Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha
Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..
Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.
MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.
TUPO PAMOJA DAIMA
Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;
https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:
https://www.facebook.com/diaryyangu/
`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;
Wednesday, November 3, 2010
Kikulacho ki nguoni mwako(Somnambulism story) 6
Niliutizama ule upanga , halafu nikamtizama mdgo wangu ambaye alikuwa kaushikilia kwa mkono wake wa kulia, na huku nahakikisha kuwa yupo katika hali njema, isije ikawa kama mke wangu ambaye alikuwa na kisu cha kuniulia mimi. Huenda hali inayosadikika ya mashetani imeikumba nyumba nzima. Nilipohakikisha kuwa mdogo wangu hana nia mbaya nikamsogelea na kumkagua vyema. Na kasha nikalichukua lile panga na kuliweka juu ya kabati.
‘Vipi saa hizi na mapanga, mlikuwa na mipango gani na shemeji yako, manake yeye alikuwa na kisu wewe sasa una panga, usiku huu mna mipango gani pamoja…’
Mdogo wangu akacheka kidogo halafu akaelekea kwenye kochi na kukaa, akaniachia nafasi ya mimi kukaa, nilikaa huku nikiwa na wasiwasi kwani picha nzima ilikuwa hainingii akilini.
‘Kaka mimi nilimsindikiza mgeni wangu, na niliona nichukue panga kwa ajili ya ulinzi na usalama wa njiani..’ akasema mdogo wangu.
‘Ulimsindikiza mgeni wako usiku wote huu, kwanini asingelala hadi asubuhi, mnanishngaza sana, na kila siku kunakuwa na mambo ya ajabuajabu humu ndani utafikiri mimi ni mgeni kabisa wa nyumba hii’ nikasema kwa kutoamini maneno yake.
‘Ilibidi achelewe, ili kuhakiki kazi yake, tulikuwa pamoja na inspekta Kero, kama unavyojua yeye ndiye aliyekuwa akiishughulikia kesi yangu’ mdogo wangu akasema na kuniweka njia panda. Ina maana inspekta Kero alikuwepo humu nyumbani usiku bila ya mimi kujua, je alikuwa anapeleleza kitu gani tena wakati walishasema kesi hiyo haina ushahidi.
‘Kaka unamkumbuka mgeni wangu ambaye nilikuambia anatokea Ulaya, ambaye alikuwa mwalimu wangu wakati nipo Kenya, ndiye tulikuwa naye usiku pamoja na Inspekta. Wote walikuwa wakitafuta ushahidi wa kitaalamu kuhuiana na kadhia ya kujeruhiwa mimi na mtu asiyejulikana.
‘Kaka Naomba uwe mvumilivu kwa haya nitakayokuambia, kwani huenda usiyaamini au hata ukiyaamini yanaweza kukuweka katika mshituko mkubwa. Hili ni swala ambalo linahiaji busara na uvumilvu, kwani kilichogundulika ni ugonjwa na ugonjwa huo hutibika...’ akazidi kunichanganya, na sikumuelewa kuwa anaongelea nini.
‘Hebu elezea nini unachoongea kwasababu naona unaongea kimafumbomafumbo, na mimi sikuelewi, ni nani mgonjwa, na kwanini nishikwe na mshituko, kuna mtu kafa, au kuna nini kimetokea tena, maana usiku wa leo sitaushahau maishani…’ nikasema huku nikijiweka tayari kumsikiliza mdogo wangu.
Kaka mimi kama unavyojua nimekuwa nikisomea udakitari, katika Nyanja hii niliamua kusomea pia matatizo ya binadamu yanayotokana na kuchanganyikiwa. Kwa mfano kuna watu wanaumwa magonjwa ya akili, lakini sio ukichaa, bali ni matatizo yanahusiana na akili, au hata kukosa usingizi, au hata ukipata usingizi, unaweza usitulize kichwa chako. Kuna matatizo mengi yanahusiana na ubongo, likiwemo hili ambalo mimi na dakitari mwalimu wangu pamoja na inspekta tulikuwa tukilifanyia kazi.
‘Baada ya mimi kuumizwa na mtu asiyejulikana, niliamua kufanya utafiti wangu mwenyewe, kwani nilishahisi kitu Fulani kinachoendelea humu ndani. Kitu ambacho kilinijia akilini siku ile nilipoumizwa ni harufu ya manukato ambayo niliisikia kabla sijapoteza fahamu. Manukato hayo yalinipeleka kudhania kuwa mtu aliyenidhuru anapenda kuyatumia hayo manukato. Na humu ndani anayependa kuyatumia ni shemji na mdogo wake!
‘Kwahiyo nilijaribu kutafiti kuwa ni nani aliingia chumbani mwangu kati ya hawa wawili. Nilimdadisi mdogo wa shemeji nikagundua siku ile alikuwa kanywa vidonge vya usingizi kwani alikuwa na mafua, kwahiyo uwezekano wa yeye kuamuka ulikuwa mdogo, kwani akivinywa hulala sana. Lakini kwa kutokana na hili tatizo tunalolishughulikia sasa, angeweza kuamuka na kufanya hivyo bila ya yeye kujua, kwani angeweza kulifanya hilo hata akiwa usingizini.
‘Hili kaka ni tatizo ambalo mtu akiambiwa ataona ni miujiza. Wengine hukimbilia kuita watu wa namna hii wana mapepo, sio kweli. Lakini kwa uhakika tatizo hili lipo, ni tatizo ambalo mtu anakuwa amelala, lakini anainuka kitandani mwake na kufanya matendo mengine huku akiwa usingizini, na akiamuka hawezi kukumbuka na hajui kabisa kama alifanya hivyo. Na hili tatizo lipo na baya zaidi kwa uchunguzi tulioufanya kuna mtu humu ndani analo hili tatizo….’
Alipofika hapo nikamwangalia kwa macho ya uwoga, ina maana gani , kwani kwa maelezo ya mdogo wangu amemuelezea mdogo wa mke wangu, lakini mimi niliyemuona akiwa na kisu ni mke wangu. Nikawaza kuwa hayo anayoongea mdogo wangu ni mengine kabisa na lile nililoliona kwa mke wangu. Basi kama ni hivyo, hawa ndugu wawili wana matatizo, mke wangu ni muuaji wa kisirisiri na mdogo wake ana huo ugonjwa wa kutembea huku amelala.
‘Sasa kaka, mwanzoni nilipomueezea inspekta kuhusu hili na kumuomba asitisha uchunguzi wake ni baada mimi kufanya uchunguzi wangu, mwanzoni alipinga kabisa, lakini alipokuja huyu mwalimu wangu ambaye ni dakitari wa maswala haya akamthibitishia kuwa tatizo hilo lipo, na ili kuhakiki, tukaanda huu `mtego’.
Mtego huu ulitakiwa mshukiwa awe na hali itakayomfanya tatizo hili limtokee, na mara nyingi hutokea pale muhusika anaposongwa na mawazo au kuwa na hasira. Na ndivyo tulivyoweza kufanikiwa kwa hili. Tulitafuta kitu kitakachomfanya mhusika kukasirika, na kaka unakumbuka kuna tatizo lako na shemeji na mdogo wake kuhusina na ndoa . Hili tuliliona kuwa linaweza kuzaa kitu tunachokitaka, ndio maana uliniona namtetea sana shemeji na mdogo wake, kitu ambacho shemeji alikuona wewe unamsaliti. …
Kati yangu na shemeji yake, au kati yangu na mdogo wa mke wangu nikajiluliza moyoni, ana maana gani hapa, sasa ni yupi mwenye tatizo hilo ni mke wangu au ni shemeji yangu. Lakini wote walikasirika siku hiyo kuhusina na swala hilo, inawezekana mtego huo walimwekea shemeji yangu na wakamgundua kuwa ana matatzio hayo, lakini mke wangu hana hilo, bali ni muuaji…
‘ Mtego huo ulifanya kazi vizuri kabisa, kwani leo usiku, dakitari mwalimu wangu na inspekta walishuhudia kile nilichowambia siku kadhaa nyuma na wamekusanya ushahidi wa kutosha, sasa kwa vile usiku umeingia sitaweza kukuonyesha kwa uwazi zaidi, kesho tutakutana mimi na dakitari wangu na inspekta tutayazungumza kwa kirefu na kukuonyesha huo ushahidi, au unasemaje kaka.’ Akasem mdogo wangu , nilitaka kumwambia kuwa anionyeshe muda huo lakini nikakumbuka kuwa kesho anamitihani na kumweka usiku kucha ni kumharibia masomo yake.
Nikakubaliana naye kwa shingo upande. Swali likabakia nikalale wapi, na sikupenda mdogo wangu ayajue haya niliyoyaona usiku, kwani anaweza kupandisha hasira na hili nililoligundua, na huenda wakawa wanamuhisi mdogo wa mke wangu, kumbe huenda sio yeye bali aliyetaka kumuua mdogo wangu ni mke wangu, hizo zilikuwa hisia zangu baada ya kuhakikisha mwenyewe tukio zima la usiku huu!.
** ** ** ** ** ** **
Wakati haya yakiendelea huku mjini, Mzee Tajiri alikuwa akihangaika na miradi yake, siku ya leo aliamuka asubuhi sana akiwa na ratiba ya kufuatilia madeni na kuhakikisha kampuni yake inakwenda kama utaratibu ulivyo. Lakini kichwani alikuwa akiwaza mengi, likiwemo la watoto wake ambao wanaishi huko Dar, alikuwa na mpango wa kwenda kuwaona, lakini shughuli za kampuni zimekuwa zikimtinga.
Aliinua simu yake kutaka kuwauliza walinzi kuwa kupo shawari huko kazini, hii ni kawaida yake kil asubuhi anapoamuka na kabla hajaondoka kuelekea huko kazini. Na simu ikapokelewa na mlinzi mkuu, akiwambia kuwa hakuna matatizo yoyote. Akaiweka simu na mara simu nyingine ikaita. Hii ni simu ya getini kwake. Akaipokea haraka, na kumsikiliza mpigaji.
‘Unasema nani kaja, mwanangu, …’ akasikiliza halafu akaguna. Kwanini mtoto wake aje asubuhi hii toka Dar, na aliondoka saa ngapi toka huko, mbona inatia mashaka. Akawaambia walinzi wampokee na kumkaribisha ndani. Aliondoka haraka kwenye ofisi yake ndogo na kuelekea chumba cha wageni, na kule alimkuta mtoto wake akiwa kalala fofofo kwenye kochi. Akagutuka, anaumwa, mbona hana hata begi, mbona….
******************
Jamani mniwie radhi tukatishe hapa, tutaonana toleo lijalo, kwani naona muda umeyoyoma. Swali kwetu huyu ni mtoto gani aliyekuja, na mbona kaja kinamna ya ajabu, kiajabu vipi? Tuwemo katika sehemu ijayo
Ni mimi: emu-three
9 comments :
Mmmmmmmmmm! hii ni kali. sasa huyu aliyeenda kwa baba yake ofisini ni yule shemeji mtu au mke wake? Mi naona kama hawa wote wanamatatizo hayo. Na huenda kaenda huko kwa baba yake akiwa usingizini pia kama ilivyokuwa kwa mke wake.
Haya tusubiri tuone nisijifanye najua.
Tupe utamu huo tuone.
Kama ni hivyo huu ni ugonjwa wa hatari sana. Manake unafanya vitu kiasilia hii ni hatari sana.
Duuuuuh! Kazi kwelikweli.
'SALUTI'
BN
M3 wewe ni mkali-DAVIS
M3 tunga kitabu, wewe ni `Chase' wa bongo, wewe ni mtunzi mzuri na visa vyako vinavutia!
Bado natamani kukujua kiundani, kwani blog yako hujajielezea vyema. Mimi nimetuma kama anyn. Lakini wewe una kitu, una blog, kwahiyo wasomaji wako tungelipenda kukujua !
Duh, you are doing this by yourself? I should u r an amazing writer so naenda kutafuta part 1 mpaka nifike hapa, I love stories like these
Tunasubiria utamu zaidi Mkuu!
jaman wewe..hivi hizi ni hadithi au habari za kweli ?
Halafu ungekua una update kila sku jamn...mimi napenda sana kusoma hadithi/habari/mikasa
Je hizi hadithi ni za kweli, je nimetunga mwenyewe, je umefikiriaje nk.
Kwa mtuzi na mtu anayependa kutunga ni rahisi kwake kwani unaweza ukanipa kisa kidogo au nikaona tukio dogo, akilini kwangu likiwa kubwa!
Kuna matukio yanaotokea na akili ya mtu ikaingiwa na udadisi sana, kwamba ilikuwaje, `hii ilikuwaje, na kwanini ikawa hivyo' majibu yake yanakupa kisa au hadithi!
Nina visa vingi sana, na kwa kuataka visipotee nikawa naandika `diary' kumbukumbu. Mwanzoni nilikuwa naandika kwenye karatasi, baadaye kwenye computa za ofisini, lakini vyote hivyo vikawa vinapotea, hasa ukiondoka kazini, makaratasi yanaharibika!
Kwakeli nilipogundua kuwa kuna nafasi kama hii unayoweza kuhifadhi kumbukumbu hizi nilishukuru sana, na nawashukuru sana ambao wananisaidia, kuwataja hapa sio mahala pake!
Sasa je hivi visa ni vya kweli, ndio ni vya kweli, nimevipata kwa watu waliotokewa na matatizo, wakati wanaelezea matatizo yao, mimi nakwenda zaidi ya lile tatizo akilini!
Karibuni sana, na nawashukuru sana wale wote wanaojali kazi hizi, na wale wote wanaoniunga mkono kwa njia moja au nyingine.
MWENYEZI MUNGU AWABARIKI! atawabariki
mmh ..haya basi hongera sana..mimi napenda sana kusoma visa kama hivi , ...ila sasa ikiwa ni kitabu ndio inanoga zaidi..sasa kila baada 30 mins nafungua nione kama ume update...all the best
Elisa na wengineo, nashukuru kwa kuwa mpenzi wa blog hii, nashukuru sana na ningefurahi kama ungejisajili kama marafiki wa blog hapo pembeni.
Ama kwa ku-update, ikiwezekana kila baada ya masaa fulani ili ikiwezekana kisa hicho kimalizike haraka, hata mimi napenda iwe hivyo, lakini kuna swala la muda, nafasi na pia hata mimi napenda kusoma habari za wenzangu na visa vyao,sasa jinsi ya kuugawa huo muda na hata gharama inaniwia vigumu. Lakini nitajitahidi kila iwezekanavyo!
Poleni sana wapendwa na wapenzi wa blog hii, kwa kuwaweka roho juu! Tuombe mungu tu, tutakuwa tunatoa kama kitabu, ikiwezekana, na tukipata wafadhili!
Post a Comment