Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Thursday, August 26, 2010

Ni nani kuwa kiongozi wetu?

 
La mgambo limelia asiyemwana aeleke jiwe, wote tunaitwa kwenye mkutano mkuu. Na mkutano mkuu hakuna wa kuukosa, kwani anayetuita ni mkuu wa heshima. Kila kona ya nchi watu walikuja, si vijana au wazee, si wake au waume. Hata wale wasiojiweza, walipewa vipandio ilimradi wafike na kumsikiliza mkuu.


‘Ndugu waungwana wa nchi hii, sitaki kuwapotezea muda, kwani muda kwetu ni muhimu kuliko mambo mengine, lakini nilichowaitia kina umuhimu kama huo wa muda, kwani kwa kulitatua hilo mtakuwa mumepunguza muda wenu katika mambo yanayowakwaza.

‘Nilichowaitia hapa ni kuwa tunamtafuta kiongozi, kiongozi ambaye ataweza kuwafikisha pale katika matarijio yetu. Kiongozi huyo ndiye atakayekuwa muhimili wa kufikia daraja la maisha mema yenye matarajio mema, kwenu na vizazi vyenu vijavyo.

‘Sasa nawaomba mnisikilize kwa makini, nataka kuwatajia sifa za kiongozi wenu ambazo zimependekezwa na wazee wanu waliojaa busara na akili tele, na wampendekeza hayo kwa manufaa yenu na vizazi vyenu. Wazee hawa wameishi humu duniani na wameona mengi ambayo hamukuwahi kuyaona na pia wana kipawa cha kugundua yajayo ambayo hamujawahi kuyafikia….’

Watu wote mle wakatikisa kichwa kukubaliana na hayo, kwani wazee hawo kila walisemalo huja kama walivyobashiri, na kwao wazee ni tunu aliyowatunukia muumba. Kwa heshima kubwa walitulia na utulivu wao ulileta ukimya usio wa kawaida. Na mvua ya rasha-rasha ikapita kuashiria mema.

‘Sifa za kiongozi wetu, kwanza anatakiwa awe mrefu kupita wote, ili aone mbali zaidi na awaone wote wakiwa chini yake,…’ wale warefu wakatabasamu na kusema labda naweza kuwa mimi, lakini kabla furaha ya moyo haijakita mahali pake wakasikia mkuu akiongezea ‘ na pia washinde wote kwa ufupi, ili awaone walio chini yake na kujua yanatokea chini kwa chini…’ hapa watu wakaguna kwa mshangao, lakini wakaujua huenda kuna ufafanuzi utakaotolewa baadaye.

‘Sifa za kiongozi wetu anatakiwa awashinde wote kwa unene, ili ashindane na wanene, hata kwenye vurugu asiweze kusukuma na kuleta kuyumba kwa nchi, na pia awashinde wote kwa wembamba kupita wembamba ili awe mwepesi kukimbia kuliko wanambio wote duniani ili aweze kuwakamata wale wote wanaotaka kuihujumu nchi kabla hawajavuka mipaka ya nchi yetu tukufu..’ watu wakabaki midomo wazi kwa mshangao, huyo mtu ni mtu kweli au ni jinni.

‘Sifa za kiongozi wetu anatakiwa awashinde wote kwa kuona, awashinde wote kwa kusikia, awashinde wote kwa kuhisi na kinyume chake…’ watu wakaguna kwa nguvu, na kabla hawajatoa kauli wakasikia mkuu akisema ‘ Akiwashinda wote kwa h hayo hakuna atakayesingizia upofu kama anaona, au usizwi kama anasikia na yule asiyeona hataweza kusingizia kuona , wakati hajaona kitu au yule anayesikia hatasingizia kusikia, kwani hakusikia kitu na kuleta sintofahamu katika nchi…’

‘Sifa za kiongozi tunayemtaka anatakiwa awashinde wote kwa akili, awashinde wote kwa utambuzi awashinde wote kwa kuelewa, akiwa kwa wanataaluma awe chachu ya kuvumbua kile kisichovumbuliwa na kwa wenye akili awe mwerevu wa kugundua matambuzi yote yaliyojificha ili wasije wakatumia akili zao vibaya na kuwadanganya watu. Na pia awashinde wote kwa ujinga, ili akiwa kwa wajinga wasimpoteze na hulka za ujingani na kwao wao wamuone mwerevu kwa ujinga walio nao…’ hapo watu wakacheka.

‘Na awashinde wote kwa kucheka, ili kicheko kiwe cha furaha ya kweli na sio huzuni na pia awashinde wote kwa kulia, ili uchungu wa mwenye uchungu uyeyeuka na kujiona sio uchungu kitu mbele ya kiongozi mwenye uchungu zaidi yao.

Sifa ziliendelea hadi mwisho yakakaribishwa maswali. Kijana mmoja akauliza, je huyo kiongozi ni kijana au mzee, jibu likatolewa kuwa huyo kiongozi ana sifa zote za ujana na uzee. Swali jingine likaulizwa je ni mwanamke au mwanaume, jibu likawa huyo kiongozi ni mwanamke na pia ni mwanaume, na anatakiwa awashinde wote kwa uuke na kwa uume pia…watu wakacheka, na kuanza kutafakari `ni kiongozi gani huyo’ na atapatikana wapi ?

‘Kiongozi huyo yupo na nyie, na mnamjua kuliko hata mie , kuliko hata wazee wa busara, na mna muda hadi mwezi wa kumi muwe mumeshamgundua. Lakini kama hamtamgundua kabla ya muda huo mtakuwa matatani. Nawapeni muda wa kunitafutia huyo mtu, na atakaye mpata atakuwa hodari wa mahodari katika vitabu vya mohodari…ahsanteni.

Watu wakatawanyika ili kumtafuta huyo kiongozi, kwani wameambiwa yumo miongoni mwao, je watampata wapi kiongozi mwenye sifa kama hizo, je kiongozi huyo ni nani na jina lake ni nani? Wadau wenzangu ni nai huyo?


Ni mimi: emu-three

6 comments :

Anonymous said...

Kweli huo ni mtihani, na hii ni taswira ya kutonyesha kiongozi ni mtu gani, mmmh, kwangu mimi nashindwa kusema ni nani, maana sijui ni kati ya hawa wanogombea, mrefu, au mfupi, mnene au mwembamba..mmmmh, hilo ni fumbo kali, naona wanafalsafa wanaweza kuligundua hilo, vinginevyo mimi nimetoka kapa!

Anonymous said...

Ni kweli kumpta kiongozi anayefaa wananchi unahitajika mchakato mrefu sana, kiongozi huyo awe anakidhi haja za kila rika, umri , imani, nk, kwahiyo kwenye hili some hapa nia ni kuonyesha kuwa kiongzi anatakiwa washinde wote katika kila jambo ili awe mfano...na kiongozi huyo anatakiwa atafutwe na watu, sio kiongozi kuutafuta uongozi kwa kujiuza, hapana

Yasinta Ngonyani said...

Nakubaliana na wasio na majina waliotangulia kiongozi inabidi awe yeye yaani kama alivyo na watu wamtafute na hili somo kwa kweli ni kali kumpata kiongozi mwenye sifa zote hizo ikitokea hii itakuwa bombi kweli. Tukaa na tumie macho na masikio.

Simon Kitururu said...

Duh!

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

kiongozi, mwenye kipaji, aliyekuwa kiroho nk au?

Anonymous said...

MI NA SIASA NI VI2 VIWILI TOFAUTI.
HUWA NAONA NI SANAA 2. CNA CHA KUSEMA HAPA.