Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Thursday, September 30, 2010

mila za kurithi wajane kumbe bado zipo!


 Baada ya kumaliza msiba wa mume wangu, wanandugu wa familia yangu na upande wa marehemu mume wangu walikutana. Hiki kilikuwa kikao ambacho sitakisahau katika maisha yangu. Mengi nilisikia kabla, na hata marehemu mume wangu akiwa hai alijaribu kuniambia kuwa jamii zao zina utaratibu huo. Muda huo tulikuwa tukiongea kiutani, na hatukujua kuwa ipo siku mimi na yeye tutaachana.


‘Wanandugu wenzangu, msiba umeisha, ingawaje majonzi hayataisha kamwe, lakini tutafanyaje, muumba ndiye aliyetuumba, na ndiye anayetupa uhai, siku ikifika huna jinsi. Sisi tuliobakia ni marehemu watarajiwa, kwahiyo cha muhimu nikuombeana heri, na kuwaombea waliotangulia walale mahala pema peponi…’ Huyu alikuwa msemaji mkuu wa familia.

Mzee huyu nilimuogopa sana, huwa alikuwa akitutembelea mara kwa mara, na akiona tunaishi kinyume na taratibu za familia zao, anakuja juu na kukemea, alikuwa hataki utani, hata marehemu mume wangu alikuwa akimheshimu sana. Mzee wa mila na desturi!

‘Taratibu za kifamilia zipo pale pale, hatuna jinsi ya kuzikwepa, na mtu anapofariki tunajua nini kifanyike. Labda kwa kuelezea zaidi ni kuwa marehemu kaacha mke na watoto. Mali kwetu sio muhimu sana, kwani tunajua kuwa mali ni mali za familia yote, ndio maana tunashirikiana kifamilia.

‘Lakini tujue kuwa mali zinatakiwa kutunzwa, na mitihani kama hii ikitokea mali zinaweza kufujwa na hata kutoka nje ya familia, na hili kwetu miaka nenda rudi tumekuwa tukililinda. Watoto watakosa matunzo bora yanayoendana na mila na desturi zetu, lazima tuwe makini kwa hili. Na kwa hiyo basi, ili mali, mke na watoto wasipotee, wasitoke nje ya familia yetu , tumekuwa na taratibi nzuri kabisa. Taratibu ya kuhakikisha kuwa mjane anakuwa mikononi mwetu, na watoto wanaendelea kuwa na baba ndani ya familia….’ Akatulia na kuniangalia.

‘Kwahiyo mwana wetu mpendwa, usiwe na wasiwasi kabisa, maisha yako yataendelea vyema, na hutapata taabu kabisa, mali , watoto na wewe mtakuwa salama kabisa. Labda nikuulize, mliwahi kuongea lolote wewe na mume wako, kuwa ikitokea kitu kama hichi, wewe utapenda kuwa katika ulinzi wa nani …’ akanikaia macho

‘Ulinzi wa nani, baba naomba ufafanuzi kidogo, kwani ulinzi mkuu ni kumtegemea mungu, na sidhani kuwa ninahitaji mtu , kwani niliyemtegemea zaidi kaondoka, na sidhani kama nahitaji mtu mwingine katika umri wangu huu, mimi na watoto wangu inatosha…’ nikasema kwa majonzi na kuanza kulia.

‘Sawa tumekuelewa, na hilo tunalijua kwa mtu yoyote, inatokea hivyo kwa muda, lakini binadamu, tumepewa kitu Fulani, kusahau, na ni swala la muda tu utasahau kabisa, itafika siku, hutamkumbuka kabisa marehemu…hii lipo, na sisi kama wanafamilia tuna uchungu mkubwa zaidi sana, kwanii huyo aliyeondoka ni mwanetu, hatuwezi kupata mtoto kama yeye, labda mwingine kwa namna nyingine, lakini sio kama yeye. Wewe kama mke utakutana na jamaa ukampenda, na hata zaidi ya ulivyopendana na marehemu, hii lipo, na ni ubinadamu..’ akaniangalia kwa makini.

‘Sisi katika familia yetu tuna utaratibu, kuwa mke akifiwa, anakuwa chini ya ulinzi wa ndugu wa marehemu, kwa jina jingine unarithiwa. Hili wanalipinga sana watu wengi, lakini sisi tumelitekeleza vizuri miaka nenda rudi na limeleta manufaa makubwa, ndio maana unaiona familia hii ni tajiri, kwani utajiri wetu hautoki nje. Sasa wewe uliolewa ndani ya familia hii, na ukakubali yote, na hili huna budi ulikubali. Unawaona wanaume wote hawa, waliokaa mbele yako, wengine wana wake wengine hawana wake, unachotakiwa ni kumchagua mmoja wao na muongee naye, na akikubali basi utakuwa mke halali wa huyo ndugu, ama uwe mke wa pili kwake, au watatu au wa kwanza,…hilo halina mjadala mrefu…’

Nilishikwa na kigugumizi. Sikuamini masikio yangu, nilitamanai mume wangu arudi nimuambie kuwa mbona haya hukunielewesha zaidi, mimi nilidhani ulikuwa utani. Nililia, na kulia, lakini hakuna aliyenionea Huruma, wao walikazania utamaduni wao huohuo ndani ya familia yao.

Mimi ni mwalimu, na kuelimisha ni jadi yangu, nilijaribu kuwaelimisha ubaya wa hili jambo, lakini nilikuwa kama mtoto anayemfundisha mzazi wake kupika, wakati yeye kila siku anapikiwa na mzazi wake huyo.

‘Uamuzi ni ndio huo, mawili, ukubaliane kukubali haya, au kama hutaki, basi umaikana familia na hatuna jinsi, tutakupa kilicho chako, na kutuachia watoto wetu, ambao wana haki zaidi katika mali zetu…narudia tena, mali zetu, kwani mali zote unazoona hapa zimetokana na ushirikiano wa familia, wewe mwenyewe umeliona hili….’ Aliendelea kuelezea mengi, lakini akili yangu haikuwepo tena ndani ya kikao hicho.

Je wanajamii hii ikoje? Hili bado lipo dunia hii, jamani tufanyeje? Tuwe pamoja ujue uamuzi gani niliuchukua!

Ni mimi: emu-three

14 comments :

Anonymous said...

Naiwahi ikiwa ya motomoto: Ni hivi kwa nchi hii kuna mambo mengi ya kizamani bado yapo, hilo sikatai, kwa mfano kukeketa wanawake, kwa mfano kuna wanaume hawaendi jando(kutahiriwa) nk.
Hii ni kuonyesha kuwa `kielimu ya kijamii,bado tupo katika enzi za ujima. Tembeleeni vijiji, nikiwa na maana vijijini, ndani ndani huko utayaona mengi.
Kwako wewe uliyetakiwa kurithiwa, kwanza nakupa pole, na pili nakupa moyo kuwa `uamuzi mkubwa upo mikononi mwako' kwasababu sio lazima uishi milele bila kuolewa, hiyo ni kumkufuru mungu.
Nasema hivyo nikiwa na maana kuwa kama kuna mmoja wa wanafamilia unampenda, kwani uliishi nao kwa muda mrefu, unawajua vyema, olewa ili uwe karibu na watoto wako.
Lakini kama hutaki, basi ...waambie mimi sitaki kaeni na mila zenu. Ina maana hapo watoto utawaacha, na sijui wana umri gani.
Najua wengi watakushauri kuwa uende mahakamani, lakini tulio na uzoefu wa mambo hayo, utaishia kupigwa kalenda, na mwisho wa siku utaambiwa urejee kwenye jamii mjadiliane na mkubaliane.
Uamuzi ni wewe kujua nini msimamo wako katika maisha...!

Anonymous said...

Mzee wa visaaa, nimekuaminia mkuuu, manake unagonga palepale na kukiweka kisa live, bila chenga!
Mimi sikubaliani kabisa na kurithiana wajane, hata awe mrembo vipi, kwasababu kwanza magonjwa, pili upendo , tatu...haiji akilini!
Lakini hapo, kwenye hiyo mila, hakibanduki kitu, inavyoonyesha, midume, imakula `amini' na sio midume tu inaonyesha hata wanawake ni wale wakupiga magoti wakimuona mkwe!
Wewe tafuta chansi toweka na watoto wako,katafute hifadhi ustaawi wa jamii, watakusikiliza, lakini hapo...mmmh, sijui!

o'Wambura Ng'wanambiti! said...

....hii kama Tarime Mara vile!

Ushauri wajameni!

Yasinta Ngonyani said...

Haya sasa mengine itakuwaje nirithiwe na shemeji yangu jamani? Ila hapo walimpa mtego, tena ni mtego mkubwa sana WATOTO. Sijui kama ni kweli mtu unaweza kumsahau umpendaye kama kweli ulimpenda kwa dhati kabisa. Hakika haya makubwa kurithiwa na shemeji... mila hizi kaazi kwelikweli...

Anonymous said...

My partner and I absolutely love your blog and find a lot
of your post's to be exactly I'm looking for. can you offer guest writers to write content for you personally?
I wouldn't mind creating a post or elaborating on a lot of the subjects you write with regards to here. Again, awesome blog!
Review my web page ... easy diets that work

Anonymous said...

Wow that was unusual. I just wrote an really long comment but after I clicked submit my comment didn't show up. Grrrr... well I'm not writing all that over again.

Regardless, just wanted to say excellent blog!


Here is my homepage; uk Best hosting Website

Anonymous said...

Ηеllo! I could have swοrn I've been to this blog before but after going through many of the posts I realized it's new to me.
Νonetheleѕs, I'm definitely pleased I came across it and I'll be bookmaгking it and checking back
often!

my weblоg :: facebook application

Anonymous said...

This functions a treat !!, I rejoice I found your post! My ML-1210 is still chugging
in addition to Windows 8 now. Many thanks.

my web-site: xerox phaser 8560 error codes

Anonymous said...

I am in fact pleased to read this blog posts which
carries tons of valuable facts, thanks for providing such information.


Feel free to surf to my page: xerox 8560 printer

Anonymous said...

I really like reading through an article that will make people think.
Also, thank you for permitting me to comment!

Also visit my website Sure flap cat flap

Anonymous said...

Being a tall person is a little bit like being blessed, your entire life is more desirable than if you were less than average height. enjoy life like the tall people and see the way in which your existence will get far better.

http://www.blurty.com/users/deelsonheels07

Anonymous said...

Hey are using Wordpress for your site platform?
I'm new to the blog world but I'm trying to get started and
set up my own. Do you need any coding knowledge to make your own blog?
Any help would be greatly appreciated!

my webpage - hostgatror

Anonymous said...

Hey are using Wordpress for your site platform?

I'm new to the blog world but I'm trying to get started and
set up my own. Do you need any coding knowledge to make your own blog?
Any help would be greatly appreciated!

Review my webpage hostgatror

Anonymous said...

Polymer clay is one thing I've all the time needed to strive as a result of you may make all kinds of things with it.

Voting this Up and Useful.