Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Friday, June 18, 2010

Tusikatae wito

Naomba niwekee hii habari.
***
  Siku hiyo nilikuwa nimechoka na kichwa kikawa hakifanyi kazi vizuri, mara simu ikalia mezani niliiangalia kwa hasira, nikikumbuka kuwa nilimwambia yule dada mpokea simu asinipigie simu yoyote. Niliipokea kwa hasira na kuanza kulalamika.
`Vipi wewe dada sinilikuambia sitaki simu yoyote leo' nikabwata
'Ndio lakini aliyepiga sasa hivi ni rafikii yako mpendwa, mara nyingi umesema yeye akipiga au akija tumruhusu umesahau kaka yangu' akasema huyo dada kwa unyonge. Kweli nilikumbuka kuwa rafiki yangu Mawazo huwa ananitemblea na huwa akija tunaongea sana, lakini tangu awe hana kazi nimkuwa sipendi kukutana naye kwasababu kila akija maongezi mengi ni matatizo yake. Na akinihadithia yananipa mawazo na huruma, na inabidi nimpe chochote nilichokuwa nacho.
 Hali hii ya kila akija lazima nimpe kitu imekuwa kama jukumu kwangu, kiasi kwamba nilimuona kama mmoja wa familia yangu ambaye ninawajibika naye. Nikaona sasa nitafute njia ya kumkwepa, lakini haikuwezekana. Leo ndio huyoo nasikia anataka kuongea na mimi, nilijua kuwa ni moja ya shida zake.
`Leo sitaki kuongea na yoyote, hujanielewa, ina maana huyo rafiki yangu sio yoyote' nikasema na kukata ile simu.
 Mara simu ya mkononi ikaita, na kuangalia ni yule yule rafiki yangu , nikaizima ile simu. Nikatoka mle ofisini nikaenda ofisi nyingine kupoteza mawazo. Na huko nikakutana na rafiki ynagu mkubwa akanipa na yeye shida zake kuwa wapo jamaa zake kila siku wanakuja kumuomba vijisenti, siunajua tena hali ya maisha ilivyo ngumu, wewe unapanga bajeti isiyopangika, haina mfadhili au benki ya dunia ya kukupa mkopo ni wewe na mkono wako.
 'Ushauri wangu kwako wakija jamaa kama wangu ni kuwalia jiwe, wakija sema haupo wakipiga simu usipokee' akanishauri jamaa yangu nami nikamuitikia na kurudi ofisini kwangu. Nilipoiwasha simu yangu nikaona meseji ikutoka kwa yule rafiki yangu, nikaifuta hata bila kuisoma.
 Mara nikasikia simu ya mezani ikiita, nilipoipokea yule dada akasema rafiki yangu kaja yupo nje. Nikamwambia kwa hasira kuwa kwanini hataki kunielewa, nikamwambia kama kachoka na kazi asema nikasema amwambie huyo jamaa ynagu nipo kwenye vikao mpaka jioni nikakata simu kwa hasira.
 Kumbe jamaa yangu alipata maelezo ya kazi mahali, alipoenda huko akaambiwa anahitajika mtu mwenye sifa kama zangu na kazi hiyo ni tonge na mdomo, yaani ipo wazi kwa siku hiyo ukiikosa siku hiyo basi atapatikana mtu mwingine. Kazi hiyo niliifukuzia siku nyingi, inalipa na inausalama wa mpangilio wa  maisha.
 Jamaa yangu alipoipata hiyo akahangaika kunitafuta kwa simu hadi mwishowe akaamua kuja hapo ofisini na bado nikamtolea nje, kwasababu nilikuwa sijui, na mihamaniko ya maisha ilishanitinga nikakataa kupokewa wito. Basi jamaa yangu akakata tamaa , kwani kila alivyojaribu kumshawwishi yule dada, yule dada hakukubali kwani naye alishakasirika na majibu yangu mabovu. Na mara akakutana na mfanyakazi mmoja ambaye alikuwa hasimu wangu mkubwa, yule rafiki ynagu hakumjua vyema zaidi ya kuwa ni mfanyakazi mwenzangu, alimwelezea kisa cha yeye kunitafuta ili aje kuniambia. Yule rafiki yangu aliposikia hivyo akatafuta upenyo huyo akaifukuzia ile kazi na sasa anapeta kwa mshahara mnono na gari lakutembelea, mimi bado napiga TZ 11
 Jamani wakalamba msipende kukataa wito, na msidharau wenzenu huwezi jua baraka yako ilipo.
 Nilipokutana na jamaa yangu huyo siku kadhaa baadaye akanihadithi hiyo nafasi na kunielezea jinsi alivyotaabika kunitafuta, ilibidi nimuombe radhi na kumweleza kwanini sikupendaa kuipokea simu au kuwasiliana na yeye siku hizo. Na akasema, sio mbaya, kwani naye sasa ana kazi, akasema yule hasimu ynagu alipopata kazi alinipigia debe mle ofisini na sasa naye ameajiriwa humohumo.
 Ujumbe wa leo, Tusikate wito, tunapoalikwa tunapopata wageni tunapoitwa kwenye simu, tuitike kwanza na kusikiliza nini tunachoambiwa baada ya hapo ndipo tunaweza kutoa maamuzi

Mpenzi wa blogi yako
Majuto

2 comments :

Anonymous said...

Kweli, wakati mwingine tunapuuzia hii miito, unaweza ukaitiwa zinga la dili, au jamaa yako kaja ana baraka za mali ukamtimua, jamani tusiwe hivyo. HONGERA KWA HEKIMA ZAKO

Anonymous said...

Lakini wengine wamezidi, ukishamsaidia anaelemea, inabidi wakati mwingine na wao wafikirie, siunajua tena hii mishahara, haizungushiki, sasa upate tegemezi mwingine siutaishia kupata vidonda vya tumbo.