Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Thursday, November 4, 2010

Kikulacho ki nguoni mwako(Somnambulism story) 7


Nilishituka toka usingizini kwa kuguswa bega, niliruka kama mwehu, karibu kukimbia, na mdogo wangu akaangua kicheko, halafu akagundua kuwa kakosa adabu na kunishika bega. Kama dakitari akaona kafanya kosa, na alijua kwanini nimeshituka kiasi kile.

‘Kaka mbona hujaenda kulala chumbani na shemeji, unajua umefanya kosa kubwa sana, akimuaka nakukukosa anaweza kujawa na wasiwasi. Ukumbuke kuwa matatizo mengine hayataki wasiwasi, mawazo na hasira akilini!’ Maneno ya mdogo wangu yaliniingia akilini na kujiona mjinga. Lakini jana nilivyopitiwa na usingizi hata sijui. Nilitaka kumwelezea nilichogundua jana usiku , lakini nikasema kama ni lazima nitamwambia baadaye, ngoja nikamuone mke wangu ambaye sasa namuona adui yangu mkuu!

Nikakurupuka kwenda chumbani, lakini nilipofika mlangoni, nikasita, halafu nikafungua mlango kwa wasiwasi.Niliwaza akilini, chumba changu mwenyewe kinakuwa kigeni kwa siku moja tu. Nilipoingia ndani kulikuwa na kigiza giza kidogo, macho yalishaanza kuingiwa na ukungu, sijui wa woga au wa kulala kwa shida. Lakini moyo ulikuwa ukinienda mbio kwa mashaka.

Harakaharaka niliangalia kitandani, halafu nikapitisha macho sehemu yote ya chumba kwa haraka, Niliangalia tena kitandani , kulikuwa hakuna mtu. Nikasogelea kitandani na kuliondoa shuka kuhakikisha, kweli hakuna mtu. Nikasema huenda mke wangu katoka. Nikasubiri kidogo , baadaye niliangalia chooni na sehemu zote, hata jikoni lakini sikumkuta mtu!

‘Deni umemuona shemeji yako huko?’ nikauliza kwa sauti

‘Mbona hajafika huku mimi nilizani bado kalala..’ akasema Deni

‘Mimi nimetoka asubuhi sana, sijamuona akitoka nje…’ akasema mdogo wake mke wangu.

Nilianza kuhisi vibaya, kuwa huenda huyu mtu kagundua kuwa hajafanikiwa kuniua na amekimbia, nikasema hawezi kukwepa makucha ya sheria, lazima atapatika tu!

‘Yeye anafikiri ni mjana sio, …’ nikasema kwa sauti, na maneno yale yalimfanya mdogo wake aniangalie kwa mshangao. Mimi sikumjali nikijua lao moja.

‘Kaka naona kuna tatizo hapa, nafikiri tuwasiliane na Inspekta ili tupate msaada, kwa askari wao wa usiku, alisema kuna mtu kamweka hapa kufuatilia ile hali niliyokuelezea jana, kwahiyo kama katoka lazima watajua wapi alipokwenda, halafu Yule mgeni wangu dakitari kanipigia simu kuwa mitihani imeahirishwa kwasababu yeye ndiye msimamizi na amepatwa na dharura , na hii itanipa na mimi nafasi ya kushiriki na kuthibitisha utaalamu huu..’ akasema mdogo wangu

‘Kwani kumetokea nini, mbona sielewi, dada yangu kakumbwa na janga gani…’ mdogo wa mke wangu akaanza kulia na kukimbilia chumbani kwangu kumwangalia ndugu yake. Nilimsimamisha na kumwambia asiwe na wasiwasi, atajua nini kinachoendelea. Nilimwangali kwa jicho la hasira, nikiwaza huenda wana njama na dada yake ahalafu anajifanya hajui, lakini huenda kasichana ka watu hakajui kitu...!

*****

Huko nyumbani kwa Mzee Tajiri, kwa mkwe wangu, nako mambo yalikuwa sio shwari, familia ilikuwa inahaha.

Endelea pale tulipoachia…

Mke wa mzee tajiri aliposikia sauti ya maongezi akavaa nguo na kukimbilia chumba cha maongezi , na alipofika akapatwa na mshituko ambao ulimpata mumewe. Alimwangalia mwanae alivyolala pale kwenye kocho, akataka kumkimbilia na kumshika ajue nini kimemsibu, lakini baba mtu alimuwahi na kumzuia. Alimwambia asubiri kwanza ili wajue nini kimetokea.

‘Unaweza ukamshitua mtoto, mwache apumzike kwanza halafu akiamuka tutajua nini kinachoendelea , hana homa, hajaumia mahala, nahisi kuna kitukimetokea huko Dar, lakini kama ni kibaya tungeshapata taarifa. Naona ni vyema niwasiliane nao, labda kuna tatizo’ mume mtu akajaribu kupiga simu za Dar, zikawa hazipatikani. Akajaribu nyingine za jirani anaowajua nazo zikawa hazipatikani.

‘Hivi kuna nini leo au mitandao ina matatizo haiwezekani watu wote nionao wajua Dar simu zao zisipatikane’ akasema kwa hasira. Na mara sauti ya mtoto wao akijinyosha ikasikika, na wote wakamsogelea karibu.

‘Mhhh, najisikia kuchoka leo, mume wangu mbona hujaniamusha…oh, hivi nipo wapi hapa, eeeh, baba , mama mumefuata nini huku Dar, mbona hatukupata taarifa kuwa mtakuja…oh, hivi jamani nipo wapi hapa, mbona sielewi’ ilikuwa sauti ya mtoto wao na wazazi wakabaki wameduwaa. Na kabla hawajongea kitu, simu ikalia, ilikuwa simu toka Dar.

‘Halloh, ni mimi, kuna nini kinaendela hebu tufahamisheni…’

‘Mnasema haonekani, nani, mke wako, ilikuwaje, mmmh, ndio yupo hapa, bado sijaongea naye vizuri, ndio maana nauliza kuwa kuna tatizo lolote limetokea, kwani namuona hayupo katika hali nzuri. Kwahiyo mnasema ametoweka, toka jana usiku, mbona hamkutoa taarifa huku…nini’ Akageuka kumwangalia mwanae na baadaye akatoka nje, ili aweze kuwasilina na watu wa Dar vizuri.

Akasikilza maelezo ya huko Dar, na baadaye akarejea kumwangalia mtoto wake ambaye alikuwa bado anashangaa, hakujua kabisa amefikaje pale nyumbani, hakujua kabisa amesafiri na kitu gani hadi kufika pale, alibakia ameduwaa, na kuwaangalia wazazi wake wakihangaika huku na kule, wakipiga simu na mara mama yake akaja pale alipokaa na kujaribu kumuinua ili waende ndani.

‘Mama mimi siondoki hapa mpaka nijue kimetokea nini’ mtoto akasema kwa sauti ya ukali

‘Wewe tuliza akili, hakuna baya lililotokea, ina maana hukumbuki umefikaje humu, hukumbuki ulipanda gari gani hadi hapa nyumbani..’ akauliza mama mtu

‘Mimi sikumbuki kabisa kwani ninachokumbuka ni kulala na mume wangu, lakini kusafiri hadi huku naona miujiza, au kuna wachawi wamenibeba na ungo nini..’ akwa anaongea na kuchekesha watu.

Ilichukua muda hadi wazazi kuelewa nini kimemkumba mtoto wao, na hapo wakakumbuka hostoria ya binti yao alipokuwa mdogo, alivyowasumbua na tatizo la kuota na hata kutembea usiku akiwa yupo usingizini. Hali hiyo ilishasahaulika kwani dakaitari aliyemshughulikia, alisema tatizo hilo halipo tena, na alikuwa dakitari mmoja mzungu ambaye pia alikuwa mwalimu katika hospitali ya MUHIMBILI, Alipomaliza mkataba wake alirudi kwao.

Baba mtu alitafuta simu yake katika kumbukumbu zake na alipoipata akaamua kumpigia, na simu ikapokelewa na mke wa huyo dakitari , na mke huyo alisema mume wake kasafiri kuja afrika mashariki, na huenda yupo Kenya au Tanzania, na akampa simu ya huko alipofikia.

Baba mtu akainakili ile namba kwenye karatasi na hakupoteza muda akaipiga hiyo namba aliyopewa ikapokelewa na dakitari mmoja katika hspotali kubwa ya huko Kenya, ambaye alimweleza kuwa dakitari huyo hayupo kasafiri kwenda Tanzania na huyo mtu akampa namba nyingine ya kuwasiliana na huyo dakitari, na alipomaliza kuongea pale akaipiga hiyo namba.

‘Ndio rafiki, nipo Dar na rafiki yangu mmoja, tuna kesi moja tunaishughulikia,kwahiyo labda nikiimaliza nitawsiliana nawewe’ Yule dakitari mwalimu alimwambia, lakini baba mtu alimwambia ana muhitajia kwa dharura kubwa , ambayo haihitaji kusubiri, kwahiyo afanye juu chini aje hapo Kibaha haraka!

‘Ni swala la Yule mtoto wako, kwani nakumbuka tulilimaliza kabisa, na sasa yupo wapi , nakumbuka mara ya mwisho ulinialika kwenye harusi yake, sikuweza kuja, natumai sio yeye mweney tatizo, ndiyo yeye, hapana, oh sasa wanaishi wapi?’ Maswali ya dakitari ni mengi sana

‘Alikuwa akiishi Dar, na mume wake, na cha ajabu kasafiri usiku kucha na sasa yupo hapa Kibaha, na hajui kafika vipi’ akasema baba mtu

‘My God, ….Mbona hata huyu ninayemshughulikia nimepewa taarifa kuwa katoweka naye anahitaji huduma yangu kwa haraka, oh hilo ni swala nyeti kidogo, sasa sijui nijigawe vipi. Ngoja nitawasiliana nawewe baada ya nusu saa hivi.’ Akasema dakitari, na kukata simu.

Mzee tajiri hakumuelewa Yule dakitari, yeye alitaka aje haraka na sasa anamwambia asubiri nusus saa, wapi na wapi, akaongea na mke wake wakasema wavute subira, kwani kama angekuwa Ulaya wangempata vipi, kwahiyo subira ni muhimu, ikishindikana watafute njia nyingine. Wakamwangalia mtoto wao kwa huzuni, ...

********

Je nini kitaendela baaada ya hapo. Tuwepo karibuni

Ni mimi: emu-three

3 comments :

Anonymous said...

Mmmmmmmmmmh! Haya, kwani nilipomaliza kusoma hii stori, nilijikuta nimeshusha pumzi nzito bila kujijua.

Kwa kweli wewe ni MKALI, upo JUU.

Hisia zangu kumbe zilikaribia na ukweli!?

Pia kama naona hapa huyu Dactari ndio yule mwalimu wa shemeji yake vile. Ambaye alikuwa nyumbani kwao usiku kwa ajili ya upelelezi na Inspecta pamoja na mdogo wa mumewe.

Hizo ni hisia zangu. Anyway, lete utamo M3. Nisijifanye kujua.

MUNGU ABARIKI KIPAJI CHAKO.

'YOU ARE THE WINNER'
BN

chib said...

Sasa si ungeimalizia tu leo leo tu

Jane said...

Ur the best wala huna mpinzani kwa visa, hujakosea BN nami nahisi hivyo hivyo kuwa ndo huyo huyo doctor. Mungu azidi kubaliki kazi kazi za mikono yako.