Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha
Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..
Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.
MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.
TUPO PAMOJA DAIMA
Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;
https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:
https://www.facebook.com/diaryyangu/
`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;
Friday, June 25, 2010
Mwenzako akinyolewa-hitimisho
‘Wewe mke wangu ondoa ushamba, ofisi siku hizi zinawekwa sehemu kama hizi ili watu wakichoka wapumzika, halafu wateja wenyewe sio ndio hawo hawo’ akasema mume mtu kwa mzaha.
Sauti ya simu ikasikika ikiita, na hiyo ilikuwa Ishara kwa wale dada wawili, kumbe pia ilikuwa ishara aliyoelekezwa mume mtu, na wale dada wawili wakasukuma mlango kuingia chumba namba 104, na Yule mume mtu naye akawa miongoni mwa watu waliosukuma ule mlango, kwa hasira, huku akimvuta baba mkwe mkono ili naye aingie, na baba mkwe akawa anamvuta mkewe mkono kuwa naye awafute nyuma. Wote wakajikuta wapo ndani ya chumba ….!
Hamadi walijikuta ndani ya chumba chenyewe kikiwa na kitanda kikubwa cha kifahari, na vitu vingine, na katika kitanda hicho alikutwa binti mrembo akiwa na nguo za kulalia na pembeni yake alikuwepo jamaa yetu akiwa ametahayari, akiwa hana hata nguo moja ya kumsitiri.
Mume mtu alishikwa na bumbuwazi , hakuamini macho yake na kabla hajatimiza dhamira yake, kama alivyokusudia Yule dada aliyepanga huu mpango akaanza kutoa hotuba fupi, na kuwaomba wote waliofika hapo watulie kwani ana jambo la kuwaambia.
‘Mimi sikujua kuwa baba na mama wa huyu binti watakuwepo au mume wake. Huu ni mpango tulioupanga ili kumkomesha huyu jamaa yetu, ambaye licha ya kuwa na mkewe mzuri bado aliingiwa na tamaa ya kumtamani mfanyakzi mwenzangu ambaye ni m ke wa mtu wa huyu jamaa aliyefika bila mimi kuwa na taarifa. Mimi sikupendelea hili swala lijulikane na watu wote hawa, tulitaka tulifanyae kimyakimya na jamaa apate fundishs bila kuwahusisha watu wote hawa.
`Kwahiyo mimi kama mhusika mkuu nawaomba tuwe na subira, nawaomba hili swala liwe fundisho na tumsamahe mlengwa kwani zote ni tamaa za ibilisi. Kwani tukiwa na jaziba hazitatusaidia kitu, kama mjuavyo hasira hasara. Leo yamemkuta huyu kesho yanaweza yakakukuta wewe kwahiyo tuwe na tahdharai kwa kujifunza kutokana na tukio hili kwani mwenzako akinyolewa nawe ufanye nini…
‘Mimi hamjaniambia kitu hapa, kwanini mke wangu asiniambie kuwa kuna mpango kama huu, au kwa vile mumeshutukiwa ndio maana mnabadili kibao, hapana hili swala mimi najua jinsi ya kulimaliza, Jamaa akawa anatoa karatasi ya kuandika talaka. Lakini wazee na wajumbe waliohakikisha hilo sakata waliingilia kati na yaliyofuata baadaye ikawa fundisho kwa jamaayetu. Tangu siku ile hataki hata kuwaangalia wake za watu kwa jichao la tamaa.
Nini tumejifunza kwenye sakata hili. Je mwasemaje na nyie?
Kwangu mimi kwa maoni zaidi nikuzidi kutabaishana kuwa tujaribi kuzishinda tamaa zetu. Kama una mke au mume basi jitulizeni na hakikisheni mnaongea, ili kuboresha ndoa zenu. Msipende kuwekeana mafundo, kwani kosa dogo linamkaribisha ibilisi kuweka zana zake za kuchonganisha. Sina zaidi kwa leo!
From miram3
3 comments :
Mahitimisho mara nyingi yanakatisha tamaa, unapenda usikie zaidi, lakini hatimaye mzinzi kabambwa, mbona hakutembeza kichapo, angalau kidogo
Sasa unataka kusemaje, kuwa ukipenda ule jiwe. Mimi nafikiri approach yake ilikuwa mbovu, sianiuzie hiyo kesi, watu wengine bwana mpaka utumie wakala.
Wewe ukifumania, usipige, kama ni mume umemfumania mke, tafuta mke wa jamaa muite nawe ujivinjari mbele yao, tuone kama atafurahia na wewe mke unfanya hivyohivyo muite mume wake fanya kama wao
Post a Comment