Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Friday, September 3, 2010

Je wangefanya wanawake ingekuwaje?2

 Mimi sina tabia yakuweka chupi zangu ovyo , na ninauhakika niliondoka kukiwa kusafi na ile chupi ni ya kike.Nilipoikagua nikagundua ni chupi ya mafanyakazi wangu wa ndani….


nikatoka kawa hasira, na mara nikakutana na mume wangu malangoni, alishangaa kuniona lakini akajifanya hakuna kitu.

‘Vipi unaumwa nini, mbona umerudi mapema’ akauliza kwa sauti yake ya Huruma.

‘Ndio nasijisikia vibaya, nimeomba ruhusa nije kupumzika, lakini na wewe vipi safari haipo tena?’ nikauliza huku ile chupi nimeishika mkononi.

‘Nitaondoka kesho, nilikua mara moja kuna vitu nilisahau nikaona nijimwagie maji’ akasema, nilitaka kumuuliza mbona alipoondoka asubuhi alioga, lakini nikaona ninyamaze tu. Alipoiona ile chupi nimeishikilia mkononi akashituka na kujibaragua kuwa anaharaka anataka kuondoka.

‘Mume wangu ni kitu gani kinaendelea humu ndani, mbona siwaelewi, au …’ nikaanzisha maneno lakini yeye akajifanya anaharaka na kuvaa nguo zake na bila kusema zaidi akaniaga na kuondoka. Yeye tangu aambiwe na dakitari kuwa, kutokana na hali yangu ninaweza kuwa na hasira, au kuchukia na vinginevyo na anachotakiwa nikunivumilia au kunidharau, hadi nitakapojifungua hiyo hali itakwisha, basi ndio ameamua kuchukua nafasi hiyo kufanya analotaka. Haiwezekanni, nikatoka mbio kumfuta Yule mfanyakazi

‘Oooh, afadhali nilikuwa tangu jana naitafuta chupi yangu, kumbe ipo kwenu, au ulisahau ukaichukua ukidhani ni ya kwako …’ akanijia na kuibetua ile chupi, huku nikijiuliza, hivi kweli hawa watu wananiona mimi mjinga au siwaelewi na huo uchafu wao wanaofanya.

‘Nakuhakikishia kuwa siku zako za kusihi humu ndani zinahesabika, musinifanye mimi sijui mnachokifanya, …’ nikaondoka kwa hasira na hadi kitandani kwangu, na mara tumbo la uchungu likanishika, niliwapigia ambulasi wakaja kunichukua na siku hiyo nikajifungua mtoto wa kike.

Kesho yake nikaruhusiwa kurejea nyumbani naikimuomba mungu mume wangu ajirekebishe ili tuishi maisha ya amani na upendo, kwa kuhakikisha hili nilimuita ndugu yangu ambaye ni mtu mungu akaja kutuombea na kutoa mawili maatatu ya nini kinahitajika katika ndoa. Mume wangu alikuwa mnyenyekevu na kusema yeye hana shaka na maswala ya ndoa atajitahidi kama alnavyofanya kila siku.

Ikapita miezi kama mitatu hivi, nikahisi mabadiliko ya huyu mfanyakazi kimwili na mara nyingi akawa hapendi kula, na dalili zilionyesha dhahiri kuwa ni mja mzito. Nilimbana lakini kama kawaida yake akakataa katakata. Nikamuuliza mbona karibi miezi mitatu sijaona ukiniuliza `pedi ‘?

‘Ninanunua kwa pesa zangu…’ akanijibu huku ananikwepa kuniangalia machoni. Na siku hiyo akasema anaumwa, basi nikamwambia nitampeleka mimi hospitali.

‘Hapana nitampeleka mimi mwenyewe, wewe hutakiwi kwenda, mtoto anakuhitaji sana’ akaniambia mume wangu.Nami nikamwambia, kama ni hivyo, yupo jamaa yetu anayetusaidia mara kwa mara ngoja ampeleke yeye kwani hata yeye anahitajika katika kumhudumia mtoto. Akakubali shingo upande. Nilimuita Yule jamaa pembeni kumwambia kuwa ahakikishe anamweleza dakitari ampime mkojo , na jamaa akanielewa.

Waliporejea mume wangu alikuwa ametoka kidogo, jamaa yangu akanipa majibu ya vipimo, na kama nilivyokisia huyu mfanyakazi wa ndani alikuwa mja mzito na mimba ya miezi miwili na kitu. Ikawa shughuli kumjua ni nani aliyempa huo ujauzito? Nikamuita mtu wa dini ambaye kwa kuheshimika kwake alimbana sana Yule binti na kukiri kuwa mimba ni ya mume wangu….nilizimia.

Je jamani kama ingelikuwa ni sisi wanawake tumefanya hivyo ingelikuwaje?

Swali hilo tumeulizwa, , naomba usicheze mbali kwani ipo sababu kubwa iliyotokea hadi huyu mwanadada akaamua kumkimbia mume wake. Ni ipi hiyo, tuonane kwenye sehemu nyingine

Ni mimi: emu-three

6 comments :

Yasinta Ngonyani said...

Wanaume janami wanaume yaani mfanyakazi wake anaanguka naye. Hata kuvumilia tu kunashindikana....nasubiri muendelezo maana hapa naona sasa panakuwa pazuri/utata..

Upepo Mwanana said...

Kabla hata picha haijaisha... mijibaba mingine.. hovyoooo

Anonymous said...

Mimi sijaoa, najiuliza sana hili swali na nakumbuka kuna mahali nimesoma pia, kuwa 'Hivi kweli mtoto wako ukimshibisha ataenda kula kwa jirani?'
Nahisi kuna walakini kwa wanandoa na hili linanipa wasiwasi sana, watu wazima mumeoana, kwanini msiambiane ukweli, kwamba nina njaa, na mwenzako pia ajua umuhimu wa kuhakikisha kuwa nyote mnashiba, nikiwa na maana tendo la ndoa.
Mimi inanipa wasiwasi kuwa , wananda ambao mumebahatika, hamtaki `ukweli' kuwa kuna walakini wa `kushibishana chakula hicho kitakatifu' sidhani kama mtu akishiba, atakuwa na haja ya kuchepuka na mfanyakazi wake.
Pili kuna `mvuto' yaani kukukubali kuwa mkioana, mnajisahau kujiweka kumvuto, mapaka mmmoja wapo anakuwa hamtamani mwenzake, inakuwa kama kaka na dada, sasa akitokea mvuto ndani yenu, na muda wote mpo pamoja, basi njaa inaongezeka, na matokeo yake mtu anakwenda kwa jirani, na kwasababu jirani kaja yupo hapo nyumbani, basi mambo yana kuwa rahisi.
Nawaombeni msidhani kuwa ninaunga mkono, kosa alilofanya huyu jamaa kutembea na mfanyakazi wake, ila naangalia ile hali halisi ninayohisi mimi , kama nimekosea mnifahamishe kwani nami nataraji kuingia kwenye ndoa karibuni.

Mimi mwanandoa mtarajiwa

Anonymous said...

Hizi stori zako bwana zinatuzalilisha wanaume, unawapa kichwa wanawake watuone hatuna maana, kosa la mtu mmoja, basi utawaona wanawake wanasema `wanaume ndivyo walivyo..'
Mimi nawaambia ukweli uovu huo haupo kwa wanaume pekee, kama mwanaume ni muovu kwa kutembea na mfanyakazi wake, mwanamke ni muovu kwa kutokuweza kumtimizia mume wake mpaka anashindwa na kutembea na mfanyakazi wake.
Na sio natetea hili, ila wanawake na wao wana maovu yao ya kutembea na hata wafanyakazi wao wa nyumbani, ngoja ipo siku nitakitafuta kile kisa nitawatumia.
Kwa ujumla nasema `sote wanaume, na wanawake hatupo kamilifu' kwasababu tumemsahau mungu, kama kweli tungekuwa tunajua kuwa mungu yupo, tungeogopa kutenda dhambi iwe ya siri au dhahiri.
Maoni yangu ni kuwa tumrejee mungu na tukifanya hivyo tutaishi kwa amani

Anonymous said...

Hayo wakati mwingine mnayataka wenyewe, binti anakuja mshmnamnawirisha anapendeza kuliko mamaaa, wewe unakaushiwa na mamaa, sasa ukizidiwa uafanyeje!

Bennet said...

Tatizo lipo kwa huyo mwanamke ambaye ni house girl kwa kutembea na Baba mwenye nyumba, najaribu kuangalia upande wa pili wa shilingi