Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha
Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..
Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.
MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.
TUPO PAMOJA DAIMA
Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;
https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:
https://www.facebook.com/diaryyangu/
`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;
Wednesday, October 27, 2010
Kikulacho ki nguoni mwako(Somnambulism story) 1
Niliwageukia askari wa upelelezi , ambao walikuwa wakipima huku na kule bila kuelewa ni nini wanachokifanya badala ya kumuwahisha mdogo wangu hospitali huenda akapona. Nikainama chini kwa huzuni, na baadaye hawa polisi walimaliza kazi zao, na kiongozi wao aliniita pembeni na kuniuliza maswali kadhaa, alitaka kujua kama mdogo wangu alikuwa na maadui wowote, na kutaka kujua marafiki zake waliokuwa wakija mara kwa mara hapo nyumbani ni nani….
Nikawaza sana kukumbuka marafiki zake lakini sikumkumbuka hata mmoja aliyekuwa akipenda kuja nyumbani mara kwa mara. Na sijawahi kumsikia mdogo wangu akigombana na mtu
‘Kwakweli sina ninayemjua kabisa, yeye mara nyingi hapendelei makundi, na akirudi hurudi mwenyewe.’ Nikasema kwa uhakika
‘Je unaweza kunielezea kulitokea nini kutwa nzima jana, Tuanzie asubuhi mpaka mnakwenda kulala, na tafadhali uwazi wa maelezo yako utatusaida sana kumpata mhalifu huyu.
Nikatafakari kukumbuka matukio yalivyokuwa siku iliyopita, na ukitafakari sana, matukio yalivyotokea unahisi kuwa huenda mhalfu huyu anaweza kutokea humuhumu ndani. Haiwezekani, sidhani kuwa kati ya wanafamilia waliopo humu wanaweza kufanya lolote, hapana, …nikakana mawazo hayo kichwani
Akilini kukawa na sauti inaniambia kuwa `kikulacho kinaweza kuwa nguoni mwako…’ Nikasonya kwa nguvu , niliisonya ile sauti akilini mwangu, nikiiona ni mchonganishi wa familia yangu. Msonyo huu ulimfanya yule askari aniangalie kwa mashaka.
Akaendelea kunihoji, lakini wakati huo akili yangu ilikuwa ikiwaza tukio zima la siku iliyopita, ili kupima ukweli wa hisia zangu. Niliona kuwa kama nitaelezea kila kitu na kuweka hisia zangu kwa hawa polisi, familia yangu itatiwa hatiani, na nijuavyo polisi walivyo watalichukulia haraka na mwisho wa siku tutakosana na kila mtu ndani ya familia, hata hivyo kulikuwa hakuna ushahidi wowote ulio wazi. Nikajaribu kuivuta kumbukumbu kuwaza mambo yalivyokuwa jana…
Siku iliyopita ilianza kwa mimi kukuta saa yangu imepotea nikaanza kumuuliza mke wangu ….
***
‘Hivi kuna nini humu ndani, mbona sielewi ,kila mara vitu vynagu vya thamani vinapotea, na cha ajabu vinapotea humuhumu ndani. Leo saa yangu ya bei mbaya siioni, nani kaichukua,?’ nikauliza kwa sauti na kwa hasira. Mke wangu akaniangalia kwa huzuni na kuniambia kuwa hata yeye anashangaa, kwani vitu vyote hivyo vimepotea nikiwa na uhakika kuwa niliviweka chumbani.
Kuacha hiyo saa, kuna vito vyangu vya thamani, kwani katika shughuli zangu za biashara wakati mwingine nanunua mikufu ya dhahabu, pete za dhahabu na kwenda kuviuza katika safari zangu, na hii imekuwa biashara yangu ya zida. Cha ajabu kila nikileta kitu nyumbani kwangu hupotea kimiujiza. Na wanafamilia waliopo nyumbani kwangu hakuna hata mmoja mwenye dalili ya wizi.
Mke wangu nimemuoa sasa tuna miaka mitano, na ametokea katika familia yenye uwezo hata kuliko familia yangu. Katika ndoa yetu tumebahatika kuwa na Watoto wawili. Na tangu tuoane sijawahi kumhisi na jambo kama hili. Kwahiyo kwa ujumla mke wangu, hawezi kuniibia hata siku moja na kwanini aniibie, kwa shida gani aliyo nayo, kwani kila akitakacho hupata, na akienda kwao anapewa kila akitakacho, sasa sioni kwanini aniibie, haiwezekani. Nikawaza na kumwangalia akiwa anajaribu kutafuta huku na kule kama labda kuna sehemu niliiweka hiyo saa nikasahau, lakini mimi nina uhakika kuwa niliiweka kwenye kabati, kwa vile nilijua kuwa karibuni nina safari na nikiiuza nitapata hela nzuri tu.
Mwingine tunayeishi naye ni shemeji yangu, mdogo wake mke wangu, huyu hata kuingia chumbani kwetu ni kwa nadra sana, labda awe ameitwa na dada yake kumsaidia kitu Fulani, ni mpole na mwenye adabu sana. Tulimchukua kwa ajiili ya kuwa karibu na shule anayosomea, ambayo ipo karibu na nyumba yetu, anajitahidi sana katika masomo yake. Sidhani kwamba anaweza kufanya kitendo kama hicho na muda gani aliingia chumbani kwangu, nikawaza, na kumuondoa kwenye hisia za wizi.
Yupo mdogo wangu yeye anaingia kidato cha sita, ni mcha mungu sana, na mara chache utamuona yupo, au akiwa nyumbani bila kushika kitabu, na mara nyingine anakwenda kwenye nyumba za ibada, hapana mdogo wangu hawezi kuniibia, namjua sana toka utotoni, wizi katika familia yetu ni mwiko kabisa! Sidhani kama anaweza kubadilika kwa siku hizi chache alizokuja kuishi na mimi!
Watoto wangu ni wadogo, mkubwa yupo darasa la pili na ingawaje anaingia ndani mara kwa mara na mdogo wake, lakini yeye hawezi kufanya vitendo kama hivyo, hawa bado ni Watoto wadogo, hawana tama ya vitu kama hivyo, na kwanza wataiba wapeleke wapi. Hapana hawa hawawezi kufanya vitendo kama hivyo. Nikakuna kichwa kwa mawazo. Nikasimama na kujaribu kutafuta kila mahali bila mafanikio!.
Kitu kingine cha ajabu ni kuwa upoteaji wa vitu hivi umeanza kipindi nilipowachukua hawa wanandugu, shemeji yangu na mdogo wangu. Kabla ya hapo, matatizo kama haya hayakuwepo, kwahiyo inaniweka katika hali ya kuwahisi hawa watu wawili zaidi. Ni mdogo wangu au ni shemeji yangu, ni nani …
**********
Naona tuishie hapa kwa leo, tusicheze mbali kwani kisa hiki ni cha kushangaza kidgogo, na hata kutisha. Vitu vimeanza kupotea kimiujiza, ni kweli kuna kidudu mtu ndani, anayeiba, au ....?
Ni mimi: emu-three
19 comments :
Sasa hii ndio kitu napenda, ngoja niisome kwanza, shukurani M3, nitacomment baadaye nikimaliza kusoma!
Haswaaaaa ! Naona hisia zangu zinazidi kuwa juu na kutamani kuyajua yajayo, m3 tupe mambo.......
Haswaaaaa ! Naona hisia zangu zinazidi kuwa juu na kutamani kuyajua yajayo, m3 tupe mambo.......
Dada storry zako nimezikubali, Du!!!!! mbona inatisha??? kila mtu ni msafi machoni na mawazoni mwake sasa nani anafanya hivyo?????? Naomba tupe mambo dada japo sina uhakika kama ni dada au kaka???
Mambo yanakuja msitie shaka, naomba nasaha zenu na kuniunga mkono kwa kunitembelea na kutoa maoni, ili nijue hisia zenu, je natoa `kitu roho inapenda' au `ninaboa?' na je nifanye nini zaidi kuborehsa `hisia zako?' msema kweli ni mpenzi wa mungu au sio!
Karibuni sana!
Yess sasa umenikuna, nakupa `tano' baadaye nitakupa `tano nyingine, zitakuwa ngapi??
Mhhh, kwa maoni, naomba usicheleweshe sehemu inayofuata, na pia usiogope kuiweka ndefu...hili ni birudisho kwetu tunaopenda kusoma! vitabu aghali, sasa tufanyeje, heri yako unatupa vitu bureee, sijui wewe unalipwa nini...usijlai atakulipa Mungu!
Jamani sio siri simulizi zako zinagusa sana, hii imenikumbusha kitabu kilichoitwa bado mmoja, nilichosoma kati ya mwaka 2000 au 2001 kama sijasahau nilipokuwa secondary na mhusika mkuu aliitwa sajuki. Tupe mambo na usichelewe kuleta part 2 yake ili tuisome bado ya moto. Nakuombea kwa mwenyezi mungu akupe afya tele ili tuendelee kupata na kujifunza mambo mengi kupitia simulizi zako. All the best my dear.
Itabidi uanze kuchangisha changisha ili watu wafidie muda unaosugua benchi kuandaa hizi stori
Chib, tuchangishe changishe, yaani tuweke kapu chakavu kwa ajili ya chochote, mmmmh hapo utafanya wengine wakimbie.
Kweny vikao vya harusi ikikaribia mwisho wengine wanaomba udhuru, wanajua kuna `kapu chakavu litapitishwa'
Ipo njia nyingine, ambayo nimejaribu lakini imeshindikana, ya kuingiza pesa, wamenitumia message kuwa `lugha hailipi'. Wanataka lugha za mataifa...mmmh, nikasema isiwe shida, mimi ni `mswahili damu' na kiswahili changu ndicho nakipigia debe, kama ni hivyo labda ipo siku hapa bongo wafanyabiashara watavutika na hii blog wataweka matangazo yao...bingo
Msikonde, kama nitakuwa ndani ya `ajira hizi za kunahatisha' aaah, kuandika tu, hainipi shida, ninachotaka ni kuviweka visa vingi vyenye mafunzo zaidi!
Karibu, na ahsante kwa kukijali kijiwe chako
Mimi naona ungeandika kitabu kabisaaa,iLi tununue na wewe ufaidike mwaego,maana mmmh.
Īighly ŠµnergetiŃ blog, I likeŌ thŠ°t bŃt.
WŃll there be a Ńart 2?
Feel free to Ī½isit my webpage :: floral decorations
hi!,I really like your writing very much!
proportion we communicate more about your article on AOL?
I require an expert in this space to resolve my problem.
Maybe that's you! Looking ahead to peer you.
My site: mafiakidpro@gmail.com
Hi, of course this article is actually fastidious and I have learned lot of things from it concerning blogging.
thanks.
my blog post ... mafiakidpro@gmail.com
Wow that was strange. I just wrote an extremely long comment but after I
clicked submit my comment didn't appear. Grrrr... well I'm not
writing all that over again. Anyways, just wanted to say wonderful blog!
Also visit my web site ... edcroom@johnston.k12.nc.us
Yesterday, while I was at work, my cousin stole my apple ipad and tested to see if it can survive a
30 foot drop, just so she can be a youtube sensation.
My apple ipad is now destroyed and she has 83 views.
I know this is entirely off topic but I had to share it with someone!
Stop by my website new music
While on each diet, I was never able to decrease my waistline, that is, until I tried then acai berry diet.
It is also high in antioxidants that help the body attain quick recovery from the toxin cleansing.
There are so many experts in the organization who use to give new and
useful suggestion to make the Quantrim much effective time
to time.
Visit my web-site: scam pound melter
tricky sana
Everything is very open with a very clear explanation of
the issues. It was truly informative. Your
site is extremely helpful. Thanks for sharing!
Hello very nice web site!! Guy .. Excellent
.. Wonderful .. I will bookmark your site and take the feeds also?
I am glad to search out numerous helpful information here within the publish, we
want work out extra strategies in this regard, thanks for sharing.
. . . . .
Post a Comment