Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha
Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..
Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.
MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.
TUPO PAMOJA DAIMA
Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;
https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:
https://www.facebook.com/diaryyangu/
`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;
Tuesday, August 17, 2010
Foleni dar sasa ni kero
Nimegundua kuwa matrafiki wanapokuwa wao ndio wanao-ongoza magari badala ya taa foleni huwa ndefu sana, kwani wao wanaita upande mmoja muda mrefu sana, wakati mwingine wanaita hata kama hakuna magari, jamani mnaita hewa. Yaani leo kila mmoja alikasirika lakini utafanyeje.
Kitu ambacho kinanisikitisha ni kuwa muda mwingi tunaupotezea ndani ya magari, na kumbuka humo ndani tumajazwa kama magunia, unasimama kwa mguu mmoja ukiteremsha wa pili utasikia kilio `umenikanyaga, wewe huoni, huna adabu….na matusi kwa kwenda mbele..’ sasa jamani utasimama na mguu mmoja kama jini, si utachoka, na wakati mwingine unakosa balansi na kumdondokea abiria mwingine hapo utaipata pata. Yule aliyekaa anajiona kama mfalme, hajui kuwa kesho naye anaweza kuwa kasimama na huko kusimama wanaita `kupaka rangi’
Sasa jaribu kufikiria mwenyewe mumeazana haswa na mabasi mengine madirisha hayafunguki vizuri, hewa ya shida, mijasho kuhemeana nk, unafikiri mwisho wa siku itakuwaje kama sio kuambikizana magonjwa. Achilia mbali watoto kuna wagonjwa ambao kusimama muda mrefu ni kuwatesa, lakini matafiki hawalioni hili wanaita upande mmoja weee, sijui ni kwanini?
Nakumbuka katika makala zilizopita nilitoa mapendeezo ambayo watu wengi wameshayaongelea kuwa zipo barabara zisizo rasmi kwanini zisiruhusiwe kupitisha haya mabasi makubwa, zirekebishwe kwa muda zitumike kuliko hili balaa la foleni. Na pia kama inawezekana watu watumia mabasi zaidi kuliko kutumia magari yao binafsi, hii imgepunguza wingi wa magari barabarani. Hizi ziwe njia zamuda mfupi huku nmikakati ya muda mrefu kama barabara za juu kwa juu zikiandaliwa au usafiri wa treni ukiandaliwa.
Hutaamini unaweza ukafika morogoro kabla ya abiria anayetoka Gongolamboto hadi Msasani hajafika mwisho wa kituo. Sasa haya maendeleo tutayapata kweli kama muda unaishia ndani ya daladala?
Ni mimi: emu-three
6 comments :
Hiyo ni kweli tunaopanda madaladala tunateseka sana, na hawa viongozi wanapopita wanasababisha foleni iwe kali zaidi, kwani mtrafiki wanatugandisha masaa kibao bila kujali kuwa ndnai ya magari kuna wagonjwa na watoto
Ni kweli kabisa hili swala linaandikwa na kuzungumziwa kila siku katika hizi blog zetu. Nakubaliana na wewe kwa nini zisifunguliwe barabara nyingi. Nilikuwa juzi naliongelea hili swala na rafiki mmoja kuhusu usafiri huu na tukafikia kuwa kwa nini kusiwe na usafiri wa treni na mabasi makubwa kwani ni kweli ni kero mno. Kwa sababu ni kweli hapo pia ndio ule vizi unatokea. Ningegombea urahisi ningetoa sheria kuwa katika mabasi hata daladala wasafiri wote lazima wawe wakae sio kusimama. kwani huko pia kunasabisha ajali barabarani. Ni mawazo yangu tu unaruhusiwa kubisha.
mummy hata mimi naungana na mkono na wewe matrafiki kwa kweli ndio chanzo cha foleni wapo pale kwa ajili ya kuwafurahisha baadhi ya watu na wakishamaliza ndio wanaondoka, mie nadhani wangeondolewa kabisa katika hiyo kazi.
suala la njia za kati ni zuri lakini itakuwa poa kama zikarekebishwa maana wengine hawakubali kuharibu magari yao kwa kuyapitisha huko licha ya kuwa haijaruhusiwa rasmi
mwenzangu yani huo mbanano nawengine wanajipatia nhapo hapo kufanya mambo yao ya ajab nini kuambukizana magonjwa kwa njia ya hewa, mtu unafika ofisini unanuka jasho kutokana na mvuke wa kila aina unaokutana nao na usiombe kupanda mabasi ya feri UTAJUTA
Blog yako nzuri! nitazidi kutembelea
Karibu sana Sophia, nitashukuru ukiwa mwenyeji hapa
Post a Comment