Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha
Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..
Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.
MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.
TUPO PAMOJA DAIMA
Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;
https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:
https://www.facebook.com/diaryyangu/
`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;
Monday, October 18, 2010
kakosa mwana na maji ya moto-2
Aliamua kufanya jambo la aina yake, akatoka nje ya korido la ile hoteli, na alipohakikisha kuwa hakuna mtu, akaingia ndani ya kuubeba ule mwili wa Yule marehemu mrembo, akatoka naye na kuelekea mwisho kabisa mwa ngazi za kushukia chini, kwa mbele kulikuwa na vyumba kama ghala la kuhifadhia vitu, hapo akaona ndio mahala pa kuuficha ule mwili.
Akaulaza chini na kuusogeza kwa ndani, na mara akajisikia kama nywele zinamcheza, hii ni dalili ya kuwa kuna kitu, akageuka haraka na kumuona Yule mkuu wa polisi anakuja kuelekea pale alipokuwa , alijikuta kamkojo kakimjia bila kupenda.
‘Vipi mzee naona unatafuta kitu huko kwenye ghala nikusaidie’ akauliza Yule mkuu
‘Ha…pana, nilikuwa …aaah, wewe mkuu mzima unisaidie mimi, hapana, usijali’ akajiumauma na kusogea mbali na pale ili amkute Yule mkuu katikati asisogee zaidi. Bahati nzuri simu ya Yule mkuu ikaita, ikambidi aipokee na kutafuta sehemu ya kuisikilizia, jamaa akachukua nafasi hiyo kuchomoka na kuelkea chumbani mwake.
Alipofika chumbani kwake akaanza kukusanya kila kilichokuwa chake na kuhakikisha kuwa anaondoa ushahidi, kwa ufahamu wake inabidi kuondoa alama za vidole kila mahala anapohisi kuwa Yule mrembo kapita, akafutafuta hapa na pale, akasema mengine yatajileta yenyewe, akafunga makabati na kumwita mhudumu aje na bili kwani anataka kuwahi kuondoka.
Mhudumu alikuja na bili, na aliyekuja sio mhudumu, alikuwa meneja wa hoteli ambaye walijuana naye kwa siku nyingi. Akamsalimia na kumwabia kuwa yeye alikuwepo hapo siku nzima kuhakikisha mambo yanaenda vyema..
‘Nilikuona na Yule mrembo yupo wapi, maana wasee mnajua sana kuchagua…’ Akawa kama kakichoma kisu ndani ya mbunge mtarajiwa.
‘Nini, mrembo…hapana, tuliachana naye jana, sijui kaenda wapi…’ Akasema kwa hamaki.
‘Usijali , umeshanisahau kuwa wakati mwingine nilikuwa nakusaidia kumwandalia huyu mrembo, najua kwenye bili nimeongeza gharamu yangu kidogo, hutajali sana…; akasema Yule meneja na kumkabidhi ile bili , huku akionyesha alama ya kushangaa, kwani sio kawaida yake, wakikutana naye
‘Sawa, lakini, Naomba sana, huyu binti tuliachana jana, hivyo ndivyo ilivyo, sijui alikwenda wapi…hakikisha unajua hivyo, sawa, na nyongeza yako nitaileta…’ akasema huku anatoka kwa haraka. Meneja akataka kumwabia mbona anasahau kabegi kadogo ka wanawake kalikobakia kitandani, lakini kwa haraka alizokuwa nazo alishindwa kumuita na jamaa alishafika chini na kuondoa gari kwa haraka.
Wakati anaingia barabara kuu, akasikia sauti ya kingora cha polisi, na kabla hajafikiria zaidi mara akawa kazungukwa na magari mawili ya polisi na aliyewahi kutoka ni Yule Yule mkuu wa polisi.
‘Mheshimiwa naona unaharaka sana, tunakuomba samahani kidogo, kuna maswali mawili matatu tunahitaji kukuuliza…’ Yule mkuu akatumia busara yake.
‘Jamani mimi nina haraka natakiwa makao makuu, na sasa nimechelewa, maswali gani hayo.
‘Unauona huu mkoba wa kike, tumeuona chumbani kwako ulipokuwa umepanga, unaukumbuka…’ akamuuliza Yule mkuu
‘Mkoba gani huo, mimi sikumbuki, jamani naombeni sana…’ kabla hajamaliza, mkuu wa polisi akaamua atumie rungu lake la dola na kumuonyesha kitambulisho chake na waraka wa kumkamata. Na jamaa akawa hana njia ila akaomba awasiliane na mkewe kwanza, ili ampate wakili wake.
‘Hilo tu mzee usijali, lakini kiutaratibu lazime tufike kituoni ili kuhojiana na kuweka mambo katika utaratibu, mengine ni haki yako. ..’ alijipapasa mfukoni na kujikuta na shilingi elifu kumi tu, akaguna na kusema sasa mzee nimeumbuka. Ina maana mke wangu atanijua kuwa nilikuwa na hawara, ina maana ubunge umeota majani, ina maana, nyumba, gari, vyote vimepotea, ina maana sasa nitashitakiwa kwa mauji, maana mtu kafa nimeenda kumficha, sijui kauwawa au kafa…ooooh, nimeumbuka
Ni mimi: emu-three
2 comments :
Kisa hiki kwakweli mtu unajifunza mengi. Tamaa si nzuri na mwisho wake huwa ndio hivi. Mke wake anafikiri mume wangu anakwenda kazini kumbe... kaazi kwelikweli, Mweh Maisha haya sijui iweje hadi kila mtu aridhike na alicho nacho?
Ataenda kuwakilisha wafungwa gerezani, sio mbaya sana!
Post a Comment