Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha
Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..
Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.
MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.
TUPO PAMOJA DAIMA
Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;
https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:
https://www.facebook.com/diaryyangu/
`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;
Tuesday, July 27, 2010
sheria ni msimemo
'Huyu mtoto wa bosi akija hapa nakosa raha, manake anataka kupanda hata juu ya computer yangu, sijui nifanyeje, juzi alikuja akaharibu barua muhimu nikabakia kulaumiwa mimi, sasa hebu nishaurini ningefanyaje naye ni mtoto wa bosi...' Hicho ni kilio cha mfanyakazi mmoja, nami sikusita kumuuliza kuwa inakuwaje mpaka anamruhusu mtoto kuchezea mali za ofisini.
'Unajua kwasababu ni mtoto wa bosi akija hapa kila mtu anampapatikia ili kumuonyesha bosi tunajali familia yake, sasa kwasababu mimi nipo hapa mbele, akija ananikimbilia mimi na mimi inabidi wakati mwingine nimpishe akae kwenye kiti na kucheza na computer..'Akasema huyu dada.
'Nikuulize swali moja je kama angekuwa mwanao ungemruhusu afanye hivyo unavyomruhusu huyu mtoto wa bosi afanye, au kwasababu ni mtoto wa bosi hawezi kuharibu na akiharibu ni bahati mbaya au sio?
'Wewe unasema tu, hivi kweli aje mwanangu hapa ni mruhusu kuchezea mali za watu, hata kama ni nyumbani watoto wangu huwa nawawekea mipaka ya vitu vya kuchezea, huyu tunafanya hivyo kwasababu ni mtoto wa bosi
'Basi kosa unalo wewe, na hata bosi akikulaumu siwezi kumlaumu. Sheria huwa haichagui kuwa huyu ni mtoto wa bosi au bosi mwenyewe, kama kuna utaratibu umewekwa basi kila mmoja anatakiwa aufuate na bosi anatakiwa kuwa msitari wa mbele kuufuata. Wewe umekabidhiwa dhamana za ofisi kwahiyo ni wajibu wako kuzilinda na kuhakikisha hakuna mtu anayezichezea bila kujali ni nani.
Kama huyo mtoto wa bosi ataharibu kitu wewe ndiye utakayebeba lawama, kwasababu yeye ni mtoto kama mtoto wako una wajibu wa kumuelezea na kumkanya pale anapokosea, hata bosi akifanya kinyume wewe una wajibu kumuelekeza na kumshauri kwani yeye kama binadamu anaweza akaghaflika. Tunapoogopa kutekeleza wajibu wetu kwa kuangalia sura na wadhifa ndipo tunapokosea na hiyo ni ukiukwaji wa uongozi bora.
'Sawa wewe sema tu kwasababu una mdomo wa kusema, lakini kama ingelikuwa ni wewe ungeona ugumu uliopo na nina uhakika kila mtu angesita kumfokea mtoto wa bosi na kujipendekeza kwake . Najua usemalo kuwa sheria ni msimeno hukata mbele na nyuma, lakini wakati mwingine Mhhhh....
'Sawa kabisa sheria ni msimeno hukata mbele na nyuma na sheria ni mizani hupima kwa uadilifu, na wewe na mimi tunatakiwa tuwe waadilifu kwa kuhakikisha sheria na majukumu tuliyopewa tanayatekeleza bila kujali ni nani tunayemtekelezea ili mwisho wa siku tusilaumiwe'.
'Haya nimekusikia na kesho akija hataamini kuwa ni mimi yule yule , nitafanya kama niwafanyiavyo watoto wangu nyumbani najua ataogopa kuja mezani kwangu tena' akasema na wote waliokuweopo wakacheka.
Ni kweli haya yanatokea maofisini na tunahitaji kukummbushana kwani udhaifu huo upo na tukikumbushana huenda tukajijengea uthabiti wa kufuatilia majukumu yetu
Ni mimi: emu-three
3 comments :
Jamani hii kitu inakera hasa ukiwa wewe ndio upo pale mbele wakija wageni wa kila namna inabidi uwahudumie, sasa anakua mtoto wa bosi anaanza kuvuruga utaratibu wako mzima. Lakini mimi sijali kuwa ni mtoto wa bosi au ni bosi mwenyewe, huwa wananiona nina kiburi, lakini natimiza wajibu wangu
Kumbuka pia kwamba bosi akiwa kijana hata wafanyakazi wazee wanaomzidi umri wanampa shikamoo. Nidhamu ya woga na kujipendekeza ndiyo tatizo.
Hayo yana mwisho jamani kitu ni kujituma na kujua wajibu wako
Post a Comment