Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha
Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..
Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.
MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.
TUPO PAMOJA DAIMA
Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;
https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:
https://www.facebook.com/diaryyangu/
`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;
Monday, September 13, 2010
Je wangefanya wanawake ingekuwaje?4
Rejea sehemu iliyopita kabla ya kuendelea na sehemu hii ya mwisho kwa kubofya hapa: sehemu ya 3
**********
Hali baada ya kifo cha mtoto wangu ilikuwa mbaya sana, nilikuwa kama mtu aliyepagawa, mpaka watu wakasema nimeshikwa na mashetani. Wakawa wananifunga kamba kitandani, kama vile kichaa. Taswira ya ile ndoto, nikiunganisha na kifo cha mwanangu ilinifanya nione kuwa mume wangu ndiye muuaji. Sikutaka hata kuonana naye. Jamani sitasahau abadani…
Wazazi wangu waliamua kunichukua kwa muda, wazo hili lilipingwa sana na familia ya mume wangu, lakini baadaye walikubali shingo upande .Nikiwa nyumbani siku moja ,mume wangu aliniarifu kuwa anataka kulijengea kaburi. Nikamwambia kuwa itabidi tujumuike wote. Sijui kwanini nilifanya hivyo, kwani nikuwa nimewaajiri vijana kuwa karibu la lile kaburi, na siku moja kijana mmoja alikuja nakuniambia kuwa wamekuja vijana kadhaa na wanalichimba lile kaburi.
`Mungu wangu…’ Niliwaka,na kama mwehu nikatoka mbio, mama yangu, na jamaa wengine wakanifuatilia nyuma hadi makaburini na kweli tuliwakuta vijana wakiwa katika harakati za kulichimba lile kaburi, Tulishangaa sana, tukawavamia na kuwauliza kulikoni, wao wakadai kuwa wametumwa na baba wa marehemu. Tukampigia simu mume wangu akaja na kudai anachofanya ni kuchukua mchanga kwa ajili ya mila zao, na pia kuliweka vizuri kwa ajili ya ujenzi. Hatukumuelewa hadi mtu wa dini alipokuja na kutuweka sawa.
Ndugu wa mume , akiwemo mama mkwe na wifi zangu walikuja kwa mara nyingine wakiwa na lengo la kuhani msiba. Na kipindi hicho nilisharejea kwa mume wangu.Waliposikia yale yaliyotokea nyuma kwa wambea, kuwa nimesema kuwa mume wangu ndiye muuaji, na alitaka kulichimba kaburi kwa mambo yake ya kishirikina wakaanza kujenga chuki , chuki hiyo ikamwingia hata mume wangu. Lakini kwa vile tulishasuluhishwa na mtu wa dini, tukawa tunaishi hivyohivyo.
Miezi ikapita na hali ikawa inarejea kuwa kama kawaida, lakini ile chuki ya ndugu wa mume dhidi yangu ikawa inazidi, kwanini nimwambie ndugu yao ni mchawi, ina maana nimeihusisha familia yao na uchawi. Ikabidi Yule mtu wa dini aitwe na kutusuluhisha, na wao wakasema yameisha ingawaje ilikuwa mdomoni tu.
Baada ya miezi sita nikajihisi mja mzito, na hii ikawa faraja kwangu, nikaamini kuwa Mwenyezimungu kanirudishia mtoto wangu kwa njia nyingine. Hali yangu ikawa kama kawaida, ingawaje hasira na chuki za kumuona mume wangu zilikuwa kila mara zikinirejea. Na miezi ikapita hadi kufikia muda wa kujifungua.
Siku moja wakati nimerudi toka kazini mapema kidogo nikawafuma mawifi zangu wakiongea na mama mkwe, nilichosikia hapo kilinifanya nishikwe na hali ya uchungu, maumivu yalikuwa makali ajabu, lakini manen yao yakawa yanajirudia kichwani mara kwa mara huku nagugumia kwa maumivu;
‘Sisi sasa kazi ni moja hadi aondoke nyumba hii, kwa vile huyu mfanyakazi keshabeba hiyo mimba, sisi tutamshawishi kaka ampe talaka huyu kinyango, na hiki chombo kiwe na kaka, mambo mengine yatajiseti baadaye…’
‘Hichi kinyago..’ sasa wananiita kinyago, halafu ina maana mume wangu katembea tena na huyu mfanyakazi wa ndani, haiwezekani….nikajihisi giza nene likitanda usoni, na kupoteza fahamu.
Nilipozindukana nikajikua hospitalini, nimezunguka na manesi, na kumbe muda wa kujifungua ulishafika, baada ya heka heka za hapa na pale nikajifungua mtoto wangu salama usalimini. Nilipotoka hospitalini, nikawa na lengo moja la kuondoka pale myumbani, lakini niliona nisichukua hatua ya haraka, kwani wao walikuwa hawajui kuwa nafahamu nini kinachoendelea.
Hali ya Yule mfanyakzi wa nyumani ikawa haina kificho, na nilipomuuliza mume wangu kuhusina na ujauzito ule, alikuja juu, na kusema nimeanza mengine, ya kumzulia uwongo, na kusema kama nitaendelea hivyo atamfukuza Yule binti. Cha ajabu Yule binti alikuwa hataki kabisa kuniambia ukweli, lakini mara nyingi alionekana mnyonge na wakati mwingine nilimfuma akiwa analia.
Mtoto wangu alianza kuumwaumwa, na hali ile ukanifanya niogope, nikawa nahangaika naye, cha ajabu si mume wangu au ndugu za mume wangu waliokuwa wakijali, na usiku mmoja mtoto alizidiwa sana, nilipomwambia mume wangu tumpeleke hospitali akasema ni usiku tusubiri hadi asubuhi.
Haiwezekani, mtoto unaona hali yake ilivyo tusubiri hadi asubuhi, mimi natafuta usafiri, …’ na kweli nikaondoka usiku huo huo hadi hospitali, cha ajabu nilipofika hospitali, mtoto akawa hajambo. Mume wangu ambaye aliamua kunifuta nyuma akamaka na kusema, `hivi wewe unadhani mimi sina uchungu na mtoto, vitu vingine ni vya kawaida kwa mtoto…’ kwa hasira akaondoa gari.
Tukarejea nyumbani na kuwakuta wanandugu wapo kwenye kikao chao cha kunisema, tulipoingia hawakutusikia, kwani walikuwa wamefungulia luninga kwa sauti kubwa.
‘Sasa mumeona wenyewe huyu aondoke, vinginevyo kaka yetu atakufa kwa shinikizo la damu. ..’ Nikawavamia kwa hasira na kuwapa Maneno yao, na kuingia ndani na kukusanya kile kilichofaa, na kuita taxi ambayo ilinifikisha kwa wazazi wangu, na wazazi wangu wakanipokea kwa mikono miwili. Tangu siku ile sijakanyaga tena kwenye ile nyumba, na sidhani kuwa nitaru tena!
Hicho ndio kisa changu kwa baadhi tu ya matukio, samahanini kwa kuwapotezea muda wenu, ila swali langu ni je kama mkasa huo ungetokea kinyume chake, ingekuwaje?
Naomba emu-three umalizie hivyo!
14 comments :
Mimi hapa nimegundua kitu kuwa wafanyakazi wa nyumbani ni muhimu sikatai, lakini iwe ni lazima sana kufanya hivyo, kama inawezekana kwanini tusichukue jamaa wetu wa karibu ambao wanahitaji hizo nafasi!
Pili hii shiriki iliyoingia hapa, huenda ni hisia tu, huyu jamaa kama kweli alikuwa na nyendo hizo nahisi alikuwa analazimishwa , na hii tabia ya kuamini shiriki inazidi kujijenga miongoni mwa watu. Hii ni mbaya sana!
Kwa ushauri wangu, kosa ni mara moja, ukirudia tena na tena umekususdia, lakini `uamuzi mkubwa' ni juu yako. Huyo mume haoleki!
Pole sana. tatizo nililoliona hapa ni kwamba mapenzi yenu na maisha ya ndoa yaliingiliwa na ndugu wa mume baada ya matatizo ya kwanza kwa hiyo badala matatizo kumalizwa ndugu wa mume wakawa wanayaongeza
Inaonyesha moja kwa moja alikuwa akubaliki katika familia aliyoolewa na hii ni fundisho wa wale wanaolazimisha kuolewa na flani hata akijua mama mkwe na ndugu za mume awamkubali.
Mwisho wa yote ni pole sana kwa muhusika ndio mitihani ya dunia hiyo.
Swala la ndoa ni tete sana, na mara nyingi mpira unatakiwa uchezwe kati ya mume na mke, labda iwe kuna walakini.
Huyu mwanadada nilipomdadisi sana alikiri kuwa bado mume wake anampenda, lakini matendo yake ndiyo yamemtia kichefuchefu...tuendelee kuchangia ili tupate zaidi , e hakuna ushauri wowote kwa huyu dada? Hakuna njia ya kumshauri wakarudiana na mumewe? sijui nawasikiliza nyie wadau mie nimewakilisha, kama ifuatavyo.
Mimi kama nilivyoongea mwanzo kuhusu ushauli juu ya huyu mama ni kitu kimoja tu! Atubu dhambi zake asali kupitia dini lake,,awe karibu na mungu,, na mengine yoote yatajiseti vizuri,,kwasababu hilo pepo la mume wake la kuwatia mimba wanyakazi wake bila kumuombea ni vigumu sana kuacha.Na kama bado anampenda huyo mume wake!bila kujikabidhi mikononi mwa Mungu hata warudiane kesho au kesho kutwa mwisho wake atapelekwa nayeye makabulini.Nampa pole sana Mungu awe naye na amlinde.
Eti Nasibu unaamini kweli upo ushirikina wa namna hiyo, kwani nilivyo-ongea naye, inagwaje anasema haamini ushirikina lakini matendo yake yanaonyesha vingine.
Nauliza hivi, je kweli upo ushirikina huo wa kufukua makaburi, ili mtu atajirike, au ushirikina wa kuchukua damu za watu hasa watoto wadogo eti kwasababu hawana dhambi ili watu watajirike, au ushirikina wa kutembea na `mabikira' eti wao wana baraka katika biashara?
Hayo alinigusia huyu dada, ingawaje mengine nilyaondoa ili kufupisha.
Hebu wadau wenye uzoefu na hili watuelezee, je upo ushirikina wa namna hiyo?
MHHHH, AMA KWELI HUJAFA HUJAUMBIKA
Mie bado nawaza tu! Stori imenigusa hii!:-(
kufuata ushauri wa wazazi ni muhimu sana kwani wao ni miungu ya dunia, ht hivyo subira inasaidia sn kwani vinginevyo huyu dada asingebaini uovu wa dada yake.
Wanawake tuweni makini na ndoa zetu na hasa watu wanaotuzunguka
Emu Three asante kwa stori nzuri, mambo hayo yapo sana tuu....Mimi ninachojiuliza kwanini mawifi huwa wanapenda kuingilia mahusiano ya kaka zao? na usikute wengine wameshaachika wanalipiza visasi kwa wengine. Pili kwanini wanaume huwa wanakuwa hawana msimamo? naamini kama mume anakupenda hawezi sikiliza ya ndugu...Masikini huyo msichana wa kazi usikute alilazimishwa tena kwa vitisho au ahadi fulani fulani.....Pole huyo mmama kwa yaliyomkuta.
Kwa hilo la ushilikina kutokana na kutafuta mali au utajiri! ni kweli hayo yapo tena hapahapa duniani kwasababu mimi nina ushahidi wa tajiri mmoja ambaye aliwahi kuwa jilani yangu kipindi bado naishi afrika,,mpaka sasa anahela isiyohesabika,,lakini familia yake yoote inakaribia kuishia kaburini mpaka wengine walishamkimbia kutokana na kugundua kwamba ndo anayewamaliza,,kuna utajiri ambao mizimu inakulazimisha kila mwaka kutoa mtu ndani ya familia yako,,hayo yapo tena saana.Tena tambueni Mungu yupo na shetani yupo tena wote wanafanya kazi hapahapa duniani,ila nguvu za Mungu zinashinda tena zaidi nguvu za shetani siku zoote.
Haya mambo ya ushirikiana kwa kweli huwa yananiacha hoi sana. Utakuta mtu anasema ei biashara haiendi ni lazima afe mtu kwanza sasa hapo ndo wanponiacha hoi je akifa yule mtu anafanya nini na huou mwili? Kama ninavyosema kila wakati mambo hhaya yanatokana na IMANI Ila huyu mwanaume naye lazima atakuwa na kasoro, Halafu huyu mwanamke naye kama kweli kama alivyosema alikuwa bado anampenda mume wake basi alibidi asimame wima na asimsikilize mtu. Mawifi na mama wakwe mara nyingi ukiwasikiliza inakuwa vurugu na taabu tu na kabisa wakiona mnapendana sana na wao hawana maisha mazuri wanajengwa na wivu.
'Hakuna mkulima anayetaraji kuvuna mavuno mazuri kwa mbegu alizopanda juu ya mwamba...unaweza kweli?' aliniuliza yule dada , nikawa simuelewi, lakini alipofafanua nikajua ana maana gani.
'Mimi nampenda mume wangu, lakini ni sawa na kupanda mbegu juu ya mwamba, hapendeki na siwezi kumtenganisha na familia yake, na...' kwakweli hapo naona sitawezana naye tena, cha muhimu nikumtakia mafanikio mema, labda nachotaka atakipata...lakini sio kutoka kwangu tena!
Hilo lilikuwa hitimisho la yule dada.
'Hakuna mkulima anayetaraji kuvuna mavuno mazuri kwa mbegu alizopanda juu ya mwamba...unaweza kweli?' aliniuliza yule dada , nikawa simuelewi, lakini alipofafanua nikajua ana maana gani.
'Mimi nampenda mume wangu, lakini ni sawa na kupanda mbegu juu ya mwamba, hapendeki na siwezi kumtenganisha na familia yake, na...' kwakweli hapo naona sitawezana naye tena, cha muhimu nikumtakia mafanikio mema, labda nachotaka atakipata...lakini sio kutoka kwangu tena!
Hilo lilikuwa hitimisho la yule dada.
Post a Comment