Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha
Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..
Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.
MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.
TUPO PAMOJA DAIMA
Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;
https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:
https://www.facebook.com/diaryyangu/
`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;
Thursday, September 2, 2010
kufa hatufi lakini cha moto tutakiona
Mara jamaa mmoja aliyesimama akanisukuma na kukifungua kile kiyoo chote, duuu, upepo , baridi vikaniandama, kiasi kwamba nilihisi mafua!.
‘Mbona unafanya hivi, huoni baridi ni kali na upepo toka nje unaniathiri, nilishafungua kiasi kidogo, ili nisiumie na nyie mpate hewa na ilitosha kabisa…’ nikasema kwa kunung’unika.
‘Wewe, usipende raha ndani ya basi, kama ungelipenda raha ungepanda taksi, acha upepo uingie kwa raha zetu kama huwezi kukaa hapo ondoka wengine wakae..’ Jamaa akasema kwa nyodo huku akiendelea kukisukuma kile kiyoo ambacho kilishafika mwisho lakini alikuwa hatosheki! Nilijiuliza akilini, hivi nani mwenye haki ya kile kiyoo, mimi niliyepata kiti cha dirishani au hawo waliosimama ndani ya basi. Ni sawa kuwa, swote mle ndani ya basi , tulihitaji hewa, lakini je kama hali ni ya ubaridi na inaniumiza kwanini huyu aliyesimama ambaye hana siti aingilie siti ya mtu mwingine?
Nilitamani gari lifike mwisho mapema, ili niondokane na adha hiyo, lakini foleni za barabarani zilikuwa hazisemeki. Nikajipa moyo, nikisema kuumia kwangu ni raha kwa wenzangu inatosha kabisa.
Tukio hili lilinikumbusha bosi wangu mmoja, baada ya kupata ajira hapa nchini, amekuwa mwiba wa kuotea mbali, yeye alipofika kwenye kampuni yetu, alikuta wafanyakazi wakipata huduma ndogondogo kama ya chai, kuangalia internet, kupata kiasi `vi-allowance’ katika kusaidia makali ya maisha, `advance salary’ nk. Yeye aliviona hivyo sio haki kwa mfanyakazi kupewa, akavindoa, na kusema `kama unapata mshahara kwanini upate vitu vingine vya ziada, ni wajibu wako kuubajeti huo mshahara wako utosheleze mahitaji yako…’alisema kwa hasira.
Watu wakamuuliza yeye kwa mwezi anapata shilingi ngapi, na matumizi yake kwa siku ni shilingi ngapi, wakijua kabisa mshahara wake ni mkubwa zaidi ya mara kumi ya mfanyakzi anayefanya naye kitengo kimoja, alijibu kwa hasira `hiyo haikuhusu’ .Hiyo haikuhusu kama hutaki acha kazi, kama kuna sehemu nyingine unaioana ni bora kwanini ubakie hapa…akaongezea kusema.
Huyu bosi chakula au matumizi yake kwa siku ni sawa na mshahara wa mtu wa kima cha chini, na anamwambia huyo mtu ambaye anapata mshahara wa kima cha chini, au nyongeza kidogo abajeti mshahara wake ili utosheleze mahitaji yake? Je hii ina uhaki za kibinadamu kweli. Hili waliliona wenzake waliotangulia, ndio maana wakaweka vitu kama chai, na vinginevyo ili huyo mfanyakazi asizimie kwa njaa akiwa anawajibika kazini!
Maisha yetu ndivyo yalivyo, unawakaribisha wageni halafu hawa wageni wanakuwa wenyeji kuliko wenyeji, watataka kufungua kiyoo hadi mwisho , sababu kubwa ni kukukomoa, na ukiuliza kwanini, utaambiwa `kama unataka raha nenda kapande taksi, huko ofisini, ukiuliza, unaambiwa nenda kzmz unona mshara haukutoshi katafute ajira sehemu nyingine! Huna njia, inabidi uvumilie ! Nikakumbuka huu usemi usemao `Kufa hatufi lakini cha moto tutakiona’
Ni mimi: emu-three
3 comments :
Huyo bosi ni ngumbaru kabisa, tena mbinafsi mkubwa
Mmmmmmmmmmh!!!!!!! Ni kweli kabisa m3. Umenikumbusha Boss wangu mmoja wa kama huyo. Lakini siku alipoambia kazi basi alinyea kama Piliton, akawa rafiki wa kila mtu na kuchati nao. Lakini alipokuwa madarakani. Loooooh! usiombe kukutana nae kosa si kosa analivalia njuga. Na sisi wabongo tuna kasumba moja kuwathamini hao wagen kuliko tunavyojithamin wenyewe. Na ukizigatia enzi za Mwalimu kimombo hakuna ni kiswahili tu eti lugha ya Taifa, kumbe lugha ya Taifa ni Kimombo na kujenga Ujamaa, basi ni taabu tupu, kuunganisha hicho kimombo cha darasani cha walimu wa UPE kukileta Ofisini!! Ni balaaaaaaaaa.
Kwa hilo, lazima hao wageni wafungue madirisha mpaka mwisho. kwani hatuna sauti tena. Tutasema nini mbele yao. Pamoja ya kuwa upo kwako lazima ufuate matakwa yao.
Usafiri wa bongo, mimi siuoni mfano wake, manake asilimia kubwa ya masaa sasa hivi yanaishia kwenye usafiri/foleni, na miili yetu inazeeshwa na kubambikwa magonjwa sababu ya kujazwa kama magunia.
Hili lingewezwa kupunguzwa kama wahusika wangekuwa nao ni miongoni mwa wanaoteseka,
Najua mtawapa kura zenu na watapita kwa mbwembwe, najua sasa hivi hatuambiwi kitu, `ushabiki wa vyama ndio umetawala, utafikiri ushabiki wa mpira' tumesahahu yale matatizo yenu ya msingi'
Sijui kuna `uchawi gani' unaowafanya watu wasahau matatizo yao yaliyopita na kuendelea kuwapa hawa watu kura tena...
Shaurilenu, mimi nataka nikimbilie nje kwa watu walio-erevuka!
Post a Comment