Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha
Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..
Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.
MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.
TUPO PAMOJA DAIMA
Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;
https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:
https://www.facebook.com/diaryyangu/
`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;
Wednesday, September 29, 2010
Tabasamu hujenga murua
Katika maisha yetu ya kila siku, tunakumbana na sintofahamu nyingi, watu tunakoseana, na hata kuwekeana visasi, na wengine hudiriki kusema, `hata nikifa usikanyage kaburi langu' . Tunajisahau kuwa sisi sote ni binadamu, na kukoseana kupo , kama gilasi hugongana kwenye beseni na kutoa mlio, na bado hupangwa pamoja kwenye kabati la vyombo,sembuse sisi binadamu ambao kukutana, na kusigishana hakukwepeki.
Kuna jamaa mmoja katika ofisi moja yeye wanamuita mtaalamu wa mabifu. Yeye mkikorofishana atakununia wiki nzima. Na akiamua kubadilika anajisifia kuwa akikosewa tena anaweza akamnunia aliyemkosea kwa mwezi mzima. Kwake yeye kufanya hivyo ni sifa, lakini hajui kuwa anajiumiza mwenyewe kisaikolojia.
Babu yangu aliniambia, wakati ukiwa hai, umepewa zawadi nzuri ya kutabasamu na kucheka na watu, zawadi hiyo ipo siku utainyang'anywa, na hutakuwa na uwezo wa kuipata tena, hata kama atakuja bingwa wa kuchekesha duniani. Muda huo watu watakulilia na hutaweza kuwachekea tena, utanuna mpaka siku ya kiyama. Ni vyema ukaitumia zawadi hiyo vyema pale ukiwa hai!
Kukosena kupo, na ukikosewa, uwe mwepesi kusamehe, na hata wewe ukimkosea mwenzako, uwe mwepesi kumuomba msamaha!
Katika kisa chetu cha `tutaonana mungu akipenda, kimejengwa na visa vya kukoseana, na watu walikoseana katika sehemu ambayo mtu mdhaifu angediriki hata kujiua, na wengine waliamua kulipiza kisasi kwa `kuwambukiza wenzao ugonjwa wa ukimwi. Je ni kisasii gani hiki. ukumbuke uliyemwambukiza, atakwenda kumwambukiza mwingine, ambaye hana hatia kabisa na ugomvi wenu huo. Je nia yako ni nini kuiangamiza dunia kwa kosa la baadhi ya watu!.
Kuna watu wapo mitaani wanajiuza, na wanajua kabisa wana huo ugonjwa... Kuna watu wanaoa, au kuolewa wakijua kuwa mwenzake aliyewahi kutembea naye alikufa kwa huo ugonjwa na hataki kupima kwanza ili kujua kuwa na yeye kaathirika au la. Na bado tunaombea dawa ipatikane, hatuoni kuwa hata akipatikana na waathirika ni wengi inaweza isitoshe na huenda ikajenga usugu, kama dawa za malaria, na matokeo yake ikawa inazunguka mumo kwa humo, unapona leo kesho unaambukizwa namwingine.
je nia yetu ni nini?
Jambo jema ni kujenga tabia ya kusameheana, tupendane hata kama kuna chuki ndani yetu, kwani kwa kupendana huko kutasafisha hiyo chuki na mwisho wa siku tutatabasamu wote kwa upendo. Kwai tabasamu hujenga murua usoni
Ni mimi: emu-three
1 comment :
Unajua mimi sijui kununa, hivi kununa kukoje, yaani inakuwaje mpaka unamnunua mwenzako,...namshukuru mungu kuwa wakati wote nacheka, natabasamu, nikijisikia kukasirika kama mnavyoita kununa, natafuta kichekesho...
msinuniane, kweli kama alivyosema M3, Ipo siku utanuna, milele, kwaninii unune leo, kabla siku haijafika
Post a Comment