Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Wednesday, June 30, 2010

Mtoto akililia wembe...

 Siku ile nilipitishwa na gari ikabidi nishukie karibu na makaburi. Pale nikaona nikatishe makaburini, ambapo miti ilikuwa mingi kidogo, mara nikasikia sauti ya mtu akilia kwa kwikwi, na kusema'
`Aheri ya kufa kuliko kuteseka hivi...
Sikuamini macho yangu, nilisogea mbele kidogo kuhakikisha kuwa ninayowaza ni ya kweli. Na hisia zangu zikawa kweli, yule jamaa akaanza kutengeneza kitanzi, siunajua kitanzi, kama kile wanachofungia ngombe, ndivyo jamaa alivyokitengeneza, akajipima shingoni akaona kipo safi, huyu akaanza kupanda juu ya mti mmoja mrefu. Hapo nikaanza kuingiwa uoga, kwani mimi sijui sana kupanda mti, mimi nimezaliwa mjini,mambo ya kudandia miti wapi na wapi. Nikasema hapa naweza kuwa shahidi au muuaji. Nitawezaje kumuokoa yule mtu akipanda juu nami siwezi kupanda.
 Yule jamaa alishafika juu akatafuta tawi kubwa la pembeni akawa anakwenda nali bila kujali kuwa atadondoka. Nikaona hapa kuna tatizo huenda yule jamaa ni kichaa, au anataka kufanya mazoezi. Hapana huyu kuna tatizo, nikaochomoa simu yangu na kumpigia rafiki yangu mmoja, yeye ni mkwezi wa minazi.
'Njoo haraka kuna dili la kukwea minazi...' nikamdanganya, na kumuelekeza wapi nilipo.
 Haikuchukua muda jamaa akaja na pikipilki lake, nami nikamuonyesha jamaa anavyohangaika kuifunga kamba kwenye lile tawi.
'Wewe vipi wenzako tunatafuta pesa wewe unatafuta balaa, huoni jamaa kachoka na maisha anataka kujiua, hapa akifa na wewe unaenda kusota jela, mimi sipo...' jamaa akawasha pikipiki kutaka kuondoka.
'Wewe mbona muoga, kama anataka kujiua, tumuokoe, hujui kakupungwa na masahibu gani...'
 Wakati tunaongea hivi , mara jamaa akafunga ile kamba vizuri na kuivika shingoni, na la kushangaza akawa kama anaomba Mungu halafu akaangalia chini tayari kujiachia. Wakati anajiachia, badala ya kudondoka na kuninginia kwa ile kamba, akanaswa na tawi kwenye shati, kwahiyo shati likawa kama kamba na ile kamba ya shingoni akawa ndefu. vinginevyo angekuwa keshamaliza kazi. Mara tukaona jamaa akitoa macho kwa woga, akiwa anaangalia juu ya lile tawi, na sisi macho yetu yakaangalia pale alipokuwa akiangalia yeye. Sijawahi kuona mdudu kama yule, niliogopa na kutaka kukimbia.
'Sasa unaenda wapi wewe siumesema unataka tumuokoe, haya sasa panda ukapambane na yule chatu...lile ni joka misili ya chatu...' akasema rafiki yangu akiwa na hamu ya kuona nini kitatokea. Nilimshangaa mwazoni alitaka kuondoka, lakini sasa hamu ya kukaa imemjia.
 Kule juu ya mti jamaa akawa anahangaika kuingoa ile kamba shingoni lakini ikawa shida, na shati likawa linazidiwa nguvu, linachanika, ikawa kukurukakara. Tukasikia mlio wa kuvunjika kwa lile tawi, lile tawi likazidiwa nguvu, na kuanza kukatika. Jamaa akihangaika kujiokoa, kwa kulikimbia lile joka ambalo lilisha nyosha shingo tayari kwa vita, lakini kikwazo kikawa ile kamba aliyojifunga shingoni, ilikuwa ngumu kuitoa na kule alipoifunga hawezi kupafikia kwani ndipo yule mdudu aliposogelea.
 Jamaa macho yakamtoka kwa woga, alishikwa na woga wa hali ya juu, hutaamini kuwa ndiye yule aliyetaka kujiua, sasa kwanini anaogopa tena. Nafikiri dua yake ilishajibiwa kuwa usihangaike sana kujiua kwa kamba huyu mdudu atakusaidia, mbona sasa unaogopa kiumbe changu...
 Hamadi lile tawi lakavunjika na kumtupa yule jamaa mbali kabisa na lile joka, lakini kamba ikawa bado imenasa juu, kule alikoifunga. Pale alipokuwa ananinginia ni karibu na chini, lakini miguu yake ilikuwa haiwezi kugusa chini. Akawa anahangaika kuitoa ile kamba kwa bidii shingoni lakini alivyozidi kuhangaika ndivyo alivyozidi kujinyonga zaidi. Juu kule yule mdudu naye akaogopa na kupotelea kwenye mawati.
 Mwenzangu alipokua alikuwa amejiandaa na panga la kufulia nazi, alilichomoa haraka na kumkimbilia jamaa alipokuwa ameninginia na kuikata ile kamba. Mimi nilikuwa karibu nijikojolee kwa woga. Mawazo yangu yote yalikuwa kwa yule mdudu. Jamanai mie naogopa nyoka, usisikie.
 Kisa hiki alipokuwa akinihadithia huyu jamaa nilikumbuka ule usemi wa `mtoto akililia wembe mpe, ukimkata atajifunza...sasa vipi jamaa anaweza kurudia tena kujitundika...sidhani , nafikiri pale alipata ujumbe toka kwa muumba, kuwa maisha ni mitihani, na mitihani hiyo katuwekea ili tupambane nayo, swala la kufa ni lake mwenyewe, anaua lini utakufa, kwahiyo subiri, pambana na maisha. Kama husikii haya, chukua wembe, ukukate ukiumia utajifunza, kwani mtoto akililia wembe mpe....

Naomba niwekee hii hwani, kwani jamaa sasa kawa mchamungu wa hali ya juu

13 comments :

Anonymous said...

Nasikia wengina mpaka wanajinyea, au kujikojolea. Unajua watu wanafikiri kufa mchezo. Hebu jaribu kujizipa pumzi kwa muda, au ingiza kichwa ndani ya maji ukose pumzi...kufa sio mchezo bwana, roho inatolewa mahala pake...acha wee..acheni mwenyewe afanye kazi yake, msitake kumsaidia, kwani hahitaji msaada!

Anonymous said...

Umenichekesha kwelikweli mtoa hoja wa kwanza. Sasa angalia jamaa kapata msaada wa joka, limtoe roho, anahaha, hapana sitaki kufa kwa hivyo...kufa ni kufa ...

Anonymous said...

Lakini nyie mwajua kwanini alitaka kujiua, huenda kapata ngoma, na kaambukiza watu kibao..au anadaiwa jamaa wanataka kumtoa roho, sasa anaona aitoe mwenyewe

Anonymous said...

Vyovyote iwavyo haihitajiki kujiua, hayo ni mapepo yanamsumbua tu.

Anonymous said...

Kama ni mapepo basi ashindwe...

Anonymous said...

All that's left is for this little girl to decide it's time.
When you have found a few bassinets that meet the above requirements
of comfort, durability and safety, you can then start choosing based on style.
A woman recovering from delivery often is instructed to not
lift heavy objects, which would hinder the healing process.
Here is my page : round crib

Anonymous said...

Undeniably believe that that you said. Your favorite
justification seemed to be at the net the simplest thing
to take into accout of. I say to you, I certainly get annoyed whilst other people consider worries that
they just do not recognize about. You controlled to hit the nail upon the top and defined out the entire thing with no need
side effect , people could take a signal. Will probably
be back to get more. Thank you
Also visit my webpage :: compare

Anonymous said...

This can be the most popular dosage of Phentermine diet
supplements recommended.
Feel free to surf my web-site ; phentermine 37.5

Anonymous said...

I've read a few excellent stuff here. Definitely value bookmarking for revisiting. I surprise how much effort you place to create such a fantastic informative web site.

Also visit my blog ... medhealthcareers.com
My webpage > medhealthcareers.com

Anonymous said...

Its like you read my mind! You appear to know a lot about this, like you wrote the book in it or something.
I think that you can do with a few pics to drive the message home
a bit, but instead of that, this is wonderful blog.

A fantastic read. I'll certainly be back.

my web site ... acheter retweet

Anonymous said...

Тhankѕ fοr ones marvelous posting! І
quite enjoyeԁ readіng іt, you could be a great authoг.
I will bе suгe to bookmаrk your blog and
ωill сome back from now on. I want to
encourage yοu to definitely continue your grеat posts,
have a nice аfternoon!

Hегe is my blog post; duongda247.com

Anonymous said...

Your style is reallу unique сompared to othеr ρeople I have rеaԁ ѕtuff from.
I aρpreciаtе уou fοr pοsting when yοu've got the opportunity, Guess I'll just
book mаrκ this web site.

Ηere іs my web-site ... www.paydayloanscash.net

Anonymous said...

There's a whole lot more оptions ωhеn it comes to
chooѕіng the system that will deliver their streaming vіdeos,
mοvies and original online content ѵia the web.


Hеre iѕ mу webpage :: phim