Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Monday, October 25, 2010

Utangulizi wa kisa kipya

Huyu mtu kwenye picha  hapa kainuka toka kitandani akiwa ndani ya usingizi na anatoka nje sijui anaelekea wapi na je huko anakokwenda kuna usalama, hawezi kugongwa na magari, au kuwazuru watu...huyu ana tatizo liitwalo somnambulism
kisa kinachokuja kitakupa kidogo yaliyomsibu jamaa, ...kisu kilishashushwa kuthamiria kuelekea ndani ya moyo wake , sijui ni mkewe kipenzi, au shemeji yake, au mdogo wake...jamani haya yapo, ........................................
 Kuna usemi usemao ukistaajabu ya Mussa utayaona ya Frauni. Ama kweli tembea uone na kutana na watu ujue na kusikia mengi. Misemo hii ilinijia kichwani pale nilipokutana na jamaa yangu mmoja ambaye baada ya kusalimiana naye akanipa kisa cha kusikitisha kidogo. Kabla sijaingia ndani ya kisa hiki, nimeona niweke utangulizi wa kuvuta hisia zako, ili tuwe pamoja.


Katika maswala la magonjwa ya akili, ni mara chache watu kugusia au kusikia wakielezea kuwa ugonjwa uitwao kitaalamu `SOMNAMBULISM’ nii ugonjwa wa akili, mimi nauona kama ni moja ya magonjwa ya akili, kwasababu matendo yake ynaendana na mapumbao ya akili. Ili kusadikisha hili nikadadavua kwenye mitandao ili labda ninaweza kukutana na maelezo yanayoelezea angalau kwa ufupi nini maana ya tatizo hili, nikakutana na mtandao huu! http://english.pravda.ru/science/tech/30-12-2005/9462-somnambulism-0/,
Kwa kweli mitando haina uchoyo ikaelezea kwa kile nilichotaka kuhakiki.

Wanasema ugonjwa huu hutokana na mtu kuwa usingizini akafanya matendo kwa vitendo akiwa ndani ya usingizini . Usichanganye na kuota ndoto. Hapana, mtu mwenye tatizo hili hutoka kitandani akiwa bado ndani ya usingizi akafanya matendo kama vile yupo macho, bila yaya yeye kujua, kwani akiamuka hawezi kukumbuka kuwa alifanya hayo matendo! Huu sio uchawi jamani, kwani wengine walidiriki kusema bibi huyu wa hiki kisa alilogwa, kwahiyo alikuwa akifanya kwa hisia za kichawi! Anatumiwa na wachawi...hapana wataalmu walithibitisha kuwa ni ugonjwa!

Hebu jaribu kureea kwenye Wikipedia : http://en.wikipedia.org/wiki/Sleepwalking itakupa maelzo ya ziada na zaidi ya hayo.

Kwanini nimetanguliza maelezo haya kabla ya kisa chenyewe, ni kwasababu wengi unapotoa visa wanajaribu kujiuliza, hivi kisa hiki ni cha kweli? Na wengine hudiriki kuuliza je umewahi kukutana au umepata wapi vitu kama hiyo. Na kuishia kusema ni `visa vyako tu' Kwakweli jamii ina mambo mengi na kama utajaliwa kuingia ndani ya majumba ya watu ukasikia mikasa na matatizo yanayowasibu kila mtu utashangaa. Jamani yapo magonjwa ya ajabu, kwani hili nalo ni ugonjwa na unawapata watu wengi .

Ugonjwa kama mapepo au wengine huuita mashetani upo sana na watu watanisadikisha nikisema siku hizi kwenye jiji hili au mikoani matatizo haya yanazidi sana, sijui kwanini? Na wengi wa wahanga ni wanawake, sijui kwanini? Namshukuru rafiki yangu kukubali nikiweke hiki kisa ili kusadikisha kuwa ugonjwa huu upo na unatibika, ila inategemea na chanzo chake kwani kuna magonjwa ya kurithi, kuna magonjwa yanatokea tu sababu ya madawa, sasa hili ni mojawapo ya gonjwa lenye utata huo.
 Labda tukione kisa chenyewe ili katika kuchangiana tutasaidiana mengi. Karibuni kwenye kisa hicho `kikulacho kinguoni mwako'

 http://en.wikipedia.org/wiki/Sleepwalking


Ni mimi: emu-three

6 comments :

Anonymous said...

Hii hatari, hivi kweli ugonjwa huu upo? Mhhh, nakingoja hiki kisa kwa hamu, lakini ninaogopa, manake huwezi jua kuwa unaolewa au kuoa, kumbe mwenzako ana tatizo hilo....tutaogopa kuingia ndoani!
Lakini magonjwa yapo mengi, kuna kifafa, mashetani nk, yote hayo ni taabu kwelikweli,na hakuna aliyeomba ayapate, je asioe, je asiolewe? Kazi kwelikweli...

Anonymous said...

Kama ni mashetani yashindwa kwa jina la Yesu....eeeh, yashindwe ....kabisa!

Anonymous said...

Don't hit around the bush, lete vitu, twanganya humu ndani tusome...hatutaki kusubirishwa, twataka tuone kweli alifanyaje?
Aaah, leo nina munkari wa kisa kipya, lmbwata limekweisha, sasa, nini tena, kisa kipya, kinahusu nini vile?

Anonymous said...

Mimi natoka nje ya mada kidogo, nauliza samahani, hivi wewe M3 ni nani? Ni mwanamke au mwanaume, kwani nimejaribu kutafuta kwenye maeleo yako, hujaandika? Ningefurahi kukujua kama hutojali!

Anonymous said...

Uliyetaka kumjua M3, mbona hata wewe mwenyewe hujajitambulisha, ni vyema ukajiweka wazi mwenyewe ili na huyo M3 awe wazi kwako, au nimekosea wenzangu. Hata mimi ningependa kumjua, lakini lazima tuwe wakweli sote!

Yasinta Ngonyani said...

Kwa kweli hii ni hatari haswaaaa! Magonjwa mengine kaazi kwelikweli jamani.