Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha
Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..
Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.
MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.
TUPO PAMOJA DAIMA
Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;
https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:
https://www.facebook.com/diaryyangu/
`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;
Thursday, August 5, 2010
Dua la kuku halimpati mwewe
Ukitaka kujua mazila na mtihani wa magonjwa fika hospitalini, kwani unaweza kujiona wewe ni nafuu, na ukitaka kujua shida za kutafuta haki nenda mahakamani unaweza ukajiuliza hivi hii haki inapatikanaje kwa hali kama hii, na kwanini isiwe rahisi kuipata.
‘Kesi yenu imeahirishwa mpaka mwezi ujao tarehe …’ maneno yanamtoka hakimu ambaye anaongea kutokana na vipengele vya sheria bila kujali ni nani anayepigwa hizo danadana. Kwake yeye hana kosa kwani mawakili ndio watakaomshawishi kisheria ili aweze kutoa hukumu yake.
Nilikuna kichwa na kutafakari, sasa takribani miaka saba kesi bado inapigwa kalenda, kila ukifika mahakamani tajiri aliyeshitakiwa anaweka pingamizi, na kwakwe yeye hakuharibiki kitu, kwasababu ana mawakili na kitengo chake cha sheria ambacho moja ya kazi zake ndio hizo za kusimamia kesi, sasa hawa watu wanaofanya kazi humo ambaoo kila mwisho wa mwezi wanalipwa wataonekanaje wanafanya kazi!
Tajiri huyu kulipa hela tunazodai baada ya sisi kukubali hata hicho kidogo alichoridhia nacho, imekuwa bado ni hasara kwake, inngawaje anaweza akalipa hela nyingi kwa jambo jingine lisilokuwa na manufaa kwake kabisa, lakini kumsaidia yule aliyemwaga jasho kwake anaona kazi! Nikajiuliza kwanini, na kabla sijapata jibu kichwani mmoja wa waliofika kusikiliza hii kesi akasema, `ama kweli tajiri kuingia mbinguni ni sawa na ngamia kupita kwenye tundu la sindano.
‘Kwanini unasema hivyo, msipende kulalamika, nyinyi fuateni wanavyotaka, hata wakiweka pingamizi mara mia, nyie kubalini na fuateni wanavyotaka…’ akasema mwanasheria wa chama cha wafanyakazi.
‘Hivii tukiamua kufuata hivyo si wote tutaishia kufa na hela hizo watazipata akina nani’ mama mmoja akasema kwa uchungu.
‘Watarithi watoto wako…’ akasema Yule mwanasheria bila ya kujali kuwa Yule mama aliyemjibu hivyo ameitumikia kampuni iliyomdhulumu zaidi ya ,miaka thelathini, na mwisho wa siku alitupwa nje kama takataka zinazonuka.
‘Mungu yupo ipo siku kilio cha wanyonge kitasikika, na kilio cha wafanyakazi wanaodhulumiwa ni kikubwa kabisa kwani wao kodi wanazilipa bila kukosa, kwani wao ndio wanaovuja jasho kihalali…’ akasema mama mmoja akiwa kachoka kwa kusimama.
‘Hiyo ni dua ya kuku mama, haiwezi kumpata mwewe, unachotakiwa si kulalamika ni kufuata sheria inasemaje, jaribuni kulielewa hilo, ukilalamika utamdhuru nani, huyo mwajiri wala haumii kitu, wewe ndiye unayeumia na roho yako’ akasema tena Yule mwanasheria.
Ni kweli wanavyosema kuwa tajiri hata umuombee dua gani haimpati, na ndio anazidi kuneemeka, kwake yeye kutoa hela sio jambo rahisi hasa akipata mwanya wa kuchelewesha atautumia hadi dakika ya mwisho, kwani shilingi mia ya leo sio shilingi mia ya kesho. Na hata hivyo hawo walioajiriwa kusimamia maswala ya sheria na utawala wataonekanaje kuwa wanafanya kazi! Mwajiri akiizungusha hiyo shilingi mia kwa miaka kadhaa atakuwa kesharudisha hiyo hasara atakayoipata kukulipa wewe. Na wale aliowapa majukumu ya sheria na utawala wataonekana wanafanyakaza, licha ya kujali kuwa leo ni sisi na kesho huenda ikawa ni zamu yao.
Kwa vyovyote iwavyo sheria bila ya mwanasheria unakuwa kama kucheza mpira pasipo na kocha. Swali ni je walala hoi ambao wameshatupwa nje ya uajiri ambao mishahara yao ilikuwa mkono kwa tumbo watawezaje kumpata huyo mwanasheria. Na hata kama wataamua kuwatafuta wale wanasheria wanaojitolea, ina maana kweli hawo wanasheria hawana njaa, kwa mfano..!
Labda tuendee kusubiri huku tukiomba dua, hata kama dua la kuku halimpati mwewe, kwaniipo siku ….
Kama umeipenda hii, unaweza kusoma pia hii:
http://miram3.blogspot.com/2010/02/imekula-kwetu.html
Ni mimi: emu-three
2 comments :
Acheni kulalamika mumejitakia wenyewe, kama kweli inawauma uchaguzi unakaribia, fanyeni kweli mlete mabadiliko
Nani alisema dua la mnyonge halimpati mdhulumati, we subiri tu tuombe uhai, angalia kesi za maraisi wakubwa wa nchi nyingine, walijua itawakuta haya, sasa hawo ni madume, sembuse sisi vijogoo wa chini. Ipo siku haki itatawala na ukweli utadhihiri, nyie timizeni wajibu wenu na mtegemeeni mungu sana. Dua itajibiwa soon!
Nakupongeza kwa blog yako na nimeona unawatembelea sana wenzako, ingawae wao hawaji kwako, usikate tamaa, unayozungumza ni ya ukweli mtupu! Na inavyoonekana wewe unayakabili maisha ya kikweli ya walala hoi!
Post a Comment