Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Friday, September 24, 2010

Mfuga Mbwa

Ukifuga mbwa akiuma watu njiani unashtakiwa wewe mfugaji. Ni kweli si kweli?


Sasa ukichagua viongozi wabovu, wezi na wasiojali umma wa watanzania kama inavyoonyesha, utakuwa umeshiriki moja kwa moja kuharibu nchi yako mwenyewe!

Wakiiba hela dawa zikakosekana hospitali watoto wakafa, ni wewe mpiga kura umeua watoto hao. Elimu ikidumaa ni wewe ndio umeidumaza. Vifo vya kina mama vikiongezeka, wewe ndo umewaua wamama! Dawa zikikosekana hospitali wewe ndio unahusika.

Na siku ya mwisho, damu za wezi hao (maana wewe ndo umewawezesha kuiba na ulijua ni wezi lakini ukawapa madaraka!) na za wote waliopotea kwa sababu

yako zitakuwa mikononi mwako.

Afadhali ungekuwa hujui kuwa ni wezi, ungesamehewa! Lakini tazama unajua kabisa mambo yote yanayoendelea na unataka kukosea tena kwa makusudi!

Na utadaiwa mbele ya haki! Kama vile yule mfugwa mbwa aliyesababisha watu kuumwa na mbwa wake akahukumiwa.


Amua sasa kuitendea haki nchi na taifa lako uepuke hukumu!, au ....

Ni Mimi D.Tillya

3 comments :

Anonymous said...

Hii ni kweli unapochagua kiongozi mbaya, kila kosa analofanya na wewe unabeba lawama na mzigo wa madhambi!

Anonymous said...

Sasa wakati mwingine sisi wachaguaji hatuna makosa, kwani wanapotiahidi ukwaani, tunaamini kuwa ni wa kweli, wakitusaliti, hiyo ni dhambi yao wenyewe.
Lakini kama unajua kuwa mtu, chama, kimejaa ufisadi ukamchagua basi wewe hutakwepa lawama.
Mimi ninachowashangaa watuu ni kuendelea kuwachagua watu ambao wamedhihiri ufisadi, wameonyesha katika miaka mitano ya mwanzo hawatufai, bado tunawachagua...hapa, wewe na yeye mtahukumiwa!

o'Wambura Ng'wanambiti! said...

....dah! nimetishika na kuupenda huu ujumbe!