Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Friday, August 27, 2010

Ni nani kuwa kiongozi wetu 2?


Nchi nzima ilizizima kwa kampeni, kampeni za kumtafuta nani mwenye sifa za kuwa kiongozi, na kwa uelevu wa nchi hii, watu walikutana kutegemeana na Nyanja zao, wakulima wakamtafuta mkulima stadi, lakini akakosa sifa nyingine, warefu wakamtafuta mrefu kuliko wote, lakini jinsi gani atajifupisha ikawa haiwezekani, wafupi wakamtafuta mfupi sana, lakini atajirefusha vipi ikawa ni kitu kisischowezekana, madakitari, wanataaluma, na watu wa kila rika wakakutana na mwisho wa siku wakakubali kuwa sasa wameshindwa kumpata kiongozi mwenye sifa husika.
‘Mimi naona tumrudie mkuu na wazee watusaidie kwa hili, kwani muda unaisha na mwisho wa siku itakula kwetu’ watu wakakubaliana. Walipofika njia panda wakakutana na kichaa mmoja, kichaa huyu haeleweki, mara nyingine huwa mzima kabisa na akawa mtu wa kawaida, na baada ya muda Fulani hali yake ya kuchanganyikiwa humrejea. Kitu cha ajabu kwa kichaa huyu ni kutabiri mambo ambayo huja baadaye kutokea, na hili liliwafanya watu wamheshimu , hasa siku akiwa mzima.

‘Nyie mnasema mumeshindwa kumpata kiongozi wa nchi hii, hahahaha, halafu mnajiita mna akili, halafu mimi mnaniita kichaa….hivi nyie na mimi nani kichaa, hivi nikiwaambia huyo kiongozi ni nani mtakubali kuwa mimi nina akili zaidi yenu…hahahahaha, eti Yule kichaa, kichaa ni nyie msiotumia akili zenu..hahahaha…’ akasogea mbele yao na kuongoza ule msafara.

‘Hivi jamani ngoja tumuulize huyu kichaa anaweza akawa anamjua huyo kiongozi wa matarajio' mmojawapo akasema kwa sauti

‘Hivi nyie mna akili kweli hamuoni kuwa siku zake za kuchanganyikiwa zimerejea, sasa hapa atawaambia nini..’ mmoja akapinga lakini wengine wakaanza kumdadisi hapohapo!

‘Hebu mtaalamu kichaa tueleze kiongozi wetu ni nani?’ ‘Au ni wewe tukuchague nini…’ maswali mengi yakaulizwa huku wengine wakiangua kicheko.

‘Heri yangu mimi sijacheka, kwani wakati wa kucheka haujafika, wakati huu ni wa kilio, na huzuni kwasababu mbele yetu bado ni giza, na giza hili limetanda ubongoni mwetu , na kushindwa kutafakari. Huu ni ugonjwa kuliko ule wa kichaa, ambaye mwisho wa siku anashindwa afanye nini, lakini ni heri ya kichaa anayejua nini kitafuata baadaye kuliko mwenye akili anayetamani kile asichokijua eti kwasababu ya sura, majina, mwenzetu lakini nini siri ya moyoni inakuwa kitendawili…’

Watu wakawa kimya huku wanatembea kuelekea kwa mkuu, na walipofika kwenye mlango wa kuingilia mlinzi akataka kumzuia Yule kichaa, na Yule kichaa akacheka kwa sauti kubwa na kusema. ‘hivi nyinyi mnajua mbwa, mbwa anatimiza matwaka ya bwana wake hata kama akiambiwa alinde mavi ambayo hayana faida zaidi ya kutupwa chooni…, mimi nina thamani kubwa sana kuliko nyie na huyo mkuu wenu kwani ninachokijua hakuna anayekijua nani kwa manufaa yenu, nani kwa manufaa yako wewe unayelinda hata kile usichokijua thamani yake…nirudi niwaachie huu mtihani…’akageulka kurudi lakini watu wakamsihi na kumuomba asirudi.

‘Hivi nyinyi mnamchukua huyu kichaa kwenye nyumba ya mkuu mnataka kusema nini, je akileta vurugu mtamlaumu nani’ akasema mkuu wa walinzi.

‘Tutahakikisha haleti vurugu, sisi tunamjua sana kuliko nyie’ akasema mzee mmoja.

Watu walizidi kufurika, hata ule mpango wa kuwa waje wawakilishi ukawa haupo tena, ni nani asiyetaka kusikia habari za kiziwi aliyesikia, ni nani asiyetaka kusikia habarii za bubu aliyesema, hakuna, kila mmoja alitimkia kwa mkuu kumsikia ni nani kiongozi , kiongozi wa matumaini. Lakini kila mmoja alijiuliza ni nani aliyemgundua huyo kiongozi ili jina lake liwekwe kwenye kumbukumbu za vitabu vya wataalamu

‘Haya wananchi wakati umefika, na nimesikia mmoja wenu amemgundua kiongozi wetu ni nani, tumamuomba apite hapa mbele..’ akasema mkuu. Kimya kikatanda, na minongono ikasikika, na minongono ya wengi na kishindo kikuuu. Dakika nyingi zikapita hakutokea mtu.

‘Jamani muda unapita ni nani huyo apite mbele…’ kimya kingine na mara upande mmoja wa watu wakasikika watu wakisukumana, na mara mlinzi akaelekea kule na kumzuia Yule aliyekuwa akitaka kupita mbele.

‘Mwacheni apite’ akasema mkuu. Na aliyepita mbele si mwingine bali Yule kichaa, na watu wakaguna na wengine wakacheka na hata kuzomea, kichaa, kichaa, kichaaa…

Baada ya muda kimya kikatawala kumsikia kichaa atasema nini. Yule kichaa akabadilika rangi na kuwa tofauti na sura yake, akaanza kutetemeka na baadaye akatulia, na hii ni dalili kuwa ule ukichaa umemtoka. Akaanza kwa kulia, halafu baadaye akacheka na kusema. ‘Hivi nikiwaambia kiongozi wenu ni mimi mtasemaje…’ watu wakacheka zaidi, na hata kuzomea, na wengine kuzihaki kuwa ncho yote itageuka kuwa ya vichaa, kama yeye ndiye anayefaa kuwa kiongozi wa nchi.

‘Basi kama mnataka niwaambie ni nani kiongozi wenu basi mnipe thamani sawa na huyo kiongozi mnayemtaka. Watu wakanongona na mara matajiri wakaanza kuleta hela, wengine zawadi, na kila wakiongeza, Yule kichaa alikuwa akivitazama  vile vitu, halafu anatizama mbinguni…anatabasamu, ikawa anafanya hivyo mara kwa mara , masaa yakawa yanakwenda, mpaka zile zawadi zinakaribia kumfunika, anaziangalia , anatizama mbinguni anatabasamu….

Watu wakaishiwa subira na kuanza kulalamika kuwa huyo kichaa anawapotezea muda wao, lakini mkuu na wazee mashuhuri wakasisitiza kufanya subira.

Je kiongozi huyo atapatikana kweli, kama mtu a
Ngoja niishie hapa, hadi siku nyingine, wakati tukimsubiri huyu mtu atutajie huyo kiongozi, na kumbuka mtu huyu ana sifa mbili, sifa ya kwanza mtabiri na sifa ya pili kichaa…je wewe ungemuamini huyu mtu, je au wewe unamjua ni nani anayestahili kuwa kiongozi wa matarajio yetu? Sifa ziameshatajwa awali , hebu waangalieni watarajiwa wetu na utoe jina moja lenye sifa kama hizo….

Ni mimi: emu-three

1 comment :

Anonymous said...

Wewe sasa unanikumbusha hekaya za Abunawasi, vitabu vya akina Shabani Robert ambao wanaweza kuandika kitu usielewe mapaka uvute tafakuri za hali ya juu.
Ngoja tuone mwisho wake, najua wengine wataona mauzauza kwasababu wamezoea vifupivifupi na picha, na hapa panahitaji wasomaji na watafakuri wa hali ya juu.
Nimeipenda hii