Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Monday, October 25, 2010

limbwata-3


Nilihakikisha kuwa mama anaongea na mwanae huko jikoni. Nikaichukua na kuifungua kwa uangalifu nikachukua kijiko cha chai. Nikaichota, kuhakikisha kuwa haizidi wakati nainua mkono ili niiweke kwenye chakula, mtu akanishika bega kwa nyuma…

Sasa endelea ......
***********
Mwili mzima ulisismuka ilikuwa kama mtu aliyekushikisha waya wa umeme, na kijiko kikaniponyoka mkononi, huku nikipiga ukulele wa `yallaah…!’ Niligeuka kwa haraka kumwangalia ni nani, lakini sikumuona mtu. Nilishikwa na woga ambao sijawahi kukutana nao katika maisha yangu. Kilichoniogopesha zaidi ni kuwa kuna mtu kanishika bega, na hilo nina uhakika nalo, lakini nilipogeuka sikumuona, nimeshikwa na nini…hapana haiwezekani kuwa ni hisia za uwoga tu…

Kuhakikisha zaidi nikaamua kwenda kuwachungulia akina mama , nikamuona mama anaongea na mwanae, na hakuna dalili kuwa aliinuka pale alipokuwa amekaa,…nikakumbuka kuwa yupo yula mama mwingine lakini alikuwa kalala chumbani kwake kwasababu alisema hjisikii vizuri. Nikajiuliza niende chumbani kwake nikahakikishe kuwa yupo au …

Mara nikasikia vyombo vikigongana , nikageuza kichwa kwa haraka na kwa wasiwasi mkubwa, nikijiandaa kukimbia. Nilishikwa na mshituko mwingine ambao kama ningekuwa na ugonjwa wa shinikizo ingekuwa mwisho wangu leo. Nikasimama kama mtu aliyemwagiwa maji, kwani pale nilipokuwa nimesimama, alikuwa Yule mama aliyekuja na mama mkwe kashikilia ile dawa ya nanihii…mmm, mungu wangu…na huku anajaribu kuilamba kwa kidole chake.

‘Mhhh, sawa kabisa, sasa nimeamini, hii ni dawa kali sana, umeipata wapi mpenzi… hii inaitwa limbwata…mmmmh, kweli vijana mna mambo, kweli vijana mna mambo, kweli….’ Akawa anayarudia hayo maneno huku anakuja mlangoni niliposimama, nilishindwa kabisa kuinua mguu wangu mpaka alipofika niliposimama na kunigusa kwa mkono wake. Akasema `tutaonana kikaoni…usitie shaka, hapa umefika, najua ulikuwa huijui hii familia eeeh, ….’ Akatoka na kwenda walipokaa kina mama

Baada ya muda mama mkwe alikuja kuniita, wakati huo nilikuwa nje natafakari kadhia nzima hii, nakujiona mjinga wa kuvamia mambo kwa pupa. Mama mkwe akaniambia nahitajika kikaoni, na kuna wanafamilia wengine wameshafika. Basi nikasema liwalo na liwe, mimi nitapambana nao huko huko kikaoni.

Kwa ufupi kikao kilianza na wanafamilia wakaniweka kiti moto, kunihoji na kutaka kujua kweli kuna kitu nimemfanyia mtoto wao. Nilitaka kukataa, lakini kila mara nilipomwangalia Yule mama, alikuwa kanitazama machoni na mkonono alikuwa kashikilia ile dawa iliyobakia. Nikaona haina haja nimeshindwa mimi. Nikapasua jipu.

‘Mimi kama mzazi wa mwanangu, nilihisi kuwa kuna jambo limemtoke mwanangu, kutokana na mabadiliko aliyokuwa nayo, kwani kila mtu aliyekuja kumtembelea aliniletea taarifa zeney utata. Na tuligundua kuwa mwana wetu amelishwa dawa mbaya, kwahiyo tunataka wewe mke wake utueleze ukweli kabla hatujachukua hatua mbaya zaidi..’akasema mama mtu.

Nilitamani nikatae, lakini nilimuogopa sana yule mama …, nikaona nikificha haitasaidia kitu ilibidi nieleze ukweli kwanini nilifanya hivyo, na kuomba msamaha kuwa mume wangu tabia yake Ndiyo iliyonituma nimpe dawa ili kumdhibiti, asiendelee kuharibika. Baada ya kauili yangu hiyo mara mume wangu akatoa talaka, talaka ambayo siyo ya kuniacha moja kwa moja, akasema anataka apate muda wa kufikiria kwani mimi nimekiuka sheria za ndoa, na kumpa dawa kama ile, akasema kuwa kuishi na mimi ni sawa na kuishi na muuaji.

Kweli nikarejea kwetu, na huko nikaanza kujishughulisha na kazi za ubinifu wa nguo na nilipata wafadahili ambao walinisaidia sana na hali hiyo iliniwezesha nijue uremo na jinsi gani ya kujiweka kama mwanamke mremabo. Nikasoma sana kuhusiana na mambo ya akina mama, na mahusiano ya ndoa. Na kwahiyo nikawa mwalimu mzuri , nikawa nafanya maonyesho ya urembo, huku nawaelimisha watu waliotaka ushauri, na kuwaasa kuwa limbwata la mapenzi ni matendo mema, kuhurumiana, kupeana , kusahihishana mkikoseana, nashukuru nimewasaidia wengi ambao walikuwa na imani hiyo!

Katika maonyesho yangu hayo siku moja nikakutana na mume wangu amabaye alikuwa kaanzisha biashara ya nguo, na alitaka kununua nguo nyingi kutoka kwangu, kipindi hicho hajanijua kuwa ni mimi. Nilimpojitambulisha kwake hakuamini kuwa ni mimi yuleyule mke wake.

Baadaye akaja kwetu akanibembeleza mpaka tukarejeana tena. Kwahiyo ndugu yangu, nimejifunza mengi ya kimaisha kiasi kwamba naweza kusema sasa , nyumba ynagu imejengwa upya kwa msingi imara na sijui kama nitafanya uzembe kama ule wa mwanzo!

Nimegundua kuwa wanandoa wengi wanaivunja ndoa yao wenyewe bila wao wenyewe kujua, kwa uzembe, na kutafuta visingizio ambavyo chanzo chake ni wao wenyewe. Hatujui, kuwa kama jambo jingine ndoa nayo inahitaji kuendelezwa, kuisomea, kuwa wabunifu , vinginevyo tutaishia katika kugombana, kuachana na mbaya zaidi kama huna akili njema utaishia kutafuta madawa! Jinsi unavyokuwa mwili unabadilika, na ukiganda bila kuurutubisha mwili kwa mazoezi, vyakula bora, urembo asilia, na nyama ya ulimi...utazeeka kabla ya umri wako, na matokeo yake yanakatisha tamaa!

Hakuna dawa ya mapenzi zaidi ya `upendo wa dhati kati ya wapendanao, na upendo huo hujengwa kwa kuijua ndoa na misingi yake, kwa kulitoa pendo la dhati kwa mwenzako na huwezi kuyajua hayo bila kuyasomea. Je unaweza kuwa meneja mzuri bila kuusomea umeneja, je unaweza kuwa daktari bingwa bila kuusomea huo udakitari…jibu ni hapana, sasa unawezaje kuwa mwandoa bora bila kuusomea uanandoa? Unawezaje kuwa mpenzi bora bila kuyasomea mapenzi...labda mtasema hilo ni kizalia mtu huzaliwa nalo...sijui kwa uzoefu wangu, hayo ni makosa makubwa!

Na uzuri wa ndoa hauhitaji kisomo cha darasani…hata nyumbani kwako unaweza ukajifunza hilo na lile ukaona hiki kinampendezesha mwenzangu nikiboreshe, ilimradi darasa lake ni kujiweka ndani ya nafsi ya mwenzako, kuwa ningelikuwa yeye ningelipenda hiki na kile…ndoa ni mwanamke shoga asikuambie mtu, mwanamke anaweza kuijenga ndoa au kuivunja ndoa yake mwenyewe kwa mkono na akili yake ..’

 Hivi nikuulize mwenzangu, hizo sherehe za `kitchen party' siku hizi zinasaidia nini, kama sio kamradi kakuwezeshana. Kama kweli ingesaidia nafikiri ndoa zisingeyumba,..., nafikiri ubunifu huo ungetoa wataalamu wakuwafunda wanandoa kabla ya kuingia chumbani, ingesaida sana, kuliko sherehe kubwa ya gharama kubwa, na mwisho wa siku tunaishia kutafuta LI-MBWA-TA...' Hapa kacheka kwa sauti huku akikuna kichwa!

Kwaheri ndugu yangu, naona nisikuchoshe sana, ila napenda kuwahadithia sana watu kuhusiana na kadhia hii, nakukaribisha kwangu, ili uone mavazi mapya na mambo mapya!’ akaaga na kuondoka, huku akimwachia mama nanihii, na sisi somo jipya la `ni nini limbwata, kumbe ipo dawa kweli inaitwa hivyo...!'

Mwisho…

Ni mimi: emu-three

6 comments :

Yasinta Ngonyani said...

Nanukuu "Hakuna dawa ya mapenzi zaidi ya `upendo wa dhati kati ya wapendanao, na upendo huo hujengwa kwa kuijua ndoa na misingi yake, kwa kulitoa pendo la dhati kwa mwenzako na huwezi kuyajua hayo bila kuyasomea. Je unaweza kuwa meneja mzuri bila kuusomea umeneja, je unaweza kuwa daktari bingwa bila kuusomea huo udakitari…jibu ni hapana, sasa unawezaje kuwa mwandoa bora bila kuusomea uanandoa? Unawezaje kuwa mpenzi bora bila kuyasomea mapenzi...labda mtasema hilo ni kizalia mtu huzaliwa nalo...sijui kwa uzoefu wangu, hayo ni makosa makubwa!" mwisho wa kunuu. Asante sana kwa kisa hiki nimejifunza mambo mengu hapa. Ndoa ina kazi yake uvumilivu, kupalilia pia
mawasiliano.

Simon Kitururu said...

Mmmmh!

o'Wambura Ng'wanambiti! said...

mie ntaitafuta.....lol!

kwa wengi maisha ya ndoa yamejengwa kwenye hisia badala ya upendo!

malkiory said...

Kila jambo hutokea kwa wakati wake na kwa makusudi fulani.

NAJUA WAJUA said...

Hivi habari za hii kitu zipo kweli? maana lisemwalo lipo!

emuthree said...

NAJUA WAJUA, unajua kuwa ipo, na kisa hiki ni moja ya ushahidi, na hizi ni dawa zinazopatikana kwa waganga wa kienyeji!
Kama upo bongo, ni rahisi tu, siku hizi wana mabango ya kujitangaza, lakini kwakweli sio nzuri kuitumnia!
Lipo limbwata la ukweli, ambalo mama kweny kisa hiki analitangaza kwa watu, nalo ni `pendo la ukweli, pendo halisi lisilohitaji dawa...mmmh!