na jirani yetu mmoja, alikuja kwasababu alituzoea, ni ujaje wake siku ile ulikuwa kama kutuaga! Alianza maongezi hata bila salamu, akasema leo kaja kutuaga, akasema


Kuwa visa vya mume wake vya uongo na unafiki vimemchosha ` nimevumilia nimeshindwa. Sijui wanaume wengine wana akili gani. Wanafikiria sote tu wajinga wakudanganywa, eeh, kweli alinipata mjinga akanidanganya akanioa, na sasa nina uja uzito wake, lakini , lakini…nyie ngojeni tu, mtanisikia makali yangu.

Dada huyu alikuja nyumbani kwetu, na katika maongezi tuligundua kuwa yeye aliolewa na huyo mwanaume baada ya kuhadaika, kwani huyo mwanaume alimdanganya kuwa ana nyumba mbili ana gari moja la kutembelea na madaladala matatu, mashamba na miradi mingii ya urithi, na ajabu vyote hivyo alionyeshwa hati ya kumiliki zake!

‘Siku mwanaume huyo aliponionyesha hati za kumiliki hivyo vitu, nilimwamini kabisa, kwani mwanzoni nilijua hizo ni hadaa za wanaume tu. Walishawahi kuja wanaume wengii kunichumbia na wote nikagundua kuwa ni waongo, lakini huyu alininasa.

Kila siku alikuwa akija na gari tofauti, na alikuwa akiniambia kuwa moja ya kampuni yao inamiliki magari ya kukodisha ila yeye mwenyewe ana gari moja la kwake binafsi, alisema kuwa hahitaji kuwa na magari mengii kwani kutokana na kazi yake na kampuni yao anaweza kuchukua gari lolote akatembea nalo!

Basi siku moja akaniomba tukatembelee miradi yao, na wazazi wangu wakamkubalia, tulizunguka kwenye shamba ambalo alidai ni la kwao, tulipotoka hapo akanipeleka kwenye kampuni yao ya kukodi magari, na hapo walikutana na wafanyakazi ambao walikuwa wakimsalimia na kumuita bosi, halafu akanipeleka kwenye nyumba yake ambayo ilikuwa katika hatua za mwisho mwisho kumaliziwa!

‘Basi tulipotoka hapo moyo wangu ulifurahi sana, nikasema ile ndoto yangu yakuolewa na mume mwenye nazo imetimia, sasa niombe nini tena. Tulipotoka hapo akanipeleka hotelini ambapo alisema tupumzike kidogo, na unajua tena kwa kumwamini mapumziko hayo yakazaa mapenzi na nafikiri ndipo nipopatia uja uzito wake.

‘Baada ya siku kadhaa alikuwa kutoa posa , na hili lilifanyika baada ya kuvalishwa pete ya uchumba. Wazazi wangu walifurahi sana, kwani hatimaye nimekubali kuolewa. Kwaweli nilikua mgumu kujiingiza kwenye ndoa, kwasababu ya kuhakikisha kweli anayenioa hanidanganyi! Niliona wanawake wengie wakijuta kwa kuolewa na wanaume eti kwasababu ya ndoa, mimi hili nililifikiria sana na katika ndoto yangu ikawa kuolewa na bosi, mtu mwenye nazo, ili mwisho wa siku nipate familia ambayo haitateseka!

Kumbe jamaa huyu alikuwa tapeli wa kimataifa, nimekuja kugundua baadaye kuwa sio mimi tu aliyeniingiza mkenge, wapo akina dada wawili ambao walilizwa na bahatti nzuri wameolewa na wanaume wengine. Mmojawapo ndiye aliyekuja kuniambia siku nimeshafunga ndoa.

Siku hiyo tulikuwa kwenye nyumba ya kupanga, hutaamini, jamaa alisema inabidi tupange nyumba ili amalizie nyumba yake vizuri, mimi kwa kipindi hicho nilikuwa nimeshamwamini, nikasema vyema. Sasa wakati mume wangu huyo akiwa kwenye mishemishe zake, na huwa akiondoka huja kuchukuliwa na gari, kumbe ni la marafiki zake aliopangana nao!

‘Hodi mwenyeji…’ nikasikia hodi toka nje, ilikuwa sina kawaida ya kupata marafiki, kwanza mwenyewe nilikuwa sipendi, lakini huyu dada alinivutia alivyo, nguo zake, mrembo kama vile madada urembo. Nikamkaribisha ndani. Alipofika akatazama mle ndani halafu akaniangalia kwa dharau, Nikajiuliza vipi kulikoni.

‘Mhhh, na wewe umehadaika na huyu tapeli, nakuonea Huruma sana, basi nikuambie mimi nilidanganyika kama wewe, nilipogundua nilitamani nijinyonge, lakini nikasema nimuachie mungu. Bahati nzuri nikampata huyu mume nianyeishi naye, nashukuru sana ,kwani hasira zote ziliniisha, vinginevyo…sijui.

`Sasa nakutonya, huyu mume ni tapeli wa kimataifa, ana mbinu nyingi za kuwahadaa wanawake, hana gari, hana nyumba ,hana kampuni, yeye anaishia mitaani kulaghai watu kwa bishara za hapa na pale, yeye kazi yake kubwa ni udalali. Kama utaamini,, au hutaamini shauri lako, poteza muda hapa akutie mimba , halafu atakuacha kwenye mataa uwe unahangaika kulea mtoto. Huyu alikuwa akiishi Nigeria, akaja Kenya , ingawaje ni Mtanzania, lakini tabia yake ndiyo hiyo utapeli!

Nilimuona yula dada kama mnafiki Fulani, ambaya niia yake ni kunidanganya, nilimtaka anithibitishie hayo, akasema atakuja kesho yake. Na kweli kesho yake akaja, na kunipeleka mahala mume wangu anapokaa kijiweni. Tulijificha mahala, na hapo tukasikia mazungumzo kati ya mume wangu na jamaa Fulani, walikuwa wakibishana kuhusu mgawo wa kazi waliyofanya, na katika mazungumzo yao nikasikia Yule mwenzake akimsaga na tabia yake ya ulaghai.

‘Hata kama mimi ni mlaghai, lakini nafanikiwa, sasa hivi nimeweka chombo kipya ndani, kikichuja natafuta kingine, nahamia mji mwingine, hata kama nitamzalisha, nitamuacha kwenye mataa, mimi nayajua maisha ya kila namna huwezi kunivunga..’ akasema mume wangu

‘Wewe utachomwa , tena moto mkali, na utapata taabu kuanzia hapa duniani, unawahadaa awanawake warembo wasio na hatia, halafu uansema unawaacha kwenye mataa, kwanza nipe hela zangu kabla sijakuharibu sura yako…’ ukazuka ugomvi, na sie tukaondoka na mwenzangu. Akanipeleka kwenye ile kampuni aliyosema anaimiliki na humo tukaulizia na kuwamabiwa kuwa Yule jamaa aliomba asaidie hivyo, kuwa aonekane ni mmoja wa wakurugenzi pale, na wao wakamsaidia kwani hawakujua ninikusudi lao.

Nilichoka, kwani kila mahala aliponipeleka, niliiishiwa kuchekwa kuwa jamaa Yule ndivyo alivyo, na ana marafiki zake kwenye hizo kampuni ambao wanamsaidia kufanikisha hilo. Nikarajea nyumbani na alipokuja huyo jamaa, nashindwa hata kumuita mume wangu tena nikamuulizia kuhususiana na uongo wake, alikuja juu,na kuniita mwanamke m-mbeya na akasema kama simuaamini njia ipo nyeupe, niondoke niende kwetu. Na maeneo ya dharau na kashifa.

Sasa bahati nzuri ana mishemishe zake katika mazungumzo yao jana, nilisikia kuwa ataletewa hela kibao, …hapo na mimi nitamuonyesha kuwa na mimi sio mjinga! Ama zake ama zangu…

Huyo dada aliondoka baada ya malezo hayo, na kesho yake jamaa, ambaye ni mume wake alikuja kwetu kuulizia kuwa mke wake aliwahi kuja hapo, tukamwambia ndio, alikuwa kuongea, na kutuaga kuwa ataondoka karibuni. Akatuulizia alisema anaondoka kwenda wapi tukamwambia hakujui kwasababu hakutuambia. Akasema mwanamke huyo kaondoka na hela za watu milioni arubaini, na sasa wenzake wanataka kumuua, …

Ama kweli nimeamini kuwa dalili za mnafiki huwa ni mwongo, pili anaahidi asichotekeleza na akiaminiwa haaminiki. Jamaa haikuchukua muda akanaswa na polisi na sasa anaichezea jela.

Jamani ahadi ni deni, kwanini tunaishi katika dunia hii kwa hadaa, tunaona ufahari kudanganya, kuahidi watu, hili na lile, kumbe ni uongo, ni unafiki…tukumbuke ahadi ni dhamana ambayo usipoitunza kwa kutekeleza kile ulichoahidi, ama mbele ya kadamnasi au mkiwa wawili, lazima utadaiwa sio tu hapa duniani , lakini hata ukifa , ujue una deni kwa uliyemuahidi.

Msemo wa leo ni Ahadi ni deni.

Ni mimi: emu-three

1 comment :

Simon Kitururu said...

Ila huyo Dada naye hana mapenzi ya Dhati. Kwa kuwa mapenzi ya kweli hayachagui sasa huyu atakuwaje kapanga kabisa aolewe na Kibosile?

Na tabia hizi za akina DADA kutaka kuolewa na Mabosi au wenye pesa ndio zifanyazo Wanaume wazidi kutongoza kwa kutumia uongo au hata kuingilia UFISADI kwa kuwa hivihivi tu hueleweki kauli ati.:-(