Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Wednesday, September 29, 2010

tutaonana mungu akipenda-7

 
 Soma sehemu iliyopita kwa kubofya hapa: sehemu ya sita

 'Ilikuwa kazi kubwa sana kumtafuta huyu ndugu yangu..’ mke wangu aliendela kunisimulia kisa chake .


`Kwani walipofika kwake walikuta nyumba imefungwa na hakuna anayejua wapi alipokwenda, basi watu wakaenda kwa Yule aliyekuwa mchumba wangu, naye walikuta hayupo. Je alipotoka nyumbani kwetu aliamua kwenda kumuona mwenzake na kusafiri, tukajiuliza bila jibu.

Baada ya msako kwa kushirikiana na polisi kushindikana, watu wakakata tamaa, lakini kesho yake ikaja taarifa kuwa kuna maiti imegundulika katika nyumba moja ya wageni. Na maelezo yake yalionyesha kuwa ndiye huyo ndugu yangu, amejiua kwa kunywa sumu.

Tulifika kwenye hiyo nyumba, na kweli alikuwa yeye…

Kwakweli iliniuma sana, iliniuma kwa sababu yote haya yamesababishwa na `wanaume’. Na tangu siku ile nikasema mimi na wanume basi, nikawa kila nikikutana na mwanaume yoyote, asinisemeshe, kwani akinisemesha namjibu kijeuri, ilimradi mimi na wao …basi tena, chuki mtindo mmoja. Unakumbuka siku ile tulipiokutana ndani ya basi, nilivyokujibu, basi ulikuwa ndio mwendo wangu wa kuwajibu wanaume. Lakini nashukuru kuwa uliweza kunielewa na kunibadili nia yangu ambayo ilikuwa ikienda pabaya….’

‘Sasa mume wangu naona kwangu inatosha kwa leo, sehemu nyingine sio muhimu sana, naomba ukamuone aliyekuwa mkeo, natumai ana mengi yakukuhadithia kwanini alifanya hicho alichokufanyia, na pia aliniambia kuwa anataka kukuomba msamaha, kwani dunia imeshamfunza, na hataweza kuishi kwa amani mpaka asikie kauli yako kuwa umemsamehe.

‘Tatizo sio kumsamehe, naweza nikasema nimemsamehe kwa kauli mdomoni, lakini je hili jereha alilolisababisha litakuwa limeisha moyoni, je watu kama hawa hawahitaji funzo Fulani. Mimi yalishakwisha siku ile uliponikubalia kuwa tuwe mume na mke, na nimejifunza mengi kuwa mimi na yeye tulioana tu kwasababu alihitaji alichokitaka na alipokipata akaamua alivyoamua..’

‘Ndio hivyo, cha muhimu nikumshukuru mungu, kwani amekufunulia kile ulichokuwa hukijui, lakini kusameheana ni bora kuliko kuwekeana visasi, nakuomba tena mume wangu nenda mkakae na umsamehe yaishe, pamoja na sabbu hizo huenda ana sababu na mengi yakukuelezea..’

‘Sawa , ingawaje muda umeisha sana, ngoja nikamuone…’ nikainuka na kabla sijatoka mle chumbani nikamuuliza swali kuwa je aliwahi kuifungua ile barua pepe aliyoambiwa aifungue na ndugu yake huyo. Alisema hajawahi kuifungua na hana hata haja ya kuifungua tena, lakini hakuwahi kuifuta. Na cha zaidi siku ya mazishi ya ndugu yake alikutana na aliyekuwa mchumba wake, na jamaa huyu alizimia alipopata tarifa kuwa yeye alikuwa mhanga wa mia moja wa kisasi cha kuambukizwa ugonjwa wa Ukimwi.

Swali likuwa ni nani na nani alitembea na huyo binti, kwani alivyosema mke wangu, watu wengi walihudhuria hayo mazishi kwa nia ya kujua nini na nani atakuwa anajijua. Na kweli matajiri wengi walikuja na mgari yao, na kila aliyekuja alikuwa mnyonge kupindikua,…je kutokana na hawo huo mnyororo wa hicho kisasi utakuwa umefikia wapi? Nikawa na hamu sana ya kuiona hiyo barua pepe…

‘Basi kesho naomba tukaifungue hiyo barua pepe ili tujue kuna ujumbe gani…’ nikamwambia nikiwa na hamu kubwa sana ya kujua nini alichokuwa amemwandikia ndugu yake huyo, Nikaondoka kuelekea chumba alipotayarishiwa mgeni wetu huyu.

Kila hatua niliyotembea ilinikumbusha machungu mengi, nikajiuliza je kama tusingekutana , angelikuwa na moyo huu wa kuja kuniomba msamaha? Labda, ngoja nikamuone , nimsikie, na nafikiri kuna haja ya kumsaidia zaidi kama ana matatizo ili ajue kuwa ubinadamu ni kutendeana wema na sio kuumizana.

Nikagonga mlango mara tatu, kimya, nikagonga tena na tena, lakini sikusikia chochote, nikaona nirudi kumuuliza mke wangu kuwa kweli alimuacha mle ndani. Mke wangu alisema alimuacha ndani baada ya kumuonyesha sehemu ya kulala, na alisema angefurahia kama wangeongela ndani ya chumba kuliko barazani ambapo watu wanaweza kuja kuwaona na kuwakatisha mazungumzo yao.

Tukaamua kuufungua ule mlango kwa ufunguo wa akiba, kwani ilionyesha kuwa ule mlango ulifungwa kwa ndani, au mfungaji kafunga na kuondoka.

‘Au kaamua kuondoka, alipoona nimekawia akadhani bado nina hasira naye’ nikamuuliza mke wang

‘Sidhani, alisema hawezi kuondoka mpaka ahakikishe umemsamehe…ngoja tufungue mlango, labda usingizi umemzidia ‘ akasema mke wangu.

Tukaufungua mlango kwa tahadhari kubwa sana na kukuta chumba kikiwa na giza, mke wangu akaiwasha taa…

‘Mungu wangu balaa gani hili tena…’nikajikuta nikisema kwa sauti.

‘Kwani vipi mume wa….mamaaaa’ naye ….

Ni mimi: emu-three

7 comments :

Anonymous said...

Bwana M3, watutisha halafu wakatisha manake nini...mmmh, nahisi kuna ubaya...nashindwa kusubiri, nikupe nini unitumie kisa chote!

Nasibu said...

Hii stori mbona inavisa vingi mr3?Kwani ukisoma usiku unaweza kuota mengine jamani,,hivi ni hadidhi?au ni ya ukweli iliyomtokea huyo bwana?

Pamela said...

mapigo ya moyo yananienda kasi sana nahisi mdada alijimaliza kule chumbani anyway nasubiri uendeleze!

Anonymous said...

Hapo kuna kitu mbaya imefanyika, tupe uhondo mzee wa visa

Yasinta Ngonyani said...

inasisimua na pia inaogopesha ni nini walikikuta chumbani humo .....fanya haraka ili tujue

o'Wambura Ng'wanambiti! said...

hicho ni kisa cha kweli kabisa!

subirini...utamu/uchungu waja

Anonymous said...

mmmmmh!