Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Tuesday, November 23, 2010

Haraka haraka Haina Baraka

  'Asubuhi nilishuhudia ajali ya pikipiki ikigonga baiskeli, pikipiki hii ilikuwa ni `bodaboda' kwani ilikuwa na abiria, ambaye inavyoonekana alitaka kufika kazini haraka. Alikuwa na suti yake safi na mfuko unaoashiria kuwa kabeba `laptop'.


'Bwana nahitajika ofisini haraka, na unaiona hii foleni, nasikia imeanzia TAZARA, Hadi hapa Mombasa, sasa sina insi naomba nikodi hii bodaboda yako , shilingi ngapi?' akauliza huku anapapasa mfukoni kwenye suti yake.

'Elifu tano tu Mzee mpaka mjini, ...' akasema yule mwenye pikipiki.

'Acha mzaha, elifu tano, kwani nakodi taksiii..' nitakupa elifu tatu..'

Wakabishana hapo baadaye wakaelewana na jamaa akapanda nyuma ya pikipiki. Sisi tukasubiri daldala na lilipofika tukaingia ndani angalau kwa kulipa nauli ya kugeuza nalo, ndio mwendo wa nauli za asubuhi.

Wakati tunaikaribia Tazara tukaona watu wamejazana, na kila mmoja akahisi kuwa kuna ajali!


‘Mwisho wa mwaka huo umeanza ajali kila mahala…’ akasema kondaki!

Na kwa vile kulikuwa na foleni, gari lilikuwa likienda mwendo wa harusi, kidogokidogo, na hatukujua nini hatima ya leo, kwani wengine tulitakiwa kufika ofisini saa mbili na hapo ilishagonga saa mbili kasoro dakika tano, fikiria nimeondoka nyumbani saa kumi na moja za alifajiri, mpaka saa mbili kasoro hatujavuka Tazara!

Kila mmoja alijaribu kutizama dirishani kuona nini kimetokea, na waandishi wa habari wa mdomoni wakaanza kuuza magazeti yao ya bure.

`Ilikuwaje hebu tupeni habari .

'Jamaa mmoja na suti yake kala mzinga, laptop kule yeye kule, pikipiki kule na baiskeli iliyogongwa kule na mayai trei tano yote nyang'nyang'a!....' akasema jamaa huku anaonyesha kwa vitendo, kiasi kwamba ilikuwa kama anaigiza ilivyokuwa. Sijui kuwa kama alikuwa kifurahia ile ajali au ni namna ya kuuza gazeti lake la bure kupitia mdomo wake!



Tukamkumbuka yule jamaa aliyeondoka na pikipiki akatuacha kituoni. Ndipo jamaa mmoja akasema `Ama kweli harakaharaka haina baraka’

Tukajaribu kuchungulia dirishani ili tuone ni nani wahanga wa hiyo ajali, ni kweli alikuwa yule jamaa mwenye suti ndiye aliyepata ajali, suti yake kwa sasa ilikuwa kama imetafunwa na panya. Inavyoonekana kwa mujibu wa magazeti ya bure. Pikipiki ilikuwa ikija kwa kasi kwenye barabara zao(service road), na mbele yao kulikuwa na baiskeli, sasa kukawa na gari linakatisha barabara kwa mbele yao ili kuingia kwenye barabara kuu, yulemwenye baiskeli ambaye alikuwa amebebea trei za mayai yaliyofungwa kitaalamu kwenye baiskeli yake alikuwa akija kwa kasi, na hakuwa na habari na hilo gari linalotaka kukatisha, hamadi, akafunga breki ya haraka,na kwa vile alikuwa kwenye mwendo kasi ikawa ni breki ya kuserereka . Hakuwa na wasiwasi kwa kipindi kile kwasababu alikuwa kwenye njia yao!


Baiskeli haina taa za nyuma za kuonyesha kuwa anasimama kumbe huku nyuma jamaa wa bodaboda naye anakuja wakawaka kwani kaahidiwa kuwa akimfikisha jamaaa yake kabla ya muda uliopangwa atalipwa hela yake taslimu. Jamaa Yule mwenye suti ana miadi na mteja wake ambaye wakikikutana na huyo mteja ataingiza dola elifu tano, na akichelewa atakosa zote na hasara juu! Dili ya pesa hiyo…

Hamadi !! Ajali haina kinga. Ile bodaboda ikaivaa ile baiskeli kwa nyuma, baadhi ya mayai yakaruka juu kama vipira vya ya tenesi , na uji wake ukatanda kwenye uso wa derevea wa bodaboda, baiskeli kule, mwenye baiskeli kule, dereve wa bodaboda na abiria wake chini wakawa wanaserereka na ile pikipiki wakiwa wamalala chini, na kwahiyo suti ya jamaa kwa kule kuserereka ikawa imechanikachanika kama imetafunwa na panya. Hilo ni gazeti la bure tulilolipata hapohapo, hata redio mbao zikathibitisha hayo!

Sisi tuakaendelea na foleni yetu huku magazeti mengine na radiombao zikikoleza chumvu ile habari, na pia kukazuka mazungumzo zaidi ya hayo!

‘Hapo ndio mwanzo wa kutimiziwa ahadi zetu, manake tangu uchaguzi uuishe nchi yetu imezama kwenye giza, hakuna umeme, na kama hakuna umeme kwa sisi tunaotumia visima ina maana hakuna maji…maji ya kuvuta kw kamba sasa, au ununue ya mikokoteni…maisha juu kwa kila Mtanzania!’ akasema jamaa mmoja.

`Na kweli nashangaa umeme sasa ni wa shida sijui kuwa mgawo umeanza au kuna tatizo gani tena. Kwa maeneo yetu tunaopata umeme kupitia njia ya Kisarawe tunajionea kawaida tu, ila kipindi cha uchaguzi umeme ulikuwa ni wa kumwaga, sasa kura wamepata , na ahadi wametoa, je hiyo ndio njia mojawapo ya kutimiza ahadi…’mama mmoja akasema kwa sauti!

`Jamani nchi hii ni yetu sote, mbona tunakimbilia kulaumu mapema sana, hatuoni jamaa alivyopata ajali, kwasababu ya harakaharaka aliyokuwa nayo, na sisi tukiwa na haraka haraka ya kutimiziwa hizo ahadi zilizotolewa kwenye kampeni tutaishia pabaya…tuvute subira, kwani `subira huvuta heri…wao sio Malaika kuwa watafanya miujiza…’ akasema mzee mmoja.

‘We mzee swala la Tanesco sio la leo, nimezaliwa nanimelikuta lipo, mara maji hayatoshi, mara mashine mabovu…mara…yaani ina maana hakuna utaalamu mwingine wa kupambana na hili tatizo, ina maana hawo wanaofuzu masomo yao Mlimani na wapi sijui ni wakufunzi wa vyeti tu…kwanini wasiweke umeme jua kwa dharura, ukawezeshwa kusambazwa, kwani hiyo haiwezekani, kila kitu mpaka mfadhili, mbona kuingia madarakani hawaiti wafadhili waje wawashikie nyadhifa zao, mbona kodi zetu hawaziitii wafadhili wazikusanye…’ tusidanaganyike na kuziweka kauli sehemu ambayo sio yake!’ akasema kijana mmoja kwa jaziba.

Mzee akauliza, ` Je wewe sio Mtanzania, kwanini hujasomea hiyo fani ili ufanye hiyo miujiza, kwanini uwatupie wengine mzigo wakati ni jukumu letu sote…nenda katoe huo muujiza wako, watanzania watakushukuru  sana kuliko kuwatupia wenzako lawama, …’ akasema Yule mzee!

‘Nyie endeleeni kusema harakaharaka haina Baraka mpaka mfe…subirini tu, wenzenu watoto wao wanasoma Ulaya, nyie haraharaka haina Baraka…haya ahadi mumepewaa, daini mtekelezewe , nyie mwasema tuwape muda kwani harakaharaka haina Baraka…sasa hivi giza, umeme hakuna, twasema harakaharaka haina Baraka, …sawa ndio maana tupo kwenye foleni za magari, ukienda benki foleni, hospitali foleni, na hata kufa tupo kwenye foleni, kwani sasa tunasubiri nini kama sio kusubiri kufa, maisha shida tupu,  kwasababu Tanzania hatuna haraka,…’ akasema mama mmoja na wote tukacheka!

Ni mimi: emu-three

6 comments :

Jane said...

Ha ha ha ha, sijacheka kwa mazuri but nimecheka majibizano utafikiri wako bungeni????????? Nimemiss Dar ile mbaya. pole kwa mwenye haraka yake ambaye imeishia pabaya. Nakumbuka mimi nilikuwa naamka saa kumi na kumi na moja kamili nimeshaanza safari ya kurasini kazini nikifika nafanya haraka kama kuna vipolo nimelaza vya kazi then kumi na mbili kamili nauchapa wa chap chap (nasinzia) But siku niliyoona mtu kakabwa na kushikiwa kisu huku akipekuliwa mifukoni niliapa kutowahi tena nikasema bora nichelewe na nifike salama kuliko kukutwa na hayo yanayomkuta huyo kaka. Maana hata nisingeweza kumsaidia huyo kaka kwa kuogopa. But hayo mengine ya mgao sijui wa umeme si nimesikia kuna transforma limeungua na ndo wanafanya taratibu za kuweka mpya???? any way ya ngoswe tumwachie ngoswe.

Yasinta Ngonyani said...

Aisee! hizi foleni sijui zitaisha lina maana sasa watu lazima wadamke ili waweze kuwaihi kuwajibika. Lakini sasa kama unaenda kazini na usingizi kibao kweli utafanya kazi? Tutamaini huu uongozi utaleta mabadiliko....

Unknown said...

Keep it up I always love your insha's

Anonymous said...

I enjoyed it thank you

Anonymous said...

😭😭😭

Anonymous said...

Si wewe uandike yako enye iko sawa Sana kuliko yake wewe ni🖕🖕🖕🖕🖕🖕🖕🖕🖕🖕🖕🖕🖕🖕🖕🖕🖕🖕🖕🖕🖕🖕🖕🖕🖕🖕🖕🖕🖕🖕🖕🖕🖕🖕 and a bitch you idiot