Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha
Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..
Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.
MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.
TUPO PAMOJA DAIMA
Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;
https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:
https://www.facebook.com/diaryyangu/
`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;
Monday, June 28, 2010
Ukitenda nawe ukumbuke kutendewa
‘Acha kabisa, acha kunikumbusha aibu hiyo, sijawahi kuzalilika kiasi hicho, unajua kuzalilika, basi mimi nilitahayari na kutafuta sehemu ya kujficha uso wangu si-ku-i-o-na…’ alisema rafiki yangu, nikahisi huenda siku hiyo alilewa kupita kiasi, lakini sikumbuki kuwahi kumuona jamaa huyu akilewa, sasa yalimkuta masahibu gani, nikakaa kimya kumsikiliza.
‘Vaa nguo twende kwenye shughuli ya jirani yetu, siunajua, shughuli ni watu na watu ndio sisi, vaa vaaa haraka twende’ akanishika mkono kunisukumia chumbani, nami bila ajizi nikaingia chumbani na kuvaa nguo za mtoko. Nilitoka nje nikamkuta mwenzangu kasimama ananisubiri tuondoke, nikamuaga mke wangu huku anajizuia kucheka, sikujua nini kinachoendelea kwa muda ule!
‘Sasa sikiliza mwenzangu, tukifika pale shughulini, tukae viti vya mbele kila mtu atuone’ akasema huku akichapa mwendo, nikaitikia kwa kichwa huku nikimshangaa kwa mabadiliko hayo. Rafiki yangu huyu akienda kwenye shughuli alikuwa hapendi kukaa viti vya mbele na ni kwanadra kumuona shughulini. Sasa leo naona mabadiliko ya hali ya juu. Nikakaa kimya nikisema huenda jamaa kaamua tu kubaiilika.
Tulipofika mbele kidogo tukakutana na ombaomba, mara akasimama nakutoa hela akamkabidhi Yule ombaomba na akaniomba na mimi nifanye hivyohivyo. Nilishngaa kwa tukio hilo, kwani jamaa yangu huyu alikuwa akiwapiga vita sana ombaomba, na aliahidi mbele yangu kuwa hatatoa hela yake kuwapa ombaomba kwani eti ni wavivu. Nikamshukuru mungu kuwa hatimaye kampa mja wake nuru njema ya wema.
‘Hawa sasa ni marafiki zangu waliniokoa kiasi kikubwa kwenye shughuli yangu' Akasema huku akimbusu Yule ombaomba mkono. Nikacheka sana, huyu jamaa yangu alikuwa akiguswa na ombaomba hukimbilia kunawa mkono, eti watamuambukiza magonjwa, leo hii anashikana nao mkono hata kuwabusu! Nikaguna na kusema moyoni ipo kitu, sio bure.
‘Unajua mimi kazi yangu naweza kusema kuwa iliniharibu, nilikuwa sijui shughuli za watu, mimi na kazi. Pale kazini kwetu ukiondoka siku moja ukirudi sehemu yako keshapewa mtu mwingine. Na ukipewa sehemu ya ovyo basi ujue wewe ni ombaomba, siunjau tena mishahara ya hawa wenzetu waliojaliwa, sisi wazawa tunaonjeshwa kitu kinachoitwa mshahara, sasa ukipata sehemu nzuri inabidi uigande ili Watoto waende choo. Nilikuwa naogopa sana kuwa kama hawa ombaomba.
‘Nikawa nadamka asubuhi narudi nyumbani usiku, hata familia yangu ikawa ngeni kwangu. Wamefiwa majirani sionekani, nikionekana naenda kutoa rambirambi halafu naaga kuwa sijapata ruhusa kazini, huyo nakimbilia kibaruani. Ikiwepo shughuli naenda kutoa mchango na kuaga kuwa nina kazi nyingi. Nikuambie ukweli ilifikia hatua nikawa hata mimi mwenyewe sipendi kabisa kitu kinachoitwa shughuli. Kumbe wanajamii wananichora, kumbe wapo watu ambao kazi yao kubwa ni kuchunguza nani ni nani anahudhuria kwenye shughuli za watu'
Jamaa yangu alikatisha mazungumzo wakati tunatafuta sehemu ya mbele ya kukaa.
Naona niachie hapa ili tuwahi kwenye hii shughuli halafu ikiisha nitakuambia nini kilitokea, au mnasemaje
Mimi jirani yako
1 comment :
Aaaah, ikawaje tena, mbona unakaisha msitimu. Halafu kale kastrori ka simu iliishaje?
Post a Comment