Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Monday, September 6, 2010

Je wangefanya wanawake ingekuwaje?3

  Soma sehemu iliyopita kwa kubofya hapa: sehemu ya pili
Kwa hasira nilichukua baadhi ya vitu vyangu, nikaita taxi ikanipeleka hadi kwa wazazi wangu ambao wanaishi humuhumu jijini. Nilipofika nilishindwa hata kujieleza nikabaki ninalia. Waliingiwa na wasiwasi wakampigia simu mume wangu ambaye mara moja alifika hapo nyumbani. Na maongezi yetu hayakusaidia kitu, mpaka tena Yule mtu wa dini alipoitwa, na baada ya masuluhisho marefu nikakubali kurejea kwa mume wangu kwa masharti kuwa Yule binti arudishwe kwao.


Baada ya tukio hilo tulikaa muda na mume wangu akajitahidi kujirekebisha na kuwa mpole kupita kiasi , kiasi kwamba nikaona maneno ya mtu wa mungu yalimjaa moyoni.

Siku moja wakati nimejipumzisha na mwanangu ikapigwa simu, nilipoipokea nikasikia mzungumzaji ambaye sikumjia vyema akisema kuwa `mke mwenzangu kajifungua mtoto wa kiume’

‘Mke mwenzangu, yupi huyo?’ nikauliza kwa wasiwasi

‘Hivi wewe kila siku ninakuambia kuwa mume wako sivyo hivyo unavyomfikiria, huyo kashindikana, unakumbuka siku moja nilikupigia simu nikakuambia mume wako anahusika moja kwa moja na kifo cha aliyekuwa mke wake wa kwanza, unakumbuka siku moja nilikuambia uende kwenye chumba kimoja cha wageni ukashuhudie nini mume wako anafanya…sasa yale niliyokuwa nikikuambia utayashuhudia mwenyewe moja baada ya jingine, hivi sasa yule mfanyakazi wenu wa nyumbani kajifungua na ….’ Simu ikakatika.

Hivi kwanini hawa watu hawataki niwe na amani na ndoa yangu, nikajisemea kwa hasira na kukimbilia ndani nikijua tu hawa ni wale wale wasioitakia ndoa yangu mema, nikasubiri mume wangu alipokuja nikamuuliza kuhusu taarifa ya kujifungua kwa mfanyakazi wetu wa ndani, akasema kwa upole

‘Mke wangu hayo siyamekwisha pita naomba tuachane nayo, huyo sina mahusiano naye tena, na kama kajifungua atajua mwenyewe…’ akasema kwa unyonge. Nilihisi kuna jambo linamsumbua sana mume wangu kwani upole wake ulikuwa sio wa kawaida.

Baada ya miezi kadhaa nikapokea tena ile simu ya mtu nisiyemtambua ikisema kuwa Yule mtoto wa aliyekuwa mfanyakazi wetu amefariki kwa kifo cha kutatanisha na mume wangu yupo matatani, kwani baada ya kufariki Yule mtoto kuna watu walishikwa makaburini wakifukua lile kaburi la huyo mtoto na walipobanwa walisema mume wangu ndiye aliyewatuma kulifukua, na hawakujua kuwa baada ya kulifukua kitafuata nini…

Haya maneno niliyaona kama upuuzi Fulani, kwanini mume wangu awatume hawo watu kulifukua kaburi la huyo mtoto. Nikamuuliza mpiga simu, je walipomuuliza mume wangu alisema nini. Yule mtu aliyepiga simu alisema kuwa mume wangu alijitetea kuwa alikuwa akihamisha msiba kwenda kwao, na hiyo hufanyika kwa kuchuku mchanga wa pale kaburini. Lakini cha kushangaza yeye alikua na kiroba, je mchanga huwo hubebwa na kiroba…

Sikutaka kuyasikiliza hayo maneno zaidi nikakata simu, ila maneno ya mwisho ya huyu mpigaji yalinipa wasiwasi kidogo, yalisema hivi..`mume wako ni tajiri, lakini hujawahi hata siku moja kuchunguza huo utajiri wake anaupata kwa njia gani, leo kwa wenzako kesho kwako…’.

Ujue muda wote huu tulishatafuta mfanyakazi mwingine, na huyu binti alikuwa haraharaka na kuwa binti mrembo sana, kiasi kwamba niliingiwa na wasiwasi kuhusiana na mume wangu, kwani ukiumwa na nyoka utaogopa hata unyasi, ingawaje kwakweli alijitahidi sana kutokuwa karibu naye.

Ikatokea siku moja nikapata safari ya kwenda kijijini kwetu, kwasababu ilikuwa dharura, sikuweza kuondoka na Yule mfanyakzi wetu mpya. Niliporejea ilikuwa jioni, nikaingia ndani na kumkuta mume wangu hayupo, nilimkuta Yule mfanyakazi akiwa analia.

‘Vipi kulikoni, mbona unalia, akasema hakuna kitu, ila anamkumbuka mama yake nyumbani..’ mimi nikambembeleza yakaisha. Nikasema nitamdadisi baadaye, kwani mtoto wangu alikuwa akilia sana.

Mara mtoto wangu kaanza kuumwa magonjwa ya ajabu, anaweweseka, tukampeleka hospitali, lakini hali haikuridhisha, tukalazwa. Nikiwa odini. Usiku huo niliishiwa nguvu sana, mara nikamuona mume wangu akija na watu wengine wawili wakiwa wameshika kisu kikali na mmoja wa hawo watu akamwamrisha mume wangu akichome kile kisu kwenye moyo wa mtoto, mume wangu akakataa, wao wakamtishia kuwa asipofanya hivyo wao kwa niaba ya mizimu yao inabidi yeye auliwe badili, au mke wake.

Mimi nilikuwa sina nguvu kabisa hata ya kuinua mdomo, nikajitahidi kuinuka lakini wapi, na hata wale watu walikuwa hawajali kuwa mimi nipo, baadaye wakamshika mume wangu mkono kwa nguvu na kile kisu kikapenya kwenye moyo wa mtoto wangu, halafu wakakinga ile damu kwenye kichupa, na kusema, damu hii changa italeta utajiri ambao haujawahi kupatikana…’ nilishituka usingizini, na nilipomwangalia mtoto wangu nikakuta kawa baridi…nilimuita dakitari, na dakitari alipompima akasema mtoto keshakata roho……

Nashindwa kuendelea hapa… kwani pigo hilo sitalisahau maishani…

 *****************

Nimemuomba huyu dada ajaribu kunielezea nini kilifuata baadaye, kwani sasa hivi ana mtoto mwingine, kwani wakati ananihadithia hili tukio alikwa kambeba mtoto wake, na kusema alizaa na huyohuyo mume wake. Sasa  ilikuwaje mpaka akamua kuondoka baadaye? Tuwepo, kwani kuna makubwa zaidi ya hayo!

Ni mimi: emu-three

9 comments :

Anonymous said...

Hii ni movie ya Nigeria, nashindwa kusubiri hatua inayofuata, na sijui niseme nini kuhusu huyu baba, lakini nampa mama bigg five kwa uvumulivu, sijui ataweza kufika mwisho, ook, let we see the next episode

Anonymous said...

Hii ni movie ya Nigeria, nashindwa kusubiri hatua inayofuata, na sijui niseme nini kuhusu huyu baba, lakini nampa mama bigg five kwa uvumulivu, sijui ataweza kufika mwisho, ook, let we see the next episode

Bennet said...

pole sana sijui hata nikushauri nini maana sina uzoefu na haya mambo ya kilozi

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

mhhh sijui

Yasinta Ngonyani said...

Nasubiri muendelezo maana naweza nikatoa maoni ambayo sio. Duniani hapa kuna mambo

Anonymous said...

Makubwa, uvumilivu wa namna hii ni kujiua wewe mwenyewe.
Mumeo hawezi kubadilika labda mpaka Yehova arudi.

Simon Kitururu said...

Duniani kuna mambo!

Nasibu said...

Mimi ni mgeni ndani yahii blog,lakini nimesoma kisa hiki tangu mwanzo! Kitu muhimu nimeona huyu mama ni mvumilivu, pia ingawa alikua anahusisha ndoa yake na watumishi wa Mungu! yeye alikua hajiweki karibu sana na mwenyenzi Mungu,kwasababu visa kama hivi kama huyu mama angejiweka mikononi mwa mwenyezi Mungu na kusali kila siku,,lazima hata siku hiyo ya usiku alivyoona hiyo mizimu ikija kuuwa mtoto wakeau yeye,,hangekosa sauti yakuyakemea katika jina la aliye juu ya mbingu na dunia,sasa ilionekana kwamba walipata urahisi flani kuvamia moyo wa malaika huyo,Mimi nimeshashuhudia mauchawi meengi yanayoshindwa kuingilia mtu aliyezungukwa na ufalme wa Mungu.Huyu dada namshauli ajikabidhi mikononi mwa Mungu tu amekoswakoswa.Pole sana .

emuthree said...

Karibu sana Nasibu, na jisikie mwenyeji.Nakushukuru sana kwa kuwa mkarimu na kutoa maoni yako, nami nitayafikisha kwa mlengwa.
Endelea kutembelea blog hii kwani wewe sio mgeni tena.
Shukurani