Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Thursday, August 19, 2010

Rushwa ni adui wa haki

‘Hebu tuambie, miaka mitano iliyopita ulitufanyia nini cha maana’ akauliza mzee mmoja


‘Nilimewafanyia wananchi wangu mengi, angalieni zile barabara mbilii za kutoka juu kwenda chini na ile ya kutoka bomba la mafuta hadi magongokuinama….hiyo ni mifano miwili tu, bado mengii nimeyafanya, nafikiri wenyewe mumeona, nipeni kura ili niweze kumalizia yale ambayo hayajakamilika kama hizo barabara tumezifukia tu mashimo na kujengea madaraka bado hatua ya pili…’ akasimamishwa muda ulishaisha

‘Lakini mheshimiwa, ukisema hizo barabara mbili umehusika wewe naona sio sawa, kwasababu wanachii wenyewe walikutana wakachangishana na kuomba matrekta ya kuchimba na kujaza kifusi, na unakumbuka kuna siku tulikuja kwako kuomba kama utatuwezesha matreakta ukasema una maswala mengii ya juu ambayo unayafuatilia kwahiyo hukuwa na nafasi ya vitu vidogovidogo kama hivyo, sasa unadai uliwahi kuzijenga kuzitengeneza hizo barabara?’ akauliza mama mmoja
'Pia utuambie ile zahanati ya maeneo yetu ambayo katika kuomba kura kwako mwanzoni ulidai utaishughulikia imeishia wapi?' akauliza mama mwingine

‘Mimi nilitoa michango mingi sana, sio lazima mimi nije kama mimi nilitumia watu wangu kushughulikia , wakafuatilia kwahiyo….’ Akakatishwa na kuzomewa.

Kwahasira akakaa chini huku akinung;unika kuwa kuna njama za kumwangusha.

Baada ya kura za maoni alionekana kushinda kwa kura nyingi sana, wananchi hawakukubali ikabidi wafuatilie na kweli iligundulika njama imetumika, na walipobanwa sana wahusika wakabatilisha matokeo.

Hili ni tukio moja tu tulilolishuhudia kwenye kura za maoni zilizofanyika karibuni, na wanachi walipoona watu wao waliowateua na kuwapigia kura hawakupita, wakadai kwa pamoja na hatimaye wakapewa haki zao. Kumbe basi, tukiwa na umoja, tukadai haki zetu tunaweza kupewa. Kwanini sasa tunaogopa kuzidai pale tunapozikosa.
Hata hivyo hili tukio mimi lilinishitu kidogo, kuwa hawo waliompa ushindi huyo jamaa ndio hao hao waliobatilisha hayo matokea, na kumpa Yule aliyeonekana kushindwa, baada ya kushauriana wao kwa wao. Je kulikuwa na nini kiliendelea hapo katikakati?

Hili limevuta masikio ya wengi na kujiuliza mengi, kuwa kama huo mchakato ulifanyika ndani ya chama na mambo hayo yakagundulika, itakuwaje vikikutana vyama vingi? Ni changamoto kwa wasimamizi wa uchaguzi huu, kwani wananchi wameshaanza kuelewa haki yao. Na hawo ni wachache tu, waliokwisha kuelewa , lakini siku zinavyozidi kwenda watu wengi zaidi wanaanza kuelewa nini maana ya demokrasia, nini maana ya kura yao, na hatimaye watu watajua nini maana ya haki zao, na ndio utakuwa mwisho wa adui rushwa.

Wimbo wa adui rushwa umekuwa ukiimbwa midomoni kila mara, na wanaoimba kwa sauti ni viongozi wetu, nasi tunabakia kuitikia, lakini je matendo yetu na viongozi wetu yanakubaliana na huu wimbo? Sijui , kwa vyovyote iwavyo rushwa ni adui wa haki zetu, na ili tumshinde huyu adui rushwa inabidi tijizatiti kwelikweli kwani zipo haki nyingi zimeshikiliwa na wanaojua utamu wa rushwa, je tutazipataje kutoka kwao, jibu ni rahisi tu, wewe ndiye uliyempa nafasi ya kuzishikilia hizo haki zako, na wewe una uwezo kabisa wa kumuondoa na kumweka mwingine ambaye anajua kuuimba huo wimbo sio kwa midomo tu hata kwa matendo yake. Ndio tuimbe kiapo hiki kwa pamoja kwa midomo yetu na kwa vitendo pia kuwa `rushwa ni adui wa haki , sitapokea wala kutoa rushwa’

Ni mimi: emu-three
Enhanced by Zemanta

2 comments :

Anonymous said...

Hii inadhihirisha wazi kuwa kamchezo hako kachafu kalikuwepo na mungu ametuonyesha dhahiri, sasa kazi kwetu, ikifikia uchaguzi, kwanza kuhakikisha kuwa sote tunapiga kura, tuwe na mawakala waaminifu, na kuzilinda hizo kura zetu

Anonymous said...

Swala la rushwa katika nchi yetu ni donda ndugu, kwani hata sisi mitaani tunasema kuwa ili tumpitishe mgombea tunataka atuonyeshe kuwa anatujali, agawe kitu kitogo, sasa huku sio kuwaomba rushwa hawa wagombeaji. Nafikiri yote haya ni sababu ya umasikini wetu