Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Monday, August 9, 2010

Penye uzia penyeza rupia

'Umati nilioukuta pale hospitali ulinifanya nikate tamaa, na hali ya mgonjwa ilihitaji huduma ya haraka sana, ikabidi nimuulize mwenzangu tufanyeje, manake kumtoa pale kwenda hospitali nyingine ni kupoteza muda, na foleni za hapa Dar. Mwenzangu akaniuliza nina shilingi ngapi mfukoni, nikashngaa, kwani maana ya kuja hospitali hizi za serikali ni kuwa hali zetu ni zofli, vinginevyo ningekuwa na pesa siku kama ya leo ya mwisho wa juma ningempeleka hospitali za watu binafsi.
'Nina elifu kumi tu' nikasema kwa wasiwasi
'Hiyo ni nyingi sana , hebu nipe elifu tano tu' akasema mwenzangu.
 Nikampa mimi nikabakia na mgonjwa na nilivyomuangalia hali yake ilikuwa inakwenda kubaya, ikabidi nichuchumae pembenei yake nakuanza kumuombea.
 Mara kigari cha kubebea wagonjwa kikaletwa na nesi mmoja, na kumchukua yule mgonjwa ambaye alipelekewa nyuma ya lile jengo ambako kuna mlango wa nyuma wa kuonana na dakitari. Haikupita muda nikaitwa ndani na dakitari akaniulza maswali mengi kuhusiana na mgonjwa na hatimaye akapewa kitanda.
Tulivyotoka nje kwa kupitia mlango ule wa kawaida tuliwakuta wagonjwa wengien taababi kama alivyokuwa mgonjwa wangu na waliowaleta wakawa wanajaribu kuwaomba wagonjwa wengine ili angalau wamuone dkitari, lakini haikuwa rahisi kila mgonjwa alidai kuwa na yeye anaumwa sana.
'Utawapisha wangapi, kila anayekuja kazidiwa , hamfanyi kama walivyofanya wengine, hawo wanaotoka walitukuta hapa sijuiwamepitia mlango gani , hapa wasingepita' akasema jamaa mmjoa aliyekuwa mlangoni akisubiri kuingia kwa dakitari.
'nyinyi nchi hii hamujui jamani, kila penye uzia, penyeza rupia, mtakaa hapaa mpaka jioni, mwishowe mnaambiwa mrudi kesho' akasema jamaa mwingine ambaaye alishakata tamaa na kujilalia pale sakafuni.'sasa kama huna hiyo rupia utafanyeje manake ndio maana tumekuja huku, kama tungekuwa na rupia tungeenda hospitali za hela ' akasema jamaa mmoja
'Sasa usilalamike waache wenye rupia watibiwe kwanza baadaye tutatibiwa sisi angalau kupewa panadol.' aksema yule jamaa aliyelel chini.
 Mimi niliiuliza maswali mengi ambayo mwisho wa siku unajikuta huna jinsi na lawama huwikwep, kwamba hilo tulilolifanya ni kosa, na je kama tusingefanya hivyo ili kumuokoa mgonjwa wetu ingekuwaje? Hiyo ni sehemu moja tu ambayo kupata huduma inakuwa shida, kwasababu wanaohitaji hiyo huduma ni wengi kulikokuliko wanaitoa hiyo huduma, kiasi kwamba muda mnaokaa kusubiri ni mrefu sana na matokeo yake kama ni mgonjwa ataumia zaidi hata kupoteza maisha kama ni mfanyabishara au mfanyakazi ataishia kupoteza siku na hata kupata hasara.
 Je unapukumbana na kadhia kama hiyo utafanyaje, ukae kimya na usubiri matokeao au upenyeze rupia, na huko kupenyeza rupia wote tunajua ni rushwa hata kama tutakuita kwa majina anuia, wengine wanaita `speed-up', wengine waanaita`ten-percent' ', takrilama na mengineyo, lakini yote lengo ni moja kupata huduma kwa mlango wa nyuma, au kupata huduma mapema kabla ya wengine, au kupata unachokitaka ili wengine wakose,ili kuokoa maisha ya mgonjwa au ili uwahi kazini au ili wewe upewe kipauumbele, na  vyovyote iwavyo.
 Sehemu kubwa ya huduma hapa nchini ni kwa mwendo waq foleni, ukienda benki folenii hata kwenye ATM, ukienda hospitali ndio usiseme, ukienda maofisi ya serikali ndio usiombe je huu muda tunautizamje? Au muda ni kwako tu, wengine hawana umuhimu na muda, au ndio danganya toto ili rupoia ipenyezwe, kama ni hivyo  simseme tu!

Ni mimi: emu-three

4 comments :

Anonymous said...

Huu usemi umekaa kifisadi fisadi na mafisadi wanautumia kinufaisha dhana yao, lakini uliwekwa hapo kwa nia njema kabisa kuwa kila kwenye tatizo kuna njia nyepesi ya kulifanya hilo tatizo liwezeshwe, kwa mfano umekwama na gari lako linahitaji lisukumwe, ili hiyo kazi ifanyike unatakiwa utoe hela kwa watu zaidi ya mmoja.
Sasa mafisadi wao wanachukulia huduma ambazo ni haki, na huduma hizo zinazembewa na watendaji kwa minajili yao binafasi, huenda wanalipwa kiduchu, huenda ndio uzembe, watu wengine wana asili ya uzembe, huenda ndio wanaotaka kupenyezewa rupia, nk.
Kama watendaji wangeliwajibika ipasavyo, huo upotezaji wa muda usingekuwepo, hebu jiulizeni mbona watu binafsi wanaojali kazi zao hawana huo uzembe...

Anonymous said...

Sikiliza bwana, kuna dharura ambayo inabidi ufanye hivyo, lakini walarushwa kila jambo lazima warushe.
Na nikwambie ukweli hali halisii ya nchi za Afrika ndiyo inayotutuma tufanye hivyo, kwasababu yule mtoa huduma mwenyewe kachoka ile mbaya , mshahara wenyewe mungu anajua sasa wewe unakuja na hela zako ataacha kupokea, na kwasababu keshajua hilo ndio maana na yeye anakucheleweshea ili utoe chochote. Hii haihitaji kuambiwa hata hawo waliowekwa kwa ajili ya kuzuia rushwa siku ikimukuta la kumkuta atakuwa wakwanza kumpa chochote nesi ili ahakikishe mgonjwa wake anapata huduma! We aacha we, kuuguliwa sio mchezo.

Fadhy Mtanga said...

M3 hii ndo Tanzania zaidi uijuavyo. Wiki mbili zilizopita nilipeleka mgonjwa pale Tmk hospital. Ndicho nilichokumbana nacho.

Kazi ipo sana.

EDNA said...

Duuh kazi kwelikweli,tutafika kweli?