Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Tuesday, September 28, 2010

tutaonana mungu akipenda-6


 Mlango ulifunguka taratibu, na kila sekunde iliyopita wakati mlango unafunguka, ilinipandisha hasira na munkari wa kutaka kufanya kitu kibaya. Nilikitafuta kisu changu nilichokuwa nimekificha kwenye gauni lla harusi, lakini sikukiona, kisu hiki kilikuwa kikikatia kamba kule nyumba ya ibada, nilikiona wakati natoka na kukificha kwenye gauni, sasa hakipo, nikajiuma mdomo kwa hasira, sikujua kimeenda wapi. Nashukuru maoni ya mama yangu kuwa chochote nitakachokiona, kabla sijafanya kitu nimuombe mungu halafu nihesebu moja mpaka kumi.


Mungu wangu, nilishikwa na butwaa, na nilichokiona mbele yangu, kiliganda akilini mwangu mpaka leo, kiasi kwamba kila nilipoonana na huyu jamaa nilikuwa nikiliona lile tendo likifanyika kwa unyama wa aina yake. Niliapa kwa hasira, kuwa kama kile kisu kingelikuwepo, leo hii tungelizungumza mengine. Nahisi mama alikiona hiki kisu na kukichukua, au kimedondoka ndani ya gari.

Nilichukua simu yangu yenye sehemu ya kuchukulia picha za video na kwa ujasiri wa ajabu nilichukua sehemu ya tendo lile na taratibu nikatoka nje, na mama yangu alikuja kunishika mkono, kwani nipofika nje hasira zilishika na kutaka kurudi tena ndani nikijiuliza kwaninii sikufanya lolote.

‘Mama hukuona ki…ulikichukua…’ nikawa nasema kwa hasira huku nikitafuta ndani ya gari

‘Haina haja mwanangu , kama umeshuhudia kuwa ni yeye na nani yupo naye, wewe twende nyumbani..’ Na juhudi za mama zilinisaidia tukarudi nyumbani na nilishangaa kuwa sikulitilia manani tena lile tukio, nikawa masaa yote namuomba Mungu anisaidie kuushinda huo mtihani.

 Siku ya pili yake  wakati tumepumzika nyumbani mara mlango ukagongwa na aliyeingia mle mlangoni alinifanya niinuke na kukimbilia chumbani. Mle ndani niliweka kisu kingine, nilichokinunua baadaye, sikujua ni kwanini nilifanya hivyo. Nilikitoa na kukificha kwenye upinde wa gauni langu, nikatoka nje, na bahati nilipotoka ikawa Yule mgeni keshatolewa nje. Nikaamua kumfuata hukohuko.

Wakati nafungua mlango, mama yangu akaniona, na alichofanya ni kumwambia baba yangu aniwahi na kunirudisha ndani, na katika ile kukurukakara, kile kisu kikadondoka, na Yule mgeni alipokiona alikimbia kama mwenda wazimu.

‘Hivi huyu hana haya, au anajua kuwa hatujui kitu gani alichomfanyia ndugu yake..’ akasema baba mmoja aliyekuja hapo nyumbani.

‘Watu kama hawa huwa hawaoni ubaya walioufanya, na wanafanya wakiwa na kusudio Fulani, la kukomoana, na raha yao nikuona unateseka, dawa nikujifanya hujali…’ akasema mama mmoja.

Mara ikaingia meseji katika simu yangu, ilikuwa meseji ndefu iliyojikatakata.

‘Ndugu yangu, najua utaniona mtu mbaya sana, lakini mimi niliahidi kuwa nitawamaliza watu wote wenye tabia kama ya huyu aliyetaka kuwa mumeo, wewe humjui kama nimjuavyo mimi, na ahadi ynagu nikuwamaliza mmoja baada ya mwingine, na hadi nitakapofikisha wahanga mia moja, ndivyo ahadi yangu ilivyokuwa. Na  huyu ndiye mhanga wa mia moja. Naomba unisamehe sana, kwani yaliyonikuta kabla ni mabaya zaidi ya unavyofikiria, na walionifanyia hivi ni watu kama hawa wenye pesa zao na wanajiona wazurii na wanaweza kufanya lolote.

Nenda kwenye e-mail yangu utakikuta kisa kizima cha yaliyonikuta. Nawatakieni maisha mema, na nawaomba mzidi kuniombea kwa Mungu baba, ili aipokee roho yangu na anisamehe madhambi yangu ambayo nimeyatenda. Ipo siku tutakutana sote na hapo yote mabaya yatafichuka, na hapo wote walionifanyia ubaya huu watahukumiwa na hakimu wa mhakimu! Mimi natangulia, nikijua wote ni maiti watarajiwa. Usifanye makosa ya kumrudia mhanga huyo, vinginenevyo, utajuta maisha yako yote…huyo hakufai na si mtu wa aina yako….

Mimi nduguyo,

Nilishikwa na butwaa, na ghafla nikapiga ukulele kuwa ndugu yangu anataka kwenda kujiua watu waende wakamuokoe....Watu waliokuwepo , na ambao walishaanza kujazana hapo kwetu wakahamaki na waliponiuliza zaidi nikawapa yale maneno kwenye simu. Na baadaye watu wakajipanga kufuatilia wapi alipo, ili wakamuokoe kama kweli ana nia hiyo ya kujiua…

Je ataokolewa ….Naona tusichoke kukisoma hiki kisa ili tugundue mengi zaidi!

Ni mimi: emu-three
Enhanced by Zemanta

5 comments :

Masangu Matondo Nzuzullima (MMN) said...

Pengine itabidi ninakilishe kuanzia sehemu ya kwanza na kusoma hadithi yote ili niweze kupata ujumbe sawasawa kabla sijakurupuka kutoa maoni.

Nitarudi baadaye....

Pamela said...

Mungu wangu jamani duniani kuna watu na viatu unawezaje kumuumiza mwenzio hivyo na bado usihisi chochote!! pole kwa mdada hata kama leo ni historia lkn du maumivu haya ni mabaya

emuthree said...

Nakushukuru sana Pamela kuwa pamoja na kisa hiki, endelea kuwepo kwani mara nyingi tukio moja husafishwa na tukio jingine ukasema..oh, kumbe kuna waliyotendewa zaidi yangu..na mwisho wa siku tunasahau na kesameheana. Je hawa walisameheana? sijui ngoja twende kwenye kisa tuone ilivyokuwa!

emuthree said...

Ndio mwalimi MMN, usichoke kusoma, najua wewe ni mwalimu, utasoma hata katikati ya mistari na kugundua siri iliyojificha...karibu sana

o'Wambura Ng'wanambiti! said...

mmmh! ngoja nkatafute kiti kwanza...