Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha
Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..
Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.
MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.
TUPO PAMOJA DAIMA
Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;
https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:
https://www.facebook.com/diaryyangu/
`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;
Tuesday, July 20, 2010
Vijana ni taifa la leo au kesho?
'Kwanini wewe hujui, hebu nikumbushe kauli mbiu yenu mnasema `vijana ni taifa la kesho?' au nimekosea.
'Hapana vijana ni taifa la leo' akasema yule kijana.
'Hapohapo ndipo nilipopataka kupasikia, nyinyi mnataka kuwa taifa la leo, kabla ya kesho haijafika au sio, maana yake mwataka kupupia kila kitu leo, wakati nafasi yenu ilikuwa kesho, kesho ikifika tunawazika. Ndio maana yake. Unajua nina maana gani. Mzee Nyerere, na wazee wengine waliposema hivyo walikuwa na maana kubwa kuwa kila jambo linahitaji uzoefu kwanza. Huwezi ukatoka shule na moja kwa moja ukapewa kile cheo unachostahili, inabidi upate uzoefu. enzi zetu hawa mahakimu unawaona ambao ni wazee walianzia ukarani, wakapata uzoefu wakapanda madaraja hadi kufikia uhakimu. Hata maofisini enzi hizo, ilikuwa hivyohivyo unaanza chini kwa kupitia kazi za chini kabla hujapewa ubosi wako. Na kwahiyo huyu mtu huwezi kumdanganya kitu kuwa eti kazi hii ngumu, kazi hii inamatatizo fulani, yeye keshaipitia utamdanganya nini.
'Nyie sasa hivi mnatoka mashuleni mnapewa umeneja wa kuongoza kampuni ya magari natoa kwa mfano, hata kuweka girisi hujui, utamuongozaje huyo mtu anayetengeneza hilo gari, kuwa hapo kakosea? Ndio maana wazee wetu wakasema nyie kwanza mpate uzoefu leo kwa kufanya hili na lile la ngazi ya chini, mpitie jeshini kwanza mjifunze maisha ili muwe sawa, halafu kesho ikifika unapewa cheo chako, hakudanganyi mtu hapo, huwezi kumfanya mwenzako mtwana, wewe ukae ofisini na kuagiza tu hiki kifanyike, kwasababu kwanza unaogopa hukijui vizuri, pili umejengeka kujiona wewe ni bosi, kazi ya chini sio yako!
'Sasa tukirudi katika swali lako la msingi, kwanini vijana wanakufa kwa wingi zaidi ni kwasababu hiyohiyo ukiiweka katika mazingira mengine. Nyie mna tamaa ya kupata kila kitu leo hamtaki kuchunguza kwanza. Mnakula kila kitu ilimradi mumesikia kuwa kinaliwa, kwasabau hamtaki kusubiri kichunguzwe kwanza. Mnaiga kila kitu kwasababu mumeona Wazungu wanafanya hamtaki kusubiri kuangalia uzuri wake na ubaya wake. Mnafanya hata yale shetani hajawahi kuyafanya eti kwasababu mnataka mpate raha ya leo kabla ya kesho. Hebu oneni, mtu ana wapenzi kibao, hata chumba cha kupanga hajaweza kukimiliki, unafikiri kichwa kitatulia hapo. Kwa mifani hiyo, nini matokeo yake mwisho wa siku, Ukimwi, magonjwa ya shinikizo, magonjwa ya zinaa , kujaa matumbo na tunaona sifa kwakuitwa tuna vitambi kumbe ni ugonjwa...yote kwasababu mna tamaa ya kupupiapupia leo badala ya kula kidogokidogo ili ujenge uzoefu na mwisho wa siku ukifika ushakubuhu. Na vingine vinahitaji muda muafaka, kwa maana yake, tusubiri kwanza umri ukifikia utaoa...unasikia sana eeeh!
'Nawausieni vijana, tusiwe na pupa ya maisha kuwa tupate kila kitu leo, hapana, kwanza tuwe na subira, huku tunajifunza, halafu tuchunguza kile tunachojifunza, baadaye kama ni lazima tujaribu hatu kwa hatua, kwani vingine havijaribiwi mapaka umri ufikie, baadaye tukiona kinafaa basi ndio tule...vinginevyo tutajaza matumbo yetu hata kile kisicholiwa na mwishowe vyote vinageuka kuwa sumu mwilini na matokeo yake ni nini...' alipofika hapo akaondoka.
`Eti waungwana mumemuelewa huyu mzee, mbona anatuchanganya na kutuacha njia panda, wewe eti usubiri mpaka kesho wakati wali umeshapakulia, siutapoa huo, hapana, ya keshoo ni uchoyo wao, sisi ni taifa la leo...mmmh, lakini tuangalie hii tamaa inatupeleka pabaya, angalia yule teja pale sio hawo anaosema wazee kuwa wanataka kupupia kila kitu...' Akasema yule kijana aliyeuliza lile swali
Haya waungwana, marafiki zangu hebu tujadili hili eti vijana ni taifa la leo au ni taifa la kesho? Na kwanini maisha yetu ya kuishi yanapungua na ukiangalia vijana wengiwanapoteza maisha yao, inawezekana kuwa ndio utandawazi na nini hasa?
Ni mimi:
emu-three
4 comments :
Kila kitu zamani ilikuwa safi. Naitamani zamani yetu. Vijana wa siku hizi ni kweli kuiga kwingi mno tunaiga hata kitu ambacho hakina faida. Ningependa tuige mambo yaletayo faida. Vijana wa siku hizi hawataki kufanya kazi wanataka kuletewa tu, hawataki kujitegemea. Hata kama anataka kuanzisha mradi anasema sina mradi yaani ile kuhenya na kupata mradi hawataki kabisa. Kwa sababu hata kama una shilingi tano ukianza na kweli unahenya utaona mtaji unakuwa na mwisho utajikuta uko mbali lakini vijana wa siku hizi ni wepesi sana kukata tamaa. Kufa haraka ni kwamba inawezekana wazee wa zamani walikuwa na lishe bora kuliko sasa. Kwa hiyo hutakuwa na taifa la kesho kama mtindo wenyewe ndio huu wa kuiga. Kwani tungeendelea kama wazee wetu basi kungekuwa na taifa la leo na pia la kesho..... ni wázo tuu. Upendo Daima...
Ndio maana wanasema cha zamani ni dhahabu, kwasababu wazee walikuwa wakifanya vitu vyao kwa kutafakari kwanza. Hebu chukulia unapotaka kuoa, walikuwa wanaangalia historia ya mahali unapotaka kuoa, kama kunafaa. Leo hii tunakutana Makirikiri Bar, au kituo cha basi mnapendana mnaoana mwisho wa siku unagundua mwenzako ana asili ya wizi uchawi magonjwa yasiyoponyeka na hatimaye mnazaa kizazi cheney matatizo.
Tusiwe na pupa ya maisha, wenzetu waliikuta dunia hii wakaiacha nasisi tutaiacha, lakini tuiacheje, tusiiache kwa mabaya ikawa historia mbovu na badala ya yakale dhahabu itakuwa ya kale kinyaa
mzee wa busara
Emu-three hivi wewe ni nani hasa, mwanaume au mwanamke, mbona unatubania kutuelezea zaidi kuhusu wewe, manake unatoa vitu!
Nimeikumbuka sana sehemu hii
Post a Comment