Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Tuesday, August 10, 2010

Lile usilolijua ni kama usiku wa giza

'Baba nanihii yupo ndani, manake nataka kukuuliza kitu, sitaki asikie' nikasikia huo mnong'ono toka nje, na wasemavyo wahenga, mvuto wa ubaya unazidi wa uzuri, nami nikajikuta nasogelea dirishani ili kusikia nini kinatetwa, wakati nilijua kabisa kufanya hivyo sioo vizuri
'Sijui ni mimi tu au wenzangu mna tatizo kama hilo, manake mimi imefikia hatua nashindwa kuvumilia...' akaanza kuongea huyo mwanamama, na kila mama nanihii alipotaka kumsimamisha asiendelee kwasababu alijua nipo ndani na uwezekano wa kusikia hayo ni mkubwa , alishindwa akawa anaishia kukatakata maneno ya `a..a...a.  we.....'
'Mume wangu ana tabia mbaya, kiasi kwamba nilitamani nimkimbie manake atanitia aibu. Mimi kama mtoto wa Kiafrika, lazima nizilinde mila na destruri zetu, sijui kama dini zinasemaje kwa hili, lakini mimi najua kuwa mila nyingi za maisha ya ndoa zinakwenda sawa. Sasa nashindwa kujua kuwa labda ndio maisha ya mjini au ni tatizo la mume wangu tu...'
'Hebu kwanza sogea huku, manake unaongea tu hata kabla sijakujibu kuwa baba nani hii yupo au hayupo umeshaanza kuropoka...' wakasogea upande mwingine wa nyumba, hawakujua kule walikosogelea ndipo sauti ninaiapata barabara, nikafungulia kinasa sauti changu cha asili nakujua hili litakuwa tukio murua la kesho.
'Tabia mbaya kwa vipi, manake nakumbuka siku kadhaa nilikuuliza maendeleo yako na mume wako ukasema ni mazuri sana , leo imekuwaje?' akauliza mama nanihii
'Mwanzoni niliogopa nikijua haya ni maswala ya ndani na nilijua kwa vile ni mwanzoni na tumeanza kuzoeana itafika siku ataacha, siunajua tena mwanzoni watu mnakuwa karibikaribu sana, au sio, lakini siku zilivyozidi kwenda nimegundua kuwa mume wangu ndio tabia yake. Na mimi siipendi ni kosa kubwa katika desturii zetu, haiwezekani  yeye aniingilie maswala yangu binafsi, haiwezekani....'akaendeeea kuongea kwa jaziba kiasi kwamba sauti yake kila alivyozidi kuongea ikawa inakuwa kubwa, kuliko mwanzoni ambapo alikuwa akinong'ona.
'Mambo gani binafsi amkuingilia, manake siku hizii dunia imeisha, kama ni mabaya lazima tuchukue hatua, au unasemaje?' akamuuliza mke wangu  kwa utani.
'Kumchukulia hatua hapana, ila kwanza nataka kujua kuwa labda hata nyie mnafanyiwa hivyo, kama ni hivyo basi nitajua ni maisha ya mjini , kwahiyo nitajua cha kufanya vinginevyo mimi nitafunga nyumba niende kwa wazazi wangu nikawaulize je huyu ndiye mume mliyesema anatabia nzuri, tabia yenyewe ndio hiyo...
' akasema na kupunguza sauti
'Unajua mume wangu ana tabia mbaya, kila nikiwa jikono haachi kunifuatafuata na kuingilia mambo yanguu ya jikono, ofisini kwangu manake jikoni ndio ofisi yangu. Sipendi, manake kwanza ananinyima uhuru wa kufanya kazi zangu za jikoni, halafu sio tabia njema kwa wanaume kuja jikoni wakati tunawajibika, mbona mimi simwingilii katika kazi zake, akiwa kwenye kikomputa chake hataki hata mtu kumsogelea, lakini mimi anakuja jikoni, mara anaonja hiki mara ..ana...'
 Unajua nilishindwa kujizuia kucheka ,sijui hiyo sauti ilisikika nje, kwani ghafla nikawaona wanasogea upande mwingine wa nyumba, na sauti ikawa inakuja kwa shida.
 Huyu mama analalamika kuwa mume wake hupenda kuja jikoni, na kufanya kazi ambazo yeye anadai kuwa ni kazi zake na huko nikuingiliwa katika ofisi yake, anasema wakati mwingine mume wake anachukua nyanya au vitunguu na kumsaidia kukatakata, anasema huko ni kumzalilisha na kuonekana kuwa hajui wajibu wake, na baya zaidi wakati mwingine anaambiwa akae pembeni ili mume wake amuonyeshe jinsi gani anavyojua kupika kitu fulani. `Mimi najua kupika tangu utoto, leo hii eti mume anifundishe...hata hii imevuka mpaka' alisema maneno haya kwa kwa jaziba na kuongezea kuwa kimila desturi hiyo mbaya kwa mfano watu wa kwao wakijua watamsema sana kuwa amemfanya vibaya mume wake. Sijui huko kumfanya vibaya alikuwa na maana gani. Labda ndio hilo wanaloita limbwata....
 Anasema ipo siku moja wakiwa nyumbani mume wake alikuja akamshika kiuno, akiwa anamtambulisha kwa watu anasemaa siku hiyo alitahayari hajawahi kutahayari kama hivyo. `Hizo ni tabia mbaya, kwetu hazitakiwi. Kama nikunishika hivyo, asubiri chumbani, tukiwa tumezima taa!'
 Unajua maswala mengine unaweza ukacheka na kumuona huyu mama ni mshamba wa mapenzi, lakini huyu mama ni wale akina mama waliolelewa kiutaratibu wa kimila na anajua kabisa mila ndio msingi wa maisha ya mke na mume, aliwaona baba na mama yake wakifanya hivyo na ndoa zao zimedumu hadi uzeeni, kwahiyo yeye hayo ndio mapenzi na utaratibu mwema wa baba na mama. Kwasababu mengine yalikuwa nyuma ya pazia hakuwahi kuyaona na kwahiyo akionyeshwa sasa anaonaa ni tabia mbaya!
 Kwanini nimeileta hii hadharani, ni kwasababu ya migongano ya ndoa inayotokea sasa hivi. Wewe na PHD  yako unakwenda kumuoa mtoto wa darasa la saba kijijini. Ujue kabisa utakumbana na mitihani, kwasababu huyu bado ni chekechea kwako, unahitajika kwanza kujishusha hadi katika uchekechea wake ili uende naye sambamba, na kila siku unatoa darasa, hadi itafikia mahali yeye atajua kuwa haya ndio maisha ya ndoa.
 Wengine wameshindwa na kukosona kabisa na wasichana wa watu wadogo toka kijijini na kuwaona eti ni washamba, sio washamba mshamba ni wewe uliyepata elimu ukashindwa kuitumia. Elimu ukishaipata unatakiwa uwaelimishe wale wasiojua ili elimu hiyo ikue na kupata changanmoto. Na moja ya mitihani na changamoto la elimu ni mabadiliko ya kimaisha, ambayo kila mtu anakumbana nayo. Wewe kwa vile umeshapevuka, na kuona hilo,unatakiwa kuitoa hiyo elimu kwa mwenza wako, taratibu na kwa busara na sio kukashifiana na kuachana , utasikia mke gani huyu au mume gani huyu hata mapenzi hajui, wewe ndio hujui kama ungelijua ungemjulisha mwenzako, kwani kile usichokijua ni sawa na usiku wa giza, kukipambazuka utakijua, swala ni subira, ambayo huvuta heri.
Ni mimi: emu-three

5 comments :

Anonymous said...

Sasa hawa watu wanatakaje, ukiwasaidia tunaingilia kai zao, ukiacha tunawanyanyasa , sasa mwatakani?
Lakini huyo mama mimi nimependa ameegemea uhalisia ambao unabadilika siku baada ya siku.

Fadhy Mtanga said...

Afadhali umesema.. Kuanzia leo siingii tena jikoni.

Ha ha haaaaaa.

Masangu Matondo Nzuzullima (MMN) said...

"Wengine wameshindwa na kukosona kabisa na wasichana wa watu wadogo toka kijijini na kuwaona eti ni washamba, sio washamba mshamba ni wewe uliyepata elimu ukashindwa kuitumia..."

Ukweli tupu. Wengi tumesoma lakini hatujaelimika na lengo hasa la elimu yetu halionekani - majivuno, kujibana katika vijieneo vyetu tulivyosomea, dharau kwa wengine na upuuzi mwingine. Ndiyo maana niliwahi kuuliza hapa kuhusu maana hasa ya usomi na msomi...

http://matondo.blogspot.com/2010/02/fikra-ya-ijumaa-ati-msomi-ni-nani.html

Kuhusu ndoa ni kwamba bila uwazi na mawasiliano yasiyo na vipingamizi haiwezekani kuwa na ndoa yenye furaha na ridhiko. Wanawake wanataka vitu vingi sana ingawa hawapendi kuvisema. Wanatuachie wanaume tuhangaike kuvigundua na wakati mwingine inakuwa "too late"

Kwa mfano mimi huwa sioni sababu ni kwa nini mwanamke asiseme tu moja kwa moja jinsi anavyopenda ligwaride lichezwe pale uwanjani (sita kwa sita) badala ya kubaki akiumia na bila kuridhika kwa miaka na miaka mpaka? Halafu anakwenda nje akitafuta afande wa kumpigisha ligwaride kwa staili aitakayo yeye. Matokeo yake ni talaka, UKIMWI na mengineyo.

Angalizo: wanawake msinipige mawe. Leo tunawaongelea ninyi tu hapa. Sisi wanaume nasi tunayo yetu tena mengi sana. Leo acheni tuwaseme...

mumyhery said...

mmhu huu kweli mtihani!!!

Yasinta Ngonyani said...

Nimesoma hii mada huku nikicheka kwa kweli wanawake wengi bado hatujafunguka. Na halafu huwa tunawalaumu wanaume hawatusaidii kazi za nyumbani. Sio kwamba nakataa mila na desturi zetu zipotee hapana. Ila kuna vitu inabidi tusaidiane katika nyumba. Na wewe mtani eti hutaingia tena jikoni kisa?