Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Tuesday, June 29, 2010

Ukitenda nawe ukumbuke kutendewa-2

Ndugu yangu kwa kutokupenda shughuli ikafikia nikamkataza hata mke wangu, nikajitahidi mpaka naye akapata kazi kwa mhindi mmoja, basi ikawa tukiamuka asubuhi tunaacha maagizo kwa mfanyakazi wa ndani, na kama kuna mchago wa shughuli tunamuachia yeye atuwakilishie. Ikawa sisi na kazi jamii na yao. Jamii ikasema ahaa nyie ndio wafanyakazi bora eee, sisi tunajifanya hatuna kazi ee…


Mke wangu kwa kiherehere chake akataka kufanya sherehe ya kukumbuka tarehe za uzawa wa Watoto wetu, huwa tunaifanya lakini sio kwa kualika watu, lakini safari hii akataka tuwaalike watu, unajua Watoto wangu wamezaliwa tarehe sawa wote hutaamini, wote wamezaliwa tarehe 25 mwezi wa sita, ingawaje ni kwa miaka tofauti. Nikamkubalia, na kujitahidi kutafuta vijisenti, nikakopa kazini na nilikuwa na mchezo kazini nikaomba nipewe mapema. Shughuli ikakamilika kinafasi, ukiwa napesa basi nafasi ya shughuli unayo. Tukaalika watu kadi, na wao wakaitikia kuwa watakuja.

Siku ya shughuli ikafika, watu walianza kumiminika, nasi tukawa tunaagiza vitu kila wanapoongezeka, Walifika watu sikuamini, marafiki wa siku nyingi, majirani wakajimwaga, nikasuzika moyoni, nakusema kumbe shughuli ni nzuri, mnakutana na marafiki majirani ambao hamjaonana nao siku nyingi. Ndio maana wanasema shughuli ni watu.

Basi bwana mwendesha shughuli alikuwa jamaa mmoja jirani yangu, watu wanampenda sana, akaanza kuwahamasisha watu , watu wakafurahi, wakawa wanaongea na kutaniana, na Watoto wakawa pale mbele kama maharusi. Ikafika muda wa shughuli yenyewe sasa, muendesha shughuli akatuomba tutulie ana jambo lakusema, akaanza hadithi ndefu mwishowe akamalizia kwa kusema `unajua kuna usemi ninaupenda sana, usemao `ukitenda ukumbuke na kutendewa’

Pale akaanza kuigiza mtu anakuja kwenye shughuli anatoa michango halafu anaomba ruhusa ya kuondoka, akarudia hivyo kwenye msiba . Halafu akasema `sasa muda wa kutendewa umefika, watu waksema kwa sautu `umefikaaa’ Akaweka kile kipaza sauti chini akaja akanipa mkono na kunitakia shughuli njema akisema anawahi kazini. Ikawa kama vile amewaamrisha watu wengine, kila mmoaja akawa anakuja ananipa mkono na kusema anawahi kazini. Mpaka mtu wa mwisho , tukajikuta tumebakia wanandugu na Watoto wangu wakiwa wanatoa machozi.

Sasa nikasema hilo ni fundish kwangu, mimi nikisikia shughuli nakumbuka msomo wa `ukitenda nawe ukumbuke kutendewa’

Aliyeniokoa kutokuharibika vyakula na vinywaji ni shemeji yangu, alitoka haraka akawakusanya ombaomba wengi, sijui aliwapatia wapi, wakafika na kuanza kushambulia vyakula na vinywaji. Wengina wakabeba, hadi mwisho wa siku tukabakia na vyombo vichafu vya kusafisha. Kwanini nisiwashukuru wale ombaomba, fikiria ningepeleka wapi ile pilau, vinywaji, nyoma choma…name kwa mara ya kwanza nikatoa sadaka.

Nilicheka, nikacheka, mwishowe nikasema kweli ukitenda ukupunguke kuna kutendewa!

Jamani na nyie hamna stori za mafunzo mkamletea jamaa akaiweka hapa ili tupate mafunzo, kila mtu anazo, lakini kujisikia kutoa ndio ngumu. Tokeni nanyi mtapata!
 
Ahsanteni

1 comment :

Anonymous said...

I'd like to find out more? I'd сarе to finԁ out more details.


Feel free to suгf tο my page :: paydayloanscash.Net