Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Monday, October 4, 2010

tutaonana mungu akipenda-8

Soma sehemu iliyopita kwa kubofya hapa: sehemuu ya saba
Polisi walituchukua usiku huo hadi kituo cha polisi, kwa ajili ya kuandikisha maelezo, mahojiano na kashikashi za hapa na pale ziliufanya usiku uwe mfupi ajabu. Sijui ilikuwaje polisi wafike haraka kiasi kile, utafikiri walikuwa wanajua kuwa tatizo kama hilo litatokea.


Kumbukumbu za tukio zima lilinijia akilini, nikakumbuka jinsi tulivyoingia mle ndani na pale mke wangu alipowasha taa, macho yangu yalitua kwenye kitanda, na kuuona mwili uliokuwa umelele kwenye dimbwi la damu, na kisu kilizama ndani ya mwili na kubakia mpini, kudhihirisha kuwa muuaji alidhamiria kuua, bila huruma.

‘Kisu hiki hiki mnakijua au alikuja nacho muuaji?’ polisi akauliza.

Nilishikwa na mshituko nilipokiona kile kisu, kwani kisu kile niliwahi kukiona mle ndani kwenye vifaa vya mke wangu, sasa iweje muuaji akipate , nikaingiwa na shaka. Nilijaribu kuificha ile shaka, lakini mke wangu alitangulia kutoa kauli.

‘Kisu hicho kama sikosei ni cha kwangu…’

‘Ni cha kwako au ni chenu’ polisi akauliza kwamshangao.

‘Ni changu kwasababu ni moja ya vitu vyangu nilivyoviweka kama kumbukumbu yangu, na hakijawahi kutumika…’

‘Mpaka kilivyotumika kwa mauaji au sio, au mlivyo…’ alidakia polisi mwingine , na huyu polisi wa kwanza, akamnyamazishia kwa kumshika mdomo.

‘Hiki kisu nilikitoa jana, kwasababu nilikuwa nataka kumhadithia mume wangu, tukio lilonitokea katika maisha yangu na kisu hiki kimo ndani ya tukio hilo. Nilipokitoa jana, nilikiacha juu ya kabati la vyombo, pale barazani, kwahiyo labda huyo muuaji alikiona na kukitumia.’ Akasema mke wangu kwa huzuni.

Kwa maelezo yake, polisi walimchukulia kama mshukiwa wa kwanza kwa mauaji, na mimi mshukiwa wa pili. Niliomba nimtafute wakili, na ombi letu lilikubaliwa kuwa tutumie simu ya mule ndani kumtafuta huyo wakili. Nilimpigia rafiki yangu ambaye kazi hiyo anaijua vyema, na aliwasili haraka iwezekanavyo.

Kesi hii ilikuwa nzito, kiasi kwamba, ushahidi walioukusanya polisi ulituangukia sisi kama wauaji. Wakili wetu alihangaika sana hakulala, kwani ushahidi aliouona, ulikuwa hautupi nafasi ya kujitetea lolote.

‘Sasa ndugu zangu jamani naona kesi hii ni nzito, na polisi kila siku wanakuja na ushahidi mnzito wa kuwaingiza hatiani. Naombeni mnihadithie kila kitu mnachokijua, huenda ndani yake tukapata ufumbuzi’

Mara wazo likanijia kichwani, sijui kwanini wazo hili lilikuja kichwani kwangu.

‘Naomba uje na komputa yako, ikiwa na mtandao(internet)’ nilimpgia simu wakili wangu, baada ya kuwaomba polisi kufanya hivyo. Alipokuja nayo, nilimuomba mke wangu aletwe, na polisi wakakubali. Alipokuja nikamuomba aifungue ile barua pepe aliyoambiwa na ndugu yake aifungue. Ilipofunguka, tulisoma maelezo yake na ilikuwa ndefu na kuwekwa baadhi ya picha za watu mashuhuri.

Wakili aliisoma na kuniambia kuna kitu kakigundua kinaweza kutusaidia, ingawaje barua pepe hiyo ni siku nyingi, lakini marehemu katajwa na maelezo yake yanaweza kusaidia kitu.

Barua pepe hiyo ilielezea kuwa marehemu aliachana na mume wake walipofukuzwa huko Ulaya, kwa kushukiwa kuwa wauzaji wa madawa ya kulevya, na marehemu alishakuwa mtumiaji wa hali ya juu wa hayo madawa. Waliporudi hapa nchini kwa kufukuzwa, mume wa marehemu akakutana na Yule marehemu ndugu wa mke wangu, na wakaanza urafiki, kwahiyo yupo kwenye orodha ya wahanga wa karibuni karibuni katika orodha hiyo. Na Marehemu akaachika na kutelekezwa na mume wake.

Mke mtu akataka kulipiza kisasi , na alichofanya ni kumchongea mume wake kwa mawakala wa madawa, kuwa mume wake aliwahi kuiba madawa mengi kinyume na makubaliano ya kikundi. Wale wauza madawa wakaanza kumtafuta huyu marehemu ili awaambie wapi hayo madawa yalipofichwa. Haya maelezo yaliandikwa kumuelezea huyu mhanga wa kisasi.

‘Mumewe marehemu ambaye walishatengana na marehemu, akaona maisha yake yapo hatarini, akatafuta njia ya kumnyamazisha huyu marehemu. Kwahiyo ikawa mara nyingi marehemu anakoswakoswa kuuwawa. Kwa maelezo yale binafsi , ingawaje siku nyingi zimepita, lakini inaonyesha kuwa, marehemu alikuwa na maadui wengi, akiwemo mumwe aliyeachana naye…’ mwisho wa kunukuu.

‘Sasa hii inaonyesha kuwa huenda hatimaye mume huyo alipata huo upenyo na kumuua marehemu, au wauza madawa wenyewe waliamua kumuondoa ili asije akatoa siri zaidi…’ Hayo ni mawazo ya wakili wetu.

‘Naomba sasa mtulie, niyafanyie kazi haya mawazo,….’

Je marehemu aliuawa na nani? Polisi wanaushahidi kuwa marehemu kauliwa na mke wangu tukishirikiana naye, ushahidi mpya unafichua mengine, je ushahidi huo utatuokoa?

Ni mimi: emu-three

5 comments :

Anonymous said...

Kama sikosei katika tukio hili kuna wanawake wawili marehemu, kwanini usingewapa majina ili iwe rahisi kuwajua. Ni wazo tu mkuu, ila kwa ujumla unahitajika kupewa nafasi za watunzi bora!

Anonymous said...

Hivi wewe ni nani hasa,maana hapo unajiita m3, sasa hakuna jinsi ya kukujua vyema?

emu-three said...

Nashukuru kwa maoni kuwa ningewapa majina wahusika katika tukio hili, nitajitahidi kufanya hivyo kwenye matukio mengine!
Na kuhusu kunijua mimi zaidi ya hapo, natumai mtanijua tu, labda kama unahitaji zaidi wasiliana nami kwenye e-mail yangu
miram3.com@gmail.com

Anonymous said...

Naona kuna haja ya kutumalizia kisa hiki maana tunasahau tulivyoanza. Nimekipenda na natamani nijue mwisho wake

Yasinta Ngonyani said...

Kazi kwelikweli Msisimio mkali. Najua hakuna kuchelewa ila ngoja nipende hapo juu kwenye mwendelezo.Grrrrryyy nyam nyam ...lol