Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha
Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..
Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.
MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.
TUPO PAMOJA DAIMA
Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;
https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:
https://www.facebook.com/diaryyangu/
`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;
Tuesday, August 3, 2010
Yote mapenzi ya Mungu
Mapikipiki yalikuwa yameongozana kuelekea makaburini, na kuleta mshangao kwa wapita njia, na wale wasiopitwa na kitu wakaanza kuyafuatilia nyuma. Na sisi ambao tulikuwa tukijua ninii kinachoendelea tuakaona ni heri tufike eneo la makaburini ili kuhudhuria mazishi ya jirani yetu. Na wakati tunatembea kuelekea huko makaburini, ndipo udadisi ukaanza.
'Hivi hizi ajali za pikipiki mbona zinaongezeka' mmoja akasema
'Lakini hii huiwezi kuiita ajali, huu ni ujambazi, kwasababu huyu hakufa kwasababu ya ajali, bali aliuliwa na majambazi' akasema mmojawapo.
Kwa taarifa tulizozipata, marehemu alikuwa kijiweni kwake akisubiri abiria, na ilipofika saa tatu na nusu usiku mwenzake akaja kumwambia kuwa waondoke, kwani muda huo sio mnzuri tena kumsafirisha abiria hasa wa maeneo ya mbali.
'Ngoja kidogo tunaweza kumpata mtu anayeelekea njia ya nyumbani' akasema marehemu. Lakini muda ukapita bila kupata abiria na wakaona waondoke. Na kabla hawajaingia barabarani, mara watu wanne wakaja, wakitaka kupelekwa huko wanapokwenda. Jamaa kwa vile walitaja njia ambayo inaelekea wanapokaa huyu marehemu wakasema sawa. Basi wawili wakapanda kwa merehemu na wawili wakapanda kwa rafiki yake, na safari ikaanza.
Walipofika kwenye bonde ambalo lipo mbali na makazi ya watu, marehemu aliyekuwa mbele akasimamisha pikipiki ghafla, na kumfanya mwenzake aliyekuwa akimfuatilia nyuma afunge `break' za haraka. Na kabla huyu rafiki yake hajajua nini kimetokea akasikia kitu kizito kikigonga kichwani mwake na nguvu zikamwishia na kujikuta anodondoka chini, na kabla hajajitetea na kilichotokea akasikia tofali likipasiuka kichwani mwake na kupoteza fahamu.
Kwa taarifa zaidi ya watu ambao wanasema walifika mahala hapo muda mfupi baadaye wanasema waliona kikundi cha watu kikikimbilia maeneo ya vichakani na pikipiki na huenda ndio hawo majambazi na inavyoonyesha ni mpango uliosukwa na kikundii cha watu, kwani waliowaona hawo watu wakikimbilia vichakani wanasema ni zaidi ya watu kumi.
'Nasikia pia biashara ya injini za pikipiki imakuwa kubwa kwani wateja wakubwa ni wavuvi wa samaki wanaohitaji kwa ajili ya kutengenezea injini za maboti' akasema jamaa mwingine.
Vyovyote iwavyo juhudi kubwa kwa polisi wa usalama barabarani kwa upande mmoja na usalama wa raia kwa upande mwingine zinahitajika ili kukomesha wimbi hili la ajali na ujambazi unahusishwa na pikipiki. Vijana wengi wamepoteza viungo kwa jali za pikipiki na wengine wapo taabani mahospitalini. Na hutaamini kila kjana ana mpango wa kutafuta pikipiki kwasababu wanasema biashara hiyo inalipa.
Majmabazi nao hawapo nyuma, wamgundua kuwa biashara ya pikipiki ni nzuri na zaid ni kuwa injini za pikipiki zinatafutwa sana kwa ajili ya maboti ya wavuvi baharini na maziwani. Wao kuua sio jrahisi sio jambo dogo, ilimradi wamepata wanachokitaka, na hapo ndipo wanausalama mnapotakiwa kuwajibika ili kutimiza ile dhamira ya kulinda raia na mali zao.
'Yote ni mapenzi ya mungu tunakubali kwa hilo' lakini tahadhari ni muhimu kwani wimbi hili la ujambazi ni kubwa kuliko watu wanavyodharau, na inavyokwendaa itafikia kuporwa kitu umeshika mkononi na mwendesha pikipikii akapotea mitaa mingine, utamkimbizaje wakati yupo juu ya pikipiki na mwendo wa pikipiki unaujua. Hii ni kwasababu pikipiki zitakuwa nyingi kuliko wateja na vijana wenye tamaa hawatakubali kukaa bila kupta pesa na hapo watahamankia na wizi huo kama wanavyoona kwenye sinema.
Tahadhari kubwa ni kwa waendesha pikipiki wenyewe kukubali kusitisha biashara hiyo inapofikia muda wa ioni kama mtu hujapata basi riziki haipo subiri kesho ili madhara hayo ya ujambzi yapungue na hata wakigundua njia nyingine bado mtakuwa mumejipanga vizuri.Na jingine ambalo mnalijua ni sheria za uendeshaji wa hiyo pikipiki je umeshaijua vyema kabla hujaingia barabrani?
Ni mimi: emu-three
2 comments :
yaani kwa kweli nadhani serikali ingechukua hatua kali za kuzuia uingizaji wa pikipiki, kwani zimekuwa zikichangia kuleta mauaji, ulemavu na umasikini.
Wachina wameamua kutumaliza kwa namna moja ama nyingine kwani pamoja na kuibiwa kwa pikipiki hizo si imara pia
Pikipiki hizi ni kero na zinazidisha presha, kwa mfano ukishuka ndani ya daladala kama vile Mombasa, unakuta pikipiki zinakusubiri unataka kuvuka ili ukaingia magari ya Moshi bar, zinakukatisha mebele, usipoangalia uanweza kugongwa.
Nafikiri zingetulia mahali pamoja, kama mtu anazihitaji aende zilipo, zio mbrrrrr, mara hii miguuni, inakera na inatia presha
Post a Comment