Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Monday, July 5, 2010

Asiyekuwepo na lake halipo

Tulikuwa ndani ya bahari, tunaelea, kila mmoja akiwa anajitahidi kuogelea. Mimi sio mjuzi wa kuogelea, lakini kwa kipindi hicho nilijifunza mumo kwa mumo, nashukuru pembeni yangu alikuwepo mzee mmoja kama namfahamu vile, lakini akili kwa muda ule haikutaka kujua ni nani, zaidi ya kuogelea na kufika mwisho kwani vinginevyo tungekufa na maji, baridi na madhara mengine yaliyopo baharini kama mamba na mengineyo.
'Kijana najua wewe ni rahisi kufika ufukweni, kama nitakufundisha mbinu za kuogelea, mimi na uzee huu nitachoka mapema, natumai nikikufundisha ukifika ufukweni utatafuta mbinu za kuja kuniokoa. Sasa fanya hivi , na hivi na sogea upande huu wa bega langu la kulia..' yule mzee akawa ananifundisha huku tunasonga mbele, na ilibidi wakati mwingine anibebe nilipotaka kuzama, na kweli baada ya muda, kwangu ikawa rahisi kuogelea na nikawa nasonga mbele. Ulikuwa ujuzi mzuri unaoweza kuufananisha na ua waridi.
 Jinsi tulivyozidi kwenda mbele mzee mfadhili na mwalimu wangu akawa anachoka, na mimi kila nilivyojitahidi kumbeba ikawa nashindwa, kwani pamoja na ujuzi niliopata, bado sikuweza kuhimili kubeba mtu mwingine. Yule mzee akatambua hilo akasema; `Najua hutaweza kunibeba,kwani ujuzi na uzoefu wako nii mdogo, hata hivyo tumechoka, na naogopa kama nitakufundisha jinsi ya kubeba mtu tutaishia kuzama wote, wewe ogelea hadi mwisho ukifika huko kumbuka , kunikumbuka, kwani vijana wangu niliwafundisha nilitaraji watakuja kuniokoa lakini hadi leo sijawaona..'
`Mzee sitakusahau kamwe kwani wema hauozi...' nilmwambia naye akainua mikono juu kumshukuru Mungu. Na hapo moyo wa kuogelea haraka nifike mwisho ukaongezeka, nikijua nina deni kubwa nyuma yangu.
 Kweli nikajitahidi hadi nikafika mwisho, nilipofika mwisho nikawa sina nguvu, ikabidi kujipumzisha na kupata matibabu mbalimbali. Na hali ilipokuwa shwari, nikakumbuka kuna msaada natakiwa niupeleke kwa wengine waliopo baharini, hususani yule mzee. Kila nilipopeleka msaada ukawa unaishia kuwachukua wale waliopo karibuni, kwani kila uliyemkuta alikuwa katika hali mbaya sana. Ikawa nawachukua baadhi kutokana na chombo kilivyo, nawafikisha mwisho, narudia tena kuwachukuwa wengine.
 Ilifikia hatua nikataka kuwasusa wengine ili nimkimbilie yule mzee lakini ikawa hakuna njia ya kupita, lazima uwapite wengine wanaohitaji msaada , na sio rahisi. Basi nikasema moyoni mwangu, Mwenyezi Mungu atasaidia hawa wataisha hatimaye nitamfikia yule mzee. Kwakweli haikuwa rahisi. Siku ikawa inaisha na watu hawaishi, nikajiuliza moyoni nifanyeje, kwani imekuwa ile methali ya asiyekuwepo na lake halipo, na fimbo ya mbali haiui nyoka...
 Nilisikia kama sauti ya yule mzee ikilalamika, na kusema mbona kijana wangu hukumbuki fadhila, wema niliokutendea mbona umeshindwa kuulipa...na maneno mengi ya kunilaumu...nilikosa raha, nikasema hataa... ngoja sasa nifumbe macho nikimbize ile mashine nikamuokoe yule mzee. Ilikuwa kazi ngumu, kwani ilibidi hata kuwagonga wengine ili upate upenyo wa kumfikia yule mzee, na mashine kufika mbele ikawa mbovu. Ikabidi niruke chini niogelee angalau nikamuokoe yule mzee. Kwa mbali nilimuona mzee wa watu akitapatapa, nikaita kwa sauti kuwa asikate tamaa nakuja, lakini kila nilivyomsogelea akawa kama anazama na kupotea....oh, ina maana nimeshindwa kulipa fadhila...nikajilaumu. Mara oooh, kumbe ilikuwa  ndoto nikazinduka, na sikuweza kulala tena kwani ndoto ile ilinipa mawazo mengi sana. Je ile ndoto ina maana gani, nini fundisho lake, na kama ni hivyo nifanyeje?
 Katika maisha yetu hadi tulipofika tumelelewa na jamii za aina tofauti, asilimia kubwa wamelelewa na wasikuwa wazazi wao, na wengi wa walezi hawo walitaraji kuwa fadhila walizozitoa sio tu watapata matunda kutoka kwako bali hata kwa mola wao wamewekeza. Matarajio ya wengi ni kupata msaada wowote wa fadhila hizo, lakini kutokana na hali zakimaisha mambo yanakuwa sivyo. Hii inatokana na majukumu ambayo mfadhiliwa anakutana nayo, na isitoshe mfadhiliwa anajikuta katika lindi la majukumu ambayo kuyatatua kwake ni mzigo, na waliojirani naye wanahitaji msaada wake na kwasababu wapo jirani unaona kuwa wao wapo katika hali mbaya zaidi.
 Hili ndio hali halisi ya jamii zetu, kwa wenye kuelewa wataniunga mkono, kwani maisha na kipato chetu ni kama mkate mdogo uliopo mkononi, haukutoshi na badoo unatakiwa kuwagaia wanajamii hasa familia sio yako na ile inayokuzunguka. Je utaugawaje huo mkate ilihali hata wewe haukutoshi? Je jamaa inayokuzunguka itakupa nafasi ili ukalipe fadhila za wazee wa watu waliokufadhili hadi kufikia kuupata huo mkate mdogo. Kumbuka jamii yako inakuona, inakuhusu na ndio imesimama katikaktii na njia ya kufikia kijijini kwa wazee ambao wanahitaji sana huo mkate, sasa ufanyeje? Oh, ama kweli asiyekuwepo na lake halipo, na sio kwamba unapenda lisiwepo ila...

 Tafakari na toa hoja za hekima.

From miram3

5 comments :

Anonymous said...

Tatizo kubwa la gurudumu la umasikini ndio hilo, mtazunguka palepale, kwani ukipata kidogo unatakiwa ukakigawe ili ulipe ulichogawiwa, vinginevyo jamii haiwezi kukuelewa.
Ushauru wangu. Tenda uwezalo, kwani huwezi kutoa kisichokuwepo

Anonymous said...

Ukikopa ujue kuna kulipa. Kukopa harusi kulipa matanga. Unachotakiwa nikujaribi sana kuwasaidia wazee wetu, hawa walipo karibi na wewe ina maana wameshafika(rejea ndoto yako) kimbilia waliopo mbali, hwa waliopo karibu wanajilemeza, kwasababu wanajua kuna msaada, waliopo mbali hawaoni huo msaada, wanajituma lakini hawapati, wakikosa, wamekosa kweli...
Hiyo ndoto yako ina mantiki ya kihekima kwa wenye kutafakari

Anonymous said...

Heri yangu mimi sijasaidiwa na mtu, nilistrugle kivyangu-vyangu na naishi kimpangilio wangu.
Nawashauri sana mjitahidi kulea watoto wenu wenyewe, haya maisha ya kutegemea ndugu awalelee, mnawatishwa wenzenu mizigo mikubwa baadaye. Kumbuke waliotishwa mzigo, uchungu kwao kwa huyo mtoto ni mdogo zaidi ya kupata fadhila, kwao ndoto yao ni kupata fadhila, hilo ni kweli kabisa.

Anonymous said...

Jamani yote hayo ni sababu ya umasikini wetu. Hali kama hiyoo haipo katika familia zenye uwezo.

Anonymous said...

Hata kama utasaidia huwezi kurejesha fadhila huyu ni sawa na mzazi wako, unachotakiwa kufanya ni kuwa karibu nawo kila iwezekanvyo. Najua hutaeleweka, lakini angalia sana maisha yako kwani ukikosea utaishia kuwa katika lawama kama unavyolaumiwa