Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Thursday, October 28, 2010

Kikulacho ki nguoni mwako(Somnambulism story) 2

 
Katika kuchunguza nikagundua sio saa peke yake, hata mikufu ya dhahabu niliyikusanya kwa ajili ya biashara zangu siku kadhaa za nyuma hazipo, hata simu yangu ambayo mara nyingi siitumii nayo imeyeyuka, hapo hasira ikanipanda nikashindwa kujizua.


‘Haiwezekani, saa, sasa naona na vitu vingine sivioni, hivi kweli inawezekana vitu vipotee humuhumu ndani kimiujiza, mnataka kuniambia nini..’nikauliza tena na tena

`Hivi kweli mume wangu una uhakikia ulikuja na hivyo vitu vyote hapa nyumbani?’ Akauliza mke wangu kwa wasiwasi.

 Nikamwambia nina uhakika na niliviweka hapa kwenye hii droo, ambayo mara nyingi naweka vitu vyangu ambavyo sitaki viguswe, siunakumbuka nilikuambia kuwa kuna mali zangu za kibishara huwa naziweka kwa ajili ya kwenda nazo safari , na mara nyingi naziweka hapa, na wewe peke yako ndiye unayejua wapi ninapoviweka,…’

‘Sasa una maana gani kusema hivyo, ndio ni mimi na wewe tunayejuwa wapi unaweka hivyo vitu , je unanihisi ni mimi nimevichukua, au una maana gani, sikumbuki kuigusa hiyo droo kwa muda mrefu sasa, labda kama ulivihamisha na wewe umesahau, na kwanini nivichukue, tumeishi miaka mingapi unaviweka na unavikita, leo hii huniamini tena...we mwanaume!’ akasema mke wangu kwa huzuni.

 Sikukubaliana naye nikaona niitishe kikao cha dharura cha wanafamilia wote ili kulijadili hili swala kwa mapana, nikawauliza kama kuna mtu yoyote aliiona saa yangu au kuichukua kwani sio hiyo saa tu, kuna vito vyangu vya thamani kila mara nikivileta humo ndani hupotea kimiujiza. Nikawaambia kuwa sina hata mmoja ninayemdhania kufanya hivyo, ila nahitaji uhakika...kimya. Nikarudia tena kwa kumuuliza mmojammoja na kila mmoja akasema yeye hajui na wala hajawahi kugusa hizo droo!

Mwishowe mdogo wangu akaniuliza, je wakati naweka nani anayejua kuwa naweka hivyo vitu kwenye hizo droo, nikamwambia ni mimi na mke wangu tu.

'Kama unauhakika huo sasa , basi ni wewe na shemeji muulizane vizuri..' akasema mdogo wangu huku anacheka.

 Maneno haya yalimkwaza sana mke wangu akaja juu, na kusema kwanini mdogo wangu aseme maneno kama hayo, ina maana kamshuku yeye kuwa ni mwizi. Majibishano makali ambayo sijawahi kuyasikia yakapamba moto kati ya mdogo wangu na mke wangu.

‘Mimi naona mdogo wako kanichoka au kachoka kuishi na mimi, na kama kafikia kunishuku mimi mwizi, basi naona hanipende na hapendi tuishi na wewe, na hili lina maana uamue moja mimi au yeye, kwani hata siku moja sijawahi kugombana na yeye, hata siku moja sijawahi kuchukua kitu cha mtu bila kuomba, na kwanini aseme hivi, hujui hapo umeenda mbali hata kuitusi familia yetu, kwa shida gani tuibe eeeh, hata mimi sikubali hili kabisa….’ maneno makali kati ya mdogo wangu na ndugu hawa wawili wakidai wamezalilishwa, …..

Ilibidi niingilie kati kwani ndoa inaingia doa… Niliingilia kati kuamua ule ugomvi na kumtaka ndugu yangu aombe msamaha, na yeye bila kukaidi akamuomba msamaha shemeji yake na mdogo wake akasema kwa msisistizo kuwa maneno kama hayo hayafai kutolewa na msomi kama yeye. Lakini baadaye ikabidi Ndugu hawa wawili wakubali kumsamehe mdogo wangu angalau kwa shingo upande na mke wangu akaondoka kuelekea chumbani kwa hasira, hakukubali kukaa nasi hata pale nilipombembeleza kuwa yameisha tuongelee maswala mengine.

 Nilijuta kwanini nimeitisha kile kikao.

Ilikuwa usiku wa manane wakati nimelala, mara nikawa naota njozi za ajabu ajabu, nikainuka kitandani na kukaa, baadaye usingizi ulinishika tena hadi asubuhi, nikaamuka nikiwa nimechoka sana, lakini kwa vile nilikuwa na shughulimuhimu ilibidi nidamuke asubuhi.

Nilitoka nikajimwagia maji, halafu nikaona nikaongee kidogo na mdogo wangu, nimkanye asije akaanzisha zogo na shemeji zake, ni bora wasiliongelee tena lile swala, nitafanya uchunguzi wangu mwenyeweMke wangu alikuwa bado kalala, ila shemeji yangu alikuwa jikoni akitayarisha chai, kwani na yeye alitakiwa kuwahi kwenye masomo yake.

‘Vipi Deni hajaaamuka, sio kawaida yake, …’ nikamuuliza shemeji yangu

‘Hata mimi nashangaa, sio kawaida yake…’ akasema shemeji yangu huku anaendelea na shughuli zake.

Nikaelekea chumbani kwa mdogo wangu, na kubisha hodi , lakini kukawa kimya, nikabisha mara mbili tatu, mwishowe nikaamua kuufungua mlango. Nilishikwa na butwaa, kwani mezani kulikuwa na kitabu na taa ya kujisomea, na kitandani mdogo wangu alikuwa kalala huku kajifunika gubigubi. Nikajua kapitiwa na usingizi. Nikalivuta shuka kwa hasira , nikidhamiria kumsema sana mdogo wangu kwanini anacheza na shule, lakini moyoni nikijisemea pia, labda kasoma sana usiku kiasi kwamba usingizi wa asubuhi umempitia.

Mama yangu,.. nilijikua nikiachia lile shuka kwa haraka, na macho yakanitoka pima kwa mshangao na woga, mwili ulikufa ganzi ghafla. Nilishikwa na butwaa ya mwaka, nikapikicha macho yangu kuhakikisha nini ninachokiona mbele yangu bila kuamini.‘haiwezekani, haiwezekani, nini hiki tena jamani …hapana , haiwezekani ….oooh, my God!

Ni mimi: emu-three

5 comments :

Simon Kitururu said...

Mmmh!

Nasibu said...

Ebana wewe ingawa hatujawahi kukuona hata picha !!naamini wewe ni mtaalam wa visa.Na habali zoote unazozileta hapa niza kuelimisha na zinamafunzo hasa.Pia Nadhani habali kama hizi zikiangukia mikononi mwa mtu kama Kanumba au Kigosi zitakua movie za kutishaaaa!

Mzee wa Changamoto said...

Ndugu una kipaji.
Mie nikiwaza kama naweza andika hivi wala sijioni nikujua hata pa kuanzia.
Una mpango wa kukusanya na kufanya kijitabu? Tulimshauri Da Koero akakimbia kabla hajatupa jibu, sasa naona weye wanogesha pia.
Hebu tueleze kama una mpango wa kuandika kitabu ndugu

HONGERA NA ASANTE SAANA

emuthree said...

Nashukuru mkuu kwa mguno wako kinamna `mmmmh', sijui ndio utamu unakolea au unatafakari.
Ndio Nasibu, hata mimi sijui tuliwahi kukutana, ila uhakika ni kuwa tumekutana humuhumu ndani ya kijiwe, nashukuru kuwa kuwa nasi. Nitashukuru kama ujumbe unafika na unaelimisha, na wataalmu wa kuigiza kama wanahitaji tunaweza kusaidiana kwa hilo.
Kuhusu kutunga vitabu kutoka kwa mzee wa changamoto, hilo ni changamoto, na kiukweli tangu udogo natamani kutuunga vitabu, nakumbuka niliandika hadithi nyingi, makaratasi yakaishia kuliwa na panya...!
Nashukuru uwanja huu wa blog, kwani kile nilichokitaka cha kuandika visa, hadithi, hata ikiwezekana vitabu, itakuwa rahisi sasa, na nia yangu ni kutoa kile ninachokijua kwa jamii...ikielimika, ikinufaika ikifurahia kwangu ni furaha, kuwa nimetimiza nami wajibu wangu wa kutoa kile nilichojaliwa na muumba!
Ahsanteni na karibuni tuendelee kuchangia!

Anonymous said...

Wewe mkali, nikisema mkali na maanisha mkali kweli kweli. Jamani sasa sijui nini kimemua????????? sijui fikira zangu ziko sawa??? Naanza kuhisi kama yeye ndo alichukua na baada ya kuona anaanza kugundulika kaamua kujiondoa kabisa kukwepa aibu. Tupe utamu.