Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha
Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..
Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.
MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.
TUPO PAMOJA DAIMA
Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;
https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:
https://www.facebook.com/diaryyangu/
`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;
Monday, November 29, 2010
Aisifuye mvua imemnyea-1
Maua mke wa docta, kama tumjuavyo, aligutuka toka usingizini, moyo wake ukawa unamwenda mbio sana, na alipoangalia kitandani , akakuta mumewe hayupo, oooh, akakumbuka ugomvi wake na mume wake jana usiku, uliosababisha wote kulala na nguo mzungu wa nne. Akajisikia vibaya sana, alijiona yeye ndiye mkosaji, amekuwa mtu wa kudai, na hata lile lisislowezekana. Lakini kwanini, mbona hali hii haikuwepo kabla, mbona haya yameanza pindi walipohamia kwenye nyumba hii mpya. Akamuomba mungu amusamehe na amsaidie wkuwe na mapenzi ya amani na mume wake kama zamani.
Alijiinua pale kitandani akapangusha macho na kutazama huku na kule, akakumbuka ile milio ya mapaka usiku, mara bundi, mara sauti za ajabu-ajabu. Hii imekuwa kawaida ya tangu wahamie hapa, lakini yeye alikazania ibada na kutokutilia manani, akijua ni mazingira ya ugenini, lazima uyazoee. Kweli tangu wahamie nyumba ile hamna raha, nyumba nzuri, manthari mazuri, lakini hakuna amani, hakuna upendo, …akatingisha kichwa, na kujiinua pale kitandani, huku akisema kimoyomoyo ni heri wakaishi nyumba ya kupanga kuliko nyumba nzuri isiyo na raha.
‘Nyumba mkae kwa amani, sasa kuna raha gani, hapa, hakuna amani…aaah, sijui huyu naye kaenda wapi masikini mume wangu…’ akasema kwa sauti huku akijinyosha.
Alipoangalia mlangoni, akakuta mlango wa chumba upo nusu wazi, akajiinua kwa shida huku mwili ukilalamika kwa maumivu ya hapa na pale, akijua kuwa mume wake hayupo mbali, mara nyingi hupenda kujipumzisha kwenye makitaba, hasa anapokuwa na kazi zake au akiwa hataki kuongea na mtu. Akaonia aende kwamngalia huko.
Ilikuwa bado kigiza na sauti za ndege wakishangilia ujioo wa mchana zilisikika, na wengi wa wanadamu walikuwa bado kitandani, wengine wakimalizia ndoto zao za usiku. Wapo ambao usiku ulikuwa kama jela, walitamani kuche ili wakajiliwaze na mwanga wa mchana, na wengine wakaikimbize shilingi ambayo haishikiki. Wapo wale wasiotamani usiku uuishe kwani raha zake zilikuwa kama kulamaba asali, na ukilamba asali watamani urudie tena na tena, lakini hauchi hauchi kutakucha tu!
Akaufungua mlango wa chumba na kuurudishia vizuri, huku akipapasa ukutani kuwasha taa ya sebuleni, mara, …oh akashika kitu chenye manyoya, akaurudisha mkono haraka,…mungu wangu nimeshika dubwana gani, akitafakari, ni kitu gani, manyoya kama ya paka, na paka angekaaje ukutani vile. Akaona kwa vile kuna mwanga kidogo, hakuna haja ya kuwasha taa, ngoja aelekee huko makitaba hivyohivyo.
Hatua ya kwanza ya pili ya tatu…akasikia sauti ya kitu kikitembea juu ya bati. Ndi, ndi ndi… Ni mlio mkubwa kama vile mtu anatembea juu, lakini iweje asubuhu kama hii,, ni mwwizi au ni nani…hali hii ikamtia wasiwasi. Mara nyingi usiku akishaomba, hulala kama gogo, hajasumbuliwa na mawangamawanga haya, lakini mume wake humwambia kuwa usiku kuna mambo hayo ya ajabu! Yee hupuuzia kwani usingizi kwake ni muhimu kuliko kitu chochote hasa ikiingia saa tatu !
Akasema hayo kama yapo hayamtishi, akapuuza, na kuharakisha kuufikia mlango wa makitaba, na mara sauti ya ajabi ikasikika, kama paka akilia mlio wa jabu akahisi nywele zikizizima. Paka? Au ndio Yule aliyemshika ukutani, hawa wadudu wanafuta nini humu ndani, na mara nyingi wanahakikisha kuwa wamefunga milango sehemu zote, na nyumba ile ilivyo, paka hawezikupenya labda awe aliingia mapema kabla hawajafunga milango!
Akatamani mume wake angekuwa karibu yake ili waongee,…sasa kenda wapi? Akajiuliza na kukosa amani, Akakumbuka jana walivyogombana, kisa kidogo tu, yeye alitaka waende kwenye harusi ya jamaa yao mikoani, lakini mue wake akasema hana nafasi. Ikawa mzozo, mke anataka mume hataki.
‘Basi bwana kama hutaki nitaenda na rafiki zangu,maana wewe hupendi kushirikiana na wenzako, wajifanya mzungu…hapa ni bongo, uzungu wako utakufanya utengwe na jamii..’ mkewe akasema kwa hasira. Lakini mumewe hakujali , kwani wakati mkewe anayasema hayo yeye alishazama kwenye lindi la mawazo, mawazo ya adha za usiku, kwanini hakuna amani katika nyumba ile, kwanini, nyumba mpya kama ile iwe na vituko usiku, akawaza bila kupata jibu.
Mkewe akasusa hata kula na kukimbilia kitandani, na kumuacha mumewe akila peke yake mezani. Huu ugomvi sio wa leo tu, kila mara inakuwa visa, ina maana upendo umepungua mle ndani siku hizi, kwanini mume wake hamsikilizi siku hizi, zamani ilikuwa akiomba chochote hupewa, leo kila kitu mpaka kiwe katika mpangilia wa gharama eti bajeti, ..bajeti hiyo imeanza siku hizi! Ina maana pesa hazitoshi, au mume wake ana nyumba ndogo siku hizi. Lazima afanye uchunguzi akasema kichwani na kujifunika gubi gubi huku akijua kalala kinyume na wanavyolala, mzungu wa nne, akiwa na maana hataki mume wake akija amsumbue.
Siku hiyo hakukumbuka kabisa kumuomba mungu, na kwa vile alichoka sana kutokana na shughuli ya jamaa yao waliyokuwa wamekwenda kwa shingo upande na mumewe . Walialikwa siku nyingi, na siku ilipofika mume wake akasema anakazi nyingi za ofisini, na ana maswala ya kuwakilsha kwa wakubwa zake ana mambo ya kitaalamu anatakiwa kuyachunguza kwa aili ya wagonjwa…mambo mengi, ambayo kwake hayakumuingia akilini.
‘Sema unaenda au huendi, kama huendi simu hii hapa wapigie mwenyewe kuwa hutaenda, mimi nimechoka kujitenga na wenzangu’ akasema huku anamshikisha simu. Mume mtu akatafakari akaona ngoja tu aende na mkewe. Walipofika huku ikawa ni shughuli ya siku nzima. Na akajitahidi kujishirikisha lakini ilikuwa hali ngumu sana kwake, alikuwa kupoteza muda ambpo kwake ulikuwa na thamani sana! Na waliporudi mume akawa hana raha, kwani hapendi siku nzima ipotee kama hivyo, na tena mkewe anadai waende kwenye shughuli nyingine mikoani. Hapo akawa hataki hata kusikiliza!
Mke mtu alipogundua kuwa jana hakuomba, akafikiria ni vyema angalau achukue dakika chache za kuomba na kumshukuru mungu kwa kuumaliza usiku salama na … …akasema haina haja, hii ni alfajiri, kama ni wanga, kama ni maaajabu gani, muda wao umeshapita, sasa ni muda wa walio hai.
Wakati anawaza hili, mara kitu kama paka toka juu, likawa linakuja kumdondokea kichwani, alipiga yowe, na kudondoka chini, na katika kudondoka kule kichwa, kwa ghafla kichwa kikagonga kwenye mlango kwa mbamizo mkubwa, na kuhisi maumivu makali. Na kutokana na uzito wake na mbamizo ule mlango wa makitaba ukafunguka kwa nguvu. Na kujikuta nusu ya mwili upo varandani na nusu umelalia ndani ya makitaba…akajaribu kuinua kichwa…maumivu…akaguna.
Akajaribu tena kuinua kichwa bila mafanikio, akahisi hali sio nzuri, akaona heri ageuze kichwa angalau aangalie kuwa mume wake yumo humo ndani, na kama yumo, ina maana hakusikia hicho kishindo. Ina maana mume wake kamkasirikia kiasi hicho, na hakutaka hata kujua nini kimetokea kwake. Alikumbuka kuwa mume wake akiwa kwenye mambo yake ayaitayo ya uchunguzi aunaweza ukaingia hata bila yay eye kujua. Anakuwa kama hauypo, na mara nyingi keshasema akiwa humo hataki usumbufu. Sasa huenda leo yupo kwenye uchunguzi wake na hataki usumbufu. Lakini kishindo cha kudondoka kwake ni kikubwa hata nani angesikia na kuja kutoa msaada.
Akajarbu kutoa sauti ya kuita, lakini koo lilikuwa kavu, akajaribu kufunua mdomo , lakini mdomo ulikuwa mzito. Akaanza kuogopa. Ina maana ndio nakufa. Hapana, kugonga kichwa huku ndio kunimalize , ndio kuniuue, hapana…ngoja nimuite mume wangu, ni dakitari ataniokoa. Mbona siwezi kufunua mdomo, mbona sauti haitoki.
Akakumbuka kumuomba mungu, oh, nilishau kabisa kuwa katika hali kama hii anayeweza kuombwa ni mungu na huyu atanisaidia. Akafumba macho na kuanza kuomba. Na wakati anaomba, akasikia kitu masikioni kikilia nziiiiiiiiiiiiiiiiiiiii! Kama vile sikioni uliingiwa na maji na sasa yale maji yakatoka, kuna hali kama wingi wa sauti huingia kwa kishindo, ndivyo alivyosikia. Na akaanza kuhisi nafuu, lakini hali haikuwa njema, akainua kichwa kwa nguvu.
‘Mamama..maumivu, kweli kichwa kimeumia, maumivu ni makali… ‘ akasema na kugeuza kichwa upende wa pili, na kwa mbali akawa anaona taswira. Ile pale ni meza anapokaa mume wake lakini hayupo, akageuza upende wa pili…kile pale ni kiti cha kukalia, kuna mtu kakisimamia juu, anachukaona kua nini kuu ya dari. Akajaribu kuinuakichwa kwa shida, na macho yakawa yanaingia ukungu…kamba imetokea juu, na huyu mtu aliyesimama kaishikilia, anataka kufanya nini na ile kamba?
Akaona Yule mtu akiifungua kitu kama kitanzie kwenye kamba...ndio kama kitanzi, akakipanua kile kitanzi, ana…ana..akawa haoni vizuri, lakini kwa kumbukumbu ina maana Yule mtu…giza likwa litanda usoni kwakasi, akajitahidi kulizuia...akajitahidi angalau aone vizuri!
‘Nini unataka kufanya Yule, mtu, sio mume wake kweli Yule, sura haionekani vyema…’ akajitahidi kufunua macho kwa nguvu na ..na akaona kitu cha ajabu kabisa. Akaomba mungu, amsaidie aone nini na ni nani yule.. na huku anajitahidi kutoa sauti kwa nguvu…….
Ni mimi: emu-three
4 comments :
haya sasa..kazi imeanza..jitahidi basi uwe na update kila siku .
Kwa hyo itakua ni bandika bandua, ikiisha moja inaanza nyingine ?
asante kwa kutujali.
Kweli Elisa kazi imeanza tena kwa kishindo, alivyogusa ukutani na kugusa kitu nilihisi mimi ndo mwili unanisisimka. Du! maskini Mr & Mrs Doctor wamehamia sehemu ambayo si nxuri, but yote yashindwe kwa kwa uwezo wake mungu. Sali kimya kimya mama hata usipotoa sauti mungu anakusikia. Hongera kwa visa M3 Mungu akupe afya njema ili tupate mengi toka kwako
Umeanza kuniogofya mapema hivyo...mmmh,natamani nisikie kitakachofuata, aliona nini huyu mke wa doctor?
Nimekuwa jacri cogopi tena hata ucku nitasoma lete uhondo M3 mzee wa kujificha jina lako!!!
Post a Comment