Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Friday, September 24, 2010

tutaonana mungu akipenda-4


 Masaa yaliyoyoma, tukaona tuondoke tuelekee huko huko kwenye nyumba ya ibada kwani miadi yetu ilikuwa wao watupitie, halafu msafara wetu na wao tuongozane. Moyo ulianza kwenda mbio na kuingiwa na wasiwasi , nini kimempata mpenzi wangu mpaka abadili nia saa za mwisho, lakini nilijipa moyo kuwa huenda wameogopa foleni,lakini mbona wasitufahamishe na kwanini tukiwapigia simu namba zao wote hazipatikani!


‘Usiwe na waswasi, tutakutana na wao huko kwenye nyumba ya ibada’ akanipa moyo mshirika mwenza mwingine, kwani Yule tuliyepanga kuwa naye na ambaye tulishona hata sare na kuhangaika naye tangu mwanzo hakuweza kufika na hakuna taarifa yoyote, na cha jabu naye simu ilikuwa haipatikani.

Tuliondoka kwa haraka, ili tuwahi ratiba yetu ya kufungishwa ndoa, kwani siku hiyo kulikuwa na ndoa nyingi zilikuwa zinafungwa. Na tulimshukuru mungu kuwa njiani kulikuwa hakuna foleni yoyote. Tulifika nyumba ya ibada na kukuta msafara wa bwana harusi haujafika. Tukajaribu kuwasiliana na jamaa zao lakini tuliowapata walisema na wao wapo njiani kuja, lakini hawana taarifa na bwana harusi, kwani wao walijua kuwa wapo pamoja na sisi!

Zamu yetu ikafika, tukaitwa majina ili twende kufungishwa ndoa, ikabidi mtu wetu aende kuomba isogezwe masaa ya mbele. Masaa yalienda kama mchezo, hadi zamu yetu ikafika tena, tukaitwa na tukaomba tusogezwe mbele, na ikataokea karibu mara nne, na mwishowe mtu wa kutufungisha ndoa akasema tutawekwe mwishoni kabisa.

Niliwaza sana, kwanini itokee hivyo, kwanini mpenzi wangu aamue kunifanyia hivyo. Niliinama kwa aibu na kutahayari nikikumbuka watu mashuhuri niliowalika, mawaziri, wageni toka nje, marafiki wangu toka nchi mbalimbali, na kumbe walikuja kuichukua aibu yangu wakaisambaze kwenye nchi zao. Nilishikwa na butwaa ya hali ya juu.

Watu walitumwa kwenda kwa bwana harusi, na yeye huishi kwenye jumba lake la kifahari nje ya mji, na waliokwenda huko hawakulete jibu mapema, wakatumwa wengine na hata wao wakakawia na baya zaidi kila aliyekwenda alipofika huko akawa akipigiwa simu hapatikani! Kwanini, kuna nini kinaendelea, au ni mkosi gani huu jamani, niliwaza na kuwazua bila jibu kichwani!

‘Mimi naona tuiharishe hii harusi , nafikiri bwana harusi amepatwa na tatizo haiwezekani itokee hivi’ akasema msemaji mkuu, na watu wakaanza kuondoka, mimi nikakataa kuondoka, nikasema nitasubiri hadi hatua ya mwisho. Na kweli watu waliondoka wote na kubakia mimi na mama yangu mzazi.

‘Mwanangu huaamini tu, wewe twende nyumbani,taarifa zote tutazipatia huko, kwani hata akija saa hizi huwezi kufungishwa ndoa tena’ akaniambia mama.

Wazo lilinijia, kwanini rafiki yangu ambaye alipangwa kuwa msaidizi wangu hakutokea, nikamshauri mama twende hadi nyumbani kwao, kabla ya kufika kwetu. Mama alipinga hilo wazo, nikamwambia kama yeye hataki nitaenda mwenyewe. Ikabidi akubali shingo upande , tukaenda hadi nyumbani kwa huyo rafiki yangu, alikuwa na nyumba yake mwenyewe, tukakuta kumefungwa. Tulipouliza watu walisema mwenyeji hapo hajaonekana tangu jana.

Kumbukumbu zilinipeleka mbali, nakumbuka siku ile wakati tunasuka, na kupambwa, bwana harusi mtarajiwa alikuja kututembelea, ingawaje alikatazwa, lakini ilibidi aje kwasababu kuna pesa tulikuwa tunzihitaji. Alipofika , alishikwa na butwaa alipomuona rafiki yangu huyu. Kwakweli rafiki yangu alikuwa mrembo, lakini sikujali kwa muda huo. Rafiki yangu alininong’oneza kwa utani.


‘Usipoangalia nitakuibia, jamaa yako ni mzuri sana, tajiri na ninaona kazimia kwangu, watu kama hwa nawatafuta sana…shauri lake anataka kuingia kwenye tundu la manyigu...’ akasema huku anacheka. Kwakweli pale kila mtu alitania kivyake, kwahiyo hakuna mtu aliyejali.

Nilijiuliza maswali mengi, je kweli rafiki yangu mpendwa, tuliyesoma naye, na tuna udugu Fulani kwa mbali, anaweza kunisaliti na kuniibia mume wangu? Hapana haiwezekani, na kama wameamua hivyo watakuwa wameenda wapi? Sikubali…niliapa kuwatafuta!

Ni mimi: emu-three

2 comments :

Anonymous said...

Naona hii stori itakuwa ndefu. Mkuu kwanini usitunge kitabu, manake mimi naona unaweza.
Haya lete sehemu nyingine tuone ilikuwaje. Naona `best lady' atakuwa kacheza hapo,...

Anonymous said...

Jamani inauma, uombe isikutokee, wewe ndio unasubiri kufungishwa ndoa mwenzako anaingia mitini, hivi mtu kama huyo ana ubinadamu kweli.
Kwanza utajiuliza, kanionaje mimi?
Je jamii itanionaje mimi?
Kwanini initokee mimi?
Kwa kweli sijui kama miminaweza kumsamehe mtu kama huyo, asiyejali hisia za wenzake!
Haya yapo, na tunakushukuru emu-three kwa stori yako, kwani tunakuwa kama vile tunaangalia `movie' fulani...