Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Monday, June 21, 2010

Mwenzako akinyolewa...

                                          
‘Dadangu naomba msaada wako, unajua kila siku nakuja kukutembelea hapa ofisini, nimekuwa nikimuona msichana mmoja, nimempenda kweli. Naomba msaada wako, nifanyie juu chini nimpate’ Alisema Yule jamaa huku akitoa noti ya elifu kumi nakumkabidhi Yule dada aliyekuwa akiongea naye.


‘Hivi wewe umechanganyikiwa nini, wewe si una mke, na mkeo namheshimu kama nini, na huyo dada unayesema ni mke wa mtu acha balaa hilo sitaki hiyo hela yako, na tabia ya ukuwadi mimi siijui’ akasema Yule dada na kwa dhihaka akijua mwenzake ana mtania pia, kumbe mwenzake alikuwa kadhamiria.

Hutaamini Yule jamaa hakuchoka kumfuatilia Yule dada ili amfanyie mipango wa kumpata mke wa mtu na hakusita kutoa Zawadi kwa Yule dada na kumuahidi kuwa pindi akifanikiwa atampa zawadi kubwa ambayo hakutegemea. Lakini dada yule haikumwingia akilini.

Yule dada akafikiria sana, akasema hata, lazima nifanye kitu, ambacho kitakuwa fundisho,

`Mimi siwezi kufanya dhambi hiyo, kwani mimi ni mke wa mtu kama walivyo wenzake, leo kwake kesho kwangu, najua kabisa mwenzako akinyolewa wewe tia maji, sasa mimi kabla sijatia maji ngoja nimkomeshe huyu jamaa...'akajisemea kimoyo moyo

Basi siku yake akaamua kufanya jambo, alichofanya ni kuongea na Yule dada anayetamaniwa na huyo jamaa...yaani huyo dada wa hapo ofisini kwao. akamueleza jinsi anavyopata taabu kwa huyo jamaa kila siku anadai kuwa anamtaka , lakini yeye ameona hilo sio jambo jema, wafanye jambo kwa ushirika kumkomoa huyo jamaa.

‘Kwahiyo mimi Naomba tumukomoe huyu jamaa, wewe jifanye kama umekubali, halafu tunachotakiwa nikuhakikisha tunaongea na mke wa huyu jamaa mengineyo yatafuta baadaye, haya ya baadaye niachieni mimi.

'Hapana mimi sitaki kujitia kwenye matatizo hayo namuogopa sana mume wangu...'mwenzake akasema hivyo.

'Sasa unatakaje maana jamaa haach kuja kwangu, au nimuambie aje muongee naye mwenyewe...?' akasema

'Hapana sitaki hata kumuona...'akasema

'Basi tufanye hivyo, najua baada ya hapo hatakuja tena, na itakuwa ni mwisho wa watu kama hao...'akaambiwa na yule mdada mwingine akaona akubali tu.

Basi wote wakakubaliana. Yule dada aliyepewa ukuwadi akatafuta siku akaenda kuonana na mke wa Yule jamaa. Mke wa Yule jamaa hakuamini, kwasababu anavyomjua mumewe ni tofauti na anavyoambiwa , na isitoshe yeye amekuwa akimshibisha kwa kila hali mumewe je leo iweje, na tabia hiyo kaianza lini, akaona akubaliane na huyu dada aliyepewa kazi ya ukuwadi, ili tu apate ushahidi, maana hakuamini hayo anayoambiwa.

Siku ikapangwa na jamaa hana hili wala lile na kwasababu keshapenda, hakutaka kufuatilia nini kinachoendelea, yeye akawa anamwaga mapesa, anatoa Zawadi huku nyumbani kwake wakiambulia dagaa na mchicha. Na mkewe kama wake wa ndoa aliridhika akijua hali ndivyo ilivyo...

Kwasababu hawa wadada hawakutaka kulichukulia haraka isije ikagundulikana kwahiyo waliendea taratibu hatia kwa hatua, na mke wa jamaa nyumbani akawa keshapangwa, japokuwa hakuamini..ila aliona matumizi yakipungua akahisi ndiyo hayo yanakwenda kwingine, alitamani amuulize mume wake, lakini akaona ngoja kwanza ahakikishe tu.

Ilikuwa siku ya Jumamosi wakati sherehe fupi ilitayarishwa kinamna, hii ilikuwa wazo la dada aliyepewa ukuwadi, akamwambia jamaa ili kumpata huyo dada vizuri inabidi tutayarishe sherehe yenye vinywaji vikali na huyo dada akilewa itakuwa rahisi kumpeleka gesti au chumba cha wageni. Na makakati huu alishaambiwa mke wa yule jamaa, kuwa kutatayarishwa sherehe na siku hiyo aje baada ya muda Fulani. Na wote pande zote wakakubaliana.

Za mwizi ni arubani, sherehe fupi iliandaliwa , ilianza muda wa saa kumi na mbili jioni, vinywaji , nyama choma na muziki vikafanyika, na Yule dada mlengwa akafanya kama alivyoelekezwa, lakini yote yanafanyika mume wa mlengwa hana habari, yeye aliagwa kuwa kuna shereha za kawaida ofisini.

Dunia haina siri, mume wa huyo mke anayetakwa, akaja kuambiwa kuwa mkewe kuna tajiri anataka kumribuni, na anayefanya hivyo ni mfanyakazi mwenzake, kwahiyo awe na tahadhari... lakini kuna jamaa alimtonya huyo mume wa dada mlengwa kuwa amegundua kuwa mkewe ana mahusinao na jamaa mmoja na kuna sherehe imeandaliwa kwa lengo la lumpata mkewe.

Jamaa hakuamini, alipaniki, kwani mkewe anampenda sana, sasa iweje amsaliti, hapana, lazima nifanye jambo la kumkomoa,  yeye alichofanya ni kwenda kumtafuta baba wa mkewe ili kama ni kweli akaitoe talaka mbele ya baba mtu.

‘Kama ni kweli unaloniambia basi mimi sitavumilia upuzi huo, sipendi kabisa tabia hiyo kwasababu mimi mwenyewe sijawahi kufanya hivyo, na ili iwe fundisho nitatoa talaka mbele ya baba yake.Wewe nipe data zote, lini wapi...

Ndugu wapenzi, kabla sijaendelea na kisa hiki chenye mafundisho,  je mna maoni gani na hili tukio. Kwasababu natumai haya yapo, umeyasikia au yameshakukuta, na kama bado juwa wazi; mwenzako akinyolewa na wewe tia maji, ipo siku yako au mwezako ana tabia hiyo, L eo kwake kesho kwako, na nina imanai kama watu watashirikiana kama alivyofanya huyu dada tabia kama hizi zitapungua. Tuoane sehemu ya pili itakuwaje.

From miram3

2 comments :

Anonymous said...

Chuna buzi hilo, nyie mtu kama huyo mnamchuna mwishowe mnamtolea nje,

Anonymous said...

Hayo mambo yamepitwa na wakati, huyo ni limbukeni wa ngono, natumai alipata fundisho, tupe yaliyotokea manake unatutengenezea movie kama za Nigeria