Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Friday, August 6, 2010

hii sio haki

'Vipi bwana mdogo mbona hujaweka umeme kwenye nyumba yako?'
'Bro, milioni moja karibu na nusu nitazipatia wapi, mambo yamekuwa magumu sana, tena baya zaidi nahitajiwa nguzo, nayo nimeambiwa niilipie!'
'Nguzo inalipiwa hiyo si mali ya Tanesco?' nikauliza nikijifanya sijui, wakati mimi mwenyewe nilinunua nguzo ili kuingiza umeme nyumbani kwangu.
'Wanasema nipo mbali na maeneo yao, kwahiyo nguzo hapo inatakiwa mimi mwenyewe nichangie, lakini hata nikiilipia bado ni mali yao kwani akihitaji mtu mwingine kupata umeme kwa kupitia kwenye mkondo ambao umetokana na hiyo nguzo niliyoilipa yeye hatalipia atapata bure, ndio maana nashindwa kwani wenzangu bado hawajahitajiumeme' akasema bwana mdogo kwa huzuni.
 Mjadala huu wa umeme ulinikumbusha tangazo nililolisikia kuwa Tanesco wamepeleka barua ya maombi kwa UWURA kuwa wameomba wapandishe bei kwa asilimia fulanii na bei hizo zitaanza January 2011 (http://www.ewura.go.tz/publicnoticeselectricity.html)

TANGAZO KWA UMMA


WITO WA KUKUSANYA MAONI YA WADAU KUHUSU OMBI LA TANESCO LA KUPANDISHA BEI YA HUDUMA YA UMEME
Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imepokea ombi kutoka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) la kuidhinishiwa ongezeko la bei za huduma ya umeme kwa kipindi cha miaka mitatu kuanzia Januari Mosi, 2011. TANESCO wanaomba bei za huduma ya umeme ziongezeke kwa asilimia 34.6 kwa mwaka 2011; asilimia 13.8 mwaka 2012; na asilimia 13.9 mwaka 2013........

. Nikajiuliza hivi lini huduma za wananchi kutoka kwa vyombo kama hivi vya Nishati zitashuka, kwani wenzetu wa mawasiliano ya simu wanashindana kushusha bei, lakini huduma hizi wanashindana kupandisha bei, wakilinganisha na nchi nyingine!
 Hebu fikiria hivi sasa mwananchi anabeba mzigo mkubwa wa gharama za kimaisha kwa mfano leo nimeona dola inauzwa kwa shilingi 1505/- kwenye maduka haya ya mitaani, manake nini, manake bei za vitu vinavyotoka nje bei yake itakuwa juu. Sasa bado mwataka kumuongezea mzigo mwingine gharama zinazotokana na nguvu ya uzalishaji mali, kwasbabau umeme ukipanda, gharama za uzalishaji zitapanda, na vitu vinavyozalishwa vitapanda bei, na madhara yake ni kwa mtumiaji ambaye ni mwananchi.
 Sawa kama mumeona hakuna jinsi lazima mpandishe lakini huduma zinazoendana na huko kupandisha ziko wapi? Kuupata huo umeme inabidi kiatu kiishe soli. Ukibahatika kuupata , uhakika wa kuwepo masaa yote ni mdogo, na hata ukipatikana ni wa mawengemawenge, unapandda unashuka kama presha., matokeo yake mnaunguza vitu vya walala hoi. Nawashauri mboreshe huduma zenu kwanza ndipo mfikirie kupandisha bei, vinginevyo mnamuonea sana mtumiaji na hii sio haki.
 Haya wananchi mumeitwa kwenda kutoa mawazo kutokana na ombi la Tanesco kwa ewura kwa kichwa cha habari cha maombi ya kupandisha bei za gharama za umeme,  simelisikia hilo tangazo au mnaangalia tamithilia za kutupumbaza akili tu, jamani jitokezeni kwa wingi basi mkajitetee. Vinginevyo baada ya uchaguzi rungu litakalofuata ni kupanda kwa bei za umeme, jingine nauli za dal-dala, na jingine, mtajaza wenyewe, halafu kinachofuatia wamachinga wote mlioanza kupanga vitu mabarabarani mtafute sehemu za biashara, kwaani kipindi hicho serikali itakuwa imerudi kazini! Labda mjiandae kuingia kwenye jengo la biashara la wamachinga na sijui ni kwa wamachinga kweli au ni kiini macho, yetu machoooo!

Ni mimi: emu-three

5 comments :

Anonymous said...

Iwe haki isiwe haki, bei za umeme zitapanda tu, hiyo haina jinsi, swali kubwa ni `huduma zao zinaendana na ghrama hiyo?'
Pili lazima watu wabadili muelekeo wa kuachana na Tanesco na kutafuta njia mbadala, umeme wa jua upo sasa, na ukiangalia gharama zao ni nafuu, kwani tatizo ni mwanzo tu, ukishaingia ndani huhitaji tena kulipia kila mwezi kama TANESCO.

Anonymous said...

Wewe dunia hii kuna haki kweli, hata watu wanajiita wa mungu ukitumbukiza rupia atakuangamiza, hkuona mauaji ya Burundi yalitokea wapi huna uhakika kuwa kuna mtu mmojawapo aliyejiita wa mungu aliwasaliti. Haki katika dunia hii hasa kwa serikali zetu za kiafrika ni kusadikika tu. Ukipata kitumie ukikosa kijutie basi

chib said...

Tanesco wananikinaisha kabisa, kila mara kuongeza bei ya umeme, lakini huduma hata hazijawa bora. Unakatika sana. HII ni Matatizo ya kutokuwa na ushindani.
Nakubaliana ana kutumia umeme wa nguvu ya jua

Anonymous said...

Swala la Tanesco litakuja kuwa kama TTCL, hili ni swala la muda tu, waache wataijutia sana hii bahati.

SHEIN RANGERS said...

KWANINI WAONGEZE BEI YA UMEME KWA HUDUMA GANI BORA WANAYOTOA WAKATI MAJUMBA YA WATU YANAUNGUA KILA SIKU NA CHANZO NI UMEME WA TANESCO.