Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Monday, March 22, 2010

kukosa radhi za wazazi

`Wewe vipi wewe, unaendesha kama umevuta unga' Ilikuwa sauti ya dereva wa daladala tulilopanda akimsemesha dereva wa daladala jingine, ambaye alimpita mbele yake bila ishara yoyote. Cha ajabu yule dereva mwenzake akamuonyeshea kidole cha katikati ikiwa ishara ya tusi, huyu wakwetu hakustahilimili akatamuka tusi kubwa ambalo mimi lilinikera sana.
'Wewe (tusi kubwa likielekezwa kwa mama zetu), inaonyesha hiyo leseni yako umeichongesha' akasema huku anaendesha kwa kasi kumpita huyo mwenzake
'Tusi kama la mwezake likielekezwa kwa akina mama likamtoka dereve mwingine'
 Ikawa matusi juu ya matusi kiasi kwamba sie tuliopo ndani ya gari tukashindwa kuvumilia na kuanza kumshambulia dereva wetu, na akina mama wakaja juu wakitaka dereva huyo aelekee kituo cha polisi, kwani pamoja na kuwazalilisha akina mama kwa matusi mabaya, angeweza kugonga kwa hasira.
 Hii inakera sana, kwanini watu wanagombana au wanaweza kabisa wakawa wanaongea mambo yao, lakini cha ajabu , matusi yanatumbukizwa humo kwenye maongezi kwa kuwaelekezea wazazi wetu ambao hawapo hapo kwenye mazungumzo yao, na baya zaidi yanaelekezwa kwa akina mama. Hivi kweli mama zetu wamewakosea nini? Hebu fikiria huyo mama unayemtukana kwa tusi ambalo kama yeye angeamua kutokuwa mvumilivu angekuharibu maisha yako. Huyu kakulea tumboni miezi tisa, kateseka kukulea hadi umefikia kusema, na kujiona kidume, na fadhila zake ni matusi!
 Inasikitisha zaidi kuwaona hata watu wazima na akili zao wanadiriki kuyatamka matusi kama hayo, mimi nilidhani ni vijana tu waliokosa adabu, lakini madereva hawa walikuwa watu wazima tu. Mbona wasitoe matusi yanayoelekeana na wao?
 Mimi nafikiri sisi kama jamii kuna haja ya kuliangalia hili, hasa akina mama, katika mambo mengi mnayodai inabidi pia kudai haki yakutokudhalilishwa kwa matusi kama haya. Nina imani kama mtatoa kilio chenu kwa wabunge, au kama wabunge huenda sheria kali ikatoka kuwa kwa yoyote atakayeonekana, na kusikika akitamka tusi kama hilo languoni, jamii imchukulie hatua na kumfikisha mbele ya vyombo vya sheria. Jamii ndiyo mashahidi na ndiyo inayoendekeza jambo kama hili.Tujue kuwa laana za kukosa baraka zitatuandama kila siku, kwa kukosa radhi za wazazi, hasa kutoka kwa akina mamazetu, kwani kukosa radhi za wazazi sio lazima akutamkie mzazi wako, hata matendo yetu yanaweza yakutalaani.
From miram3

No comments :