Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha
Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..
Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.
MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.
TUPO PAMOJA DAIMA
Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;
https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:
https://www.facebook.com/diaryyangu/
`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;
Monday, July 19, 2010
Maji yakimwagika hayazoleki
Kila mtu alishituka kusikia kauli hiyo. Unajua huyu alikuwa nani!
Kauli hii ilitoka kwa shemeji mtu, na anamwambia mdogo wa dada yake na ni mbele ya mke wake, mkwe wake, yaani mama wa mkewe na wanafamilia wengine. Kila mtu aliduwaa, kwani huyu jamaa ni mtaratibu sana na hana tabia yoyote ya kihuni. Na angeamini kuwa huyu jamaa angefanya hili, ama kweli umdhaniye siye kumbe ndiye.
Maua alikuja kwa dada yake hapa mjini, safari hii hakuja kwa likizo tu bali pamoja na mataibabu, kwani kwa kipindi cha miezi miwili hivi kumekuwa kukija taarifa kuwa Maua anaumwa magonjwa yasiyojulikana na anakosa vipindi mara kwa mara. Basi dada mtu akaona amchukue ndugu yake huku mjini ili pate matibabu na mara nyingi huja kwakwe akiwa likizo na kupata ada za shule.
Hata likizo iliyopita alikuja na akaa likizo nzima, na aliondoka akiwa hana matatizo ya kiafya zaidi ya homa, homa na tumbo, kwahiyo walihisi safari hii ameondoka na malaria sababu ya mbu za Dar!
‘Naona tumchukue shemeji yako aje hapa ili apate matibabu na uchunguzi zaidi’ mke akamwambia mumewe
‘Sawa, mimi sina matatizo na hata ikiwezekana aje asomee huku, naona maisha ya shule za kijijini yanamshinda’ akasema mumewe kwa furaha.
‘Hapana, hiyo sikubalini nayo, maisha yenyewe hapa ni yakubangaiza, isitoshe vyumba tulivyo navyo ni viwili, yeye akija analala kwa shida na watoto. Lakini kwa dharura sio mbaya, akija akikaa mwezi sio mbaya, lakini sio aje asomee hapa, una pesa za kumtafutia chumba chake..’ mkewe akasema.
‘Nilikuwa na mpango wa kutafuta nyumba yenye nafasi, vyumba viwili na sebule, unaonaje mpango huo’ akasema mumewe.
‘Hahahahah..hebu usinichekeshe, hali yenyewe ngumu, hapa tunatakiwa kuwatafutia watoto shule nzuri, kwani huoni jinsi kiwango chao cha elimu kilivyoshuka safari hii. Wewe unataka kutafuta nyumba kubwa ya kupanga, kama hizo hela zipo kwanini tusianze kufyatua matofali tujenge kibanda chetu angalau viumba viwili, kiwanja kipo kwanini tuendelee kupanga’ mkewe akasema huku akimrekebisha mumewe nguo alizovaa.
‘Wewe hayo niachie, huji nina mipango gani kichwani, tutajenga nyumba muda si mrefu ngoja tuyamalize haya matatizo madogo madogo’ Mumewe akasema huku anatoka kwenda kwenye mishemishe zake.
Maua alifika akiwa mnyonge na alimkuta dada yake akiwa katika biashara zake ndogondogo, walisalimiana na maongezi yao yalikuwa sio mazuri kama kipindi cha nyuma mpaka dada mtu akashangaa.
‘Vipi mbona upo hivi, ndio huko kuumwa kumekubadili namna hiyo. Hebu chukua chakula hapo juu ya kabati ule’ akasema dada mtu akipanga vyombo vyake vilivyotoka kwenye biashara ya mama lishe.
Mara Maua akatoka mbio kuelekea nje, kiasi kwamba dada mtu akashituka na kumfuatilia huko nje, akahisi kuwa huenda mdogo wake ana mashetani, asije akakimbia na kupotelea mitaani na mara akasikia akigugumia kutapika toka chooni. Mhhh, dada mtu nguvu zikamuisha, akajisemea moyoni huenda ni malaria hiyo, mmmh, lakini mbona namuona kama ….hata haiwezekani. Akawa anajisemea hadi Maua alipotoka chooni.
‘Wewe Maua hebu sema ukweli upo sawa wewe’ dada mtu akadadisi kwa hasira.
‘Sawa kwa vipi, najisikia vibaya tu, sijui sababu ya usafiri na kule kuumwaumwa…’ akasema huku anarudisha chakula bila kula.
‘Sasa mbona huli chakula…
Sauti ya mumewe ilisikika ikipiga hodi na alipoingia akasalimiana na shemeji yake na mara Maua akakimbilia chumbani, na huko akaangusha kilio kwa chinichini.
Baada ya wiki ya kukaa hapo siri ikagundulika, kwani walipompeleka hospitali iligundulika kuwa ana ujauzito na kivumbi kikawa ni ujauzitoni wa nani!.
Mara akasema ni kijana aliyekuwa akisoma naye ndiye aliyempa uja uzito huo, mara akasema ni jirani yao wanayeishi naye huko kijijini. Ilimradi kila aliyembana alitoa jibu tofauti hadi Ikabidi kiitishwe kikao cha wanandugu akiwemo mama wa huyo binti , kaka wa mume mtu na mzee mmoja wa huko kijijini mwenye mafungamano na wazazi wa mke.
‘Wewe binti, hiki ni kikao ambacho tunataka kujua ni nani kakupa hiyo mimba, nia yetu ni kutafuta ufumbuzi wa kudumu wa tatizo hili, na ukitudanganya ujue unajidanganya mwenyewe. Hii ni kwa faida yako na kwa faida ya familia yako pia. Hebu tuambie kwa uhakika ni nani kakupa huo ujauzito…’ akaanza yule mzee.
‘Mimi nilishawaambia sina uhakika ni ninani hasa..’ akaanza kulia kwa sauti.
‘Ina maana wewe ulikuwa Malaya, unatembea na wanaume kibao na udogo wote huo, hiyo tabia imetoka wapi kututia doa katika familia…’ dada mtu akakurupuka kwa hasira akitaka kumpiga mdogo wake.
‘Mimi sio Malaya, nimetembea na huyo huyo aliyenipa mimba sijawahi kutembea na mtu mwingine…sasa, …’ akaanza kulia kwa sauti.
Mara shemeji mtu aliyekuwa kimya muda mwingi akainuka na kutembeatembea na baadaye kuelekea mlangoni na alipohakikisha huko nje hakuna mtu akasogea hadi alipokuwa yule binti akilia na kumshika bega.Maneno yalimtoka kwa shida , lakini yalieleweka na aliyoyasema yaliwafanya chumba kizima kitulie kimya kwa muda
Wote walishindwa kuamini kuwa kweli huyo jamaa anaweza kufanya hicho alichokisema. Kila mtu aliguna, na kabla mzee ambaye ndiye kama mwenyekiti hajasema neno, mkewe jamaa akasimama kwa haraka kama mtu aliyeapagawa na mara akaingia chumbani, alipotoka alikuwa kashikilia kisu kirefu na mbio akaelekea alipokaa mdogo wake. Isingekuwa mama yake ambaye alikaa karibu na binti yake aliyebebeshwa mimba ambaye kwa haraka alikiona kile kitendo na kumdaka mkono mke mtu na bahati nzuri kile kisu kikamkosakosa Maua na kuzama ndani ya godoro la kochi.
Ikawa kukuru kakara, hadi walipofanikiwa kumnyanganya yule mke mtu hicho kisu.
‘Nasema ama mimi ama yeye , lazima mmoja atatangulia ahera, simtaona. Kama yeye kaona mimi nafaidi basi aniondoe duniani kwanza ili aishi na huyu baradhuli wake, vinginevyo mimi nitammaliza…’ Na kauli hiyo ikamfanya mama yao mzazi apandishe shinikizo la damu, na kudondoka chini na ikawa hekahekka nyingina ya kumuwahisha hospitali.
Sijapata zaidi ya hayo na ni-nini kimeendelea lakini, mume mtu alishasema yeye kafanya hivyo kwasababu amempenda mdogo mtu na yupo tayari kumuuoa. Kila mtu alimshangaa kwa kauli yake hiyo na walimwabia wazi hiyo haiwezekani kwasababu hawezi kumuoa mtu na dada yake
'Hiyo ni laana unatuletea katika familia ulisikia wapi mtu anaoa mke na mdogoo wake, umekosa mke mwingine, wanawake wapo kibao...hiyo ni tamaa yako tu '
Yeye akasema, kama haiwezekani basi, limetokea la kutokea, na maji yameshamwagika hayazoeleki.
Haya kisa hicho nimekileta kwenu, kimetokea karibuni naomba tusaidiane kwa hili. Wewe kama mtu wa hekima ungewashauri nini hawa, Kwani ndoa ipo hatarini, na matatizo ya watoto yanahatarisha afya za wazazi je maswala kama haya tutayamaliza vipi, kwani sio siri yanaongezeka na ni nani hasa wa kulaumiwa. Wanawake wansema ni tama za wanaume. Wanaume wanasema ni makosa ya wanawake kutokujali wajibu wao wa ndoa. Wajibu upi?
Ni mimi
emu-three
4 comments :
Mbona mila za makabila fulani hiyo ni kawaida tu...ukipenda tunda, penda na tawi lake ...aah, sio kwamba napenda hiyo tabia hapana ila wao ndivyo wanavyosema
Kiafya sio nzuri, kidini hairuhusiwi na halafu mbona watoto mtawapa shida ya kuangalia asili ya mama...naona kuna...lakini anyway hebu kama kuna wataalam watupe ubaya wake ni nini
MMMH! HII DUNIA SASA TUNAVYOIPELEKA SIO. BORA TURUDI KWA MUNGU WETU. NI MAPEPO TU, NA ROHO ZA UZIZI ZINATAWALA HAPO. HAPA MIMI NAONA MWENYE KOSA NI SHEMEJI. NDIO WA KULAUMIWA, KWANI HUYU MTOTO NI MDOGO HAJUI HAYO PIA AMETOKA KIJIJINI, LABDA AMEMDANGANYA NA KUMPA AHADI NYINGI NA CHIPS KUKU ZA MJINI ZIMEMCHANGANYA, MPAKA AMESHINDWA KUMWAMBIA DADA YAKE, PENGINE NA VITISHO VYA HAPA NA PALE. PIA HAPA NAE MAUA ANALAUMIWA KWA KUTOKUWA WAZI KWA DADAYE. (SIWEZI JUA UKARIBU WA MAUA NA DADAYE UKOJE NA KUTOKANA NA HII STORI YAKO INAONEKANA HUYU DADA ALIKUWA ANAMWAMINI SANA MME WAKE KIASI KWAMBA ALIKUWA HANA WASIWASI NAE KABISA, KUMBE NI FATAKI.
KAMA NINGEKUWA MIMI NISINGEMZURU HUYO MDOGO WANGU. NINGEMSHITAKI HUYU MUME KWA KOSA LA KUTEMBEA NA MWANAFUNZI NA KUMTIA MIMBA NA KUTAMBA MBELE YA KIKAO CHA FAMILIA. AKAOZEE JELA FATAKI MKUBWA HUYO HATA KAMA NI MME WANGU. ILI IWE FUNDISHO KWA WATU KAMA HAO.
Huyu shemeji naye duh! amependa kuku na mayai yake. kwa kweli kwa mila nyingine sio shida lakini kwa mila yangu mimi si haki kabisa kama alivyosema asiye na jina 19/7/2010 4:13 PM Binti Maua ni mtoto mdogo na anatoka kijijini na shemeji kampa maneno mazuri si ajabu kwa binti Maua kukubali na inawezekana alimtisha. Kwa hiyo hapa Dada hana kosa, ana haki kabisa ya kukukasirika kama alivyokasirika. Nadhani ningekuwa mie ningezimia na pia nisingemkaripia mdodo wangu ila ningemvamimia mume wangu. Kwa hiyo hapa kimsingi twaweza kusema mwenye kosa ni wote shemeji na binti Maua . Nimesema Binti Maua ana kosa kwa vile angaweza kusema kwa dada yake nini kinaendelea kama kweli angekuwa anawaza mbali. Ni mawazo yangu tu.
Post a Comment