Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha
Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..
Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.
MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.
TUPO PAMOJA DAIMA
Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;
https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:
https://www.facebook.com/diaryyangu/
`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;
Monday, July 26, 2010
mteja ni mfalme
Ilikuwa leo asubuhi nilipofika kituoni katika kuhangaikia tumbo, nakapita eneo nakukuta kikundi cha watu wamejazana kweli nikaona ngoja niangalie nini wanachochungulia. Oh, kumbe watu wanaangalia magazeti ambayo mengi yalipambwa na mambo ya uchaguzi. Nami nikaona nisogee niangalie nini kulikoni. Wakati nahangaika angalau nipate kuona vichwa vya habari akaja ndipo akaja huyu dada aliyesimamisha gari lake pembeni na kutaka kununua gazeti.
'Hivi jamani huyu muuzaji atapata hela kweli kama wote mnaishia kusome hapohapo mezani. Wewe muuza magazeti tupe gazeti kwani hata sioni ninuulie gazeti gani, wasionunua wametuziba' akadaikia jamaa mwingine.
Ilibidi mimi niondoke haraka kwa aibu, kwani ni kweli wasoma vichwa vya habari walitanda kila kona ya ile meza, kiasi kwamba huwezi kuona nini kinachouzwa pale mezani na muuzaji hana jinsi, kwani mteja ni mfalme. Unaweza ukasema vibaya kumbe kati ya wale wanaosoma vichwa vya habari wakawa miongoni mwa watakaonunua.
Wakati mwingine inakuwa kero, lakini wakati mwingine ni njia ya kuwavuta wateja katika bishara, kuwapa nafasi ya kukagua kile wanachotaka kununua, na kama muuzaji unatakiwa usiwe mkali, hasa bishara hizi za mashindano. Ninashangaa sehemu nyingine zinazotoa huduma kwa watu na watu ndio wateja wao kunakuwa na kutowajali wateja. Unaweza ukafika ofisini na hata karibu usiipate na yule mpokea wageni anaweza akajifanya kuwa hajakuona, na wakati huo anaongea na simu, na anachoongea ni habari za jana kwenye starehe zao.
Hili lilinikumbusha mashirika mengi ya umma yalivyoteketea, kwasababu ya kutowathamini wateja, kwani kipindi cha nyuma, bidhaa zilikuwa adimu na kuzipata ilikuwa lazima uhangaike sana. Niliwahi kufanya kazi katika kampuni moja iliyokuwa ikizalisha mifuko ya kuwekea mbolea. Mali zilikuwa chache kuliko wateja wanavyohitaji, kwahiyo hata wazailishaji walikuwa wakichoka na kubweteka. Na ilipokuja biahsra huria makampuni kama hayo yakawa mengi na matokeo yake wateja wakawakimbia na kufuata kule kwenye nafuu ya bei na kwa vile mashirika haya yalishabweteka na hali ya kukimbiliwa na wateja basi ikawa ndio kifo chao.
Sidhani kwamba hatuna wataalamu wazuri wakuyaendesha mashirika yetu mengi yaliyokufa, kwani wateja ni wengi kwa mfano shirika la umeme, lina wateja wengi na haliwatoshelezi, nitashangaa kusikia kuwa haliwezi kujiendesha. Na kama kutatokea tanesco mwingine akashindana na hili huenda ikawa kama yalivyopotea mashirika mengine. Kwanini? kwasababu tunapokuwa na wateja wengi tunasahau kuwathamini hawo wateja na wakati mwingine kuwaona kama kero. Wanapojazana maofini mwenu kutafuta hizo huduma hatuwahudumii ipasavyo, na wakati mwingine hatuwajali na kujali muda wao. Hili ni kosa tukumbuke vyovyote iwavyo `mteja huwa ni mfalme, mthamini na umjali kwani ndiye anayerudisha gharama zako ulizotumia, ukimkosa utaishia kupata hasara!
Ni mimi: emu-three
4 comments :
Sina Komenti ingawa ninakomenti kudai kuwa ingawa sikomenti kijiweni hapa nipo kama kawa :-(
TUKOPAMOJA!
NAKUSHUKURU SANA S.Kitururu, tupo pamoja
Suala la huduma kwa wateja bado sana. Nilienda kufungua akaunti katika benki moja na nilishangaa nilivyohudumiwa. Utafikiri nilikuwa nimekwenda kuomba mkopo. Pengine ni benki inayoendeshwa kwa hasara huku ikitegemea kupigwa jeki mara kwa mara na pesa za walipa kodi...
Halafu nikaenda Voda kununua modemu ya mtandao. Binti alikuwa amenuna amefura kama chatu. Niliambiwa kwa kiburi kwamba hizo modemu zimekwisha, hajui ninakoweza kuzipata na pengine haina haja! Niliondoka kimya kimya...
kwa kweli hata mimi umenigusa tanesco customer care ni ZERO ! nilikwenda kuripoti mita ni mbovu walinizungusha ingia hapo ingia pale mwisho wa siku waliniambia nimeiba umeme mita imechezewa nikalipa faini roho inaniuma sana likija shirika lingine la umeme nahama haraka iwezekanvyo
V.M
Post a Comment