Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha
Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..
Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.
MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.
TUPO PAMOJA DAIMA
Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;
https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:
https://www.facebook.com/diaryyangu/
`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;
Tuesday, November 16, 2010
Asiye na bahati habahatishi-3
`Anameremeta, bibi harusi anameremeta ana meremeta…’ kelele za washangiliaji harusi zilimshitua yule binti aliyetoroka ndoa, na alipoamuka akawa anashangaashangaa na kugeuka huku na kule, alijikuta kalala kwenye majani, na mbaya zaidi ni kichakani. Alijiuliza amefikaje pale, na wakati anatafakari vyema, mara akasikia kitu cha ubaridi kikipita miguuni mwake, akashituka na kuangalia, mama yangu…mwili mzima ukafa ganzi, macho yakamtoka kwa woga, hakuamini alichokiona. Nyoka…!? Ndio ni nyoka, jamani nyoka! Anavyoogopa nyoka, hata kwenye picha hapendi kumungalia nyoka mara mbili…sasa leo huyu hapa, tena miguuni mwake. Alitoa macho zaidi ya pima!
Akatulia tuli, na Yule nyoka aliyekuwa kalala nusu kwenye miguu yake na nusu nyingine imejificha kwenye majani, alipoona kuna mtikisiko na joto lisilo la kawaida akaanza kujiondoa taratibu kuzama kwenye majani, na hali hii ilimfanya binti wa watu asisimukwe na mwili mzima, jinsi mdudu huyo alivyokuwa akipita kwenye miguu yake kutokomea majanini. Chichichi…Na alipomalizika na kutoweka, Yule binti akakurupuka kama mtu aliyeambiwa haya kimbia, katika mbio za masafa mafupi.
Aliupita ule msafara wa harusi, akigongaa na watu ambao walikuwa hamjali, kwni kila mmoja alikuwa na shauku ya kumuona bwana bna bibi harusi. Binti huyu hakujali, akwa anaendelea kupigana vikumbo na watu huku akikimbilia nyumbani kwao, bila hata kujali ni ni nani anayeolewa hadi alipofika kwao na kukimbilia chumbani kwake. Alikpakuta pakiwa kimya, kwani watu walishafuata msafara wa harusi na waliobakia na akina mama wasee wawili
‘Huyo aliyerudi si ndio Yule binti aliyetoroka kufunga ndoa…’ mama mmoja akauliza
‘Achana naye , atakuja kujuta, lakini hakijaharibika kitu kama kakataa yeye dada yake kakubali, mwenye hasara ni nani, kama sio yeye, anafikiri bahati ya kuolewa ipo tu wakati wote…’ akasema mama mwingine.
Kwa kusikia manno yale fahamu zikamrejea kidogokidogo, na kuanza kukumbuka, kuwa kumbe yeye katoroka kuolewa, i, akaanza kuhangaika huu na kule kulitafuta gaun lake la harusi, ina maana leo yeye alitakiwa kuolewa, je ina maana harusi imeshapita, ina maana yeye kakataa kuolewa, mbona hakumbuki kufanya hivyo. Akainuka kwa haraka na kwenda chumbani kwa shangazi yake akakuta hakuna kitu. Jamani ina maana ….
Wakati anawaza haya msafara wa harusi ulishafika barabara kuu, bwana na bibi harusi wakaagana na wasindikizaji na wao wakaingia ndani ya magari yao. Waliagana kwa mara ya mwisho , wakaondoka na magari yao. Wakiwa ndani ya gari, Bwana harusi alimwangalia mke wake, na kusema moyoni, ingawaje siye chaguo langu, lakini ameniokoa katika sehemu muhimu sana. Akajaribu kukisia ni nini kilichomfanya mchumba wake wa awali amkatae tena siku ya ndoa akakosa jibu. Akasema moyoni, kama kafanya hivyo makusudi atajuta kunikataa…
Kumbukumbu ya tukio zima ilizizima kichwani mwake kama mchezo wa kuigiza. Alikumbuka jinsi walivyotoka nyumbani kueleka kwa bibi harusi mratajiwa akiwa na shauku ya kumuona binti alyempena sana, nai walipofika na msafara wao nyumbani kwa bibi harusi walikuwa watu wanawasubiri kwa hamu, na vifijo vikatawala, wakakaribishwa sehemu ya kufungia ndoa, na baada ya masaa kadhaa wakaona kimya, wakaulizia vipi mbona muda unakwenda na hawaoni chochote kikifanyika, wakaambiwa wasubiri, baadaye bwana harusi alimtuma mshenga wake ajue nini kinachoendelea.
Wakati amekaa, na mkao wake ulielekea dirishani, kwa mbali akamuona binti anatoka kwenye nyumba mojawapo na kukimbilia vichakani, moyo wake ukamdunda.
‘Yule siye bibi harusi mtarajiwa kweli, anakwenda wapi porini, lakini labda sio yeye huenda ni dada yake, akajipa moyo. Lakini mbona kuna kucheleweshwa kusikokuwa kwa kawaida kuna nini kimetokea akajiuliza bila jibu. Baadaye wakaja watu kumuelezea kuwa kumetokea tatizo kwani bibi harusi katoroka, na haijulikani wapi alipo.
‘Kwanini atoroke wakati jana tuliongea naye vizuri na kukubaliana vyema, …kumetokea nini..’ akauliza lakini hapakupatikana jibu. Baadaye shangazi wa bibi harusi akaja na wazo kuwa kama yupo tayari atayarishwe dada yake ambaye ndiye aliyechaguliwa kuolewa na yeye mwanzoni, ili gharama na muda wake usipotee bure. Akawaza sana, lakini baadaye alikubali .
Alimuwaza huyu dada mtu jinsi siku ile alivyomtolea ne kuwa anamtaka mdogo wake badala yay eye. Kauli hiyo aliitoa kesho yake baada ya kugundua kuwa Yule binti alyemuona njiani ni mdogo wa mke matarjiwa aliyechaguliwa na wazazi wake. Yeye aliporudi nyumbani akawaambia wazazi wake kitu alichogundua . Wazazi wake walimwambia kiutaratibu, haitawezekana kwasababu dada mtu yupo hajaolewa, na dada mtu ndiye aliyekomaa na umri wake unaruhusu.
‘Hata mimi nitamuoa mdogo mtu , huyo dada mtu atapata mtu mwingine’ jamaa alitoa kauli yake ya mwisho. Wazazi wake wakakutana na kutuma ujumbe tena kwa maharusi, na kule baada ya mvutano wakakubali, kazi ikawa kumshawishi dada mtu akubali matokea, na hapo kukaanza uhasama kati ya dada mtu na mdogo mtu.
‘Najua tu mdogo wangu kafanya mpango akamshawishi mchumba wangu ili amchukue yeye, lakini sidhani kama atafanikiwa…’ akasema na kuondoka kwenda kijiji cha jirani kwandugu yao mwingine, kwa ushauri aliopewa ili asikae pale na kuleta mgongano. Alirejea siku ya harusi ya mdogo wake, na kumbe ndio bahati yake ilimuita aje.
Watu waliosindikiza harusi wakawa wanarudi na hatimaye shngazi mtu akaja, na kukutana na bibi harusi aliyetoroka. Shangazi mtu hakutaka hata kuongea naye, lakini kwa kumpa matumaiani alimuita na kukaa naye chumbani kwake.
‘Hebi niambie una matatizo gani mwanangu?’ akamuuliza kwa upole
‘Shangazi hata mimi sijui, kwasababu mimi sikumbuki kugoma kufunga ndoa, ila…mungu lile joka…oooh, sitaki hata kukumbuka..’ akasema huku naficha macho
‘Joka gani hilo, mbona unanipa wasiwasi, hivi akili yako imetulia kweli…’ shangazi mtu akamwngalia Yule binti kwa wasiwasi na akilini mwake akasema, `huyu mtoto ana matatizo inabidi aongee na wazazi wake waaribu kumtafutia `wataalamu’ akabadilisha maongezi ili kuvuta muda lakini kila alivyokuwa akiongea, alijikuta anaongea peke yake kwani mwenzake ailikuwa kadidimia kwenye lindi la mawazo. Hivi ina maana harusi imenikosa, hivi ina maana ndio basi tena, dada ndiyo kaolewa badala ya mimi….lakini kwa nini dada alisema athakikisha siolewi…lazima nitamuuliza mama!
Usiku ndoto za ajabu zilimuandama binti aliyekataa kuolewa, na ilipofika asubuhi na mapema akazindukana kama mtu aliyeshitulia na kitu, akatazama huku na huko, baadaye akainuka haraka na kuvaa nguo za kutokea, na bila kujua nini anachokifanya akaelekea nje. Huko nje, kulikuwa ukimya wa asubuhi, ndege na jogoo kuwika ndicho kilichoashiria siku mpya, kutokana na kibaridi watu wengi walikuwa bado vitandani. Yeye hakuliona hilo, akaongoza njia kuelekea asikokujua.
Alitembea hadi alipofika eneo la vichakani, huku mawazo yakimtuma kwenda mbele , lakini hapo kichakani akawa anapita kwa tahadhari. Sijui kwanini alifanya hivyo, labda sababui ya umande au kuogopa wadudu, ila kwa muda ule hata wadudu wengi hawana nguvu, lakini mara akasikia mchakato-mchakato kama kitu kinatembea na kuvunja vunja vinyasi vidogovidogo, akakumbuka kitu Fulani, ndio alikumbuka nyoka. Mwili ukazizima na nywele kusimama. Kwa kumbukumbu za mbali hapa aliwahi kuona nyoka, lakini hakumbuki lini, mungu wangu nimefuata nini huku! Akajiuliza akilini, lakini miguu ilikuwa ikichapa mwendo!
`Ndio nafuatilia mume wangu…’,akasema kwa sauti. `Sikubali kwanini dada yangu amchukue mume wangu, nitawafuata mpaka niwakute kabla hawajatokomea huku waendapo…’ akasema kama mtu anayeongea na mwenzake! Akaaanza kukimbia, alikimbia kwa mawili, la kuogopa nyoka, na pili la kuharakisha eti atalikuta gari lilomchukua bwana na bibi harusi. Akakimbia kama mwehu, na hata wanyama kama paka au mbwa aliokutana nao asubuhi ile walikimbia wakijua wanafukuzwa wao!.
Alikimbia mpaka miguu ikawa haina nguvu tena na mwili wote ukaloana jasho, na pale alipochoka kabisa akadondoka chini, akainuka na kujizoazoa tena, huku akili ikimwambia nyoka anakuja nyuma yake, nyingine ikimwambia kimbia haraka gari lilimbeba mume wake lipo karibuni! Akakimbia, akakimbia… ingawaje kila hatua mwendo ulikuwa ukipungua kidogokidogo, lakini hakukuta tamaa.
Jua lilishaanza kutoka, lakini yeye hakuliona, akilini mwake ni mambo mawili, nyoka anakuja nyuma, mbele analikimbilia gari, na hatimaye alipochoka kabisa akaanza kutembea kwa mwendo wa harakaharaka, huku anaimba nyimbo za harusi, nyimbo za kitoto, na hata nyimbo za maaskari wakiwa kambini, ilimradi asichoke. Saa tano, bado anatemba, saa sita bado anatembea, saa saba, akawa hoi, na Bahati nzuri akawa kafika kwenye mto, akaona bora ajimwagie maji na kunywa kidogo huku akitazama huku na huko kama ataona tunda au chochote cha kuweka tumboni.
Mbele yake kulikuwa na shamba dogo lenye mapapai na matunda kadhaa, akasema atachuma moja ale, lakini moyoni akakumbuka kuwa kuchukua kitu cha mtu bila ridhaa yake ni kosa, ataitwa mwizi, lakini afanyeje afe na njaa. Kaona papai moja liloiva likiwa chinichini akalichuma na kukaa karibu na mto alilila lile papai kama kima, akajisikia nafuu. Akanywa maji, na kujimwagia mengine, akaamua kuoga kabisa, wakati akiwa anaoga mara akasikia mchakato nyuma yake, akangalia lakini hakuona kitu, ila hisia zake zilimtuma kuwa kuna mtu anamchungulia. Akaziendea nguo zake haraka akazivaa, na wakati anavaa akaona kwenye maji kitu kikiibuka na kuzama….mamba.
Alikumbuka hadithi za bibi yake kuwa masafa ya mbali kwa wachungaji wa ngombe kuna mito yenye mamba, ambao asili yake ni wa kufugwa na wachawi, kama wakitaka kumdhuru mtu hutumiwa hao mamba, Hasa watu wanapokuwa wanaoga, au wakilisha mifugo yao. Akaona hapo hapafai, akatembea hadi mbali kidogo na ule mto kwenye mti mkubwa uliojitanda kama mwavuli akakaa kwenye shina lake, huku akihisi kuna mtu anamwangalia au kumfuatilia, lakini hakuona wapi mtu huyo alipo.
Kutokana na uchomvu mwingi alipojiegemeza tu kwenye ule mti, mara usingizi ukamchukua akalala fofo. Hakujua amelala muda gani, lakini alihisi harufu, au joto au moto upo karibu yake, na alipofumbua macho akajikuta yupo kwenye kitanda kilichotengenezwa kwa ngozi ya ngombe, na mbele yake upo moto na nyama ya mbuzi imebanikwa. Na mara akaona kitu kama kivuii kikitembea kwa mbele ya ule moto, kwasababu ya giza hakuona vizuri ni kitu gani.
Akainua kichwa kungalia yupo wapi na je amefikaje pale, akakumbuka mamba, akaumbuka kulala kwenye shina la mti, lakini sasa pale yupo wapi na kafikaje. Wakati anawaza hilo mara kile kivuli kikaonekana wazi. Mungu wangu, ni mtu au mnyama. Mama yangu upo wapi… Akainua uso kuangalia vyema, akaona ni mtu kava ngozi ya wanyama, …
Alikuwa pandikizi la mtu , sura kidogo ya kutisha, labda kwasababu ya ile midevu iliyoisokotasokota, hajawahi kukutana na mtu wa aina hii kabla, meno yake yalikuwa na rangirangi. Mtu Yule wa jabu alikuwa na kazi ya kugeuza geuza ile nyama, na mara nyingi alikuwa akitupa jicho pale kwenye kitanda, na alipoona namwangalia akatabasamu na kuonyesha meno yake ya rangi rangi, aliinuka na kungalia tena pale kwenye kitanda, akatabasamu na kuguna, mguno wake ulikuwa kama ngurumo ya paka linaponguruma,akainuka pale lilipokuwa na kukatakakata vipande vya nyama na kuviweka kwenye kitu kama sahanai halafu akamsogelea Yule binti pale kitandani na kuiweka ile sahani mbele ya binti wa watu, akamuonyeshea ishara ya kula, …..sijui wanaongea lugha gani hawa watu!
Njaa ilikuwepo, na hamu ya kuila ile nyama ilikuwepo, lakini woga ulitawala mwili mzima, hawa ndio wale wafugaji wa milimani, watu wanoogopewa kama simba, na wanaitwa watu-wala-watu. Wengine wanasema wanaiba wanawali wakiwa visimani na kuwaficha kwenye mapango yao na kuwafanya wake zao, na ukibisha unakuwa kitoweo chao. Inasadikiwa kila mara wasichana maneno yanayouzunguka huo msitu wanapotea wasichana na inasadikiwa kuwa wanaibiwa na hawa watu wa milimani. Wakishawaiba. Huwabaka na hatimaye kuwazalisha Watoto, na ndio maana vizazi hivyo vimekuwa vikiongezeka.
Binti mtoro wa ndoa akaanza kulia, na kumuomba mungu, alijuta kwanini kafanya kosa lile, kwanini alikataa kuolewa, kwanini, ikawa kwanini, lakini hakuweza kujua jinsi ganai ataokoka na janga lile. Akaingalia ile nyama, hamu ya kuila ikamjia, kaoana ni heri ale asija akafa na njaa, na ili apate nguvu za kutoroka . Akaanza kipande kidogo, akaona tamu, akaongeza, kingina, na kingine, na kingine mapak shanai ikawa nyeupe, akajisikia kushiba, ….mara akasikia unywele ukimsimama. Alihisi woga, na woga ule ulimuashiria hatari. Akawaza, sasa ana nguvu, cha muhimu haina haja ya kuangalia nyuma, na kukurupuka hapi kitandani na kukimbia kama mwehu.
Akahesabu moja, mbili tatu….
Ni mimi: emu-three
6 comments :
Huyu dada nafikiri alipigwa kipapai na dada yake, unajua mambo ya ndoa haya yanaweza yakawakosanisha mtu na ndugu yake toka nitoke!
Eee mwenyezi mungu mnusuru na hatari yoyote iliyo mbele yake, yaani tangu mwanzo wa story ya leo mpaka mwisho mwili wangu unanisisimka. Inatisha kweli. Keep it up M3,but sijafanikiwa kuwa member nikiclik hakuna kitu kinacho tokea sasa sijui kama kuna icon nyingine hazitokei kwa computer yangu au nini hasa.
Unachotakiwa ukitaka kujisajili kama `rafiki' wa blog hii ni kubofya `icon' yenye maneno mbele yake FOLLOW.
Labda computer yako wameweka kizuizi, kama ni hivyo unaweza kujaribu computer nyingine au office nyingine au internet cafe!
Nashukuru sana kwa kupenda na kuwa `mdau' muhimu wa blog hii!
Mmmmmmmmmmh!!!!!!!! m3. Mbona unazidi kunitia woga?!!!!! Mungu amuokoe na jaga hili huyu binti wa watu, ni nini tena, Mungu wangu?
Haya lete huo utamu.
Kwa kweli wewe una KIPAJI mno.
Siwezi sema zaidi. UBARIKIWE.
BN
haya mimi nasubiri kinachoendelea..maana sina hata la kusema
Msiwe na wasiwasi tupo pamoja, ila nawaomba muwe wavumilivu, na muondoe woga, na nitajitahidi nisivuke maadili, kwani kuna sehemu kama ningeileta kama ilivyo...mmmh
Karibuni sana!
Post a Comment